Tundu Lissu aibukia Ivory Coast kwenye Kambi ya Taifa Stars

TRAT

Member
Nov 29, 2022
41
117
Mwenye picha ya video yake akitabainisha kuwa atakuwa huko na timu kwa mechi 2 dhidi ya Morocco na DRC na baadae kuweka nao kambi nchi ya jirani anaweza kutuwekea.

=======

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu ni miongoni mwa Watanzania waliosafiri hadi Ivory Coast kushuhudia ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Africa la TotalEnergies (AFCON) ambapo amerekodi video hii fupi akiwa nje ya Uwanja wa Quattara Jijini Abidjan na kusema Timu ya Tanzania Taifa Stars itarudi na kombe hilo nyumbani.

“Tumepuuzwa kiasi cha kutosha, tumedharauliwa kiasi cha kutosha, unyonge wetu ndio uliotufanya tupuuzwe na kudharauliwa, Vijana wetu wamesema sasa basi, wamekataa kuendelea kupuuzwa na kudharauliwa…. huu ni wakati wa kuwaunga mkono uwanjani wanakochezea, tuko hapa kwa ajili hiyo

Mwenye picha ya video yake akitabainisha kuwa atakuwa huko na timu kwa mechi 2 dhidi ya Morocco na DRC na baadae kuweka nao kambi nchi ya jirani anaweza kutuwekea.
Kama hilo ni kweli, Sasa hivi utatumwa ujumbe mkali wa kutoruhusu Lisu kukanyaga kwenye timu hiyo. Na atakachoambiwa Lisu ni maagizo toka juu asiitembelee hiyo team. Hiyo ni team ya ccm, na wanaitumia kujitangaza kisiasa hasa kuelekea uchaguzi, Sasa mpinzani makini kama Lisu itakuwa kama anataka kupora kete Yao.
 
Mzigo kaamua kuwapelelkea mwenyewe. Kaogopa wazee wa kuchangisha na kubadili matumizi.
 
Kama hilo ni kweli, Sasa hivi utatumwa ujumbe mkali wa kutoruhusu Lisu kukanyaga kwenye timu hiyo. Na atakachoambiwa Lisu ni maagizo toka juu asiitembelee hiyo team. Hiyo ni team ya ccm, na wanaitumia kujitangaza kisiasa hasa kuelekea uchaguzi, Sasa mpinzani makini kama Lisu itakuwa kama anataka kupora kete Yao.
siku zote mawazo ya mtu mjinga ni ujinga mtupu 🐒
 
Hivi Taifa stars ni ya ccm pekee au huyu Tundu Lissu sio Mtanzania kama walivyo hao wachezaji? Ingefaa na yeye awemo kwenye timu atupe burudani, labda wangemuhurumia :)
 
Back
Top Bottom