CHADEMA yapewa saa mbili kuondoa bendera zake kwenye barabara ya Sam Nujoma eneo la Mlimani City. Polisi yafika kushusha bendera hizo

Besta Mlagila

Senior Member
May 29, 2018
101
191
1576659118686.png
Mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic amekiandikia barua chama cha Chadema na kukipa saa mbili kuondoa bendera zake zilizowekwa barabara ya Sam Nujoma karibu na ukumbi wa Mlimani City unakofanyika uchaguzi wa viongozi wa chama hicho.

Bendera hizo ziliwekwa katika barabara hiyo takribani wiki mbili zilizopita ulipoanza uchaguzi wa mabaraza ya chama hicho. Mkutano mkuu wa chama hicho kuchagua mwenyekiti na makamu mwenyekiti utafanyika kesho Jumatano Desemba 18, 2019.

Katika barua hiyo ya leo Jumanne Desemba 17, 2019 kwenda kwa katibu mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji ambayo Mwananchi imeona, mkurugenzi huyo amesema manispaa ya Ubungo ndio inayoihudumia barabara hiyo inashangazwa kuona bendera za chama hicho zikiwa kwenye bustani.

Dominic amesema bendera zimewekwa kama matangazo kinyume na utaratibu wa kibali.

"Kwa barua hii nakutaarifu kuwa unatakiwa uondoe bendera hizo ndani ya muda wa saa mbili baada ya kupokea barua hii. Agizo hii lisipotekelezeka bendera hizo zitaondolewa kwa utaratibu mwingine," inasomeka sehemu ya barua hiyo.

Meya wa Ubungo ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, Boniface Jacob alipoulizwa kuhusu agizo hilo la mkurugenzi amesema, “bendera hizo haziondolewi kwa sababu Chadema tuna haki ya kutumia maeneo ya wazi ya umma kama vyama vingine vya siasa kwa mujibu wa sheria.”


Chanzo: Mwananchi
===


MWENDELEZO
Polisi wamefika eneo la Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar unapofanyika Mkutano wa CHADEMA na kuagiza bendera za chama hicho zilizowekwa kushushwa

Awali, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic alikiandikia barua chama hicho kikuu cha Upinzani Nchini kutaka kishushe bendera hizo
 
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic amekiandikia barua chama cha Chadema na kukipa saa mbili kuondoa bendera zake zilizowekwa barabara ya Sam Nujoma karibu na ukumbi wa Mlimani City unakofanyika uchaguzi wa viongozi wa chama hicho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu hawana akili kabisa, CHADEMA wanamkutano wao hapo, huo mkutano haudumu hata kwa wiki 2 wanachingaika nao ni nini, wakimaliza watafungu na kuondoka, na CHADEMA wameweka bendera kwenye uzio wa ukumbi wa mkutano sio i kama ni tatizo
 
Hivi kuna sheria yoyote ile inayohusu utaratibu wa kuweka bendera, mabango na matangazo? Kama ipo je, imefuatwa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom