Chadema wamezidi kuanguka Uzini ukilinganisha na Uchaguzi wa 2010 - Jussa

Ngoja waje Pro-Chadema JF kina Molemo, MKE GANI, Tumaini Makene.

Yaani kutoka kura 617 hadi kura 281 ndio kujitahidi?

Na CCM kutoka kura 6,651 mwaka 2010 hadi elfu 5,300 miaka 2 baadae ina ashiria nini?Kwa nn Ritz hukuweka akilini kuwa wapiga kura walipungua mno mwaka huu?Kutoka zaidi ya elfu 7 mwaka 2010 hadi elfu 5 tu mwaka huu?
 
Naamini member wote wa hii forum ni great thinker kwa hiyo huwezi toa comment ya kwamba matokeo hayo yanatofautiana na ya 2010. Kwa kuangalia, fanya analysis kwa kutumia chi square ndio utajua kama kunautofauti au la, bila hivyo utashauri watu vibaya.
 
Zanzibar imeshakombokaaaaaaaaaaa! Maalim Seif+Raza+Jussa=Vunja Muungano. Zanzibar Daimaaaaa, na nyinyi piganieni Tanganyika yenu sasa.
 
haaaaaa! mkuu ulitumia maneno makali; afadhali mods wameyaondoa. Punguza jazba
Hakuna kitu kibaya kama mtu kutosoma na kuelewa post yako...akakujibu kulingana na post zilizopita

Jussa kapindisha kijanja sana hoja hii, yaani imetulia...inahitaji akili kugundua na kutafuta hoja ya kumpinga, from no where jitu linakuja na CD nyingine kabisa......then anakuwa amejibu hoja ya Jussa?????, watu kama hawa unawafanyaje?? is he a part of GT? au inambidi umpe kubwa abaki akifurahi mm kupigwa ban na yy kuonekana mjinga?? hivi vitoto ( ID date) huwa vinaboa, vinajifanya vinaipenda chadema weee , vingi vinafiki mno,

Hili jukwaa linapendeza na tumekua hivyo watu wakitofautiana mawazo, na kujua kujenga hoja is a measure of intelligence!! by the way anashindwa hata kusoma signature yangu AKANIELEWA! mtu aliyejiunga siku 40 zilizopita ananijuaje kama siyo TISS au walipigwa bani na wamebadili ID??
 
Hakuna kitu kibaya kama mtu kutosoma na kuelewa post yako...akakujibu kulingana na post zilizopita

Jussa kapindisha kijanja sana hoja hii, yaani imetulia...inahitaji akili kugundua na kutafuta hoja ya kumpinga, from no where jitu linakuja na CD nyingine kabisa......then anakuwa amejibu hoja ya Jussa?????, watu kama hawa unawafanyaje?? is he a part of GT? au inambidi umpe kubwa abaki akifurahi mm kupigwa ban na yy kuonekana mjinga?? hivi vitoto ( ID date) huwa vinaboa, vinajifanya vinaipenda chadema weee , vingi vinafiki mno,

Hili jukwaa linapendeza na tumekua hivyo watu wakitofautiana mawazo, na kujua kujenga hoja is a measure of intelligence!! by the way anashindwa hata kusoma signature yangu AKANIELEWA! mtu aliyejiunga siku 40 zilizopita ananijuaje kama siyo TISS au walipigwa bani na wamebadili ID??

kweli mkuu, hivi vitoto vinaboa ile mbaya, kuna kamoja leo nusura kasababishe nipigwe ban, hovyo sana hivi vitoto tundu,
nilipo'bold nimecheka sana, na ndo vingi kweli asaivi hapa JF, na huko tunakoelekea CDM itakuwa kama CCM, mavuvuzela huwa hawajibu hoja kwa hoja bali kupuliza taralila ili waonekane.
 
Ismail Jussa on facebook say "kura za vyama vyote
ikiwemo CCM zimeshuka. Hiyo ni kwa
sababu hata wapiga kura
wamepungua kwa takriban watu
3,000 ukilinganisha na wapiga kura
zaidi ya 8,000 wa mwaka 2010. Nimetoa mfano wa Chadema kutokana
na wao kuibua hoja ya matokeo haya
kama vile yameonesha kitu kipya
wakisahau takwimu za 2010."
 
kutokana na matokeo ya mwaka 2010 kura waliuzopata CCM 6,651 CHADEMA 617 CUF 524 kura walizopata kwenye uchaguzi mdogo CCM 5,377 CHADEMA 281 CUF 223 kutokana na data hizo hapo utagundua vyama vyote vimepata kura pungufu ukilinganisha na 2010 utaona wote wameanguka asilimia zifuatazo? sasa kupungua kwake CCM 19.2% CHADEMA 54.5% CUF 57.4% kwa hio utagundua kuwa CHADEMA na CUF wote wameanguka zaidi ya nusu ya kura walizopata mwaka 2010. ni kweli CHADEMA ukilinganisha na CUF wao slightly wako afadhali ukilinganisha na CUF lakini kwa kiwango hicho, na nguvu zilizotumika inaonekana chadema wakiri bado hawakubaliki
...Katika haya mahesabu na ubishani wenu kuhusu ushindi huu na blah blah nyingine, msisahau jambo moja la muhimu katika uchaguzi, nalo ni mgombea mwenyewe. Muulizeni Mhe. Shibuda na CCM watawaeleza inavyokuwa.
 
Wakuu zangu,
Kwa Chadema kuendelea kupigania kura Zanzibar ni muhimu sana tofauti na jinsi watu mnavyotaka ieleweke. Maana swala la chama sio kutafuta Ushindi kwa njia zozote zile kama CC, bali kufikisha Ujumbe wkwa wananchi wa Zanzibar wapate kufahamu Chadema ni chama cha aian gani na kinataka kuongoza nchi nzima. Mkisema Chadema isijipange zanzibar basi ni sawa na kusema Chadema haiko tayari kuongoza nchi nzima hivyo ijikite ktk baadhi ya maeneo.

Hizi ndizo siasa za baadhi ya watu wanaamini hivyo na tuliwaambia viongozi wa Chdema mapema hukusu kukipeleka chama kwa wananchi iwe vijijini hadi Zanzibar maana chama ni WATU na sio nembo na bendera..Hivyo hata kama wametumia mabillioni lakini maadam wananchi wa Zanzibar leo wanajua kuna chama kinaitwa Chadema na kina malengo kadhaa wa kadhaa basi haya ndio matumizi yanayokubalika.

Huyu Jussa mchawi tu sijui kenda shule kushinda mitihani au ana akili timamu. hata kama utachukua matokeo ya mwaka 2010 kama ni wagombea Uwakilishi (jambo ambalo halikutokea) bado hakuzingatia kwamba mwaka huu 1/3 ya wapiga kura hawakujitokeza na pia kuna kura ambazo zimeharibika. Hivyo ukizingatia kura hizo ninaweza kabisa kutoa sura tofauti na mwaka 2010. La muhimu ni kwa vyama vyote iwe CCM, CUF na CDM ni kujiuliza kwa nini Wananchi wapiga kura wa Uzini hawakujitokeza kwa wingi maana yawezekana kabisa kura zao zimechakachuliwa..

Chadema nawapa pongezi sana kuwafikia watu wa Zanzibar na juhudi hizo ziendelezwe hadi kufikia sehemu zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kujali ni kiasi gani kinatumika maana hii ndio kazi ya ruzuku mnayopewa na sio kujilipa mishahara na misafara yenye isiyokuwa na malengo.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Raza hakushinda uchaguzi, kafanya mauaji ya kikatili sana kwa chadema huku anacheka. Hongera Raza, umetuaminisha kuwa kundi zima la chadema likiongozwa na mwenyekiti wao wa taifa si lolote si chochote kwako.

2015 ndio kabisa Zanzibar, maana kuna Jussa huko anapakaza ile mbaya.
 
Sindano zingine jamani ni chungu; sema tu inabidi ustahimilivu, iwe ya kwinini au shubiri, ukishindwa kuhimili unaomba tu mtu akushikilie wakati bomba la dawa linasokomezwa!!!
 
Sindano zingine jamani ni chungu; sema tu inabidi ustahimilivu, iwe ya kwinini au shubiri, ukishindwa kuhimili unaomba tu mtu akushikilie wakati bomba la dawa linasokomezwa!!!

Naamini wewe ni Greater Thinker.
 
Ukisikia spinning basi hii ndiyo yenyewe.

Jussa anasema hivi " CUF kwa kuzielewa siasa za Zanzibar hatukusumbuka kutumia fedha nyingi. Tumetumia milioni 7 tu wakati Chadema wamenambia wametumia milioni 60 (haidhuru mimi naamini wametumia zaidi kwa mambo tuliyoyaona kule)".

Labda Jussa angefafanua, CUF wanaelewa kitu gani hasa kuhusu siasa za Zanzibar? Anaamanisha nini anaposema 'kuelewa'? kugawana vyeo? Na kwa nini watumie milioni 7? za nini wakati wanaelewa siasa za Zanzibar? CUF kushindwa Igunga ilikuwa kigugumizi lakini watu walidhani ni kwa sababu CUF hawana 'time' na Tanganyika, sasa Zanzibar kwa nini CUF ishike nafasi ya3? tena CUF inayoelewa siasa za Zanzibar? Wanaelewa nini hawa wajomba?
Millioni saba si hela haba pia sasa kwa kujua kwa 100% wanashindwa na kwa kuzijua siasa za zanzibar kwa nini walisimamisha gombea? si wangeweza kumuunga mkono mume wao CCM kuliko kupoteza million 7 for nothing??
 
Jusa we ushakubali ndoa na Magamba so acha kelele ujenge na kulea familia yako, jirembe kwa hina, shedo, wanja wa pusi, jichore piko mwili mzima, jistiri kwa Hijab au hata mtandio, ukitoka kujimwagia maji mtoto unatakiwa usiburuze Miguu, mpikie MR Gamba chakula maridhawa, kifunike kwa kawa na wala si kwa hotpot, Magamba akiwa anakula shurti uwe pembeni yake kumwimbia twaarab huku ukimpepea...
 
Ilianza IGUNGA, ikaja UZINI sasa ARUMERU......! Ndugu wakigombana chukua jembe ukalime wakipatana chukua kapu ukavune!!! Vita vya panzi furaha ya kunguru.....! Mpaka muelewane kazi itakuwa nzito.....HONGERENI NCCR kwa kufuta kesi za chaguzi,huo ndio mshikamano na hatua za kuungana. Mkifanya vitu kama hivyo kumi mtakuwa mbali
 
Na wewe Jussa ebu tumia akili kidogo,hauoni hata idadi ya wapiga kura imepungua?maana hata idadi ya kura kwa vyama vyote ilivyokua 2010 ni pungufu ya sasa!hacha fikra mgando!

Huyu Bwana mdogo huo uchambuzi wake kauokota wapi, mimi nadhani huyu jamaa ni sawa na mfa maji tu. Mara siasa tunazielewa, mara tulijua tunachofuata, mara tumetumia million 7. Wapi bwana mdogo.... Lete hoja za kwanini mmeshindwa hapo Uzinzi.
 
Back
Top Bottom