CHADEMA yasusia Uchaguzi Wabunge wa EALA

SemperFI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
1,054
2,222
Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema chama hicho hakitashiriki uchaguzi wa kuwapata wabunge watakaoiwakilisha Tanzania kwenye Bunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashiriki (Eala).

Uchaguzi huo utafanyika katika mkutano wa Bunge la Tanzania utakaoanza Septemba 13, 2022 jijini Dodoma.

Mnyika amesema vikao vya Chadema bado havijajadili msimamo wake kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ambao walisema matokeo yake hawayatambui.

Katibu Mkuu huyo ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Septemba 5, 2022 wakati akizungumza na Mwananchi Digital, kuhusu ushiriki wa wao Eala baada ya vyama vya ACT - Wazalendo na CUF kukamilisha mchakato wa uteuzi wa majina ya wagombea wao watakaowakilisha vyama hivyo katika uchaguzi huo.

Wakati ACT-Wazalendo na CUF vikiteua wagombea wao leo Jumatatu CCM inamalizia mchakato wa uhakiki wa majina ya wagombea wao waliowasilisha vielelezo na sifa za kuwania ubunge wa Eala.

“Hatutashiriki, vikao vya chama havijabadili bado msimamo wetu kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Tunasisitiza kuharakishwa kwa mchakato wa kupata KatibaMpya, Tume Huru ya Uchaguzi.

“Pia kushughulikia wa athari na madhara yaliyotokana na uchaguzi mkuu wa 2020. Ni vema dhamira ya kufungua ukurasa mpya kuonyeshwa kwa haraka kwa masuala yenye kuhitaji utekelezaji wa Katiba na sheria mfano haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara,” amesema Mnyika.

Mbali na hilo, Septemba 14, mwaka 2021 Chadema kilisusia uchaguzi mdogo wa marudio wa jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga, kikisisitiza hakitashiriki mchakato wowote hadi Tume Huru ya uchaguzi itakapopatikana.

Pia Chadema kilisusia kikao cha ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa na wadau wa demokrasia uliofanyika jijini Dodoma na kufunguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
100,312
174,699
JamiiForums753274111.jpg
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
17,167
18,390
Taarifa hizi ziwafikiwe wadau wetu wa kanda hii ya Afrika Mashariki kuwa Tanzania kisiasa kuna mushkeli mkubwa unaohitaji njia nyingi mbadala kuisitua serikali ya mfumo wa utawala wa chama kimoja uliofanikishwa ktk uchafuzi wa uchaguzi usio huru wala haki ulioasisiwa na mchakato mzima wa kuwanyima nafasi ya vyama vingine kushiriki jatika demokrasia.
 
Hakika
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
50,072
86,370
Kususa haijawahi kuwa suluhu... Vyama vingine vinashiriki.

Ni kweli kabisa, lakini itakuwa bonge la upuuzi kushiriki uchaguzi ambao unajua kabisa hata uchaguzi uliotoa nafasi ya hivyo viti ni wa kihuni. Hata Mbowe nilimuona hana maana kwa kukubali kukutana na mama Samia kwenye ule utapeli uitwao maridhiano. Kukubali kushiriki kwenye michakato ya kihuni ni kuendelea kubariki uhuni kufanyika.
 
chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
8,814
12,073
Lissu ana roho mbaya sana, kwa kuwa yeye hana cheo chochote, anafanya juu chini na wenzake wakose, hata kesi ya akina mdee ni yeye ndio anashinikiza ili wakose ubunge, kwenye bunge la Afrika mashariki pia amezuia ili wakose wote
 
Maulaga59

JF-Expert Member
Feb 1, 2021
2,163
2,006
Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema chama hicho hakitashiriki uchaguzi wa kuwapata wabunge watakaoiwakilisha Tanzania kwenye Bunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashiriki (Eala).

Uchaguzi huo utafanyika katika mkutano wa Bunge la Tanzania utakaoanza Septemba 13, 2022 jijini Dodoma.

Mnyika amesema vikao vya Chadema bado havijajadili msimamo wake kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ambao walisema matokeo yake hawayatambui.

Katibu Mkuu huyo ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Septemba 5, 2022 wakati akizungumza na Mwananchi Digital, kuhusu ushiriki wa wao Eala baada ya vyama vya ACT - Wazalendo na CUF kukamilisha mchakato wa uteuzi wa majina ya wagombea wao watakaowakilisha vyama hivyo katika uchaguzi huo.

Wakati ACT-Wazalendo na CUF vikiteua wagombea wao leo Jumatatu CCM inamalizia mchakato wa uhakiki wa majina ya wagombea wao waliowasilisha vielelezo na sifa za kuwania ubunge wa Eala.

“Hatutashiriki, vikao vya chama havijabadili bado msimamo wetu kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Tunasisitiza kuharakishwa kwa mchakato wa kupata KatibaMpya, Tume Huru ya Uchaguzi.

“Pia kushughulikia wa athari na madhara yaliyotokana na uchaguzi mkuu wa 2020. Ni vema dhamira ya kufungua ukurasa mpya kuonyeshwa kwa haraka kwa masuala yenye kuhitaji utekelezaji wa Katiba na sheria mfano haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara,” amesema Mnyika.

Mbali na hilo, Septemba 14, mwaka 2021 Chadema kilisusia uchaguzi mdogo wa marudio wa jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga, kikisisitiza hakitashiriki mchakato wowote hadi Tume Huru ya uchaguzi itakapopatikana.

Pia Chadema kilisusia kikao cha ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa na wadau wa demokrasia uliofanyika jijini Dodoma na kufunguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Msusie msisusie, mfoke msifoke, mlie msilie, mnune msinue, mbweke msibweke, haiwasaidii kitu maana kuvuja kwa pakacha ni nafuu ya mchukuzi. Wabunge watapatikana tuu hata wote wakitoka CCM. Nyinyi mtabaki kufoka tu wenzenu wanacheka na nyavu! Kama baadhi ya vyama vimeshakubali kushiriki, CHADOMO ni mdudu gani mbele ya umma wa kitanzania! Leo watasema hawashiriki, kesho utashangaa wanakinga bakuli la njaa ya ruzuku! Hawa ni njaa tupu sasa hivi, hawana mbele wala nyuma wala kushoto wala kulia!
 
mangikule

JF-Expert Member
Jun 11, 2012
5,295
4,326

Hata nyang'au wanaita mizoga inayonuka ni mboga murua!
 
Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
22,342
27,712
Kwa nchi yetu ilivyo, usishangae ukasikia kuna mtu karejesha fomu yenye Saini ya Mnyika wakati hakuna mahali chama kimetoa fomu!!

Haya mambo yanatia hasira sana, inabidi ifike hatua hata Mbowe aajiri snipers Ili tuheshimiane kidogo.
Malalamiko fc!

Chukueni hatua
 
Maulaga59

JF-Expert Member
Feb 1, 2021
2,163
2,006
Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema chama hicho hakitashiriki uchaguzi wa kuwapata wabunge watakaoiwakilisha Tanzania kwenye Bunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashiriki (Eala).

Uchaguzi huo utafanyika katika mkutano wa Bunge la Tanzania utakaoanza Septemba 13, 2022 jijini Dodoma.

Mnyika amesema vikao vya Chadema bado havijajadili msimamo wake kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ambao walisema matokeo yake hawayatambui.

Katibu Mkuu huyo ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Septemba 5, 2022 wakati akizungumza na Mwananchi Digital, kuhusu ushiriki wa wao Eala baada ya vyama vya ACT - Wazalendo na CUF kukamilisha mchakato wa uteuzi wa majina ya wagombea wao watakaowakilisha vyama hivyo katika uchaguzi huo.

Wakati ACT-Wazalendo na CUF vikiteua wagombea wao leo Jumatatu CCM inamalizia mchakato wa uhakiki wa majina ya wagombea wao waliowasilisha vielelezo na sifa za kuwania ubunge wa Eala.

“Hatutashiriki, vikao vya chama havijabadili bado msimamo wetu kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Tunasisitiza kuharakishwa kwa mchakato wa kupata KatibaMpya, Tume Huru ya Uchaguzi.

“Pia kushughulikia wa athari na madhara yaliyotokana na uchaguzi mkuu wa 2020. Ni vema dhamira ya kufungua ukurasa mpya kuonyeshwa kwa haraka kwa masuala yenye kuhitaji utekelezaji wa Katiba na sheria mfano haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara,” amesema Mnyika.

Mbali na hilo, Septemba 14, mwaka 2021 Chadema kilisusia uchaguzi mdogo wa marudio wa jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga, kikisisitiza hakitashiriki mchakato wowote hadi Tume Huru ya uchaguzi itakapopatikana.

Pia Chadema kilisusia kikao cha ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa na wadau wa demokrasia uliofanyika jijini Dodoma na kufunguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Wanajua ngoma iliyo mbele yao maana wanaelewa kuwa wanaenda kuwa wasindikizaji hawa CHADOMO, wakithubutu kutia mguu hawapati hata kura ya kujipigia wenyewe, watakuta wanampigia mtu mwingine!
 
Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
22,342
27,712
Ni kweli kabisa, lakini itakuwa bonge la upuuzi kushiriki uchaguzi ambao unajua kabisa hata uchaguzi uliotoa nafasi ya hivyo viti ni wa kihuni. Hata Mbowe nilimuona hana maana kwa kukubali kukutana na mama Samia kwenye ule utapeli uitwao maridhiano. Kukubali kushiriki kwenye michakato ya kihuni ni kuendelea kubariki uhuni kufanyika.
Mama anaupiga mwingi!

Siyo dhalimu...

Tunapumua
 
12 Reactions
Reply
Top Bottom