CHADEMA Special Thread

CHADEMA Special Thread

Akaunti ya X (Twitter) ya Chadema iliyokuwa ikijulikana kama ChademaTz. Akaunti hii, ambayo kwa muda mrefu imekuwa chombo muhimu cha mawasiliano na taarifa za Chama, imechukuliwa na kuuzwa kinyume na taratibu na maadili ya Chama.

Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa aliyekuwa Afisa wa Chadema, Abdulkarim Muro, alihusika kuiuza kwa John Marwa, ambaye sasa anaitumia kupitia chombo chake kingine cha habari cha Royal Television.

Kwa kuzingatia hali hii, tunatoa wito kwa Abdulkarim Muro na John Marwa kurejesha akaunti hiyo kwa Chama ndani ya muda wa siku tatu kuanzia leo.

Iwapo watalazimika kupuuza wito huu, tutatangaza hatua ya pili ya kuchukua.
1774110406799.jpg
 
JOPO LA MAWAKILI WA CHADEMA TAYARI LIMEWASILI DODOMA.

Timu ya mawakili wa CHADEMA imewasili salama mkoani Dodoma, tayari kwa ajili ya kesi za marejeo Mahakama ya Rufaa kuanzia tarehe 24/03/2025.

Timu yetu inaongozwa na Wakili Mwandamizi, Mpale Mpoki Kaba, Dr Rugemeleza Nshala ambaye pia ni mwanasheria Mkuu wa Chama, Gaston Garubindi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sheria wa Chama, Dickson Matata ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu, Wakili Mwasipu Hekima na wakili Nashon Nkungu.

Mtakumbuka kwamba, Mahakama ya Rufaa itafanya Revision kwenye kesi ya Madai namba 8323/2025 baina ya Said Issa Mohamed na wenzake dhidi ya Bodi ya wadhamini wa Chama na Katibu Mkuu wa Chama, pamoja na Maombi madogo yaliyotokana na kesi hiyo ikiwa ni pamoja na Maombi yaliyosababisha Chama kuzuiwa kufanya shughuli za chama, Maombi ya kumtaka Jaji Mwanga kujitoa na kukataa na Maombi ya wadai kupatiwa nyaraka za chama !

Marejeo yote haya, yamepewa namba kama revision No. 1 /2026, civil Revision No 2/ 2026, Civil Revision No. 3/2026 na Civil Revision No. 4 /2026.
1774197216568.jpg
 
Binti aliepoteza mguu wake October 29, 2025.

Imeanzishwa media ya kuwakumbuka ndugu zetu waliouwawa Tarehe 29.10.2025.

Media hii itapost kumbukizi zote za uovu WOTE wa Serikali.

Media inatwa @mo29_tv kila MTU afanye ku Subscribe

LINK MO 29 TV
1774198639297.jpg
 
Ujumbe wa Prof Anna Tibaijuka

MAWAKILI WA CHADEMA WAKIWASILI DODOMA KUTETEA CHAMA CHAO: Ni haki kwa mlalamikaji yeyote kutafuta haki yake mahakamani ila historia inaonesha matumizi ya mifumo ya mahakama kutatua migogoro ya vyama vya siasa hayajaonesha mafanikio ya kudumu barani Afrika. Mfano mashuhuri ni ANC iliyopigwa marufuku mwaka 1960 na Makaburu, ikalazimika kufanya shughuli zake kwa siri, takriban miaka 32 viongozi wake wakifungwa au kukaa uhamishoni.

Matokeo ANC ikajijengea uhalali mkubwa ndani na nje ya nchi na hatimaye, Mfumo wa ubaguzi ulipoanguka, ANC iliibuka ikiwa na nguvu zaidi na kushinda uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia mwaka 1994 chini ya uongozi wa Nelson Mandela. Jaribio la kukiondoa chama hicho kupitia sheria liliishia kukiimarisha.

Pili ni Senegal, chama cha PASTEF kilipigwa marufuku mwaka 2023. Hatua hiyo ilichochea hisia za wananchi dhidi ya kile kilichoonekana kama ukandamizaji wa kisiasa, na mwaka mmoja tu baadaye, 2024, viongozi wanaohusishwa na chama hicho walishinda urais. Tukio hili linaonyesha jinsi hatua za kisheria zinavyoweza kubadili chama cha upinzani kuwa alama ya mapambano ya kisiasa.

Tatu, Gambia, wakati wa utawala wa Yahya Jammeh, vyama vya upinzani vilikumbana na vizuizi vikali, ikiwa ni pamoja na kupigwa marufuku. Hata hivyo, vyama hivyo vilijipanga upya, vikaungana, na hatimaye kushinda uchaguzi wa mwaka 2016. Hivyo basi, ukandamizaji haukuondoa nguvu zao bali uliwafanya wawe na mshikamano zaidi.

Tanzania tunatambuliwa kuvisaidia vyama vya ukombozi wa Afrika hadi uhuru wao, huku vikiwa vimepigwa marufuku na tawala za kikoloni ikiwemo: ZANU-PF ya Zimbabwe, MPLA ya Angola, na FRELIMO ya Msumbiji.

Matumizi ya mahakama katika ushindani wa kisiasa hakulipi. USHAURI WANGU TUJISAHIHISHE NDANI NA NJE YA VYAMA VYETU kushindania uongozi bora hasa wakati huu tunapohitaji MARIDHIANO na MSHIKAMANO ili kulileta taifa letu Pamoja.
1774241129594.jpg
 
Tarehe 29 Mwezi huu ni siku ya kuwaenzi na kuwakumbuka watanganyika wenzetu waliouwawa kwenye maandamano MO 29 TV kuwa sehemu ya maadhimisho haya #share
1774343251048.jpg
 
George Sanga, msaliti wa Watanzania, amezua mjadala mpana katika jamii kufuatia hatua yake ya kubadili msimamo na kuacha njia ya mapambano ya haki na demokrasia. Kitendo chake kinatazamwa na wengi kama usaliti mkubwa dhidi ya jitihada za pamoja zilizojengwa kwa muda mrefu kwa gharama na mchango wa wananchi waliomuamini na kumsimamia katika nyakati ngumu.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za matukio yaliyoshuhudiwa na umma, George Sanga aliwahi kukumbwa na kesi nzito ya mauaji iliyokuwa na adhabu kali. Katika kipindi hicho kigumu, Watanzania waliinuka kwa pamoja na kumuunga mkono kwa hali na mali, wakimchangia fedha za chakula akiwa gerezani, kusaidia familia yake kwa mahitaji ya kila siku, pamoja na kugharamia ada ya elimu ya mtoto wake. Baada ya kutoka gerezani, wananchi hao hao walimchangia mtaji ili aweze kurejea katika maisha ya kawaida.

Vilevile, viongozi na wanachama wa CHADEMA walionyesha mshikamano mkubwa kwa kufunga safari kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania kwenda kumtembelea na kumtia moyo alipokuwa kifungoni. Hatua hizi zilidhihirisha wazi imani na matumaini makubwa yaliyowekwa juu yake kama sehemu ya harakati za kuleta mabadiliko ya kweli nchini.

Hata hivyo, katika hali inayozua masikitiko makubwa, George Sanga ameondoka katika chama hicho na kujiunga na CHAUMA, huku akianza kutoa kauli za kejeli na dharau kwa wapigania haki na demokrasia. Aidha, hatua yake ya kuonekana kuwatetea wale waliowahi kumuweka gerezani imeibua hisia kali za kusalitiwa miongoni mwa wananchi waliowahi kusimama naye.

Mabadiliko haya ya ghafla ya msimamo yanaibua maswali makubwa kuhusu uaminifu, uadilifu na dhamira ya kweli ya viongozi ndani ya harakati za kijamii na kisiasa. Jamii inatarajia uwajibikaji na msimamo thabiti kutoka kwa wale wanaopewa dhamana ya kuongoza na kuwakilisha sauti za wananchi.

Wito unatolewa kwa wadau wote wa haki na demokrasia kuendelea kuwa imara, kushikamana na kutetea misingi ya haki na ukweli bila kuyumbishwa na matukio ya mtu mmoja. Mapambano ya haki na demokrasia hayawezi kusimamishwa na mabadiliko ya msimamo ya mtu binafsi, bali yataendelea kwa nguvu ya umma.
1774582330768.jpg
 
Sisi huyu tunazika wenyewe, Challenge ya Milioni 5 mpaka kesho Jumanne saa Tano Asubuhi.

BWEGE alijiunga na Chadema wiki chache kabla ya KIFO Chake.
1774914289487.jpg
 
Wanachama na Viongozi kutoka Kanda ya Pwani asubuhi hii wameanza safari ya kuelekea Kilwa Kusini kushiriki kazishi ya Selemani Bungara (Bwege). Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara, Mheshimiwa John Heche ataongoza wananchi kwenye mazishi hayo leo saa saba mchana.
1774941394187.jpg
 

Attachments

  • 1774941387733.jpg
    1774941387733.jpg
    297.5 KB · Views: 6
  • 1774941390780.jpg
    1774941390780.jpg
    450.6 KB · Views: 4
Leo tarehe 31 Machi 2026 imetolewa tamko la mshikamano la Pan-African lililotolewa Nairobi, nchini Kenya likionyesha wasiwasi mkubwa juu ya hali ya haki za binadamu Tanzania na Uganda, huku likitoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa wafungwa wote wa kisiasa.
1774966603196.jpg
1774966600238.jpg
1774966597258.jpg
 
‼️TAHADHARI‼️

Wapendwa WANACHADEMA pamoja na Wapenda Mabadiliko wote popote pale mlipo.

Nawaomba sana kuweni makini na hawa Vijana mnaowaona kwenye hizi picha.

Huyu upande wa kulia anaitwa Daniel Naftal na huyu wa kushoto anaitwa Bruce Cuthbert, hawa watu wanajitambulisha kwamba wao ni Wanachama wa CHADEMA lakini kazi ambayo wanafanya ni ya kuhujumu CHADEMA.

Hawa watu kwa kushirikiana na watu wa TISS kupitia ofisa wa TISS ambae anaitwa Frank Malaki mwenye namba za simu +255 742 007 799 wapewa fungu la pesa ili wapite huko Mikoani washawishi Viongozi wa CHADEMA kwenye majimbo, Wilaya, Mikoa na Kanda ili watangaze kujiuzulu nyadhifa zao kisha badae watangaze kujiunga na CCM au CHAUMWA.

Wanaambia VIONGOZI wa CHADEMA kwamba CHADEMA inaenda kufutwa so bora wahame waende CCM au CHAUMA.

Walianza kuwashiwishi Viongozi wa CHADEMA Kanda ya Nyasa lakin hawakupata mtu, halafu kila wanapoenda kukutana na Viongozi wa CHADEMA wanaenda kama Makamanda kumbe wamebeba ujumbe wa MACCM.

Walienda Kanda ya Kusini wakatoka kapa,

Wameenda Kanda ya Kati wamepata Kiongozi mmoja ambae anatarajia kutangaza kuhama hivi karibuni maana kadanganywa, kaambiwa alete CV atatafutiwa kazi Serikali.😂

Sasa hivi wapo Kanda ya Kaskazini, wameweka kambi yao Arusha mjini na mpaka sasa tayari kuna Viongozi wa Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga wameshafikiwa lakin bahati nzuri Viongozi wetu wengi wamekataa na wamewambia hawa madalali kwamba katu hawawezi kusaliti Mapambano.

Nawapongeza Viongozi wa maeneo yote ambao mmekataa pesa na ahadi za kutafutiwa kazi Serikalini kutoka kwa hawa Madalali wa Siasa.

Viongozi wa CHADEMA ambao bado hawajafika kwenye maeneo yenu kaeni RADA mkiona tu sura zao kwenye maeneo wakija na story za kuwashawishi/kuwapa pesa ili mtangaze kujiuzulu wapeni HAKI YAO YA KIKATIBA ILI IWE FUNZO KWA MADALALI WOTE WA SIASA.
1775072112665.jpg
1775072106870.jpg
 
Back
Top Bottom