Bendera iliyochanika lakini bado inapepea.
Katika sanaa ya kisiasa, bendera iliyoharibika mara nyingi huashiria kuwa kundi au harakati imepitia mashinikizo, migogoro, au mashambulizi ya kisiasa. Bendera bado ipo juu ya mlingoti na inapepea. Hii ni ishara ya ustahimilivu na kuendelea kuwepo.
Upepo mkali unaopeperusha bendera.
Upepo tunaweza kutafsiri kama nguvu kutoka nje—pressure ya kisiasa, vyombo vya dola, au mazingira magumu ya ushindani wa kisiasa. Kwa mtazamo wa kisiasa, upepo unatafasiriwa kama ishara ya nguvu au shinikizo linalotoka kwa dola au mfumo wa utawala.
Mawingu mazito angani.
Mawingu katika sanaa mara nyingi hutumika kuonyesha hali ya sintofahamu, mgogoro, au kipindi kigumu. Hivyo anga lenye mawingu linaweza kuwakilisha mazingira ya kisiasa yenye mvutano katika Tanzania, hasa wakati wa ushindani mkali uliopo kati ya CHADEMA na DOLA.
Mlingoti mrefu unaoshikilia bendera.
Huu unaweza kuashiria msingi wa harakati—yaani wanachama, wafuasi, au misingi ya chama. Hata kama bendera imechanika, mlingoti bado umesimama na umenyooka wima, ikimaanisha kwamba msingi wa harakati bado haujaanguka. Bado upo imara.
Kwa kuzingatia harakati nyingi za kisiasa barani Afrika, harakati za wananchi zinapofikia hatua fulani, haziwezi tena kusimamishwa na nguvu tu za dola. CHADEMA imepita maumivu mengi — viongozi kufungwa, mikutano kupigwa marufuku, wanachama kunyanyaswa.
Katika historia, harakati zinazozaliwa kutokana na kile wananchi wanachoona kama ukandamizaji mara nyingi huimarika zaidi kadiri shinikizo linapoongezeka. Kila shambulizi kutoka kwa “dola katili” linatafsiriwa kama uthibitisho harakati hiyo ina ukweli unaoogopwa.
CHADEMA sasa ni imani. Itikadi ya CHADEMA imejikita ndani ya mioyo ya watu. Kitalaam, taasisi ikishafikia hatua ya kuwa harakati (movement), inakuwa vigumu kuizima kwa kutumia nguvu za dola pekee, kwa sababu huwezi “kufunga” au “kupiga marufuku” fikra.
CHADEMA imeshambuliwa sana na dola katili la CCM lakini bado inapepea. CHADEMA ni movement siyo tena chama cha siasa. Dola katili ya MaCCM inatakiwa kuelewa kwamba, CHADEMA ni imani ya watanzania. Hakuna idadi ya vitisho ambayo itawaogopesha.
NB; huu ni mtazamo wangu binafsi. Ukweli na usahihi wa kazi hii ya sanaa ni wa mtunzi, Masoud Kipanya