CHADEMA Special Thread

CHADEMA Special Thread

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepiga fataki katika Makao Makuu yake, Edwin Mtei House, Mikocheni jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya miaka 20 tangu kufanyika kwa mabadiliko makubwa ya chama mwaka 2006.

Shughuli hiyo imefanyika usiku wa leo huku wanachama na viongozi wa chama wakishiriki katika kumbukizi hiyo inayorejea kipindi kinachoelezwa kuwa kilikuwa na umuhimu mkubwa katika historia ya CHADEMA.

Kwa mujibu wa chama hicho, maadhimisho hayo yanalenga kukumbuka hatua za mageuzi zilizofanyika mwaka 2006 na mchango wake katika safari ya kisiasa ya CHADEMA ndani ya Tanzania.

Fataki hizo zimepigwa katika eneo la Makao Makuu ya chama kama ishara ya kuadhimisha miaka 20 ya mabadiliko hayo ya kihistoria.


View: https://www.facebook.com/share/v/1W4drie9e1/
 
#BREAKINGNEWS

Wakili wa Serikali mkuu Nassoro Katuga anaiambia Mahakama kuwa upande wa Jamhuri umeoana ushahidi ambao umekwishatolewa unajitosheleza hivo basi hakuna sababu ya kuongeza ushahidi mwingine. Jamhuri wanaomba kufunga ushahidi wao kwa idadi ya mashahidi hao 17. Tundu Lissu
 
TAARIFA

Mwalimu John Ngoni (kushoto pichani) ameachiwa huru leo baada ya kuchukuliwa na Polisi takribani wiki mbili.
simu zake zote zinashikiliwa kwa uchunguzi na hizo hazirudi tena.

Polisi sasa wamejigeuza mahakama wanakamata MTU wanakaa nae Mpaka siku 40 wengeni wiki tatu wengine wiki 2.
1786970263135.jpg
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Katavi kimepiga yowe kwa mawakili na asasi za haki za binadamu nchini kujitokeza kwa wingi kutoa msaada wa kisheria kwa kijana Lubamba Geremia Lubamba (21), anayeendelea kusota mahabusu kwa shtaka la uhujumu uchumi lisilo na dhamana.

Taarifa kwa umma iliyotolewa leo Agosti 18, 2026 na Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Katavi, Deus Kamoja, imeeleza kuwa kijana huyo alikamatwa tangu Julai 5, 2026 Mlele kwa tuhuma za uchochezi, kabla ya kufikishwa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Julai 30 na kusomewa shtaka hilo zito la uhujumu uchumi (Shauri Na. 17065/2026).

Kamoja amebainisha kuwa ingawa uongozi wa CHADEMA Mkoa wa Katavi chini ya Mwenyekiti Rhoda Kunchela tayari umemtafuta Wakili Kenani Chombala kutoka Tabora, uzito wa shtaka hilo unahitaji jopo pana zaidi la mawakili ili kuokoa haki ya kijana huyo.

"Lubamba anaendelea kushikiliwa katika Gereza la Mpanda kwa kuwa shtaka linalomkabili halina dhamana. Tunaendelea kuwaomba wadau wengine wa haki za binadamu kuongeza msaada wa kisheria, ikiwemo kuongeza idadi ya mawakili katika shauri hilo," amesisitiza Katibu Kamoja.

CHADEMA imetoa wito kwa wananchi na watetezi wa haki za binadamu kujitokeza kwa wingi katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda tarehe Agosti 27, 2026, wakati shauri hilo litakapotajwa tena.

#SasaLive #CHADEMA #Katavi #Mpanda #MsaadaWaKisheria HakiZaBinadamu TanzaniaNews
1787115159263.jpg
 
Juzi baada ya kumpost Bibi yake Deusdedith Soka, watu wengi mliomba tufanye jambo kwa ajili ya Bibi yake Soka.

Sasa, jana Mwenyekiti wetu wa Bavicha Kanda ya Pwani John Nguti Wa Chadema pamoja Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Kilimanjaro Achibod Mmbando walienda Kijijini kumtembelea Bibi yake Soka baada ya kuzungumza nae, kuna vitu vya muhimu ambavyo Bibi anahitaji ikiwemo ni Bima afya.

Hivyo tunaomba kila mmoja aliyeguswa na jambo hili atume mchango wake kwenda kwenye-;

Mpesa : 0740498941
Jina: Theresia Soka.

NB. Tunakusudia kukusanya milioni tano.
1787206308660.jpg
 
Aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Jimbo la Mbeya Vijijini, mtia nia wa ubunge wa jimbo hilo mwaka 2015 na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo ya CHADEMA Kanda ya Nyasa, Chance Mwaikambo, amesema aliwahi kukamatwa na kufichwa kwa zaidi ya miezi mitatu wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Mwaikambo ameyasema hayo Hivi karibuni wakati akizungumzia matukio ya mauaji, utekaji na kupotea kwa raia nchini Tanzania, akidai kuwa matukio hayo yameendelea kujitokeza katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni.

Amesema akiwa Meneja wa Kampeni katika uchaguzi wa mwaka 2020 katika Jimbo la Lupa, Chunya, alikamatwa na polisi na hakufikishwa kituo cha polisi hadi baada ya siku mbili.

Kwa mujibu wa Mwaikambo, baada ya kufikishwa kituoni alifichwa kwa zaidi ya miezi mitatu bila familia yake wala chama chake kupewa taarifa kuhusu alikokuwa.

Mwaikambo anadai kuwa wakati huo alipangwa kuuawa, lakini baadaye aliokolewa baada ya mmoja wa askari polisi kumtetea, akieleza kuwa alikuwa ametoa ushirikiano mzuri kwa polisi na kuwa na mwenendo wa kiungwana.

Amesema matukio ya aina hiyo yameendelea kutoa taswira mbaya kwa Tanzania, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikitambulika kama nchi yenye amani na utulivu.

Mwaikambo ameitaka Serikali kuchukua hatua za kukomesha matukio ya utekaji, kupotea na kuuawa kwa raia, akisisitiza kuwa tofauti za kisiasa zinapaswa kujibiwa kwa hoja za kisiasa badala ya vitisho na vitendo vinavyoweza kuhatarisha maisha ya watu.

Mahojiano full Tembelea YouTube ya SasaLive

Amesema kuendelea kwa matukio hayo kunaweza kufifisha thamani ya utu, udugu, amani na umoja wa kitaifa, pamoja na kuathiri maendeleo ya nchi.

#SasaLive #ChanceMwaikambo #CHADEMA #HakiZaBinadamu #SiasaTanzania
 
Back
Top Bottom