SHUKRANI ZA CHAMA MKOA WA MARA
Ndugu Viongozi na Wanachama, hususani Mama zangu
BAWACHA
Nawasalimu nyote kwa salaam za Chama.
Leo tarehe 9 Machi, 2026
Mmendelea kuthibitishia Dunia kuwa ninyi ni watafuta mageuzi wa kweli
Vitisho , unafiki , usaliti uliokuwa umetandazwa na mawakala wa shetani miongoni mwetu kusema ya kukatisha tamaa ili msifike na
wengine kuamua kukaa kimya wasionekane sehemu ya lawama yatakapowakuta lakini ninyi mkasema kwa vitendo kuwa MARA TUNAENDA.
kwa mliokamatwa barabarani mama zangu wa Pwani , Kagera , Kilimanjaro, Dodoma, Iringa na Njombe msifadhaike ninyi kwetu ni washindi na tunwapongeza sana kwa utayari wenu.
Kwa mliofika tukawaona nyuso zenu-;
Ruvuma
Manyara
Mbeya
Tabora
Kigoma
Morogoro
Mwanza
Simiyu
Tanga
Arusha
Shinyanga
Kilimanjaro
Tuseme nini juu yenu? neno langu kwenu ni kwamba sisi Mkoa wa MARA kwa niaba ya Baraza la Uongozi
MMETUACHIA DENI hivyo tunayo kazi ya kulipa.
Wapo Wazee wetu ambao mliongozana nao, tunawapongeza na wao kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kila kitu kinaenda sana.
KUHUSU RABSHA
Jeshi la Polisi Tanzania kwasababu za kuwafurahisha watawala walifanya juhudi kuzuia ukumbi na eneo la kukutana Rasmi, Wakatumia kila mbinu kuzuia maombi kanisani.
Walitumia nguvu wakapiga mama zetu mabomu na virungu, Wakaharamisha alama ya
CHADEMA Musoma hata
Kitenge chenu kizuri kikawa chukizo mbele ya macho yao.
Viongozi wetu Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa Mhe. Sharifa Suleiman na Katibu Mkuu wa BAWACHA Taifa Mhe. Pamela Massay wakawa wanted kama waasi mwisho wa siku ni historia mpya ya Mkoa wa MARA 2026 pamoja na majeruhi,
Uharibifu na upotevu wa mali zetu na wengine kumwagiwa Pili Pili makusudi wakiwa mikononi mwa polisi nawambia kwamba
NINYI NI WASHINDI na mmethibitisha hilo kwa vitendo nami ni shuhuda wa ana kwa ana katika hili.
OMBI NA USHAURI
TUKIO HILI LIWE KIELELEZO CHA NINYI KUJUANA KAMA JESHI KUWA MKIAMKA KWENDA VITANI NANI NA NANI NI WAPIGANAJI.
Sisi kama Mkoa wa MARA hatujaazimisha hivyo tutakaa tutajiandaa kwa ajili ya tukio hili na tunategemea mtatufikiria Haki yetu ya kuadhimisha sawa na utaratibu mliojipangia maana tunatamani mrudi tena Mkoani kwetu.
MARA TUKO TAYARI
Mwisho Kitenge chenu cha mwaka huu mkiweke kwenye rekodi sahihi ya kitenge cha kimageuzi,
Kitenge cha MARA,
Kitenge cha reforms,
Wekeni library iwe kumbukumbu lakini pia ziwemo picha za kumbukumbu ya mashujaa wote waliolala Polisi wakiongozwa na Katibu Mkuu wenu Mhe. Pamela Maasasay.
Karibuni tena Mkoani wa Mara kwa wakati mwingine.
Mnaosafiri siku ya leo kurejea majumbani kwenu, nawatakia safari njema.
Mwl. Chacha Heche,
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mara.