CHADEMA Special Thread

2030 CDM wanachukua nchi.


Mark this comment!
Tume'Mark'; lakini kwanza tueleze Samia na Genge lake atakuwa wapi kabla ya wakati huo.!

Haiwezekani kamwe kwa Samia na Genge lake lote waamue tu kukaa pembeni 2030 kuwapisha CHADEMA. Hilo haliwezekani kamwe.

Usalama wao ni kuachaina madaraka miongoni mwao ili kulinda wasiwajibishwe kwa maovu yao..

Ni rahisi tu kusema kama ulivyosema hapo, lakini uhalisia wa kazi iliyopo ili hayo matamanio yako yawezekane ni ngumu sana.

Genge hili liko tayari kuendelea kuua waTanzania ili mradi tu liendelee kuwepo madarakani, kama alivyofanya Samia.
 
Sasa sijui kama hili la mwisho nimelieleza vizuri ili lieleweke.
Lengo ni kuwa CHADEMA haiwezi kudhoofishwa kwa kuwazuia viongozi wake kufanya shughuli za chama..
 
Nimekupata vena mkuu Kalamu jana jeshi letu la police limefanya jambo moja la fedheha kubwa sana duniani.. Kuwazuia BAWACHA kushiriki SIKU YA WANAWAKE DUNIANI huku ikiwakamata wengi wao na kuwabambikia kesi za kuwa walikuwa wanaenda kufanya uhalifu! Just imagine kwamba jeshi letu la police limefikia hatua hii
 
BAWACHA waliofika Musoma kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani baada ya kuachiwa huru kutoka Polisi wamekutana na Viongozi wa Mkoa wa Mara pamoja na Kanda ya Serengeti kwa ajili ya chakula cha pamoja na kutiana moyo wa kuendeleza mapambano.

Cc. Ngoto Lucas Chacha Heche
 
Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Amani Golugwa, amewasili katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu iliyopo Arusha kuhudhuria usomaji wa hukumu ya kesi inayohusu madai ya ukiukwaji wa haki za kiraia na kisiasa katika muktadha wa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2020.

Kesi hiyo ilifunguliwa mwaka 2020 na aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na kiongozi wa upinzani Seif Sharif Hamad, aliyepinga madai ya ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi. Baada ya kifo chake mwaka 2021, Mahakama ilimteua Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, kuendelea na shauri hilo kama muombaji mbadala.

Waombaji wanadai kulikuwa na ukiukwaji wa haki za kisiasa na taratibu za uchaguzi, ikiwemo kuenguliwa kwa wagombea, kusitishwa kwa kampeni za upinzani, vitendo vya vurugu dhidi ya wanasiasa wa upinzani na vikwazo kwa vyombo vya habari na mawasiliano wakati wa uchaguzi.

Uamuzi wa Mahakama katika shauri hili unatarajiwa kutoa tafsiri ya kisheria kuhusu uwajibikaji wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika katika kulinda haki za binadamu na kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa misingi ya haki, uwazi na utawala wa sheria.
 
Waandishi wa habari Philipo Mawazo na Leah Mnyambwa wamekamatwa na Jeshi la Polisi mjini Musoma mkoani Mara wakati wakiripoti taarifa za mkutano uliokuwa umeandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, uliokuwa umepangwa kufanyika leo Jumapili, Machi 8, 2026.

Akizungumza kuhusiana na tukio hilo, Meneja wa Watangazaji wa Kituo cha Jembe FM Mwanza, Albert G. Sengo, amesema amesikitishwa na kukamatwa kwa wanahabari hao wakati wakitekeleza majukumu yao ya kihabari.

G. Sengo amesema waandishi hao walikuwa wakifanya kazi yao halali ya kuhabarisha umma, kama ambavyo askari polisi walivyokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kiusalama, hivyo hakutarajia kuona wanahabari wakikamatwa.

Amesema wanahabari wana mchango mkubwa katika kuelimisha na kuifahamisha jamii kuhusu matukio yanayoendelea, na hivyo ameliomba Jeshi la Polisi kuwaachia mara moja bila masharti.
 
SHUKRANI ZA CHAMA MKOA WA MARA

Ndugu Viongozi na Wanachama, hususani Mama zangu BAWACHA

Nawasalimu nyote kwa salaam za Chama.

Leo tarehe 9 Machi, 2026
Mmendelea kuthibitishia Dunia kuwa ninyi ni watafuta mageuzi wa kweli

Vitisho , unafiki , usaliti uliokuwa umetandazwa na mawakala wa shetani miongoni mwetu kusema ya kukatisha tamaa ili msifike na
wengine kuamua kukaa kimya wasionekane sehemu ya lawama yatakapowakuta lakini ninyi mkasema kwa vitendo kuwa MARA TUNAENDA.

kwa mliokamatwa barabarani mama zangu wa Pwani , Kagera , Kilimanjaro, Dodoma, Iringa na Njombe msifadhaike ninyi kwetu ni washindi na tunwapongeza sana kwa utayari wenu.

Kwa mliofika tukawaona nyuso zenu-;

Ruvuma

Manyara

Mbeya

Tabora

Kigoma

Morogoro

Mwanza

Simiyu

Tanga

Arusha

Shinyanga

Kilimanjaro

Tuseme nini juu yenu? neno langu kwenu ni kwamba sisi Mkoa wa MARA kwa niaba ya Baraza la Uongozi
MMETUACHIA DENI hivyo tunayo kazi ya kulipa.

Wapo Wazee wetu ambao mliongozana nao, tunawapongeza na wao kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kila kitu kinaenda sana.

KUHUSU RABSHA

Jeshi la Polisi Tanzania kwasababu za kuwafurahisha watawala walifanya juhudi kuzuia ukumbi na eneo la kukutana Rasmi, Wakatumia kila mbinu kuzuia maombi kanisani.

Walitumia nguvu wakapiga mama zetu mabomu na virungu, Wakaharamisha alama ya CHADEMA Musoma hata
Kitenge chenu kizuri kikawa chukizo mbele ya macho yao.

Viongozi wetu Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa Mhe. Sharifa Suleiman na Katibu Mkuu wa BAWACHA Taifa Mhe. Pamela Massay wakawa wanted kama waasi mwisho wa siku ni historia mpya ya Mkoa wa MARA 2026 pamoja na majeruhi,
Uharibifu na upotevu wa mali zetu na wengine kumwagiwa Pili Pili makusudi wakiwa mikononi mwa polisi nawambia kwamba
NINYI NI WASHINDI na mmethibitisha hilo kwa vitendo nami ni shuhuda wa ana kwa ana katika hili.

OMBI NA USHAURI

TUKIO HILI LIWE KIELELEZO CHA NINYI KUJUANA KAMA JESHI KUWA MKIAMKA KWENDA VITANI NANI NA NANI NI WAPIGANAJI.

Sisi kama Mkoa wa MARA hatujaazimisha hivyo tutakaa tutajiandaa kwa ajili ya tukio hili na tunategemea mtatufikiria Haki yetu ya kuadhimisha sawa na utaratibu mliojipangia maana tunatamani mrudi tena Mkoani kwetu.

MARA TUKO TAYARI

Mwisho Kitenge chenu cha mwaka huu mkiweke kwenye rekodi sahihi ya kitenge cha kimageuzi,

Kitenge cha MARA,

Kitenge cha reforms,

Wekeni library iwe kumbukumbu lakini pia ziwemo picha za kumbukumbu ya mashujaa wote waliolala Polisi wakiongozwa na Katibu Mkuu wenu Mhe. Pamela Maasasay.

Karibuni tena Mkoani wa Mara kwa wakati mwingine.

Mnaosafiri siku ya leo kurejea majumbani kwenu, nawatakia safari njema.

Mwl. Chacha Heche,
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mara.
 
Pamoja na Serikali ya Idd Amin Mama kutumia nguvu kuzuia BAWACHA tusifanye maadhimisho yetu lakin hajaweza kuzima sauti zetu, tumefanya maadhimisho kwa kushiriki Misa takatifu katika Kanisa Kuu la Roman Catholic Musoma.

Hongereni sana watu wa Musoma na wote mliosafiri kutoka Mikao mbalimbali na kuingia Musoma, leo tumedhihirisha kwamba BAWACHA NI JESHI KUBWA.

Ndo maana Idd Amin Mama na vibaraka wiki nzima, tumewafanya wameacha shughuli zao zote wako busy wanahangaika na BAWACHA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…