Bunda Part 01.
Naomba part 01 tuanzie katika mwendelezo huu.
Anasimama Wakili Aloyce Osewe akimhoji shahidi wa Wasila.
Aloyce; je Ulitumia Utaalamu Upi Kutambua Hiyo Petroli?.
Shahidi; Kwa Kunusa.
Aloyce; Nisahihi Hujasema Gari La Mkuu Wa Wilaya Iliwachukua Wapi?
Shahidi; Kituo Cha Polisi.
Aloyce; Umesema Hapa Mahakamani Kwamba Magari Hayakwepo Ndiyomaana Mlitumia Gari La Mkuu Wa Wilaya
Shahidi; Sijasema.
Anapelekewa Maelezo Yake Ili ayaone na Kusoma.
Kuna Bonge La Tusi Shahidi analisema Hapa Lakini Kwenye Maelezo Yake Hilo Tusi Halipo🤣🤣🤣, anaulizwa kulithibitisha lakini anashindwa kwa sababu Hilo Tusi Kaliongeza Yeye mwenyewe😅
Anakaa wakili Aloyce .Anasimama Wakili Massaba.
Massaba; Nataka nikuonyeshe haya Maelezo ili ujue ni ya kwako ama ni mtu mwingine.
Anaendelea Massaba, Hebu ieleze mahakama namba yako ya polisi iko wapi hapa?
Shahidi; haipo.
Massaba; Anamwambia Hebu Soma Haya Maelezo ya Copy na Haya ya original.
Masaba; Hebu Ieleze Mahakama Ni Lini Uliitwa Kwenda Kuedit Tena?
Shahidi; Sijaitwa .
Massaba; Umesema Wewe Ulikua Kwenye Jengo la nini?
Shahidi; Ccm.
Massaba; Ulikua Unamiliki Simu Gani?
Shahidi; Smartphone
Massaba; Kuna Ushahidi Wowote Kwamba Ulileta Ushahidi Wa Kwamba Jengo Lilikua Zima na Sasa Limechomwa?
Shahidi; Sijasema.
Massaba; George Wilson Mauma Unamfahamu?
Shahidi; George Simfahamu, Namfahamu Mauma.
Massaba; Nikweli Kwamba Wakati Unatoa Ushahidi, Hukusema Wamevaa Nini, Husema Rangi Zao?
Shahidi; Sikusema.
Yaani huyu Shahidi Foustina Kila Kitu anajibu Sifahamu, Sijui, Sikusema. Watu wanacheka sana hapa🤣🤣🤣
Anapelekewa Tena Maelezo Yake ayasome.
Massaba; Umesema Jengo la Ccm Liko Sehemu Gani?
Shahidi: SARANGA
Massaba; Hapa Imeandikwa Wapi?
Shahidi; Bunda Store.
Watu wanaangua kicheko🤣🤣🤣
Faustina anachekesha Kwa kweli mpaka naye inabidi acheke tu😅.
Massaba; Kuna Mahali Umeeleza Kua Taarifa Ulizotoa Ndizo Zilisaidia Washtakiwa Kukamatwa.
Shahidi; Sijasema
Massaba; Kuna Mahali Ulieleza Muonekano Wa Watu Hao Ili Iwe Sehemu Ya Kusaidia Ukamataji?
Shahidi; Sikueleza.
Massaba; Kuna Mahali Umeeleza Namna Watu Hao Walivyochoma Jengo ?
Shahidi; Sijasema.
Massaba; Umesema Aliyewasha Moto ni nani?
Shahidi; Sifahamu.
Massaba; Kuna Mahala Umemtaja Jina Mkuu Wa Wilaya?
Shahidi; Hapana
Massaba; Humfahamu Mkuu Wa Wilaya?
Shahidi; Simfahamu.
Kichekoooo🤣🤣
Massaba; Tunakubaliana na Wewe Kwamba Jiwe Haliwashi Moto?
Shahidi; Nikweli.
Massaba; Nikweli Ulishuhudia Moto Unawaka?
Shahidi; Ndiyo
Massaba; Kuna Mahali Umeeleza Mahakama Kua uliwapigia Zima Moto?
Shahidi; Hakuna .
Anaketi wakili Massaba, Anasimama Wakili Dickson Matata..
Part 02 inakuja post inayofuata.
Naomba nisaidie kushare ili watu wengi zaidi wajue kinachoendelea Bunda.
Usisahau kufollow account ya Shija Shibeshi