CHADEMA Special Thread

CHADEMA Special Thread

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA Taifa (BAVICHA), Deogratius Mahinyila , amesema vijana wa chama hicho hawatakubali kile alichokiita siasa za udalali na usaliti ndani ya chama, akisisitiza umuhimu wa kulinda mshikamano wa wanachama.

Mahinyila ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Nyamongo, ambapo amesema vijana wa CHADEMA wataendelea kusimamia masuala wanayoamini ni muhimu kwa chama na kwa wananchi.

Amesema mwanachama yeyote anayefanya vitendo anavyodai vinaweza kuvuruga mshikamano wa chama, kuwakwamisha viongozi au kuwasaliti Watanzania katika mapambano ya kisiasa hatapata uungwaji mkono kutoka kwa vijana wa CHADEMA.

“Sisi vijana wa CHADEMA kauli yetu ni kwamba yoyote anayefanya siasa za udalali, yoyote anayefanya mambo ya kumsaliti mwenyekiti wetu aliye gerezani bila hatia, yoyote anayewakwamisha, yoyote anayewasaliti Watanzania, yoyote anayewakera Watanzania kwenye mapambano tuliyonayo, sisi vijana wa CHADEMA, hata kama atakuwa na mapembe makubwa kwenye uongozi, tutampita juu,” amesema Mahinyila.

Aidha, Mahinyila amesema vijana wa chama hicho hawatakubali kuona wanachama wakifanya vitendo ambavyo, kwa mtazamo wake, vinaweza kudhoofisha mshikamano wa CHADEMA, akisisitiza kuwa hata viongozi waliowahi kushika nafasi ndani ya chama wanaweza kukataliwa iwapo wataenda kinyume na msimamo huo.

Amesisitiza kuwa tofauti za kisiasa ndani ya chama zinapaswa kushughulikiwa kwa namna inayolinda umoja na mshikamano wa CHADEMA.
1791515372949.jpg
 
Back
Top Bottom