CHADEMA Special Thread

CHADEMA Special Thread

Leo, Septemba 27, 2026, CHADEMA imefanya warsha iliyowakutanisha viongozi wa Chama ngazi ya Taifa na viongozi wa Kanda. Warsha hiyo imefanyika katika Makao Makuu ya Chama, Edwin Mtei House, Mikocheni, Dar es Salaam.
1790526194648.jpg
1790526185311.jpg
1790526191397.jpg
1790526188379.jpg
1790526181787.jpg
1790526178743.jpg
1790526175611.jpg
1790526171785.jpg
 
Picha mbalimbali zikionesha matukio katika maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyoandaliwa na Baraza la Wazee Chadema (BAZECHA), leo Oktoba 1, 2026, wilayani Tarime, mkoani Mara. Mgeni rasmi akiwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Mhe. John Heche.
1790888249987.jpg
1790888246792.jpg
1790888243566.jpg
 
Bunge la Ulaya pamoja na vyombo vya juu vya kidiplomasia barani humo vimefikishiwa taarifa rasmi inayoeleza kuwepo kwa mkwamo wa kisiasa na uminywaji wa demokrasia nchini Tanzania.

Hatua hiyo imejiri kufuatia kukamilika kwa ziara ya siku tatu jijini Brussels, Ubelgiji, iliyofanywa na Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje wa CHADEMA, Deogratias Munishi, kwa lengo la kuimarisha diplomasia ya chama hicho na wadau wa kimataifa.

Katika taarifa rasmi iliyotolewa leo Oktoba 1, 2026, na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, Munishi amefanya mfululizo wa mikutano na viongozi wa taasisi mbalimbali za maamuzi ndani ya Umoja wa Ulaya (EU).

Miongoni mwa vyombo vilivyofikiwa ni pamoja na Chombo cha Utekelezaji wa Ushirikiano wa Kimataifa (EEAS), Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Ulaya, Idara ya Haki za Binadamu ya EU, pamoja na wataalamu wa ulinzi na uchumi kutoka chama cha European People’s Party (EPP).

Taarifa hiyo imebainisha kuwa CHADEMA imetumia jukwaa hilo la kimataifa kushinikiza uwajibikaji wa kiutawala na kulinda misingi ya haki za binadamu na demokrasia nchini.

#SasaLive #CHADEMA #DeogratiasMunishi #Brussels #Ubelgiji UmojaWaUlaya EU SiasaZaTanzania HakiZaBinadamu SasaLiveUpdates
1790913912062.jpg
 
#BahariaMEMORY Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA Bara Aman Golugwa, ametangaza kuwa chama hicho kimeandika barua kwenda kwa Mabalozi wa Nchi za Nje, Umoja wa Mataifa (UN) pamoja na Jumuiya ya Madola (Commonwealth) kulalamikia kauli iliyotolewa na Katibu wa Oganaizesheni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Chacha, aliyedai kuwa najeshi ya ulinzi na usalama ni mali ya chama tawala.

Akitangaza hatua hiyo leo Oktoba 3, 2026, katika mkutano wa hadhara uliofanyika mkoani Mara wilayani Bunda, Golugwa amebainisha kuwa wametekeleza aqizo la Makamu Mwenyekiti wa chama hicho ili kuifahamisha dunia jinsi kauli hizo zinavvoivunjia heshima vyombo vya dola vilivyoundwa kuhudumia Watanzania wote bila ubaguzi wa kisiasa.

Aidha, Golugwa amerejea historia ya kuundwa kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Septemba 1, 1964, akimnukuu Muasisi wa Taifa, Mwalimu Julius Nverere, aliyesisitiza kuwa jeshi hilo inatakiwa kuwa la kizalendo na lenye utii wa moja kwa moja kwa wananchi na si kwa kikundi au chama fulani cha siasa.

Mbali na hayo, kiongozi huyo amewataka Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini. akiwemo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF Jacob Johr mkunda na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP)Camillus Wambura, kujitokeza na kukanusha kwa umma kauli hiyo badala ya kukaa kimya na kusubiri shinikizo kutoka kwa wananchi au jumuiya za kimataifa.
1791065442192.jpg
 
Wapiganaji salamu!

Kesi ya Katibu wa Kanda ya Serengeti Mhe. Jackson Mnyawami na Wenzake 16 itaendelea tarehe 7/10/2026 Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Shinyanga.

Anza kuweka ratiba Mapema ili siku hii usikosekane.

Njooni tuonyeshe umoja kwa Makamanda wetu hawa ambao wamepewa kesi ya Uogo ya UGAIDI.

#FreeTunduLissu#FreeMnyawamiand16Others.
1791065636479.jpg
 
Back
Top Bottom