CHADEMA Special Thread

CHADEMA Special Thread

IMG-20260717-WA0040.jpg
 
VIJANA HAWA WAMETEKWA NA POLISI WA KITUO CHA TEMEKE CHANG'OMBE DAR.

Polisi waliomteka Deudedith Soka na wenzake Mwaka 2024 wamehusika na tukio la kuwateka Vijana hawa pichani Mkoa wa Temeke Kata ya Chamanzi, siku zaidi ya 6 hawajulikani walipo, mmoja alitekwa nyumbani kwake akiwa na mke wake POLISI hao waliovalia Maski usoni walimwambia mke wa Zacky Shija akimwambia MTU yoyote kama mume wake ametekwa watamuua.

Majina ya Vijana hawa ni

1 piter seleka
2 kenda
3 Zacky Shija
1784476515146.jpg
 
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) Taifa, Wakili Deogratias Mahinyila, amesema hakuna msingi wa kumtaka Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, akae pembeni kwa madai ya kupisha uchunguzi, akieleza kuwa hana mamlaka ya kuzuia uchunguzi wowote ndani ya chama.

Akizungumza katika mahojiano na Jambo TV jijini Dar es Salaam, Jumatano Julai 22, 2026, Mahinyila alisema taratibu za ukusanyaji wa michango ndani ya CHADEMA ziko wazi na hazisimamiwi na ofisi ya Makamu Mwenyekiti.

"Leo tunaona watu wanaandamana wanasema Heche apishe uchunguzi. Heche ni nani kwenye chama? Heche ndiye anayepokea michango kwenye chama? Ofisi ya Makamu Mwenyekiti wa chama inazuia vipi uchunguzi wowote kufanyika ndani ya chama mpaka umwambie akae pembeni?" alihoji Mahinyila.

Aliongeza kuwa mifumo ya usimamizi wa fedha na michango ndani ya chama imeainishwa katika taratibu za chama, hivyo hakuna sababu ya kuhusisha ofisi ya Makamu Mwenyekiti na kuzuiwa kwa uchunguzi wowote.

"Taratibu za kukusanya michango kwenye chama ziko wazi. Makamu Mwenyekiti hakuna mahali kokote atazuia uchunguzi wa aina yoyote," alisema.

Kauli ya Mahinyila inakuja wakati kukiwa na mijadala mbalimbali kuhusu masuala ya uongozi na uwajibikaji ndani ya CHADEMA, huku baadhi ya wananchi na wanachama wakitoa maoni tofauti kupitia majukwaa mbalimbali.
 
Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, imetangaza kufuta rasmi uamuzi wa kumsimamisha kazi Katibu wa chama hicho Mkoa wa Morogoro, Barnabas Okola, na kuagiza arejee kwenye majukumu yake mara moja.

Uamuzi huo umetolewa kupitia barua rasmi iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa CHADEMA, Gaston Shundo, kwa niaba ya Katibu Mkuu, baada ya kupitia rufaa iliyowasilishwa na Okola kupinga hatua iliyochukuliwa dhidi yake na uongozi wa CHADEMA Kanda ya Kati.

Kwa mujibu wa barua hiyo, Ofisi ya Katibu Mkuu ilipokea barua ya rufaa ya Okola ya Julai 15, 2026, na kumpa nafasi mlalamikiwa—ambaye ni Katibu wa Kanda ya Kati—kuwasilisha maelezo yake ya kujitetee, ambapo aliwasilisha maelezo hayo Julai 19, 2026.

Baada ya kupitia maelezo ya pande zote mbili, Ofisi ya Katibu Mkuu ilijiridhisha kuwa Okola hakupewa haki ya msingi ya kusikilizwa kabla ya kuchukuliwa kwa hatua ya kusimamishwa uongozi, jambo linalokiuka misingi ya haki.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uamuzi wa Kanda ya Kati wa tarehe 9 Julai, 2026 umefutwa rasmi, na kueleza kuwa kama Kanda bado ina malalamiko dhidi ya Okola, inapaswa kufuata utaratibu wa kikatiba unaoelekezwa katika kanuni ya 6.5.5 ikisomwa pamoja na kanuni ya 6.5.6 za Chama hicho.

Itakumbukwa kuwa Julai 9, 2026, Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kati, Ashura Mashaka Masoud, alimsimamisha kazi Okola kwa tuhuma za kukiuka kanuni za maadili ya viongozi baada ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kutoa shutuma za ubadhirifu wa fedha dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho (Bara), John Heche.

#SasaLive #CHADEMA #JohnMnyika #BarnabasOkola #SiasaTanzania
1785052240184.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom