CHADEMA Special Thread

CHADEMA Special Thread

TAARIFA YA MCHANGO WA KIKAO CHA BARAZA KUU LA CHADEMA

Hadi sasa, tumepokea jumla ya Shilingi 7,300,000 za michango kwa ajili ya kuwezesha kufanyika kwa Kikao cha Baraza Kuu la CHADEMA kitakachofanyika tarehe 15 Septemba 2026.

Jumla ya gharama zinazohitajika kwa ajili ya maandalizi na uendeshaji wa kikao hicho ni Shilingi 334,000,000. Tunawaalika wanachama, wapenzi, marafiki na wadau wote wa CHADEMA kuendelea kutoa michango yao ili kufanikisha shughuli hii muhimu.

CHANGIA SASA

M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ

NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
1783838481716.jpg
 
HAWA ni wanachama wetu wa CHADEMA wapo kituo Cha polisi Kahama, wameshikiliwa tangu tarehe 6.7.2026 wanatuhumiwa kwa kuhamasisha MAANDAMANO ya 7/7
1783935978583.jpg
 
Wakati huo wa CHADEMA ya enzi ya operesheni sangara wewe ulikuwa na wadhifa gani CHADEMA?.
ANAANDIKA ALOYCE NYANDA

Ukweli lazima usemwe kwa sasa huenda John Heche ni moja ya wanasiasa aliefanikiwa na highest level ya Human Capital, anasikilizwa na anaaminika kwa kundi la umma

We fikiria mtu ametuhumiwa kula hela, lakini hajawahi kujibu. Kwenye video yake ya kwanza hadharani anaomba mchango wa milioni 300, na watu wanamchangia.

Mpaka jana wamefikisha milioni 15. Hilo ni jambo ambalo linahitaji kufanyiwa analysis nzuri. Attack haipaswi kuelekezwa kwa chama au mtu, bali kuvunja imani ambayo imejengwa.

Binafsi nasema Chadema kimehama kutoka kuwa chama cha siasa na kuanza kuwa chama cha kiimani.
Wakina Heche wamejikita kufanya politics of development na social politics, Wameacha kabisa kufanya party politics, jambo ambalo linafanya vyama vingine viendelee kufanya siasa za hamasa zenye propaganda.

Wamefanikiwa kuwa na The Highest level ya human capital na mtaji wa watu hupatikana pale watu wanapokuona ni wako na wako salama, mali zao ziko salama wakikuona, wanakuona mwenzao ni mtu wao hata ukiambiwa umekula hela wanasema kula tu tumekupa sisi.

Mimi kama mtu wa kufanya uchambuzi niseme mzani kati Chadema na Wananchi umelalia upande mmoja atakaebisha aje tufanye uchambuzi.
Mtozi less

CHANGIA SASA

M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ

NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
 
Asanteni kwa mwitikio wenu mkubwa na moyo wa kujitolea. Kwa ushiriki wenu, mpaka sasa tumefanikiwa kukusanya TSh. Milioni 34.8, sawa na asilimia 10 ya lengo letu la TSh. Milioni 334 kwa ajili ya kufanikisha Baraza Kuu la Umma.

Hii ni hatua kubwa inayodhihirisha kwamba tukisimama pamoja, hakuna lengo lisilowezekana. Kila mchango una thamani, na kila anayechangia anakuwa sehemu ya historia ya kujenga CHADEMA imara.

Safari bado inaendelea. Tunawaalika wanachama, wapenzi na Watanzania wote kuendelea kuchangia na kuwahamasisha wengine kushiriki ili kwa pamoja tufikie lengo la TSh. Milioni 334. :H
1784052631361.jpg
ECHE
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemsimamisha kufanya shughuli yoyote ya chama aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Rombo, Joseph Roman Selasin, huku kikimpa siku 14 kujieleza kwa maandishi kwa nini asichukuliwe hatua kali zaidi za kinidhamu kufuatia tuhuma za ukiukaji wa maadili.

Hatua hiyo imekuja kufuatia kikao cha dharura cha CHADEMA Kata ya Makiidi kilichoketi jana Julai 14, 2026, ambapo kilijadili mwenendo wa mwanasiasa huyo anayetuhumiwa kutumia vyombo vya habari kutoa shutuma na matamko dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa (Bara), Tundu Lissu, badala ya kutumia mifumo rasmi ya chama.

Kupitia barua rasmi iliyotolewa leo Julai 15, 2026, uongozi wa chama hicho umebainisha kuwa Selasin, ambaye ni mwanachama mwenye kadi namba CDM 496369, anazuiwa kujihusisha na shughuli zote za uongozi na utendaji kuanzia sasa:

"Kuanzia tarehe ya kupokea barua hii, huruhusiwi kushiriki kuongoza wala kutekeleza shughuli zozote za Chama hadi utakapokamilisha utaratibu wa kujieleza na shauri lako litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi kwa mujibu wa katiba na kanuni za Chama."

Barua hiyo imefafanua kuwa kitendo cha kutoa shutuma hadharani dhidi ya viongozi wakuu wa chama ni ukiukaji wa wazi wa Ibara ya 10.1(iv) na 10.1(v) ya Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006 (Toleo la 2019). Selasin sasa ana hadi mwishoni mwa mwezi huu kuwasilisha utetezi wake wa maandishi chini ya Ibara ya 63.6(c) ili kuepuka rungu la kufukuzwa uanachama.

#JosephSelasin #CHADEMA #TunduLissu #Rombo #Kilimanjaro SiasaZaTanzania SasaLive
1784132382267.jpg
 
ANAANDIKA GODBLESS LEMA

Kwa wafuasi wote wa CHADEMA na mageuzi, wapenda haki, ukweli na demokrasia nchini.

Baada ya Katibu Mkuu wetu, John Mnyika, kutangaza maazimio ya Chama chetu, ikiwa ni pamoja na kikao cha Baraza Kuu kinachotarajiwa kufanyika siku sio nyingi , vilevile alizindua mpango maalumu wa uchangiaji wa fedha kupitia Tone Tone.

Kwa siku kadhaa sasa, kampeni hii imeendelea kwa nguvu kubwa mitandaoni, ikibebwa na viongozi wetu, wanachama, wananchi pamoja na wana harakati mbalimbali. Nawashukuru kwa dhati kabisa wote mlioamua kubeba jukumu hili; kuanzia anayehamasisha michango hadi anayetoa mchango wake. Kila mmoja wenu ni sehemu ya historia inayoandikwa.

Hata hivyo, pamoja na shukrani hizi, kuna ukweli ambao hatupaswi kuogopa kuusema. Wakati mwingine ukweli huwa ni sehemu muhimu ya kujitathmini kama taasisi na kama watu wenye maono ya pamoja.

CHADEMA ni Chama chenye wafuasi wengi kuliko Chama chochote cha siasa nchini. Wakati wa operesheni ya CHADEMA ni Msingi tulikuwa na kanzidata ya wanachama zaidi ya milioni saba. Kwa tafiti na tathmini zetu za sasa, si jambo la kupindukia kusema kuwa wapenzi wa demokrasia, haki na mabadiliko nchini wanafikia au hata kuzidi asilimia 65 ya Watanzania wazima. Kama tunakubaliana na ukweli huo, basi ni lazima tukubaliane pia na wajibu unaoambatana nao.

CHADEMA haipaswi kuwa na upungufu wa fedha za kuendesha shughuli zake. Kama watu milioni moja tu wataamua kuchanga shilingi 1,000 kila mwezi, Chama chetu kitakuwa kinapata zaidi ya shilingi bilioni moja kila mwezi. Katika kampeni hii ya kuhakikisha kikao cha Baraza Kuu kinafanyika, watu laki tano pekee wakichanga shilingi 2,000 kila mmoja, tayari watakuwa wamechangia takribani shilingi bilioni moja kwa Chama chao.

Hii ina maana kuwa changamoto yetu siyo idadi ya watu, bali ni kiwango cha dhamira yetu (commitment) katika kuwekeza kwenye kile tunachokiamini. Ni lazima tujifunze kwamba mapambano ya demokrasia yana gharama zake. Haki ina gharama yake. Mageuzi yana gharama yake. Hakuna taasisi inayoweza kuwa huru kama utegemezi wake unatoka mahali pengine isipokuwa kwa watu wake wenyewe. Vyama vikubwa vya siasa duniani vimejengwa kwa michango midogo lakini ya kudumu kutoka kwa wananchi wanaoviamini. Nasi tunapaswa kujenga utamaduni huo.

Tusifanye uchangiaji kuwa jambo la misimu au la kusubiri vikao maalumu. Uchaguzi wa mwaka 2025 ulipita na Chama chetu hakikushiriki. Hivyo, hatuna ruzuku tunayoitegemea. Tunachokitegemea ni imani, mshikamano na mchango wa wananchi wenyewe. Huo ndio mtaji mkubwa wa CHADEMA.

Ni jambo lisilo na mantiki kusema tuna mamilioni ya wafuasi huku tukishindwa kukusanya fedha za kuendesha shughuli zetu za msingi. Tukitaka kuwa Chama kikubwa, imara na huru, ni lazima tukubali kubeba gharama za ukubwa huo. Tusitarajie wachache wabebe jukumu ambalo mamilioni yetu yanaweza kulifanya kwa wepesi kabisa.

Ni rai yangu kwa kila mwanachama, mfuasi na mpenda mageuzi popote alipo, afanye jukumu hili kuwa sehemu ya maisha yake ya kisiasa. Elfu moja yako inaweza kuonekana ni ndogo, lakini inapoungana na elfu moja za wengine, hujenga taasisi kubwa. Michango yetu midogo ndiyo itakayolinda uhuru wa maamuzi yetu na uimara wa Chama chetu.

Tusichangie kwa sababu tunaombwa kuchangia. Tuchangie kwa sababu tunaamini katika Tanzania yenye haki, demokrasia na utawala wa sheria. Tuchangie kwa sababu tunaamini kuwa mageuzi tunayoyatamani hayawezi kujengwa kwa maneno pekee, bali kwa kujitoa kwetu kwa vitendo.

Your small donation can make a very big change.

Nawashukuru sana kwa upendo wenu, mshikamano wenu na imani yenu katika mapambano haya. Historia ya mageuzi huandikwa na watu wanaoamua kufanya zaidi ya kushangilia. Naamini tutafanya zaidi ya tuliyoyafanya jana.

Mungu akubariki , asanteni kwa wale wote mliochanga na mnaoendelea kuchanga na ni wito wangu kwa kila mtu kujali kwa vitendo jukumu hili muhimu , tena sio mara moja bali kila wakati.

NAMBA ZA KUCHANGIA

M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ

NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
1784177472327.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom