CHADEMA Special Thread

CHADEMA Special Thread

UTEKAJI UNAUMIZA WANANCHI.

Rhoda Kunchela Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Katavi amewatembelea wazazi wa Juma Kaswahili ambaye ameripotiwa kupotea katika mazingira yasiyojulikana tangu Mei 18, 2025 huku familia yake ikiendelea kuiomba Serikali kusaidia kupatikana kwake.

Akizungumza baada ya kutembelewa na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baba mzazi wa Juma Kaswahili, Gerevasi Makwani amesema familia imekuwa katika majonzi makubwa tangu kutoweka kwa kijana huyo.

“Mimi ni mzazi wa Juma Kaswahili, kijana aliyepotea katika mazingira yasiyojulikana. Tarehe 18 Mei 2025 kijana wangu alipotea mpaka leo hajulikani alipo. Nimehangaika mitandaoni na vituoni lakini hapatikani mpaka leo,” amesema Makwani.

Amesema kutoweka kwa mwanawe kumeiathiri familia kiuchumi na kijamii kwa kuwa alikuwa msaada mkubwa kwa wazazi wake na familia kwa ujumla.

“Naiomba Serikali kusaidia, huyo kijana alikuwa ni msaada wetu kwa sababu tumemsomesha ili aisaidie familia lakini mpaka sasa tuna majonzi makubwa sana. Kiuchumi tumeteteleka, kwa msaada na maneno alikuwa anatusaidia sana yule kijana,” amesema.

Aidha, amewashukuru viongozi wa CHADEMA pamoja na wanachama wa chama hicho kwa namna wanavyofuatilia suala hilo.

“Tunawashukuru viongozi wa chama chetu cha CHADEMA kama John Heche na wanachama wengine kwa namna ambavyo wanalishughulikia sana jambo hili,” ameongeza.

Kwa upande wake, mama mzazi wa Juma Kaswahili, Teleza Rukasi amesema bado ana maumivu makubwa kutokana na kutofahamu alipo mwanawe wala hali yake.

“Hili linanisikitisha sana mwanangu kupotea hivi hivi sijui alipo, sijui amekufa au yupo hai. Naiomba Serikali ilifanyie kazi kabisa hili jambo ili mwanangu arudi, alikuwa ananisaidia,” amesema kwa huzuni.

Mpaka sasa, hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu mahali alipo Juma Kaswahili huku familia na viongozi wa CHADEMA wakiendelea kuitaka Serikali na vyombo vya usalama kuongeza juhudi za kumtafuta.
 
"Nyie polisi ndugu zetu, mmehusika kwenye mauaji yetu Oktoba 29 na hiyo ni bila kuficha. Saa hizi sisi (CHADEMA) na wananchi tumetulia, lakini mtajiunga na CCM dhidi yetu ama muwe upande wa wananchi tupambane. Mkichagua kuwa upande wa moto, sisi hatutawabembeleza, hatuogopi na tutawapelekea moto," amesisitiza Mnonela.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mwenyekiti wa Kanda ya Kusini, Bele Mnonela, ameweka


View: https://www.facebook.com/share/v/18TBA9otPP/
 
Geita Mjini imeitika.

#KatibaMpya
#FreeLissu
1779090238712.jpg
1779090236179.jpg
 
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, @hechejohn , ameikosoa vikali kauli ya Mwenyekiti wa UWT Taifa, @marypiuschatanda , akidai kuwa viongozi wa CCM wameanza kutoa kauli za vitisho dhidi ya wapinzani kutokana na hofu ya mikutano ya kisiasa inayoendelea nchin

Heche amesema kauli ya Chatanda iliyodokeza kuwa angepewa mamlaka asingewaacha wapinzani “wawepo”, ni ishara ya siasa za hofu na ukandamizaji badala ya kujibu hoja za kisiasa kwa njia ya kidemokrasia.

“Huu ni mkutano wa tatu tu tayari wamepanick vibaya. Chama hakiwezi kujibu hoja kinataka wapinzani wake wauwawe, watekwe au wapotezwe,” amesema Heche.

Pia amerejea matukio ya vurugu na watu waliopotea baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, akiwataja baadhi ya watu waliowahi kuripotiwa kutoweka huku akihoji hatma yao.

Kauli hiyo imeendelea kuchochea mjadala mkubwa mitandaoni kuhusu uhuru wa kisiasa, haki za binadamu na matumizi ya lugha kali kwenye siasa za Tanzania.
1779292032209.jpg
 
🚨TAARIFA MBAYA🚨
Usiku huu watu wenye silaha ambao hawajajitambulisha wamemkamata David Jumbe (kushoto) ambaye ni Msaidizi wa Tundu Lissu nyumbani kwake Mabwepande Bunju, jijini DSM. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mke wake, Jumbe alikuwa anarudi nyumbani na alipofika getini alifuatwa na watu hao, wakamkamata na kumwingiza kwenye gari aina ya Land Cruiser kisha kuondoka kwa mwendo mkali. Jumbe alipiga kelele na kujaribu kujitetea lakini watu hao wakamzidi nguvu. Majirani walipofika walijaribu kuikimbiza gari hiyo bila mafanikio. Wameishia kuambulia kiatu ambacho Jumbe alikidondosha katika purukushani.
Je, huyu Chitanda aliyesema angepewa urais dakika moja, angemaliza wanachadema, ndiyo anamalizia?
1779337814796.jpg
 
Back
Top Bottom