CHADEMA sasa yawaadhibu wananchi: NAPE

CHADEMA sasa yawaadhibu wananchi: NAPE

Mafisadi CCM lazima wavue gamba

Kutoka Gazeti la Habarileo

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, amesema yeye ni sawa na mtu aliyeteuliwa kufanya kazi ya kunyonga mkosaji aliyehukumiwa adhabu hiyo na Mahakama, hivyo hawezi kuogopa kutekeleza hukumu hiyo.

Akifafanua kauli hiyo jana mjini Morogro, Mukama alisema uamuzi wa ngazi za juu wa CCM ukishatolewa kuhusu kuvua gamba watuhumiwa wa ufisadi, hakuna kiongozi atakayepuuza kuutekeleza.

“Ufisadi unasemwa dhahiri na wananchi kwa kuwataja watuhumiwa hadharani wakiwahusisha ana EPA (Akaunti ya Malipo ya Nje ya Benki Kuu), Dowans, ununuzi wa rada na Richmond … na vikao vya chama vimetoa uamuzi.

“Kilichobaki ni utekelezaji tu…na hukumu ikishatolewa na Mahakama hakuna njia nyingine isipokuwa kutekeleza agizo hilo,” alisema Katibu Mkuu huyo alipokuwa akizungumzia madai, kwamba anaogopa kutoa barua za kujivua gamba kwa watuhumiwa wa ufisadi.

Akihutubia mahafali ya wanafunzi wanachama wa CCM wanaomaliza Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro, Mukama alisema hataogopa kusimamia kikamilifu uamuzi wa chama hicho wa kuwatosa watuhumiwa hao.

Alisema vitendo vyao vimesababisha CCM na Serikali ichafuke mbele ya Watanzania.

Mbali na kuwavua gamba, Mukama alisema CCM pia itashughulikia suala la wafanyabiashara wasio waadilifu wanaojipenyeza ndani ya chama hicho, na itapambana na saratani ya kujilimbikizia madaraka na kukiondoa chama hicho katika utegemezi wa matajiri na wahisani wanaokiweka pabaya.

Alisema, hakuna mwananchi asiyejua kuwa ndani ya CCM wapo viongozi wenye nyadhifa kubwa wanaotuhumiwa kwa ufisadi kuanzia wa EPA, Richmond, Dowans, Rada na kashfa nyingine.

Katibu Mkuu huyo alisisitiza kwamba ili kukisafisha chama hicho mbele ya jamii na kukifanya kikubalike katika uchaguzi wowote, ni lazima watuhumiwa hao watoswe ili kurudisha imani kwa Watanzania.

Mukama alionesha katuni aliyodai imemchora hivi karibuni, akiwa na barua mkononi ikionesha kuwa ameshindwa kutoa uamuzi na kusisitiza kuwa uamuzi huo ni wa chama, hivyo utatekelezwa kama ilivyopangwa.

Awali katika risala ya wanafunzi hao, walitaka viongozi wote wa CCM kujikita kuwaletea maendeleo wananchi, ili baadaye wapimwe kwa kazi zao.

Wanachama hao waliwataka viongozi wahubiri amani badala ya kuendeleza malumbano na vyama vya upinzani na kuwataka watumishi wa Serikali kuachana na siasa wakati wakiwa watumishi wa umma.​


Ni juzi tu uchaguzi wa Igunga watu walikuwa wanampigia magoti Rostam ili CCM isishindwe leo hii tayari wameshinda wameaanza kukemea ufisadi? Ni dhahiri huo ni uongo uliopea mipaka. Tunasubiri kikao kijacho cha NEC tuone maamuzi magumu.
 
Chadema msilalamike, jamaa wanasaidia kukitangaza chama chenu ili kisambae nchini kirahisi bila kujua. Wanadhani wananchi ni wajinga!
 
unaweza kumtambua mtu kwa aina nyingi sana na mojawapo ni ni maneno anayoongea;
hili la nepi linaonyesha zaili anauwezo mdogo wa kufikili, na hata kama ni mapenzi kwa chama chake basi yanachangai kumdharaulisha
nadhani sio kila kitu anapaswa kuongea vingine awe anavichunia pia ilibidi awe na mshauri wake wa mambo ya siasa nadhani hana kama anaye aidha mshauri wake naye akili zake kama za nepi au nepi afuati ushauri
 
Namuweka Nape ktk orodha ya vijana wachumia tumbo ambao wanawasaliti vijana wenzao kwa kutetea wanaowatesa vijana wanaojaribu kujiajili baada ya serikali ya CCM kushindwa kuwapa ajira.
 
JF members

Nimeisikia hii habari via TBC[SUB]1[/SUB] magezeti asubuhi hii kuwa Nape anasema baada ya CHADEMA kushindwa kwenye uchaguzi ulio pita sasa kimeamua kuuwaadhibu wananchi kwa kupitia vurugu zinazoendelea nchini

My take:
Naomba sana tuwe wakweli Mfano hizi vurugu zilizo fanyika MBY kwa masaa zaidi ya 30 mfululizo chanzo chake nini ?

Ukweli ni kwamba watu hasa machinga walichoka kunyanyaswa na migambo wa jiji ambao walikuwa wakiwafukuza ktk maeneo yao ya kazi na kuwafukuzia ambako hata wao ( migambo) hawakujui

Pili migambo kumwaga michele, mbogamboga, matunda ya akina mama ambayo wanauza kando ya barabara

Tatu wenye maduka kuwazuia kabisa kutoa bidhaa yeyote ya dukani nje kama sample othewise wanachukua hiyoo bidhaa eg nguo

Nne huu ni mwezi wa mavuno kwa machinga kwani tunaelekea kwenye sikukuu

NAOMBA SANA TUWE WAKWELI SI KILA JAMBO NI SIASA MENGINE NI MASUALA YA KAWAIDA SANA AMBAYO VIONGOZI WA JIJI WALISHINDWA KUYA WEKA SAWA MAPEMA

Ujue huyu nepi anakurupuka ktk kuongea kwakd akidhani ndo watu watakikubali chama chake ccm kumbe ndo anazidi kukipalia mkaa mfano hii ya kujivua gamba alifikiri ndo watakubalika kumbe ndo kinazidi kuzorotesha chama kwani ata wale aliowataja wavue gamba wamegoma na hajaweza kuwafanya kitu chochote
 
kama ndo hivyo basi alitakiwa kusema kuwa cdm inaiadhibu serikali kupitia vurugu na si cdm kuwaadhibu wananchi.au anafikiri serikali haipati shida kwa vurugu hizi? btw hapo ameongea utumbo.

Au angesema cdm kinaiadhibu serikali na waziri mkuu kwa kuwanyima usingizi
 
Nape has become IRELLEVANT tangu ile siku alipoitaka chadema itoe msimamo kuhusu swala la mashoga kwenye lile azimio la waziri mkuu cameron alipozitaka serikali za nchi za kiafrika kuheshimu haki za mashoga naye nape the next kwa domo lake kaya eti akataka chadema itoe msimamo kuhusu azimio la cameron huku akijua wazi kuwa chadema haina serikali. JK anachagua viongozi dhaifu km akina Nape ili kuficha udhaifu wake.

ujue kufanya mambo kwa kukurupuka ndn hali kama hiyo inajitokeza
 
Jamaa anasema ukweli, CDM wanafikiri siasa za fujo ndio zitawaendeleza. Hii serikali inawaendekeza sana. Wao wanahamasiha fujo halafu mambo yakicharuka wanatia mbio huku wakiwaacha wanachama wao wale bakora. Mfano mzuri ni yalio tokea Arusha. Viongozi wao walipotea ghafla wakati bakora zikitembezwa. Mmoja karuka ukuta na mwingine kajificha kama panya kwenye sanduku.

'Mmoja karuka ukuta na mwingine kajificha kama panya kwenye sanduku'.Teh teh teh jaman mbavu sina mwenzenu.
 
Jamaa anasema ukweli, CDM wanafikiri siasa za fujo ndio zitawaendeleza. Hii serikali inawaendekeza sana. Wao wanahamasiha fujo halafu mambo yakicharuka wanatia mbio huku wakiwaacha wanachama wao wale bakora. Mfano mzuri ni yalio tokea Arusha. Viongozi wao walipotea ghafla wakati bakora zikitembezwa. Mmoja karuka ukuta na mwingine kajificha kama panya kwenye sanduku.

You must be sick au una kichaa au mimba changa hii si kawaida kuongea kama umekali kitu chenye ncha kali kwa nyuma .
 


NAOMBA SANA TUWE WAKWELI SI KILA JAMBO NI SIASA MENGINE NI MASUALA YA KAWAIDA SANA AMBAYO VIONGOZI WA JIJI WALISHINDWA KUYA WEKA SAWA MAPEMA
Awali ya yote, Halmashauri ya Jiji hilo lina wadiwani wangapi toka Chadema?
 
Kama wale waliofanya vurugu za Mbeya sio wananchi basi Nape a.k.a Nepi atueleze wananchi ni akina nani? Nijiavyo mimi Polisi wa CCM ndio waliwaadhibu wananchi kwa kuwapiga mabomu na bakora. Huyu jamaa kilaza sana, ashukuru kuwa aliyemuweka naye ni kilaza hivyo hawezi kuona ukilaza wa mwenzie
 
Nasikia huyu jamaa ni graduate, sasa inamaana elimu aliyosoma haikumkomboa, duh aise huyu anamatizo inshort jamaa ni mweupe kichwani
 
Tatzo la huyu Mmakonde ana mtindio wa KIFIKRA,ameshindwa kuelewa tatzo lililotokea Mbeya limegusa maisha ya wakazi wa mji ule,Nadhani kama Prof.Mwandosya angelikuwepo akaenda kuongea na watu wana Mbeya wangemsikiliza on behalf of SUGU kwani yeye ni mtu wa kujishusha sana kwa Wananchi kwahiyo na hapo tungesema chanzo ni CCM?Mara ngapi JK amezomewa Mbeya lakn akaokolewa na Mwandosya?Na hapo Nape ameshndwa kutambua kuwa tatzo ni wao CCM na badala yake atupia mpira kwa CDM.Serikali ya CCM endapo itaendeleza utawala wa KIIMLA itambue fika kuna watoto wadogo hawajafikisha umri wa kupiga KURA na hao 2015 kwa hasira wataiadhibu CCM,kama vile watoto wa shule moja ya secondary walotendwa vibaya na polisi kwa kupigwa na kuwekwa lumande.NAPE OPEN YOUR EYES,leo Wazanzibar wanataka kujitenga na MUUNGANO but kuna siku SOUTHERN HIGHLAND watataka kujitenga.

jamani tusiweke ukabila, mbona tulikuwa na Rais jasiri na shupavu 'MKAPA'
 
Jamaa anasema ukweli, CDM wanafikiri siasa za fujo ndio zitawaendeleza. Hii serikali inawaendekeza sana. Wao wanahamasiha fujo halafu mambo yakicharuka wanatia mbio huku wakiwaacha wanachama wao wale bakora. Mfano mzuri ni yalio tokea Arusha. Viongozi wao walipotea ghafla wakati bakora zikitembezwa. Mmoja karuka ukuta na mwingine kajificha kama panya kwenye sanduku.

Mtabwajaja sana awamu hıı CDM ımewashıka pabaya, hata mkıtubeza vıpı yote sawa make tunajua sıku zote hızı CCM hamna huruma yoyote na Wananchı but Revolutıonal day ıs knockıng the door, very soon kıtaeleweka.
 
Kwanza katoroka mirembe...Mi nashanga hoja za HUYU MCAMEROONIWA NAPE tunahangaika kuzijadili hapa.Kwaherini siwezi kuumiza finger tips zangu na button za PC yangu kwa maneno ya huyu binti wa kiume Nape.Byee..!
 
Nape ni Mhuni, hakuna Chama Makini kinachoweza kuchagua mhuni kama Nape kuwa Katibu mwenezi zaidi ya CCM. Nashukuru kwamba kauli zake za hovyo zinatusaidia maana kuropoka kwake kunazidi kuififisha CCM kila uchapo, tuendako ataropoka-ropoka sana kama bado atakuwepo.
 
Inashangaza sana kuona bado kuna watu wanamsikiliza na kumjadili Nape wakiwa siriaz.
 
Jamani Nape anatembea na Shangingi V8, toka ateuliwe ameongezeka uzito mara tatu kutokana na posho nono anazoipata kila anapobwabwaja hovyo.
Sasa mtu kama huyu hawezi kujua mateso ya wananchi. WaTz wanateswa na mfumuko wa bei, kushuka kwa thamani ya Shilingi yetu na kutokuwepokwa munguko wa fedha kabisa kutokana na Serikali kushuindwa kutimiza majukumu yake ya kuwalipa watoa hauduma mbali mbali. Nilikuwa nazungumza na mama ntilie mmoja anadai kutokana na kupanda sana kwa ghrama za vyakula wanashindwa kupata faida kabisa na wakiongeza bei wateja wao wanashindwa kula chakula kutokana na mzunguko mdogo wa fedha' hivyo basi wengi wao wanalazimka kufunga biashara zao hadi hapo bei za vyakula zitakapopungua kidigo. Hali hiyo ni hap Dar, Je mikoani pakoje? Haya ndio mateso kwa watanzania.

Kutokana na ukata serikali imeshindwa kununua mahindi ya wakulima hivyo hivi sasa wakulima wanateseka na njaa ilihali mahindi wanayo na wamezuiwa wasitafute wanunuzi wengine; haya ndio mateso kwa watanzania.
 
Analipwa mshahara mkubwa na ccm,asiposema lolote anahisi atanyang'anywa mshahara
 
Back
Top Bottom