CHADEMA sasa ndicho chama tawala

2015ready

JF-Expert Member
Feb 15, 2011
372
130
Martin Kaswahili

TANGU kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge, na madiwani mwezi Oktoba mwaka jana, nchi yetu imeshuhudia matukio kadhaa ya kipekee ambayo huenda yakawa kiashirio cha matukio mengine makubwa na ya kihistoria katika siasa za Tanzania katika siku za usoni.

Si nia yangu katika makala hii kudodosa kila jambo lililojitokeza wakati na baada ya uchaguzi huo ambao matokeo yake, hasa yale ya urais, yaliacha minongono na miguno miongoni mwa wananchi kiasi cha kuamsha chuki na uasi wa kimoyomoyo (passive resistance), uliopelekea kujengeka kwa ujasiri wa kupinga waziwazi yale yanayofanywa na watawala.

Ujasiri huo ndiyo umekuwa chanzo cha maandamano makubwa na ya kihistoria ambayo yameitisha si serikali iliyoko madarakani tu bali hata chama kilichotakiwa kuwa chama tawala. Nitafafanua.

Kwa kawaida, baada ya uchaguzi kumalizika na serikali kuundwa, kazi kubwa ya serikali mpya ni kuanza kutekeleza kwa vitendo ahadi zilizoahidiwa na viongozi wa chama tawala wakati wa kampeni za uchaguzi kwa mujibu wa ilani yao ya uchaguzi.

Kwa upande mwingine, vyama vya upinzani navyo huanza mara moja kutimiza wajibu wao wa kidemokrasia wa kuikosoa, kuisimamia, na kuiwajibisha serikali iliyoko madarakani, kwa njia ama ya bunge (kama chama kimepata wabunge) au kwa njia nyingine za kisiasa.

Kwa mantiki hii, mara baada ya uchaguzi wananchi hutarajia kuona serikali yao ikianza kwa nguvu kutimiza wajibu wake wa kutatua kero zao bila kujali mashambulizi ya vyama vya upinzani kupitia bunge au majukwaa ya kisiasa. Hii ndiyo kawaida katika ulingo wa siasa za vyama vingi katika nchi zote zinazofuata mfumo wa kidemokrasia.

Hutasikia mahali popote serikali iliyowekwa madarakani kwa kura halali za wananchi walio wengi ikitolewa kirahisi kwenye ajenda yake muhimu ya kuwatumikia wananchi walioichagua na kuanza kutumia muda wake mwingi kushughulikia chama au viongozi wa upinzani, kama inavyotoea sasa hapa nchini.

Kwa upande mwingine, kazi ya chama kinachokuwa kimeshinda uchaguzi ni kuisaidia serikali na viongozi wake katika kutekeleza majukumu yao ya kufanyia kazi yale yaliyoahidiwa katika ilani ya chama hicho. Chama tawala hutakiwa kuwa mlinzi wa serikali iliyopo madarani kwa kuikumbusha wajibu wake na kuitetea kwa wananchi kwa njia za kisiasa.

Kwa maneno mengine, CCM kwa kutumia jukwaa la kisiasa, kilitakiwa kuwa cha kwanza kuitetea serikali yake dhidi ya mashambulizi toka vyama vya upinzani badala ya kuiachia serikali kujitetea yenyewe kwa kutumia nguvu ya dola ya vitisho, mabavu, na propaganda za enzi za mfumo wa chama kimoja.

Tangu siku ya kikao cha kwanza cha bunge la sita, ambapo wabunge wa CHADEMA waliamua kutoka nje ya ukumbi wa bunge wakati ya hotuba ya Rais ya ufunguzi wa bunge kuthibitisha msimamo wao wa kutokubaliana na ujanja uliotumika katika kuhalalisha ushindi wa rais Kikwete, serikali na chama tawala viliingia katika majaribu makubwa ambayo bado hawajaonekana kuyashinda.
CHADEMA, kama chama cha upinzani chenye nia ya dhati ya kutwaa madaraka ya nchi kwa njia ya kidemokrasia, kilikuwa kimejipanga kuihenyesha serikali iliyoko madarakani tangu siku hiyo ya kwanza kazini.

Na kwa vile wengi wetu tulikuwa hatujawahi kuona siasa za upinzani wa kweli zinavyofanya kazi, tuliduwazwa na kitendo cha wabunge wa CHADEMA kuondoka bungeni kiasi cha kuingiwa na hofu kuwa serikali na chama tawala wasingekubali kurambwa chenga za maudhi katika dakika hizo za mwanzo kabisa za mchezo bila wao kujibu mapigo kwa pupa. Tulihisi kuundwa haraka kwa mkakati maalumu wa kuichezea CHADEMA rafu za kila aina ili wasizidi kuiadhiri serikali na chama chake kwa kutumia mbinu zao za siasa za kidot.com!

Na kama ilivyotarajiwa baada ya tukio hilo la kushtukiza bungeni, CCM walijipanga kuhakikisha CHADEMA inanyamazishwa kwa njia yoyote ile. Mbinu ya kwanza ilikuwa ya kutumia vitisho kupitia katibu wa itikadi na uenezi wa wakati huo, yaani John Chiligati.

Kwa mtindo wa amri za kijeshi unaotokana na kazi yake ya zamani, Chiligati alitoa aliwaamuru wabunge wa CCM kuangalia uwezekano wa kupeleka azimio la kuwafukuza bungeni wabunge wote wa CHADEMA kwa kitendo chao cha kumdalilisha Rais wa nchi.

Baadhi ya watu waliamini jambo hilo lingewezekana na kwa hiyo wabunge wa CHADEMA wangesimamishwa wasihudhurie vikao vya bunge. Lakini kwa wale wanaelewa demokrasia ya vyama vingi, na hasa inapotokea kuna chama makini cha upinzani kama CHADEMA inavyoinukia wakati huu, mbinu za CCM na serikali yake zilionekana za kizamani na hazikufua dafu mbele ya chama kinachoungwa mkono na nguvu kubwa ya umma uliochoshwa na ubabaishaji wa muda mrefu wa serikali ya CCM.

Mwisho wa siku wabunge wa CHADEMA hawakufukuzwa au kuzuiwa kuhudhuria vikao vya bunge, na kazi ya kuihenyesha serikali ndio kwanza ikashika kasi. Umaarufu wa CHADEMA kama chama chenye msimamo na kisichobabishwa ukazidi kuongezeka. Kwani kila aliyekuwa na hofu kwamba CHADEMA ingetishwa, ingeminywa, na hatimaye kufyata mkia, alishangaa kuona ujasiri mpya wa kidemokrasia ukiota mizizi nchini.

Vidonda vya maumivu ya kuporwa matokeo ya urais waliokuwa nayo wananchi nchi nzima yalianza kupata ahueni ya ghafla. Matarajio ya CCM na serikali yake ya kujiendeshea mambo kama vile nchi hii ni mali ya kundi dogo la watu wanaojiona wenye bahati ya kipekee yalianza kutoweka ghafla. Hofu kuu ikaanza kuwaingia viongozi wa serikali na Chama tawala, na mkakati wa kuibinya CHADEMA kwa nguvu zaidi ukapangwa.

Yaliyotokea kwenye maandamano ya Arusha ulikuwa ni ushahidi wa wazi wa kuwepo kwa mkakati maalum wa kuhakikisha CHADEMA haiendelei kuipigisha kwata serikali na kukifunika chama tawala, kama ilivyotokea katika awamu ya kwanza ya utawala wa Kikwete. Mabavu yaliyotumika kushambulia waandamanaji na hata kuzuia mkutano halali wa kisiasa, vikifuatiwa na propaganda za kufunika ukweli wa kilichotokea huko Arusha vilinikumbusha utawala wa kikomunisti wa Urusi ezi zile.

Ni mtindo huo huo uliotumiwa zamani na wakoloni kwa lengo la kuwadhibiti waafrika wasidai haki yao ya kuwa huru kwa njia ya maandamano na mikutano. Kwa wanaoelewa historia ya serikali zinazotumia udikteta wa kidemokrasia, ukatili wa askari wetu kule Arusha ulikuwa wa kisiasa zaidi badala ya mbinu za kawaida za kuthibiti fujo.

Linganisha matukio ya Arusha na maandamano yaliyofuatia kanda ya ziwa ambapo katika mikoa minne hakuna mtu hata mtu mmoja aliyeripotiwa kupoteza hata kandambili kwa kukimbia kipigo cha askari! Kule Arusha askari ndio waliowashambulia wananchi wasiona na silaha wala nia ya kupambana na mtu yeyote. Watanzania hawana utamaduni wa kushambulia askari bila kuchokozwa.

Lengo la matumizi ya mabavu katika maandamano ya Arusha ilikuwa ni kutengeneza jukwaa la propaganda maalum ya kuuaminisha umma kwamba CHADEMA ni chama cha fujo, kinachochea vurugu na ni hatari kwa nchi. Hata hivyo pamoja na jitihada za serikali na CCM kuelekeza lawama kwa CHADEMA kama chanzo cha vurugu na mauaji huko Arusha, wananchi waliamua kuzipuuza propaganda hizo na kuzidi kuiunga mkono CHADEMA.

Kinyume na mipango na matarajioa ya CCM na serikali yake, tukio la Arusha liliamsha hasira ya wananchi nchini nzima dhidi ya uonevu, ukandamizaji na unyanyasaji wa serikali ya chama tawala ambao huko nyuma ulivumiliwa kwa maumivu ya kimya kimya. Hali ya uasi wa kimomoyo ikazidi kushamiri. Huruma kwa wahanga wa mauji ya Arusha ikaongeza hamu ya wananchi kutaka kuwaonesha hadharani nguvu walio nayo kupitia chama kinachotetea maslahi ya wanyonge walio wengi.

Kwa wepesi wao wa kuelewa mambo, CHADEMA wakaamua kukidhi kiu ya walio wengi. Wakaanzisha maandamano ya kupinga unyonyaji, unyanyasaji na dhuluma za wazi zinazofanywa na viongozi wa serikali na chama tawala.
Hata hivyo kabla CHADEMA hawajanza maandamano yao nchi nzima, CCM wakapanga mkakati mwingine wa kucheza rafu bungeni.

Kwa kumtumia spika wa bunge, ambaye tangu kuchaguliwa kwake ilijulikana wazi jinsi ambavyo asingeweza kuvaa viatu vya mtangulizi wake, wabunge wa CCM waliamua kupindisha kwa makusudi kanuni za bunge ili kuizuia CHADEMA isiunde kambi rasmi ya upinzani, kama ilivyokuwa kwa CUF katika awamu mbili huko nyuma.

Mpango huu ulilenga kuzuia uwezo wa CHADEMA kuibua uoza ndani ya serikali kupitia kamati tatu za fedha wabungeni. Mkakati huu pia ulilenga kukigombanisha CHADEMA na vyama vingine vya upinzani ili kuwaaminisha wananchi kwamba CHADEMA wanapenda kujitega na ni chama chenye ubinafsi.

Kwa bahati mbaya mkakati huu ulifanikiwa kwa sehemu kubwa, na wananchi wakajionea wenyewe mchezo unaochezwa na CCM dhidi ya upinzani nchini. Vyama vya NCCR-Mageuzi, TLP, CUF, na UDP vilijikuta vikiungana na Chama tawala katika kuunda kambi isiyo ramsi ya upinzani dhidi ya CHADEMA.

Na kwa mara ya kwanza katika historia ya mfumo wa vyama vingi nchini, chama tawala kilivipiga busu vyama vidogo vya upinzani kwa lengo la kukishambulia chama kikuu cha upinzani! Siku hiyo CHADEMA kilionekana kama ndio chama tawala kwa jinsi kilivyovizidi umaarufu na mbinu vyama vingine vyote hata wakajikuta wanafunga ndoa ya dharura (marriage of convenience) ili kukikabili.

Na tangu siku hiyo CCM na vyama vingine vimekuwa vikifanya kazi kama ndivyo vyama vya upinzani dhidi ya chama tawala CHADEMA. Lakini hata baada ya kuvipa kumbato vyama vingine vya upinzani bungeni, serikali na CCM hawakujua kuwa bao jingine la kisigino lilikuwa linakuja muda si mrefu.

Maandamano ya kihistoria ya Mwanza yalipeleka msiba mwingine kwenye kambi ya CCM na serikali yake. Tofauti na matarajio ya wengi kwamba vurugu na kipigo cha Arusha vilikuwa fundisho tosha kuwatisha waandamanaji wengine kujitokeza kuwaunga mkono CHADEMA, maandamano ya Mwanza yalidhihirisha kile ambacho watawala wetu wamekuwa wakidhani hakipo yaani ujasiri wa watanzania kujitokeza hadharani na kuwaambia watawala hatutaki kusukumwa!

Watu wa Mwanza, ambao huko nyuma walionekana kama wateja watiifu wa CCM, waliushangaza ulimwengu kwa kuonesha ujasiri ambao haujazoeleka hapa nchini. Damu ya mauaji ya Arusha ilikuwa imeanza kujenga taifa la wanaoweza kudai haki zao bila kutishwa na binadamu wenzao.

Kuanzia Mwanza, Mara, Shinyanga hadi Kagera, CHADEMA walibeba kilio cha wanyonge juu ya ugumu wa maisha, kupanda kwa bei za bidhaa kulikochochewa na kupanda kwa bei za umeme, na wakati huo huo kuwepo kwa mgao wa umeme nchi nzima.

CHADEMA iliwakumbusha wananchi juu ya ahadi walizopewa na viongozi wa CCM na jinsi ambavyo ahadi hizo zilikuwa hazitekelezwi kwa visingizio vile vile vya siku zote vya kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na kuharibika kwa uchumi wa dunia.

Kwa umahiri wao mkubwa katika kuwasilisha ujumbe, viongozi wa CHADEMA waliendelea kuushawishi umma kwamba serikali iliyopo madarakani haina uwezo wala nia ya dhati ya kutatua matatizo yao sugu bali ipo kwa ajili ya kuneemesha vigogo wachache na familia zao kwa njia za kifisadi kama vile ya Dowans, ambayo serikali ilikuwa tayari kuilipa mabilioni ya fadha za walipa kodi bila hata chembe ya woga wala aibu.

Kama chama cha siasa chenye kuzijua kanuni za mchezo wa siasa za kidemokrasia, CHADEMA waliishambulia serikali kiasi cha kuifanya ilazimike kutekeleza baadhi ya madai halali ya wananchi. Moja ya mambo ambayo serikali ilikubali kuyatekeleza baada ya shinizo la CHADEMA ni pamoja na kuwepo kwa mchakato wa kuandika upya katiba ya nchi, kitu ambacho CCM haikuwa tayari kukifanya na wala haikukiingiza katika ilani yake ya uchaguzi uliopita.

Jambo jingine lililotimizwa na serikali kwa shinikizo la maandamano ya CHADEMA ni amri ya Waziri Mkuu ya kuwataka wafanya biashara wa sukari nchini kushusha bei ya bidha hiyo toka shilingi 2000 hadi 1700. Suala hili lilitekelezwa muda wa saa chache tu baada ya CHADEMA kuanza kulitumia kama mfano wa bidhaa zinazozidisha ugumu wa maisha ya wananchi wa kawaida.

Baadaye tukasikia Rais, akiwa katika ziara ya kutembelea wizara ya
nishati na madini, akiomba bei ya umeme ipunguzwe ili kupunguza makali ya maisha kwa wananchi. Yote haya yalikuja kutokana na shinikizo la chama kimoja cha upinzani kinachojua wajibu wake. Kweli CHADEMA waliipelekesha serikali utadhani wao ndio chama tawala!

Hata hivyo, wakati CHADEMA wakifanikiwa kuiadabisha serikali kiasi cha kuanza kutimiza matakwa ya wananchi, CCM waliamua kuja na rafu kali zaidi kuizuia CHADEMA isiendelee kuchukua nafasi yake. Safari hii Rais na mwenyekiti wa CCM aliingia ulingoni kuongeza nguvu za mapambano dhidi ya CHADEMA. Kupitia hotuba yake ya mwisho wa mwezi wa pili, Rais aliudhirishia umma wa Tanzania jinsi CHADEMA ilivyokuwa inaihenyesha serikali yake.

Mbali na kujikuta akijibu baadhi ya madai ya CHADEMA yaliyotakiwa kujibiwa ndani ya siku tisa, Rais alianzisha propoaganda mpya za kuishambulia CHADEMA kwa kulalamika kuwa ilikuwa ikiwachochea wananchi waanzishe vurugu za kuipindua serikali yake kwa njia ya maandamano. Wengi waliduwazwa na maneno hayo ya woga kutolewa na amiri jeshi mkuu wa nchi.

Hata hivyo baadhi yetu tuligundua mapema kuwa huu ulikuwa ni mkakati mwingine wa kuhakikisha CHADEMA inadhibitiwa. Mpango huu ulilenga mambo kadhaa. Kwanza kuwatisha tamaa wananchi ili wasizidi kuiunga mkono CHADEMA, kwa kuwaaminisha kuwa CHADEMA kilikuwa kinaandaa maasi nchini, kitu ambacho serikali ingekuja kukizima kwa nguvu ya dola na kusababisha wananchi wengi kuumia vibaya.

Pili, kuharibu taswila CHADEMA kwa kukionesha kuwa ni chama cha vurugu na viongozi wake washari wanaopenda madaraka kwa gharama yoyote.
Tatu, kuwapa makada wa CCM na baadhi ya viongozi wa serikali, hasa mawaziri, kitu cha kufanyia propaganda nchi nzima kwa lengo la kuuaminisha umma kwamba mandamano ya CHADEMA hayana lengo zuri la kisiasa hivyo wananchi wasiyaunge mkono na ikishindikana nguvu zitumike kuyadhibiti, ikiwa pamoja na viongozi wake kupigwa, kuumizwa, au hata kuundiwa mashitaka ya uongo kwa kisingizio kwamba serikali ililazimika kuchukua hatua za ziada kuepusha umwagaji damu nchini.

Sote tunakumbuka kilichotokea baada ya hotuba ya Rais. Waliokuwa wametayarishwa katika mkakati huu walianza kujitokeza. Kwanza tulimskia waziri wa nchi mahusiano, Stephen Wassira, kama kawaida yake, akitumia lugha za kibabe kuwatisha CHADEMA eti wasije kuilaumu serikali kwa kutumia nguvu kuwashughulikia kama hawataacha uchochezi kwenye mikutano yao.

Kisha tukamsikia msajiri wa vyama vya siasa bwana John Tendwa akiwaandikia CHADEMA barua ya kuwaonya wasitumie lugha za matusi katika mikutano yao vinginevyo angekifutia chama usajiri wa kudumu. Baadaye wakafuata kina Anna Kilango Malecela na viongozi wengine wa aina hiyo, kabla Sophia Simba na Bernard Membe hawajaja na mpya kwa kudai kuwa maandamano ya CHADEMA yalikuwa yanafadhiliwa na mataifa ya nje kupitia balozi zake hapa nchini. Kana kwamba haitoshi, tukasikia vijana wa Dar es Salaam wameandaa maandamano kupinga maandamano ya CHADEMA.

Nasikia maandamano haya ya vijana yalizuiwa na polisi kwa kisingizio cha kuleta usumbufu kwa wakazi wa jiji. Taarifa zilizoko ni kwamba mpango huu wa maandamano ya vijana ulipangwa ili polisi wawanyime kibali cha maandamano kwa lengo la kuandaa mazingira ya kuja kuwanyima CHADEMA kibali cha maandamano watakapotaka kuandamana popote Dar es Salaam. Tunasubiri kujionea.

Baada ya kiini macho cha maandamano ya vijana wa Dar es Salaam, yalifuatia maandamano ya kina mama kupinga maandamano ya CHADEMA, ambayo pia hayakuleta mvuto wowote. Baadaye tukasikia mpango wa maandamano ya vyama vyote vidogo vya siasa nchini kupinga maandamano ya CHADEMA, kabla hajatokea Profesa Lipumba huko Tanga na kuwashangaza wengi kwa kuishambulia CHADEMA kwa namna ambayo iliwadhihirishia wengi kwamba kweli sasa CUF ilikuwa imeungana rasmi na CCM kikishambulia CHADEMA.

Hapa ndipo nilipoamini bila shaka yoyote kwamba kwa sasa, CHADEMA ndio chama tawala, ambacho hakikupewa tu nafasi ya kuunda serikali kutokana na kuibiwa matokeao ya uchaguzi mkuu. Itakuwaje serikali na vyama karibia vyote vya siasa vijikute vikiungana katika kuishutumu, kuibeza au kuishambulia CHADEMA kana kwamba ndio chama tawala?

Ndio maana wananchi wameamua kuweka pamba masikioni na kuwapuuza wale wote wanaojaribu kuihujumu CHADEMA. Tangu Rais alipotumia muda wake mwingi wa hotuba kuishambulia CHADEMA ikifuatiwa na maandamano-maigizo na vitisho vyote vya kuishughulikia CHADEMA, wananchi wamezidi kuelekeza mioyo yao kwa CHADEMA huku wakiiona CCM na serikali yake kama wasaliti.

Iweje chama ambacho hakina serikali, hakina idadi kubwa ya wabunge, na hakina pesa kama CCM, kitese akili za viongozi wa nchi kwa kiasi hiki? Kwa nini chama kinachounda serikali kiungane na vyama vingine vyote nchini kukishambulia chama kimoja tu cha upinzani utadhani ndio chenye serikali iliyoko madarani?

Kwa nini serikali ihangaike kuandaa watu, vikundi, na hata dola kushughulikia namana ya kuzima harakati halali za kisiasa za chama kimoja tu cha upinzani nchini? Nadhani haya yote yanatokea kwa sababu moja tu, kwamba katika mioyo ya watu wengi, CHADEMA kwa sasa ndio chama tawala japo hakiongozi toka ikulu. Ukweli ndio huo. (Source - Tanzania Daima)
(Wana JF- Naomba tujadili hii article kwa undani zaidi)
 
Martin Kaswahili

TANGU kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge, na madiwani mwezi Oktoba mwaka jana, nchi yetu imeshuhudia matukio kadhaa ya kipekee ambayo huenda yakawa kiashirio cha matukio mengine makubwa na ya kihistoria katika siasa za Tanzania katika siku za usoni.
Si nia yangu katika makala hii kudodosa kila jambo lililojitokeza wakati na baada ya uchaguzi huo ambao matokeo yake, hasa yale ya urais, yaliacha minong’ono na miguno miongoni mwa wananchi kiasi cha kuamsha chuki na uasi wa kimoyomoyo (passive resistance), uliopelekea kujengeka kwa ujasiri wa kupinga waziwazi yale yanayofanywa na watawala.
Ujasiri huo ndiyo umekuwa chanzo cha maandamano makubwa na ya kihistoria ambayo yameitisha si serikali iliyoko madarakani tu bali hata chama kilichotakiwa kuwa chama tawala. Nitafafanua.
Kwa kawaida, baada ya uchaguzi kumalizika na serikali kuundwa, kazi kubwa ya serikali mpya ni kuanza kutekeleza kwa vitendo ahadi zilizoahidiwa na viongozi wa chama tawala wakati wa kampeni za uchaguzi kwa mujibu wa ilani yao ya uchaguzi. Kwa upande mwingine, vyama vya upinzani navyo huanza mara moja kutimiza wajibu wao wa kidemokrasia wa kuikosoa, kuisimamia, na kuiwajibisha serikali iliyoko madarakani, kwa njia ama ya bunge (kama chama kimepata wabunge) au kwa njia nyingine za kisiasa.

Kwa mantiki hii, mara baada ya uchaguzi wananchi hutarajia kuona serikali yao ikianza kwa nguvu kutimiza wajibu wake wa kutatua kero zao bila kujali mashambulizi ya vyama vya upinzani kupitia bunge au majukwaa ya kisiasa. Hii ndiyo kawaida katika ulingo wa siasa za vyama vingi katika nchi zote zinazofuata mfumo wa kidemokrasia.
Hutasikia mahali popote serikali iliyowekwa madarakani kwa kura halali za wananchi walio wengi ikitolewa kirahisi kwenye ajenda yake muhimu ya kuwatumikia wananchi walioichagua na kuanza kutumia muda wake mwingi kushughulikia chama au viongozi wa upinzani, kama inavyotoea sasa hapa nchini.
Kwa upande mwingine, kazi ya chama kinachokuwa kimeshinda uchaguzi ni kuisaidia serikali na viongozi wake katika kutekeleza majukumu yao ya kufanyia kazi yale yaliyoahidiwa katika ilani ya chama hicho. Chama tawala hutakiwa kuwa mlinzi wa serikali iliyopo madarani kwa kuikumbusha wajibu wake na kuitetea kwa wananchi kwa njia za kisiasa.
Kwa maneno mengine, CCM kwa kutumia jukwaa la kisiasa, kilitakiwa kuwa cha kwanza kuitetea serikali yake dhidi ya mashambulizi toka vyama vya upinzani badala ya kuiachia serikali kujitetea yenyewe kwa kutumia nguvu ya dola ya vitisho, mabavu, na propaganda za enzi za mfumo wa chama kimoja.

Tangu siku ya kikao cha kwanza cha bunge la sita, ambapo wabunge wa CHADEMA waliamua kutoka nje ya ukumbi wa bunge wakati ya hotuba ya Rais ya ufunguzi wa bunge kuthibitisha msimamo wao wa kutokubaliana na ujanja uliotumika katika kuhalalisha ushindi wa rais Kikwete, serikali na chama tawala viliingia katika majaribu makubwa ambayo bado hawajaonekana kuyashinda.
CHADEMA, kama chama cha upinzani chenye nia ya dhati ya kutwaa madaraka ya nchi kwa njia ya kidemokrasia, kilikuwa kimejipanga kuihenyesha serikali iliyoko madarakani tangu siku hiyo ya kwanza kazini.
Na kwa vile wengi wetu tulikuwa hatujawahi kuona siasa za upinzani wa kweli zinavyofanya kazi, tuliduwazwa na kitendo cha wabunge wa CHADEMA kuondoka bungeni kiasi cha kuingiwa na hofu kuwa serikali na chama tawala wasingekubali kurambwa chenga za maudhi katika dakika hizo za mwanzo kabisa za mchezo bila wao kujibu mapigo kwa pupa. Tulihisi kuundwa haraka kwa mkakati maalumu wa kuichezea CHADEMA rafu za kila aina ili wasizidi kuiadhiri serikali na chama chake kwa kutumia mbinu zao za siasa za kidot.com!

Na kama ilivyotarajiwa baada ya tukio hilo la kushtukiza bungeni, CCM walijipanga kuhakikisha CHADEMA inanyamazishwa kwa njia yoyote ile. Mbinu ya kwanza ilikuwa ya kutumia ‘vitisho’ kupitia katibu wa itikadi na uenezi wa wakati huo, yaani John Chiligati.
Kwa mtindo wa amri za kijeshi unaotokana na kazi yake ya zamani, Chiligati alitoa aliwaamuru wabunge wa CCM kuangalia uwezekano wa kupeleka azimio la ‘kuwafukuza’ bungeni wabunge wote wa CHADEMA kwa kitendo chao cha kumdalilisha Rais wa nchi.
Baadhi ya watu waliamini jambo hilo lingewezekana na kwa hiyo wabunge wa CHADEMA wangesimamishwa wasihudhurie vikao vya bunge. Lakini kwa wale wanaelewa demokrasia ya vyama vingi, na hasa inapotokea kuna chama makini cha upinzani kama CHADEMA inavyoinukia wakati huu, mbinu za CCM na serikali yake zilionekana za kizamani na hazikufua dafu mbele ya chama kinachoungwa mkono na nguvu kubwa ya umma uliochoshwa na ubabaishaji wa muda mrefu wa serikali ya CCM.

Mwisho wa siku wabunge wa CHADEMA hawakufukuzwa au kuzuiwa kuhudhuria vikao vya bunge, na kazi ya kuihenyesha serikali ndio kwanza ikashika kasi. Umaarufu wa CHADEMA kama chama chenye msimamo na kisichobabishwa ukazidi kuongezeka. Kwani kila aliyekuwa na hofu kwamba CHADEMA ingetishwa, ingeminywa, na hatimaye kufyata mkia, alishangaa kuona ujasiri mpya wa kidemokrasia ukiota mizizi nchini.
Vidonda vya maumivu ya ‘kuporwa’ matokeo ya urais waliokuwa nayo wananchi nchi nzima yalianza kupata ahueni ya ghafla. Matarajio ya CCM na serikali yake ya kujiendeshea mambo kama vile nchi hii ni mali ya kundi dogo la watu wanaojiona wenye bahati ya kipekee yalianza kutoweka ghafla. Hofu kuu ikaanza kuwaingia viongozi wa serikali na Chama tawala, na mkakati wa kuibinya CHADEMA ‘kwa nguvu zaidi’ ukapangwa.
Yaliyotokea kwenye maandamano ya Arusha ulikuwa ni ushahidi wa wazi wa kuwepo kwa mkakati maalum wa kuhakikisha CHADEMA haiendelei kuipigisha kwata serikali na kukifunika chama tawala, kama ilivyotokea katika awamu ya kwanza ya utawala wa Kikwete. Mabavu yaliyotumika kushambulia waandamanaji na hata kuzuia mkutano halali wa kisiasa, vikifuatiwa na propaganda za kufunika ukweli wa kilichotokea huko Arusha vilinikumbusha utawala wa kikomunisti wa Urusi ezi zile.
Ni mtindo huo huo uliotumiwa zamani na wakoloni kwa lengo la kuwadhibiti waafrika wasidai haki yao ya kuwa huru kwa njia ya maandamano na mikutano. Kwa wanaoelewa historia ya serikali zinazotumia udikteta wa kidemokrasia, ukatili wa askari wetu kule Arusha ulikuwa wa kisiasa zaidi badala ya mbinu za kawaida za kuthibiti fujo.

Linganisha matukio ya Arusha na maandamano yaliyofuatia kanda ya ziwa ambapo katika mikoa minne hakuna mtu hata mtu mmoja aliyeripotiwa kupoteza hata ‘kandambili’ kwa kukimbia kipigo cha askari! Kule Arusha askari ndio waliowashambulia wananchi wasiona na silaha wala nia ya kupambana na mtu yeyote. Watanzania hawana utamaduni wa kushambulia askari bila kuchokozwa.
Lengo la matumizi ya mabavu katika maandamano ya Arusha ilikuwa ni kutengeneza jukwaa la propaganda maalum ya kuuaminisha umma kwamba CHADEMA ni chama cha fujo, kinachochea vurugu na ni hatari kwa nchi. Hata hivyo pamoja na jitihada za serikali na CCM kuelekeza lawama kwa CHADEMA kama chanzo cha vurugu na mauaji huko Arusha, wananchi waliamua kuzipuuza propaganda hizo na kuzidi kuiunga mkono CHADEMA.

Kinyume na mipango na matarajioa ya CCM na serikali yake, tukio la Arusha liliamsha hasira ya wananchi nchini nzima dhidi ya uonevu, ukandamizaji na unyanyasaji wa serikali ya chama tawala ambao huko nyuma ulivumiliwa kwa maumivu ya kimya kimya. Hali ya uasi wa kimomoyo ikazidi kushamiri. Huruma kwa wahanga wa mauji ya Arusha ikaongeza hamu ya wananchi kutaka kuwaonesha hadharani nguvu walio nayo kupitia chama kinachotetea maslahi ya wanyonge walio wengi.
Kwa wepesi wao wa kuelewa mambo, CHADEMA wakaamua kukidhi kiu ya walio wengi. Wakaanzisha maandamano ya kupinga unyonyaji, unyanyasaji na dhuluma za wazi zinazofanywa na viongozi wa serikali na chama tawala.
Hata hivyo kabla CHADEMA hawajanza maandamano yao nchi nzima, CCM wakapanga mkakati mwingine wa kucheza rafu bungeni. Kwa kumtumia spika wa bunge, ambaye tangu kuchaguliwa kwake ilijulikana wazi jinsi ambavyo asingeweza kuvaa viatu vya mtangulizi wake, wabunge wa CCM waliamua kupindisha kwa makusudi kanuni za bunge ili kuizuia CHADEMA isiunde kambi rasmi ya upinzani, kama ilivyokuwa kwa CUF katika awamu mbili huko nyuma.

Mpango huu ulilenga kuzuia uwezo wa CHADEMA kuibua uoza ndani ya serikali kupitia kamati tatu za fedha wabungeni. Mkakati huu pia ulilenga kukigombanisha CHADEMA na vyama vingine vya upinzani ili kuwaaminisha wananchi kwamba CHADEMA wanapenda kujitega na ni chama chenye ubinafsi.
Kwa bahati mbaya mkakati huu ulifanikiwa kwa sehemu kubwa, na wananchi wakajionea wenyewe mchezo unaochezwa na CCM dhidi ya upinzani nchini. Vyama vya NCCR-Mageuzi, TLP, CUF, na UDP vilijikuta vikiungana na Chama tawala katika kuunda ‘kambi isiyo ramsi ya upinzani’ dhidi ya CHADEMA.
Na kwa mara ya kwanza katika historia ya mfumo wa vyama vingi nchini, chama tawala ‘kilivipiga busu’ vyama vidogo vya upinzani kwa lengo la kukishambulia chama kikuu cha upinzani! Siku hiyo CHADEMA kilionekana kama ndio chama tawala kwa jinsi kilivyovizidi umaarufu na mbinu vyama vingine vyote hata wakajikuta wanafunga ‘ndoa ya dharura’ (marriage of convenience) ili kukikabili.
Na tangu siku hiyo CCM na vyama vingine vimekuwa vikifanya kazi kama ndivyo vyama vya upinzani dhidi ya ‘chama tawala CHADEMA’. Lakini hata baada ya kuvipa ‘kumbato’ vyama vingine vya upinzani bungeni, serikali na CCM hawakujua kuwa bao jingine la kisigino lilikuwa linakuja muda si mrefu.

Maandamano ya kihistoria ya Mwanza yalipeleka msiba mwingine kwenye kambi ya CCM na serikali yake. Tofauti na matarajio ya wengi kwamba vurugu na kipigo cha Arusha vilikuwa fundisho tosha kuwatisha waandamanaji wengine kujitokeza kuwaunga mkono CHADEMA, maandamano ya Mwanza yalidhihirisha kile ambacho watawala wetu wamekuwa wakidhani hakipo yaani ujasiri wa watanzania kujitokeza hadharani na kuwaambia watawala ‘hatutaki kusukumwa’!
Watu wa Mwanza, ambao huko nyuma walionekana kama ‘wateja watiifu’ wa CCM, waliushangaza ulimwengu kwa kuonesha ujasiri ambao haujazoeleka hapa nchini. Damu ya mauaji ya Arusha ilikuwa imeanza kujenga taifa la wanaoweza kudai haki zao bila kutishwa na binadamu wenzao.
Kuanzia Mwanza, Mara, Shinyanga hadi Kagera, CHADEMA walibeba kilio cha wanyonge juu ya ugumu wa maisha, kupanda kwa bei za bidhaa kulikochochewa na kupanda kwa bei za umeme, na wakati huo huo kuwepo kwa mgao wa umeme nchi nzima. CHADEMA iliwakumbusha wananchi juu ya ahadi walizopewa na viongozi wa CCM na jinsi ambavyo ahadi hizo zilikuwa hazitekelezwi kwa visingizio vile vile vya siku zote vya ‘kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia’ na ‘kuharibika kwa uchumi wa dunia’.

Kwa umahiri wao mkubwa katika kuwasilisha ujumbe, viongozi wa CHADEMA waliendelea kuushawishi umma kwamba serikali iliyopo madarakani haina uwezo wala nia ya dhati ya kutatua matatizo yao sugu bali ipo kwa ajili ya kuneemesha vigogo wachache na familia zao kwa njia za kifisadi kama vile ya Dowans, ambayo serikali ilikuwa tayari kuilipa mabilioni ya fadha za walipa kodi bila hata chembe ya woga wala aibu.
Kama chama cha siasa chenye kuzijua kanuni za mchezo wa siasa za kidemokrasia, CHADEMA waliishambulia serikali kiasi cha kuifanya ilazimike kutekeleza baadhi ya madai halali ya wananchi. Moja ya mambo ambayo serikali ilikubali kuyatekeleza baada ya shinizo la CHADEMA ni pamoja na kuwepo kwa mchakato wa kuandika upya katiba ya nchi, kitu ambacho CCM haikuwa tayari kukifanya na wala haikukiingiza katika ilani yake ya uchaguzi uliopita.
Jambo jingine lililotimizwa na serikali kwa shinikizo la maandamano ya CHADEMA ni amri ya Waziri Mkuu ya kuwataka wafanya biashara wa sukari nchini kushusha bei ya bidha hiyo toka shilingi 2000 hadi 1700. Suala hili lilitekelezwa muda wa saa chache tu baada ya CHADEMA kuanza kulitumia kama mfano wa bidhaa zinazozidisha ugumu wa maisha ya wananchi wa kawaida.

Baadaye tukasikia Rais, akiwa katika ziara ya kutembelea wizara ya
nishati na madini, akiomba bei ya umeme ipunguzwe ili kupunguza makali ya maisha kwa wananchi. Yote haya yalikuja kutokana na shinikizo la chama kimoja cha upinzani kinachojua wajibu wake. Kweli CHADEMA waliipelekesha serikali utadhani wao ndio chama tawala!
Hata hivyo, wakati CHADEMA wakifanikiwa kuiadabisha serikali kiasi cha kuanza kutimiza matakwa ya wananchi, CCM waliamua kuja na rafu kali zaidi kuizuia CHADEMA isiendelee kuchukua nafasi yake. Safari hii Rais na mwenyekiti wa CCM aliingia ulingoni kuongeza nguvu za mapambano dhidi ya CHADEMA. Kupitia hotuba yake ya mwisho wa mwezi wa pili, Rais aliudhirishia umma wa Tanzania jinsi CHADEMA ilivyokuwa inaihenyesha serikali yake.
Mbali na kujikuta akijibu baadhi ya madai ya CHADEMA yaliyotakiwa kujibiwa ndani ya siku tisa, Rais alianzisha propoaganda mpya za kuishambulia CHADEMA kwa kulalamika kuwa ilikuwa ikiwachochea wananchi waanzishe vurugu za kuipindua serikali yake kwa njia ya maandamano. Wengi waliduwazwa na maneno hayo ya woga kutolewa na amiri jeshi mkuu wa nchi.

Hata hivyo baadhi yetu tuligundua mapema kuwa huu ulikuwa ni mkakati mwingine wa kuhakikisha CHADEMA inadhibitiwa. Mpango huu ulilenga mambo kadhaa. Kwanza kuwatisha tamaa wananchi ili wasizidi kuiunga mkono CHADEMA, kwa kuwaaminisha kuwa CHADEMA kilikuwa kinaandaa maasi nchini, kitu ambacho serikali ingekuja kukizima kwa nguvu ya dola na kusababisha wananchi wengi kuumia vibaya.
Pili, kuharibu taswila CHADEMA kwa kukionesha kuwa ni chama cha vurugu na viongozi wake washari wanaopenda madaraka kwa gharama yoyote.
Tatu, kuwapa makada wa CCM na baadhi ya viongozi wa serikali, hasa mawaziri, kitu cha kufanyia propaganda nchi nzima kwa lengo la kuuaminisha umma kwamba mandamano ya CHADEMA hayana lengo zuri la kisiasa hivyo wananchi wasiyaunge mkono na ikishindikana nguvu zitumike kuyadhibiti, ikiwa pamoja na viongozi wake kupigwa, kuumizwa, au hata kuundiwa mashitaka ya uongo kwa kisingizio kwamba ‘serikali ililazimika kuchukua hatua za ziada kuepusha umwagaji damu nchini’.

Sote tunakumbuka kilichotokea baada ya hotuba ya Rais. Waliokuwa wametayarishwa katika mkakati huu walianza kujitokeza. Kwanza tulimskia waziri wa nchi mahusiano, Stephen Wassira, kama kawaida yake, akitumia lugha za kibabe kuwatisha CHADEMA eti ‘wasije kuilaumu serikali’ kwa kutumia nguvu kuwashughulikia kama hawataacha uchochezi kwenye mikutano yao.
Kisha tukamsikia msajiri wa vyama vya siasa bwana John Tendwa akiwaandikia CHADEMA barua ya kuwaonya wasitumie ‘lugha za matusi’ katika mikutano yao vinginevyo angekifutia chama usajiri wa kudumu. Baadaye wakafuata kina Anna Kilango Malecela na viongozi wengine wa aina hiyo, kabla Sophia Simba na Bernard Membe hawajaja na mpya kwa kudai kuwa maandamano ya CHADEMA yalikuwa yanafadhiliwa na mataifa ya nje kupitia balozi zake hapa nchini. Kana kwamba haitoshi, tukasikia vijana wa Dar es Salaam wameandaa maandamano kupinga maandamano ya CHADEMA.

Nasikia maandamano haya ya vijana yalizuiwa na polisi kwa kisingizio cha kuleta usumbufu kwa wakazi wa jiji. Taarifa zilizoko ni kwamba mpango huu wa maandamano ya vijana ulipangwa ili polisi wawanyime kibali cha maandamano kwa lengo la kuandaa mazingira ya kuja kuwanyima CHADEMA kibali cha maandamano watakapotaka kuandamana popote Dar es Salaam. Tunasubiri kujionea.
Baada ya kiini macho cha maandamano ya vijana wa Dar es Salaam, yalifuatia maandamano ya kina mama kupinga maandamano ya CHADEMA, ambayo pia hayakuleta mvuto wowote. Baadaye tukasikia mpango wa maandamano ya vyama vyote vidogo vya siasa nchini kupinga maandamano ya CHADEMA, kabla hajatokea Profesa Lipumba huko Tanga na kuwashangaza wengi kwa kuishambulia CHADEMA kwa namna ambayo iliwadhihirishia wengi kwamba kweli sasa CUF ilikuwa imeungana rasmi na CCM kikishambulia CHADEMA.

Hapa ndipo nilipoamini bila shaka yoyote kwamba kwa sasa, CHADEMA ndio chama tawala, ambacho hakikupewa tu nafasi ya kuunda serikali kutokana na kuibiwa matokeao ya uchaguzi mkuu. Itakuwaje serikali na vyama karibia vyote vya siasa vijikute vikiungana katika kuishutumu, kuibeza au kuishambulia CHADEMA kana kwamba ndio chama tawala?
Ndio maana wananchi wameamua kuweka pamba masikioni na kuwapuuza wale wote wanaojaribu kuihujumu CHADEMA. Tangu Rais alipotumia muda wake mwingi wa hotuba kuishambulia CHADEMA ikifuatiwa na maandamano-maigizo na vitisho vyote vya kuishughulikia CHADEMA, wananchi wamezidi kuelekeza mioyo yao kwa CHADEMA huku wakiiona CCM na serikali yake kama wasaliti. Iweje chama ambacho hakina serikali, hakina idadi kubwa ya wabunge, na hakina pesa kama CCM, kitese akili za viongozi wa nchi kwa kiasi hiki? Kwa nini chama kinachounda serikali kiungane na vyama vingine vyote nchini kukishambulia chama kimoja tu cha upinzani utadhani ndio chenye serikali iliyoko madarani?
Kwa nini serikali ihangaike kuandaa watu, vikundi, na hata dola kushughulikia namana ya kuzima harakati halali za kisiasa za chama kimoja tu cha upinzani nchini? Nadhani haya yote yanatokea kwa sababu moja tu, kwamba katika mioyo ya watu wengi, CHADEMA kwa sasa ndio chama tawala japo hakiongozi toka ikulu. Ukweli ndio huo. (Source - Tanzania Daima)
(Wana JF- Naomba tujadili hii article kwa undani zaidi)
ni ukweli ulio wazi, chadema ndio chama tawala kwa sasa, maana chama cha magamba kwa sasa kipo ICU kinatoa hayo magamba, kila siku wanaongelea kauli za cdm au utekelezaji wake. Tunasubiri msimamo wa mapacha watatu, kama watakipa O2 au watataka mashime za kupumulia ziondolewe ili kife rasmi. yetu macho
 
anigif_the-best-monique-gif-ever-7172-1278428215-3.gif
 
Ni ukweli mtupu huo kwenye hiyo article,licha ya CDM kushambuliwa na kuundiwa mikakati ya kuiangamiza,lakini pia serikali imeendelea kutekeleza maagizo ya CDM!
 
khaaa ndefu kweli...sijasoma yote lakini naunga mkono ni safi...kama wanabisha funga milango tupigane bana
 
kama chadema ndicho chama tawala mbona mnashinda barabarani mnaandamana? kila kukicha mko vyuoni kusaka wanafunzi kwa ajili ya migomo. 4sure chadema mnatia aibu kujiita eti mna hazina ya wasomi. ivi hizo ndio solution za kisomi? kama chadema mmekuwa watawala pangeni wakuu wa mikoa, wakurugenzi, tengueni uwepo wa spika bibi
 
unachekesha sana kweli hata chizi akisoma post yako atecheka na atajiona ana nafuu kuliko wewe
 
<p>
kama chadema ndicho chama tawala mbona mnashinda barabarani mnaandamana? kila kukicha mko vyuoni kusaka wanafunzi kwa ajili ya migomo. 4sure chadema mnatia aibu kujiita eti mna hazina ya wasomi. ivi hizo ndio solution za kisomi? kama chadema mmekuwa watawala pangeni wakuu wa mikoa, wakurugenzi, tengueni uwepo wa spika bibi
</p>
<p>&nbsp;</p>
wewe utakufa na GAMBA HILO SANUKA KAKA muda wa mabadiliko huu CDM ndio inaongoza nchi hii,waziri mkuu mwenyewe umemuona jmosi iliyopita alikataa unafiki kwa maslahi ya Taifa na kuunga mkono hoja ya kamanda Lissu mia kwa mia na madam spika hakuamini masikio yake akamuuza mara 3.Sasa ni mwendo wa nguvu ya UMMA tu.
 
Crap ya Kujifariji baada ya Kushindwa Uchaguzi!

You must be pregnant!!! You see nothing, hear nothing, think nothing, simply because you are married by ccm and now you are pregnant. The pregnat given to you by ccm-magamba. You will deliver a dead child.
 
kuna mlengo wa kati mr makamba (mr mak) hawaelewi nini wanachofanya na inaonekana wameshakataa ya kuwa huru siku moja nakupeni pole sana..
 
kama chadema ndicho chama tawala mbona mnashinda barabarani mnaandamana? kila kukicha mko vyuoni kusaka wanafunzi kwa ajili ya migomo. 4sure chadema mnatia aibu kujiita eti mna hazina ya wasomi. ivi hizo ndio solution za kisomi? kama chadema mmekuwa watawala pangeni wakuu wa mikoa, wakurugenzi, tengueni uwepo wa spika bibi

Kwa maelezo haya unaonyesha ni jinsi gani akili yako ilivyoganda,....harakati zote duniani zimeanzia kwa wasomi hasa wanavyuo na wafanyakazi....kama unaona CDM wanahangaika huko subiri uone moto wa wasomi upoje ndipo utakapoona wakurugenzi na wakuu wa mikoa si ishu kubwa sana ya CDM kwani katiba mpya itaweka utaratibu mzuri wa kuwapata hawa viongozi
 
You must be pregnant!!! You see nothing, hear nothing, think nothing, simply because you are married by ccm and now you are pregnant. The pregnat given to you by ccm-magamba. You will deliver a dead child.

Sema: The pregnancy (samahani naweka rekodi sawasawa) ila ujumbe wako uko njema sana na nakubaliana nao kwamba jamaa atakuwa amemimbwa
 
Magamba mengine ni magumu kuvuka kwahiyo CCM wasitufanyie kiini macho. Kama CCM hawajui nguvu ya Umma, basi 2015 ndio watapatwa na mshituko wa Magamba. Tunakuja na JF-Revolution hadi kieleweke.
 
Mtu yeyote makini anajua kabsa kuwa CHADEMA ndiyo kinaendesha SERIKALI YA CCM.
Sera zote wanazotekeleza CCM kwa sasa ni zile zilizokuwa zina nadiwa na CDM wakti wa kampeni za 2010. Hakuna hata sera hata moja wanayotekeleza CCM iliyokuwa kwenye ilani yao ya Uchaguzi. Nitaje mambo 2 tu ambayo CCM wanatekeleza kutokana na CDM-drive:
  1. Mchakato wa kupata KATIBA mpya Tanzania ni wazo la CHADEMA walipoanza ku-walk out Bunge session!
  2. Kupiga vita MAFISADI ni wazo la CHADEMA tangu CDM walipokuja na 'list of shame'.
Bado yako mengi.
 
Magamba mengine ni magumu kuvuka kwahiyo CCM wasitufanyie kiini macho. Kama CCM hawajui nguvu ya Umma, basi 2015 ndio watapatwa na mshituko wa Magamba. Tunakuja na JF-Revolution hadi kieleweke.

Pole sana kwa kujifariji, CCM itaendelea kuongoza. Tunasafisha chama kwanza ile tuone kama CHDm watakuwa na hoja.
 
kama chadema ndicho chama tawala mbona mnashinda barabarani mnaandamana? kila kukicha mko vyuoni kusaka wanafunzi kwa ajili ya migomo. 4sure chadema mnatia aibu kujiita eti mna hazina ya wasomi. ivi hizo ndio solution za kisomi? kama chadema mmekuwa watawala pangeni wakuu wa mikoa, wakurugenzi, tengueni uwepo wa spika bibi

Bwana Mak inauma lakini ndio ukweli, mzee wa kaya leo anatetea kupandisha gharama za umeme kesho anawaomba tanesco washushe wewe unafikiri nini kinaendelea hapo? Pia usifikiri kwendas vyuoni ni kutafuta migomo la hasha kule nikutafuta kuungwa mkono na hiyo ndiyo kazi kuu ya siasa sasa hilo nalo lakuumiza? Kama ni aibu kufanya hayo hakika kwa tanzania ujue maendeleo hayatapatikana..
 
Ni kweli kabisa Chadema ndicho chama tawala mana kina nguvu ya uma na ukitaka kujua kuwa kina nguvu ya uma angalia mikutano yake watu wanavyojaa ukilinganisha na chama cha wakoloni weusi CCM,Chadema viva ALUTA CONTINU.....
 
Back
Top Bottom