CHADEMA: Ole wenu mkiipokea Mizoga ya CCM!

Mutu

JF-Expert Member
Mar 30, 2008
1,331
0
Rev. Kishoka,
Mkuu wangu pengine umesahau au huelewi kwamba vita ya Chadema ni kuwaondoa CCM madarakani. Dhamira hii haijabadilika kwani hii ni Vita baridi ya kisiasa..Na kutokana na kutoelewa huku ndiko kumewafanya wengi wenu msijiunge na Chadema ktk vita hii toka awali. Chadema will use all means hata iwe vifaa vya CCM wenyewe kupata ushindi kama Nyerere alivyompiga Idd amin na mizinga yake mwenyewe kushinda vita.

Kwa hiyo mnashindwa kuelewa kwamba hapa sii swala la demokrasia at it's best, ila ni kuitumia demokrasia hiyo hiyo inapowezekana kutumika kwani Mungu katukataza kuua lakini ukiwa vitani huwezi kuweka silaha chini ukisema ati Mungu alikataza kuua na haitakuwa haki kkuua ili upande kumshinda adui yako..

Strategy ya Chadema ni ya Ushindi by all means hayo ya Demokrasia na Itikadi huu sio wakati wake na ndio maana hadi sasa hivi mnashindwa kuwaelewa Chadema kwani kama ingebidi kuchukua silaha ingekuwa hatuzungumzii tena demokrasia wala usalama wa Taifa isipokuwa kwa uzito wa hatua walizochukua.

Alichofanya Zitto ni kuchekecha hao mizoga ili kupata kinachoweza kulika. Zitto baada ya kutopa taarifa za hao waliojiunga wale wenye woga na kujificha wamekimbilia kukana kujitoa CCM. na kama nilivyowahi kusema siku za nyuma kutoka CCM na kujiunga Chadema haitakuwa kazi ndogo kwao. Watatangazwa magazetini na hakuna Usiri, watavikwa majezi na penbgine hata kupewa wajibu ambao hawatapenda kuufanya ili mradi wanapimwa Uaminifu wao kwa chama na hasa vita hii.

Kwa Chadema hili swala lipo beyond maslahi ya Chama au matakwa ya demokrasia - ni swala la Mustakabali wa Taifa letu ambao uko hatarini. Uhatari ambao pengine nyie mnashindwa kuusoma au kukifikiria isipokuwa mnaona tu sheria na taratibu za demokrasia ambayo haipo nchini to begin with..Tukishindwa sasa hivi, they will be no 2015...Take my word for that!

WEWE jamaa una akili !
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
54,560
2,000

Mazee,

Either chama kina principles au hakina principles, hakuna habari za wakati wake wala nini.

Na CHADEMA so far wanajionyesha hawana principles, na kama hawana principles katika upinzani, nini kitatufanya tuamini kwamba watakuwa na principles wakipata serikali ?
 
TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
21,997

at last, kuna mtu ameweka maswali yangu vizuri... this is something which bothers me sana tu!!! it seems chadema hawajui magnitude ya wanachotafuta
 
Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,486
2,000
Mazee,

Either chama kina principles au hakina principles, hakuna habari za wakati wake wala nini.

Na CHADEMA so far wanajionyesha hawana principles, na kama hawana principles katika upinzani, nini kitatufanya tuamini kwamba watakuwa na principles wakipata serikali ?
hapana mkuu ni wewe hufahamu Chadema wamelenga kitu gani. Nitarudia kusema hivi wengi wenu hapa mnafikiria kwa kujiuza kwamba haya mapambano yana demokrasia ndani yake.. Mkuu wangu hakuna demokrasia hapa vitani, ni kama vile watu mlioko vitani. Unabeba silaha na yeyote anayejiunga nanyi kupiganana adui mnampa silaha na kumweka msitari wa mbele wa wapiganaji...Mgeni siku ya kwanza mpe jembe akalime.

Kama kungekuwepo na demokrasia labda hapo tungezungumzia kuuza sera na ilani na hapo ndipo maswali yenu yalihitaji majibu mnayoyataka, lakini kwa Chadema sasa hivi hii ni vita. Vita baridi ya kurudisha hadhi ya Tanzania kama taifa huru lisilotawaliwa na watu wachache wanaojiona wao ni untouchables.

Hivyo nguvu kubwa imewekwa ktk kupigana vita hii kwanza na principles zilizopo ni za ushindi wa vita. Kisha baada ya vita Chadema watahakikisha Ufisadi unakoma, Uhuru wa nchi hii unarudishwa mikononi mwa wananchi wenyewe na kukata matumizi yote mabaya ikiwa ni pamoja na ukubwa wa serikali, na mengine mengi ambayo yako wazi kabisa ukisoma sera za chama.

Tatizo lenu mnashindwa kuelewa kwamba Chadema wapo ktk hatua za awali nazo ni kupigana vita hii na silaha pekee inayoweza kuwashinda CCM ni UMOJA wetu kuunda jeshi lenye nguvu ktk kupambana nao hakuna yakhe yakhe na kulemba maneno.

CCM hawatatumia sera au ilani kupambana na chama chochote kile isipokuwa ni nguvu ya ushawishi ambayo inatokana na wagombea wenye uwezo wa kuuza, kubomoa na kutingisha mpinzani ktk jukwaa la siasa. Hivyo tunahitaji majemedali wazuri wanaojua strategy ya kivita na sio kutumia dialogy hali CCM wamebeba silaha kali.
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,512
2,000
Kwa mazingira ya kisiasa tuliomo CHADEMA wako sahihi kuwapokea "makapi" haya ya CCM. Hii ndio namna moja ya kuipasua CCM ili hatua nyingine zifuate. CCM isipopasuka upinzani wa kweli nchi hii ni ndoto. Tatizo bado liko kwenye vyombo vyetu vya DOLA. Bado vinafanyakazi kwa staili ileile ya mwaka 1995 Mrema alipoondoka CCM.
 
Nungunungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2007
312
195
Walifuata ubunge NCCR ya Mrema baadae wakarudi CCM:

1. Stephen Wasira
2. Paul Ndobo
3.
 
Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,536
2,000
hapana mkuu ni wewe hufahamu Chadema wamelenga kitu gani. Nitarudia kusema hivi wengi wenu hapa mnafikiria kwa kujiuza kwamba haya mapambano yana demokrasia ndani yake.. Mkuu wangu hakuna demokrasia hapa vitani, ni kama vile watu mlioko vitani. Unabeba silaha na yeyote anayejiunga nanyi kupiganana adui mnampa silaha na kumweka msitari wa mbele wa wapiganaji...Mgeni siku ya kwanza mpe jembe akalime.

Kama kungekuwepo na demokrasia labda hapo tungezungumzia kuuza sera na ilani na hapo ndipo maswali yenu yalihitaji majibu mnayoyataka, lakini kwa Chadema sasa hivi hii ni vita. Vita baridi ya kurudisha hadhi ya Tanzania kama taifa huru lisilotawaliwa na watu wachache wanaojiona wao ni untouchables.

Hivyo nguvu kubwa imewekwa ktk kupigana vita hii kwanza na principles zilizopo ni za ushindi wa vita. Kisha baada ya vita Chadema watahakikisha Ufisadi unakoma, Uhuru wa nchi hii unarudishwa mikononi mwa wananchi wenyewe na kukata matumizi yote mabaya ikiwa ni pamoja na ukubwa wa serikali, na mengine mengi ambayo yako wazi kabisa ukisoma sera za chama.

Tatizo lenu mnashindwa kuelewa kwamba Chadema wapo ktk hatua za awali nazo ni kupigana vita hii na silaha pekee inayoweza kuwashinda CCM ni UMOJA wetu kuunda jeshi lenye nguvu ktk kupambana nao hakuna yakhe yakhe na kulemba maneno.

CCM hawatatumia sera au ilani kupambana na chama chochote kile isipokuwa ni nguvu ya ushawishi ambayo inatokana na wagombea wenye uwezo wa kuuza, kubomoa na kutingisha mpinzani ktk jukwaa la siasa. Hivyo tunahitaji majemedali wazuri wanaojua strategy ya kivita na sio kutumia dialogy hali CCM wamebeba silaha kali.

Mkandara,

5 years later, Chadema wamepata Atomic bomb,,,will they use it or now contemplate morality of using the atomic bomb?
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
10,600
2,000
Rev. Kishoka - You warned about this mess five years ago and it is still valid but it seems that "CHADEMA owners" don't see it that way. For the last five years, Shibuda had been a heavy burden for CHADEMA, thanks he was powerless within the party. The advent of Lowassa and his former CCM cronies at the helm of CHADEMA means a lot of uncertainty to the future direction of CHADEMA. I am afraid that unless for sure it acquires the majority status in the Bunge, and occupies the Magogoni castle, it is likely to disintegrate into tiny fragments immediately after the election.
 
Last edited by a moderator:

Azimio Jipya

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
3,364
1,195
The Hypnotic Force of EL, what about that moment when he pulls off his mask .. OMG!!

No one will come near him. No one will alter a word from this power monger ... OMG, .. CDM what got in your gray matter ... ! But wait, theres a good side out of all this.

You look in all those pictures when everybody is near this "incarnate" you read the body language .. all of them seems to tremble with yes sir, .. anything you say sir!

What was early known as CDM is no longer their ... completely and totally compromised .. by the evil incarnation ..

No more the innocent CDM but the Dark-side of CCM grouping UP.

As it was long time predicted; now we have two of them. One belonging to Magufuli and this new one Belonging to the Hypnotic Power Monger Creatures.

I have a predication to make: Just a simple prediction. The Pressure and hell intimidation from newly formed CCM will make Magufuli and associates reform whether they like it or not. This will be like bringing the second innocence of this nation. AND honestly that is the good side of the CDM yielding to those ... and "political power shuffling" at the present.
 
Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,486
2,000
Mkandara,

5 years later, Chadema wamepata Atomic bomb,,,will they use it or now contemplate morality of using the atomic bomb?
Dah mkuu kweli kabisa miaka mitano ilopita niliipenda sana Chadema na watu tulowategemea walikuwa kundi la kina Sitta walopingana na Mtandao lakini safari hii imetisha wameupokea Mtandao wenyewe kama vile Marekani kuwapa ISIS silaha dhidi ya Assad kumbe ndio kutafuta makubwa zaidi.. Mkuu nakubali kabisa yalikuwa makosa mwaka 2010 na yameendelea kuwa makosa. Unajua tena, Ukipenda sana huoni chongo!!...
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
10,600
2,000
Mazee,

Either chama kina principles au hakina principles, hakuna habari za wakati wake wala nini.

Na CHADEMA so far wanajionyesha hawana principles, na kama hawana principles katika upinzani, nini kitatufanya tuamini kwamba watakuwa na principles wakipata serikali ?

Nadhani sasa hivi kuna ushahidi wa kutosha kuwa CHADEMA haina principles, kwa hiyo jiulize tena kama wakipewa serikali itakuwaje.

Umma ndio una uamuzi wa nani aongoze serikali; iwapo tuna umma unaoangalia principles basi hakuna wasiwasi mambo yatajijibu, ila iwapo tuna umma usiojua maana ya principles bali ubwabwa, khanga na kofia basi ndiyo imetoka hivyo! Kumbuka kuwa Wenyeviti wengi wa CCM waliotokana na uchaguzi wa 2012 walichaguliwa kwa mtindo wa ubwabwa, khanga na kofia na ndio hao wako likely kuhamia CHADEMA pamoja na Lowassa, kwa hiyo majibu yako wazi.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
21,067

..wananchi wamepigika kwa umasikini, ujinga, na maradhi, hawaangalii tena kama chama kinasimamia principles au la.

..hoja iliyopo mbele yetu ni kama tunataka kuendelea na Ccm na mfumo huu uliopo au tunataka mabadiliko.
 
Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761

Wengine hawaishii kwenye hoja ya mabadiliko pekee bali wanaenda mbele zaidi na kujiuliza, mabadiliko ya aina gani?

Hata kufanya uchaguzi ni mabadiliko achilia mbali kuiondoa CCM madarakani.

Kwa sasa linatumika neno mabadiliko wholeheartedly kuficha madhaifu ya hoja ya msingi ndani ya vyama vya upinzani.
 
Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
4,969

Jokakuu;

Naona mkuu umeingiza ushabiki wa mpira. Huko tayari kulazimisha goli.
 
Mapendekezo ya katiba ya mwanzo yagetoa mabadiliko. Lakini CCM hawakutaka kujifunga magoli ya kisigino. Wameichelewesha.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
21,067
2,000
Wengine hawaishii kwenye hoja ya mabadiliko pekee bali wanaenda mbele zaidi na kujiuliza, mabadiliko ya aina gani?

Hata kufanya uchaguzi ni mabadiliko achilia mbali kuiondoa CCM madarakani.

Kwa sasa linatumika neno mabadiliko wholeheartedly kuficha madhaifu ya hoja ya msingi ndani ya vyama vya upinzani.

..mimi sijamkataza mtu kupanua fikra zake kuhusu mabadiliko wanayoyataka.

..i actually tried to make the choices more clearerto kwamba, mabadiliko yatapatikana kwa kuchagua ccm, au yatapatikana kwa kuchagua ukawa/cdm?
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
21,067
2,000
Jokakuu;

Naona mkuu umeingiza ushabiki wa mpira. Huko tayari kulazimisha goli.

..LOL!!

..i am just trying to be realistic here.

..tuseme ccm wana principles. Wao ni chama cha ujamaa na kujitegemea. Sasa tujiulize kama uchaguzi uliopita walishinda kwasababu wapiga kura wanaamini kwamba Ccm inasimamia principles za Ujamaa na Kujitegemea.

..lakini vilevile tuna choices mbili mbele yetu. YES, tunataka mabadiliko lakini kati ya ccm na ukawa chama kipi ni more likely kutupatia mabadiliko tunayoyataka?

..kwa mfano: mpiga kura anayetaka serikali 3 ajiulize chances za mabadiliko hayo kama atapigia ccm au ukawa.

..vilevile anayepiga vita rushwa ajiulize kama vita dhidi ya rushwa itakuwa na mafanikio akichagua ccm au ukawa.

..kwenye umasikini napo ni hivyo hivyo. Siyo kama ccm haifanyi kazi, ila ni kama umasikini unapigwa vita kwa kasi ya kutosha. Sasa wanaotaka mabadiliko kwenye suala la umasikini waamue kama wameridhika na ccm au wajaribu kwa ukawa.

Cc Nguruvi3, Mag3
 
Last edited by a moderator:

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
Mapendekezo ya katiba ya mwanzo yagetoa mabadiliko. Lakini CCM hawakutaka kujifunga magoli ya kisigino. Wameichelewesha.
You are absolutely right!

Kwa kumpitisha Lowassa kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA, hoja ya Katiba Mpya itakuwa kimantiki ni kaput. Hana tena moral authority ya kusimama na kusema hakubaliani na Katiba Inayopendekezwa kwa sababu alikuwa ni mmoja wa wajumbe waliokuwa wanaitetea ndani ya bunge akifahamu itakuja kumsaidia katika utawala wake.

Mzee Butiku alishawahi kumzodoa Lowassa kuhusu hoja ya serikali tatu katika thread hii,
Ambapo alisema katika kipande hiki,
Aliyefunguka na kutoa ya moyoni leo hii si mwingine ni bali ni mwenyekiti wa kigoda cha mwalimu Foundation, MZEE WETU Butiku, ambaye amewataja mapapa yanayotaka mchako wa katiba uwanufaishe maslahi yao huku wananchi walio wengi matatizo yao yakiacha solemba,

Amewataja viongozi hao ambao wamekuwa na ushawishi mkubwa katika vyama vyao kuwa ni pamoja na Mbunge wa Monduli kupitia chama cha CCM, Mh. Edward Lowassa, pamoja na Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF, na kusema kuwa watu hao wasipobadilika hatima ya serikali tatu hapa nchini ni ndoto.

Butiku ameenda mbali na kusema, inashangaza kuona watu hao ambao wanaushawishi mkubwa sana, wameamua kulivalia njuga suala la serikali mbili huku wao wenyewe wakishindwa kutoa hoja za msingi na badala yake wanatumia watu wanaowaongoza kutumbukiza hoja zao ambazo zinawanufaisha wenyewe.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom