CHADEMA: Ole wenu mkiipokea Mizoga ya CCM! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA: Ole wenu mkiipokea Mizoga ya CCM!

Discussion in 'Great Thinkers' started by Rev. Kishoka, Aug 15, 2010.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  CCM wameshaamua nani watawawakilisha kwenye Ubunge, wamechuja chuya, wametupa makapi na mizoga.

  Sasa natoa tahadhari kwa CHADEMA; Ole wenu mkiipokea hii mizoga ya CCM na kuipa kadi na hata kuwafanya wagombea wenu kwenye majimbo, mtajishushia hadhi na kuonekana chama kisicho na maana na ni hifadhi ya mizoga na makapi.

  Jiulizeni kwa nini hawa mizoga, makapi na pumba kwa nini walisubiri kuenguliwa na CCM ndipo wakakimblia kwenu? Kwa nini tangu awali hawakufanya uamuzi wa kuhamia CHADEMA kabla ya kushindwa ndani ya CCM na hivyo baada ya kutalikiwa wanakuja kwenu nanyi mnawapa Ufestiledi kwenye majimbo?
   
 2. Mchizi

  Mchizi JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2010
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 675
  Likes Received: 847
  Trophy Points: 180
  Kwanza ni lazima ufahamu si watu wote waliopo ndani ya CCM si safi.Kuna watu safi na wenye uchungu na nchi pengine kuliko hata waliopo ndani ya upinzani.Hivyo kama kuna mtu safi ambaye hakupita kwenye kura za maoni za CCM ,pengine kwa mizengwe sioni kwa nini asipokelewe CHADEMA kama lengo ni kupigania maendeleo ya nchi.CHADEMA inawahitaji watu hawa kwa vile watakuwa na mchango mkubwa kuliko unavyodhani.
   
 3. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135

  Si wote walioachwa ni mizoga maana mshindi lazima awe mmoja. Unaweza ukawa na wagombea 10 wote ni wazuri lakini kwa vile mgombea lazima awe mmoja haina mana kuwa wale waliochwa wote hawafai. Kumbuka pia CCM ni chama cha mafisadi kwahiyo wengine wanaweza kuwa wameachwa kwa kuwa wako kinyume na maslahi ya wanamtandao wanaojinufaisha wao wenyewe bila kujali maisha ya watanzania kwa ujumla.
   
 4. M

  Machamle Member

  #4
  Aug 15, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kila mtu atahukumiwa alivyo na kwa aliyoyafanya; hivyo waacheni chadema nao wachambue huenda ndani kuna almasi iliyofichika.
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kama ni wasafi na sizoga, kwanini walisubiri hadi watoswe???

  Nafsi na nadhiri ni muhimu sana, as far as i am concerned, hawa ni mizoga tu, if they were clean, they would have left before conclusion of primaries and nominations
   
 6. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  chonde chonde waheshimiwa

  Waliotupwa wote si mizoga. Dr. Slaa alitupwa na CCM ndipo akaondoka na kwenda Chadema.
  Tukubaliane kuwa ndani ya CCM ni fedha inayotakiwa si mtu. Na sasa imeonekana kuwa ni ruksa kucheza rafu za raushwa wakati wa kura za maoni, maana NEC haina muda wa kupitia rufaa za watu. Mimi nawashauri walioachwa waende Chadema.
   
 7. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,068
  Likes Received: 4,000
  Trophy Points: 280
  Mkuu siasa ni comprimize we need Raila's caliber to excell on our change agenda! tusibague watu kisa hawakufanya maamuzi kwa wakati muafaka!
   
 8. k

  kibebii Member

  #8
  Aug 15, 2010
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 80
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  ukipenda chongo unaita kengeza !!!
   
 9. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2010
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,722
  Likes Received: 1,213
  Trophy Points: 280
  Hivi si wewe mchungaji Kishoka uliyekuwa na mpango wa kuanzisha chama cha siasa?

  Wanachama wako ungewatoa mbinguni?
   
 10. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,062
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa vipi katokea wapi unafikiri kushindwa kwenye kura za maoni ndiyo kutofaa, mfano msindi kapata kura 14,000 anayemfuata kapata 10,000 kwa hiyo wa pili ni mzoga, basi wewe ndiye mzoga kabisa huna lolote, ina maana wewe darasani toka la kwanza ulikuwa unakuwa wa kwanza tu ukiwa wa pili ni mzoga, naona akili zako hazina akili kabisa wewe endelea kukaa huko huko Canada tuachie sisi na nchi yetu.
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nimeipenda hii mkuu, je why did they wait until watoswe rasmi??? and then waje kuwareplace akina regia and rachel and many more committed chadema young blood?? if they are really for change and if they love their country five year from now is not too much to wait considering that we have had more than fourty years after independency, waje chadema lakini wasigombee... CHADEMA SHOUDL NOT BE A CONDUIT FOR POLITICAL BITHCES

  you are one of the people
   
 12. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #12
  Aug 15, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kama kweli hawa mizoga ni wana mapinduzi nani wapiganaji, kwa nini walishindwa kuona alama za nyakati mapema na wakajitoa huko CCM? Kwa miaka mingi tumekuwa tukiuelezea uozo wa CCM. Miaka hii mitatu ya mwisho imekuwa ni wazi kuhusu uozo wa CCM< kwa nini basi hawa hawakujitoa mapema CCM na si kusubiri watemwe na CCM, ndipowaanze kukimbilia kwingine wakidai wana uzalendo na nia ya kuleta mapinduzi? Je ni mara ngapi tumekuwa tukiimba kuwa CCM ni chama kilichokosa mwelekeo? Je wao wamelivumbua hili baada ya kuswekwa ndani na TAKUKURU, kushindwa kura za maoni au kutemwa na NEC?

  Nikianzisha chama sitakimbilia kuwapa madaraka mateka au uwakilishi, na kawme sitapokea mateka, mizoga au makapi miezi miwili kabla ya uchaguzi.

  Kama kweli una nia, jiunge Januari ya 2011 iwe ni CHADEMA, CUF, TLP au DP lakin si leo Jumapili baada ya kupigwa panga na CCM.
   
 13. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #13
  Aug 15, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mkiikimbilia hii mizoga na kuifanya wagombea wenu, mnautangazia umma kuwa nyie bado hamna uwezo wa kujijenga na kuongoza Tanzania! Mnasubiri makapi na pumba visalie mziokote mjitape kuwa mmepata lulu!
   
 14. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #14
  Aug 15, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,062
  Trophy Points: 280
  Hivi mizoga kwako ina maana gani, ukibaki CCM si mzoga ukitoka mzoga, Bilal alikuwa wa pili kwa Shein ina maana Kikwete alibeba mzoga na anatembea na mzoga wa Bilal, i think your reasoning capacity is limited.
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Aug 15, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Rev. Kishoka,
  Mkuu mimi nakubaliana na wewe kama hoja ni kupewa majimbo hawa jamaa ya kugombea uchaguzi huu....Lakini nadhani kupokelewa kama wanachama wapya inaruhusiwa sana tu na inaongeza sura ya chama Chadema..
  Hoja ni hawa watu kusimama kugombea majimbo au uongozi wa chama ndio waisipewe hadi watakapo weza kukaa kwa muda ndani ya chama. Kwa vile uchaguzi wetu ni miaka mitano mitano basi next uchaguzi wakiwa bado wamebakia Chadema watapewa nafasi ya kugombea lakini sio sasa hivi..

  Ila nakubaliana na mawazo ya kwamba kwa kila mwana CCM kuhesabika kahamia Chadema inaongeza nguvu ya chama sii lazima wagombee uongozi lakini kuikubali Chadema na sera zake ni mwanzo mpya wa kuvutia wananchi.
   
 16. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #16
  Aug 15, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mchungaji;

  1. Tunae Dr slaa .... He was a reject! ...But Now see!!?

  2. Kuna makundi mawili ya hao reject. a. Realy apportunist b. Real character kama Dr slaa vile!

  3. Wale safi wamehukumiwa kwa Credibility na Nobility zao .... CHADEMA Pls .. dont reject this ones!!
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Aug 15, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  THANKS REV

  post number 11 tells it all, kama wana uoendo na nchi, wasubiri five years from now... one can not transform in 3 weeks to know sera za chama, watu wake culture yao na pia kuwawakilisha kwenye uchaguzi

  down with political prostitutes
   
 18. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #18
  Aug 15, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Bunge lilivunjwa rasmi mwisoni mwa mwezi Juni. Tunajua ndani ya vikao vya CCM kalaya Juni 2010, kila kilicholeta maana kwa Tanzania kilipigwa ngwara na maslahi ya CCM yakawekwa mbele ikiwa ni pamoja na Ufisadi na kuwalinda mafisadi.

  Kwa nini hawa makapi hawakukihama chama ikiwa wanafahamu wazi tangu kile kikao cha Butiama mwaka jana au mwaka juzi ni tayari CCM afisadi walikuwa wameshika hatamu na kudhaminiwa na Mwenyekiti?

  Upuuzi wa CCM ni wao, wakipokea mizoga na mateka ni wao, omyo hili ni kwa CHADEMA, CUF na hata wengine. Kwa nini mkimbilie kudai na kufananisha upuuzi wa Bilali kukubali ugombea wenza na lile la tuseme Seleli sasa kuhamia CHadema na kuwa mgombea wa CHadema? Kwani Seleli hakujua tangu alipovaa vazi la kipiganaji kuwa alikuwa anapigana vita asiyo na uwezo ndani ya CCM? Kwa nini aling'ang'ania kubakia CCM?
   
 19. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #19
  Aug 15, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Azimio,

  If we have people with crediility and nobility, why are they clinging to CCM a rotten party which everyone knows will never reform?
   
 20. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #20
  Aug 15, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Mheshimiwa Baba Mchungaji

  Nadhani umepitiwa tu kuwaita mizoga hao watu wanaotarajia kuhama. Kubali yaishe, tuendelee na hoja nyingine.
  Watahadharishe Chadema wawe waangalifu kabla hawajamkubali mtu yeyote anayekimbia kutoka CCM.
   
Loading...