Sikutegemea,nilijua angebabaika,angetetemeka na kumung'unyamung'unya maneno wakati wa kusoma sehemu ya Rasimu ya Katiba inayohusu muundo wa muungano.Hakutetereka wala kusita,alikiutaja mbuyu moja kwa moja bila kuuzunguka,alisema maoni na matakwa ya wananchi kuhusu muundo wa muungano kuwa ni serikali 3!!
Na wao walijua angesita na kulinda maslahi ya chama,wakapigwa na bumbuwazi kuona mzee akiusema ukweli bila kumtizama mtu usoni kwa haya,alikuwa mkavu,uso wa mbuzi. Aliwapa makavu laivu.
Mzee Warioba alinikonga sana aisee,alinifanya nielewe maana ya kuwa Mzee mwenye hekima.Nilielewa kua mzee mwenye hekima ni yule tu ambaye anapaswa kuumia anapogundua kuwa UKWELI hausemwi kama unavyotakiwa,hivyo,anajitahidi kutumia fursa yoyote ili auseme UKWELI kabla hajatwaliwa na kifo.Mzee mwenye hekima na busara ni yule anayejua kuwa yeye ni hazina na rejea ya mambo ya msingi kwa jamii yake na yupo tayari kusema ukweli wakati wowote.Mzee mwenye hekima na busara anatambua kuwa hana maisha ya kupoteza hapo baadae.
Kama Nyerere,Warioba amenifanya nizidi kumuomba Mungu anifikishe uzeeni nikiwa na ujasiri na mwenye kutegemeka na jamii yangu.
CCM msimchukie mzee huyu,ila mjifunze kutoka kwake