CHADEMA ndani ya Domo la Chatu Siku ya Wanawake Kitaifa-Arusha

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,411
Nawasalimu ndugu Watanganyika,

Hiyo Leo 8-3-2023 zitapigwa picha na video za kuombea mikopo kuwa Rais TZ ana practice Fair Democracy kwa kufungua Mkutano wa Women Wing Council ya Chama Kikuu cha Upinzani.

Risala zitasomwa na zitajibiwa kwa hotuba na maneno mazuri lakini kiukweli behind hiyo Sinema hamna Demokrasia. Covid 19 wataendelea, Mauaji ya Polisi palepale na Katiba Mpya hakuna.

Rais anawaambia watu wake wapige kazi na kujiamini wasisingizie Maagizo kutoka Juu halafu gapo hapo anaagiza kesi zifutwe.

Kuna tofauti kubwa. Zamani walikuwa strong na sasa kwa kiasi fulani kuna kulainika.Ilikuwa likitoka azimio au tamko basi nchi nzima italipuka kwa furaha na kulikubali. Kwa sasa wanachama na wafuasi wanahoji, wanagawanyika na kuwa na mashaka mashaka.

Wale wengine si wajinga. Mbinu waliyotumia wanajua inafanya kazi sasa. Mpe mtu njaa alegee kisha msogezee chakula tena japo ni haki yake lakini matumaini mapya ya uhai na shibe huleta malevya ya vitendo na fikra hufifia.

Hata Kiongozi Shupavu na imara si yule yule wa kabla ya kushikiliwa na baada ya kuachiliwa magerezani. Labda tu matumaini yapo kwa sababu alikuwa akila chakula cha nyumbani ila wale watu si wema kwa mbinu chafu za madhara yasiyoonekana mara moja.

Hivi vikao vya mtu mmoja mmoja, maamuzi ya papo kwa papo,Misimamo juu ya mazungumzo yasiyoisha wala kujulikana hatima imekuwa chanzo cha malalamiko.

Anyway bila kusema hawawezi kujua mixed feelings zilizopo,acha yasemwe ili yatafakariwe.

Ruzuku ni haki yao! Ni uamuzi sahihi tu kuzichukua kuwasaidia kuendesha chama kuliko kuhangaika kiuchumi kwani ni haki yao na jasho lao.

Kuziacha ingekuwa ni kuwaachi fisi mfupa wazitumie tena kuwaumiza wao wenye fedha huku mabaki wakiyatumia kwa kufuru kununua magari ya fahari, kulipana posho na nyingine kuzihamishia China.

Jambo la hatari ni fikra yoyote juu ya wale waasi 19 [Covid ]kwa kisingizio cha maridhiano.

Fikra au attempt yoyote ya kukubali yaishe italeta mpasuko usiotarajiwa. Itawavunja miyo wanawake wote wapambanaji na waaminifu kwa chama. Italeta nguvu juu ya mashaka ya jambo lenyewe likivyotokea au hisia kuwa ilikuwa ni inside job.

Jeuri, dharau na kiburi vilivyoonyeshwa na waasi halafu washinde vita hiyo itakidharaulisha chama na kuua credibilities zake completely.

Kwa kifupi wajaribu waone kwani fundisho la mfano lipo kwa Prof. Lipumba alibaki na chama jina tu bila wanachama kutoka kwenye chama kikuu cha upinzani nchini.

Ni vema kujifunza na si lazima wote kupitia njia inayofanana ila wote mnaweza kujikuta mnaishia destination inayofanana. Haya maneno si matamu masikioni ila ndiyo ukweli.

Mtego mkubwa huo, vita Haijaisha ila inapiganwa kwa mbinu nyingine.

CUF Chali.
NCCR Taabani.

Sasa ni zamu ya CHADEMA ila kwa utaalamu na tahadhari kubwa ili wajiue wenyewe.

Unakuja mfupa wa marekebisho ya Katiba (Minimum Reforms) hasa kwenye Tume ya Uchaguzi ambako kila mwenye tamaa ya Ubunge atahisi kushinda na kuonja mema na neema za Ubunge.

Hapo tena haitakuwa fight ya Chama wala ya Wananchi bali itakuwa fight ya maslahi binafsi.

Kwani hata wakipatikana Wabunge 30-50 unadhani CCM wanajali? Wanajua watapunguza kelele ila hakuna kitakachobadilika.

Ikiisha term hiyo ndiyo basi tena akina Mbowe wanakuwa kwenye kuitafuta Seventy, Wakina Dr. Slaa watakuwa past eighty's na no one will be able to fight again.

Mapambano yanaanza upya kupata akina Lissu wapya ambayo si kazi ndogo. Uviko-19 na Double Standards kwenye sheria hiyo hiyo moja.

Bunge lilipopokea barua ya kuondolewa uanachama Wabunge wa CUF liliwavua Ubunge haraka japo na wao walikuwa wameenda mahakamani pia.

Walisubiri maamuzi ya mahakama wakiwa nje ya Bunge,Sasa kwanini akina Uviko 19 wasubiri wakiwa Bungeni?

Sabaya kakata rufaa lakini anasikilizia rufaa yake akiwa anatumikia kifungo...Rufaa haitengui maamuzi ya awali kabla ya hukumu.

Wale Wabunge wa CUF hukumu imekuja kutoka baadaye sana kuwa waliondolewa isivyo halali na kwamba walipotezewa muda wao na maslahi ya miaka kama miwili maana hata kipindi chao cha Ubunge kilishamalizika!

Na hivyo wanastahili kulipwa stahiki zao ama wafungue madai.

Sasa tujiulize hawa Uviko-19 hukumu ikitoka kuwa walivuliwa Uanachama kihalali toka chama chao kilipoliarifu Bunge. Je, watatiwa hatiani na kutakiwa kurejesha mabilioni ya walipakodi ambayo wamejipatia isivyo halali kwa kipindi wakiwa ni wabunge haramu?

Mahakama za Bongo kweli nazo uwepo wake ni mashaka ndiyo maana zinapokea maagizo kutoka juu kufuta kesi za kubambika za wanasiasa wakati zipo nyingi za kubambikizwa Wafanyabiashara na Wananchi walalahoi hazifutwi.

Kesi ya Covid-19 haikupaswa kusikilizwa for more than 2 weeks. Mianya kwenye taratibu mbovu inatumika vibaya ili kufanya uendeshaji wa kesi Tanzania ni kama kupanda Mbuyu na kusubiri kuvuna ubuyu wenyewe.

#Mengi tutayaona, ila kwa ujumla vijana CHADEMA wameanza kumchoka mbowe aliyelegea na mwenye kauli tata#
 
Hao wanawake hawawezi kurudishwa Chadema kirahisi kama wengi wanavyodhani, zile zilikuwa ni mfululizo wa propaganda toka lumumba tu.

Zilianzia pale ambapo ilithibitika Chadema wameanza kupoekea ruzuku, kama vile kufanya hivyo lilikuwa ni kosa kwao, wakati wanajua kabisa hayo ni matokeo ya maridhiano, wanafiki wale kwao maridhiano yaguse pote pengine isipokuwa kwenye ruzuku tu!.

Baadae propaganda zikaongezwa pale ilipofahamika Rais Samia mgeni rasmi wa siku ya wanawake duniani, itakayoadhimishwa na BAWACHA, baada ya Mbowe kutangaza, hapa ndipo kelele za covid 19 zikaibuliwa.

Baadae tena baada ya wakina Kibatala na wenzake kuiambia mahakama hawana haja ya kuendelea kuwahoji kina Mdee na wenzake, hapo kelele zikazidi kuongezwa, eti kwamba Samia na Mbowe wamekubaliana kwenye maridhiano wale wanawake 19 wasamehewe!.

Hayo matukio tajwa hapo juu, ukiyatazama kwa umakini, utaona yote yanajitegemea, hakuna tukio linalohusisha hatua zilizochukuliwa ndani ya chama, zikajadiliwa kwenye maridhiano, wanachokosea wengi hawajui Chadema ndio iliwaadhibu wale wanawake 19, pale hakuna ushirikiano wowote na serikali ya CCM.

Maridhiano yanahusu matendo yale ambayo Chadema kama taasisi, iliumizwa na matendo ya CCM na serikali yake, kama kuzuia mikutano ya kisiasa, kuumizwa watendaji wa chama, kufungwa kwa kubambikiwa kesi za uongo, utekaji [ Ben], mauaji [Mawazo].

Binafsi siioni njia ya mkato ya wale wanawake kurudi Chadema, ni lazima waombe radhi public, kwa wafuasi na wanachama wote wa Chadema duniani, lakini sio kurudishana chamani kimya kimya kwa kisingizio cha maridhiano, huu utapeli hauwezi kukubalika kamwe.
 
ambo la hatari ni fikra yoyote juu ya wale waasi 19 kwa kisingizio cha maridhiano.

Fikra au attempt yoyote ya kukubali yaishe italeta mpasuko usiotarajiwa!

Itawavunja miyo wanawake wote wapambanaji na waaminifu kwa chama!
Yooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooote hapa tuko pamoja. Wasifanye kosa hili! Ngoja nimtahadharishe Erythrocyte , never do that mistake! Acha kesi yao iishe, then huko mbele mtaagalia repentance yao ikoje! Kutbu na kusamehe siyo sasa! italeta mgawanyiko mkubwa.
 
Yooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooote hapa tuko pamoja. Wasifanye kosa hili! Ngoja nimtahadharishe Erythrocyte , never do that mistake! Acha kesi yao iishe, then huko mbele mtaagalia repentance yao ikoje! Kutbu na kusamehe siyo sasa! italeta mgawanyiko mkubwa.
Wewe utafanya nini? Zaidi utaishia kusonya tu na kubadili gia

Mbowe ashajua huko chadema anaendesha majuha
 
Yooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooote hapa tuko pamoja. Wasifanye kosa hili! Ngoja nimtahadharishe Erythrocyte , never do that mistake! Acha kesi yao iishe, then huko mbele mtaagalia repentance yao ikoje! Kutbu na kusamehe siyo sasa! italeta mgawanyiko mkubwa.
Watu mnahangaika sana bila kuwa na ukweli wa jambo lililopo mezani.
 
Watu mnahangaika sana bila kuwa na ukweli wa jambo lililopo mezani.
We are trying to predict the probable consequences na hiyo si mbaya! Ni tahadhali tu! Mimi ni muumini wa chadema sana ndiyo maana najibu vinginevyo you just skip the thread!
 
Hakika CHADEMA wakifanya hili kosa itakuwa wamejipiga risasi wenyewe mguuni.
Yooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooote hapa tuko pamoja. Wasifanye kosa hili! Ngoja nimtahadharishe Erythrocyte , never do that mistake! Acha kesi yao iishe, then huko mbele mtaagalia repentance yao ikoje! Kutbu na kusamehe siyo sasa! italeta mgawanyiko mkubwa.
 
Back
Top Bottom