CHADEMA na CUF walazimika kuomba msamaha Bungeni

CHADEMA na CUF walazimika kuomba msamaha Bungeni

Kufuatia msimamo wa Wenje kukataa kufuta kauli yake jana, baada ya kuhituhumu CUF kuwa ina hafiki masuala ya kishoga na usagaji kutokana na kuwa mwanachama wa jumuiya ya kiliberali, leo CHADEMA imekiri kuwa imekidhalilisha chama hicho na imeomba radhi.

My take;

CHADEMA imekusudia kupeleka siasa za maji taka bungeni, na hili lina dhihirishwa na hotuba kadhaa zilizo somwa na wabunge wa CHADEMA.

Tukija kuangalia uhalisia wa CUF kuwa mjumbe wa Liberal, ni kama vile Tanzania kuwa nchi mwanachama wa jumuiya ya madola, jumuiya ya madola ina zitambua haki za mashoga na usagaji, je, Tanzania tuna zitambua?

Ni akili finyu ya viongozi wa kambi ya upinzani ikiongozwa na CHADEMA kwa kushindwa kwake kuchambua mambo madogo madogo kama haya, na kupelekea vurugu zisizo na lazima bungeni, na kulitia taifa hasara.

Nakiri kusema CHADEMA ni janga la bunge,janga la siasa na ni janga la taifa.
Kuomba radhi hakumaanishi kuwa kuna siasa za maji taka kwani maji unayosema yanafanywa na Lipumba na CUF kutaka ninyi muoane Cuf walihudhuria mkutano wa kutambua haki za mashoga je ulishasikia kiongozi wa Cuf akiwapinga maliberali kwenye mkutano?We mwendawazimu kweli huna kumbukumbu kwamba CUF ni chama cha magaidi kwa mujibu wa Mahita?
 
Ujumbe umeshafika, asante sana Wenje na Mohamed Rashid kwa kutupa hii nondo,ya "Haki sawa kwa Wote"
 
Hawa jamaa CUF kwa mambo haramu wapo: Walaji na wauzaji mirungi -Haki sawa, ushoga-haki sawa....
 
Kumbe na CHADEMA nao pia ni wanachama wa ushoga eeeh!
 
Acha nikapate ugali samaki maana badala ya kutujulisha kinachoendelea sisi ambao hatuangalii Bunge naona mnaleta story za vijiwe vya kahawa!
 
kwanini hawakutolewa nje ya kikao kama kawaida wapishe wenje awasilishe hotuba yake ,badala yake waombwe radhi .hii inatupa tafsiri gani kwa mh.spika anapendelea vyama fulani au ni msimamo yake tu kisiasa
 
Sasa nimeshapata sababu ya kutoliangali bunge letu tena!
 
kwanini hawakutolewa nje ya kikao kama kawaida wapishe wenje awasilishe hotuba yake ,badala yake waombwe radhi .hii inatupa tafsiri gani kwa mh.spika anapendelea vyama fulani au ni msimamo yake tu kisiasa

Kwani hujui Naibu Spika nae mliberali
 
washindi wote wawili ( CDM na CUF) hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Bunge halijasema kuwa CDM wameongea uongo,ila walichoongea kimeawadhalilisha CUF.Lakini Bongo hata kusema Albino siku hizi si kosa,unatakiwa useme mlemavu wa ngozi.Hata Chumvi hutakiwi iita chumvi usiku ila "dawa ya mboga".Sasa CUF wakapata aibu ...."pengine wenye alipaswa kuwauliza CUF waseme vyema HAKI SAWA NA NA KAULI MBIU YA UMOJA WA MALIBERAL DUNIANI"

Kwa hiyo ni wazi CUF wanayokazi kwa waumini na wazanzibar..Km walipewa moyo na mabasha ili waendelee wafaidi wenzao huko pwani.Sasa wataumbuka wengi tuu.
 
chiligati anajenga scene ya kulazimisha ngoma kuwa draw,na kuwafanya CDM guilty km watakataa hilo.Lakini CUF hawajatangaza rasmi kuwa wanaungana na Tanzania ktk kukataa ushoga.Wakati wanasema haki sawa.NI vipi waseme kuwa si yote,wakati chama chenyewe kinasema kuwa kina muunganiko na watu wenye mission hiyo duniani.
........
Lakin ihakuna kosa..CUF wajitete kwani ule mtandao kila mtu atautembelea.
.......

This is crazy...CCM waliwahi waweka CDM ktk uongo ,kwa kusema kuwa wanapokea hela kwa Cameron.Huku ni kuwapa kichwa CUF.Ingawa najua hilo halitoita bure.
........

wametoa sauti ktk hotuba ya mbowe.

.......

sasa CCM wantaka ku capitalize haya na kujenga hisia kuwa CDM wamekosea.
tayari ndugai anachombeza kuwa is vyema kuweka kipengele cha kuwakwaza wengine.Mtu anakwazwa vipi na sifa zake.

.....

Mbowe kaweka wazi,kuwa ni umoja wa kitaifa tuu..ila kaweka wazi kuwa kuwa kutoa majeshi ni shemu ya mikakati pia.

....

Hao jamaa CUF kwani nani hajui ukanda wanaotoka ndipo abia za kishoga na ubasha ndio sifa zao.

.....


Siamini kuwa eti kwa sababu Conservative ya Cameroon wanaafiki ushoga na kuupigia debe na ni chama rafiki na CDM basi nawao CDM ni sawa na Conservative cha UK vile vile siamini CDM kuwa na uhusiano na Christian Democratic Union cha ujerumani basi na CDM ni chama cha kikristo! Vile vile siamini kuwa kwakuwa Tanzania ni wanachama wa jumuiya ya madola nchi zenye kupigania haki za mashoga nyingi zimo kwenye jumuiya hiyo kunaifanya Tanzania kuwa nchi inayopigania haki za mashoga unless and only I was stunted when I was under 5 years and my brain stunted too!


Mnadhimu wa CUF kwa niaba ya CUF na Mh Freeman Mbowe kwa niaba ya CHADEMA wameombana radhi Bungeni baada ya kikao cha jana kilichokaa mpaka usiku.


CHADEMA.
CHADEMA japokuwa hawabadilishi msimamo wao kuhusu ukweli kwamba CUF wapo ktk umoja wa vyama vya kilibirerali ambavyo msingi wake mkuu ni kutetea haki za watu binafsi ikiwepo ushoga na usagaji hata hivyo, kwa ajili ya mustakabali mwema wa Tanzania CHADEMA wakawaomba radhi CUF pale waliopokwazwa na maneno yaliyotumika.
Mbowe pia amemwomba spika radhi kutokana usumbufu wa kuahirishwa Bunge kutokana hotuba yao.

CUF.

CUF wamewaomba radhi CHADEMA kupitia kwa kiongozi wao kuhusu matusi, kejeli na Kashfa walizomwambia Wenje. Wenje alisoma kwa niaba ya CHADEMA, siyo hotuba binafsi. Matusi dhidi ya wenje ni matusi dhidi ya kambi nzima ya CHADEMA.
Pili, Cuf walichana hotuba ya CHADEMA bungeni.
Tatu, CUF walifanya vurugu zilizosababisha Bunge kuahirishwa.
aamlishwa kumuomba radhi naibu spika kwa kosa la Wenje kumdhalau naibu spika,na pia anatakiwa kuomba radhi bunge lote.


My take.
wote wamefanya jambo jema.
 
Ha ha haaaaaaa!!!!!!! WALIBERALI,jana wakati wa sekeseke nje ya bunge kuna mbunge mmoja wa CUF alisema ndani ya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kuna wabunge wanawake ambao ni wasagaji.wakuu hakuna mwenye majina yao atuwekee hapa?
 
Kikubwa ujumbe umefika kwa walengwa maana ninahakika hata wabunge wa CUF wengine hawakuwa wanajua ukweli kuhusu moja ya misimamo ya vyama vya kilberali,jana ndio wameamka usingizini,hata wabunge kama kina Kessy wa CCM aliekuwa anatukana hovyo jana huku akishabikia vurugu za CUF naamini hakuwa anajua kitu juu ya jambo hilo,na ni watanzania wengi waliokimbilia kuwalaumu CDM kwa kudhani Wenje katunga mambo ya kutaka kuwadhalilisha CUF tena kwa kiswahili cha kuwatukana matusi wakati ni kweli wao ni full member wa waliberali na moja ya hoja zo ni kutetea usagaji na ushoga.na ndio maana nakubali mambo wakati mwingine huisha kiutu uzima huku ujumbe ukiwa umefika mahali pake.
 
Chadema kifute kwa kuidhalilisha Cuf. Kuizushia uongo!!!
siku hizi intaneti mpaka kwenye simu za kichina inamaana hata hiyo huna?jaribu ku-google utawakuta hao CUF kwenye mtandao wa waliberali na ni full member,na huko utakuta koja ya hoja zao ni kuetetea ushoga na usagaji na hii ndio haki sawa......
 
Sasa ni bifu zito.

Mjadala unaendelea bungeni kwa sasa!!

CHADEMA.
1.Sasa yale maneno ya kuhudhi pg7-9 kuondolewa.
2.Sasa CHADEMA waamliwa kuomba radhi.
3.Mbowe aamlishwa kumuomba radhi naibu spika kwa kosa la Wenje kumdhalau naibu spika,na pia anatakiwa kuomba radhi bunge lote.

CUF:
Nao waambiwa wawaombe radhi CHADEMA kwa kuchanana hotuba yao. Pia wote waamliwa kumuomba radhi naibu spika kwa kufanya vurugu bungeni jana.

Hahhaa! Nimekumbuka kauli ya Mh. Kafulila; Watawala wetu kwa KUBALANSISHA hawajambo.

Walipokosa namna ya kuiadhibu Radio Imaan, wakaitafutia sababu Kwa Neema FM.
 
Sasa ni bifu zito.

Mjadala unaendelea bungeni kwa sasa!!

CHADEMA.
1.Sasa yale maneno ya kuhudhi pg7-9 kuondolewa.
2.Sasa CHADEMA waamliwa kuomba radhi.
3.Mbowe aamlishwa kumuomba radhi naibu spika kwa kosa la Wenje kumdhalau naibu spika,na pia anatakiwa kuomba radhi bunge lote.

CUF:
Nao waambiwa wawaombe radhi CHADEMA kwa kuchanana hotuba yao. Pia wote waamliwa kumuomba radhi naibu spika kwa kufanya vurugu bungeni jana.

Taarifa yako iko kiunafiki akkuna mtu aliye lazimishwa kumuomba mwenzake radhi ila kilicho fanyika kwenye kamati ya maadili ni kwamba wamekaa na wakazungumza na kwa mstakabali wa taifa letu wakaamua kuondoa chuki zao na kuombana radhi ila akuna aliye lazimishwa kuomba radhi
 
Nashukuru kwa upatanisho huo,pia shukrani ziwaendee waliokubali kosa naamini yote hii ni katika kuwekana sawa juu ya mustakabali wa Taifa, sasa na sisi walipa kodi tunaomba posho za jana msizipokee na badala yake ziende kwenye kampeni ya fistula au popote penye mahitaji ya kijamii.....
 
Bunge limekua kijiwe cha wavuvi tu sasa... Mibwabwajo milioni utendaji nehi che zaidi ya kusubiri samaki wanase kwenye nyavu
 
Back
Top Bottom