CHADEMA mnataka mteremshiwe gunia la chawa?

Baada ya ripoti ya tume ya jaji Manento ambayo ndio tume halali yenye mamlaka ya kisheria yanatakiwa yafanyike maandamano ya yasiyo kuwa na kikomo mkoani Iringa kuhakikisha kuwa Kamanda Kamuhanda,Mwema, chagonja na Nchimbi wanang'oka kwenye nafasi zao. Kuna mambo viongozi wetu wa chama wanatakiwa kuongozwa na busara lakini sio hili ambalo mara baada ya tukio chama kikapakwa matope kupitia vipindi vya kupika kwenye runinga.

1. Dr slaa.
2. Mbowe
3. Lissu
4. Zitto
Popote mlipo, amkeni mhamasishe umma wa wana Iringa ili kumtendea haki marehemu Daudi Mwangosi,ally zona na wengine wengi walio uwawa mikononi mwa Polisi, ile kauli ya hakuna kulala mpaka kieleweke ndio inatakiwa kutumika hapa kuwaondoa mabaradhuri walio sababisha vifo vya watanzania wenzetu! Chama kitatuangusha kama kitanyamaza baada ya kutolewa ripoti yenye nguvu za kisheria.

Tusisubiri kesho, tuanze sasa maana ukimya wetu ni mauti kwa wengine, 'hakuna kulala mpaka haki ipatikane, na ikipatikana wahusika wawe wameshapoteza nafasi zao'

Ninachojua ni kuwa M4C inaendelea mkoani Iringa muda si mrefu, tuwe na subira kidogo nadhani mziki wake utakuwa mzito sana, watu wa iringa wana hasira ya kufa mtu.
 
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
(THBUB)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

3.0 MAONI NA MAPENDEKEZO

Kwa kuzingatia Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Na. 7 ya mwaka 2001 Kifungu cha 15(2)(c) na 28 Tume inapendekeza yafuatayo:
1. Kamati za ulinzi na usalama za Mkoa na Wilaya ziwe makini na vitendo vya uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utalawa bora vinavyofanywa na mamlaka mbalimbali kwenye maeneo yao. Aidha, kamati hizo zihusike moja kwa moja na usalama wa wananchi na mali zao kwa kujadili masuala yote ya kiusalama kabla hatua hazijachukuliwa na vyombo vinavyotekeleza sheria.

2. Viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao waepuke malumbano na vyombo vya dola kwa kutii maagizo yanayotolewa na vyombo hivyo bila shuruti. Pale wanapogundua kuwa pana uonevu au upendeleo ni vyema busara ikatumika ili kuepusha madhara makubwa yanayoweza kutokea.

3. Jeshi la Polisi na Msajili wa Vyama vya Siasa waepuke kufanya maamuzi au matendo yanayoibua hisia za ubaguzi au upendeleo miongoni mwa jamii wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kisheria. Mfano, Jeshi la Polisi lilizuia mikutano ya CHADEMA kwa sababu ya sensa wakati huo huo Chama cha Mapinduzi (CCM) walikuwa wakifanya uzinduzi wa Kampeni huko Zanzibar. Aidha, rai ya Msajili wa vyama vya siasa haikuzingatiwa kwa upande wa CCM Zanzibar huku CHADEMA walishurutishwa na Polisi kutii rai hiyo.

4. Demokrasia ya mfumo vya vyama vingi iheshimiwe na kulindwa.

5. Elimu ya vyama vya siasa na sheria ya Polisi kuhusu vyama vya siasa itolewe kwa askari polisi ambao wanaonekana kutozifahamu kabisa.

Ukipitia na kuisoma sawa sawa kazi ya tume hii katika maeneo mengine utafurahi na kuona kuwa kweli hawa ni watu wanaofanya kazi yao kwa kuheshimu sheria.Lakini ebu jisomee mapendekezo haya kama kweli yanagusa kiini cha kilichotoke Nyololo (Kifo-Mwangosi)

MMK Naheshimu hisia zako ila siamini kuwa hisia zinatawala busara bali busara inatawala hisia

1. Uongozi makini huwa unajipanga ili kufanya kitu kunachokuwa na impact inayostahili wanapochukua hatua that is the CDM I know

2. Kwenye hili sakata, CDM wamekuwa kisingizio cha ubakaji wa demokrasia, haki za binadamu kinachotumika na dola; waathirika wakubwa ni sisi sote tumetafakari na kuchukua hatua gani? Kama ni kuwashinikiza CDM waongoze mkakati na harakati za kuibana dola wamelifanya kwa ujasiri tayari kulingana na ripoti hizi zote. Basi mwenye busara ye yote atatoa kamba ndefu ili mhusika ajinyonge. Watawala wanasubiliwa wafanye move yao ya mwisho ili wapewe kibano watakapo chakachua.

3. Hatua za awali zimechukuliwa na CDM kupitia Mh. V. Nyerere; na katika busara ya hali juu ametaka ripoti kamili zipelekwe bungeni kwa hoja ya upinzani rasmi bungeni. (Bila shaka watawala watajitahidi kuzima lakini hapo hapo utakuwa ushahidi tosha wa mapungufu ya dola)

4. CDM wamebambikiwa taswira ya vurugu, je wathibitishe hiyo kauli kwa kufanya matendo yatakayojenga taswira hiyo? Mahesabu ya muda yanasemaje? Is it the right time for right impact with available resource (ie reports and responses)

Katika umri wangu wa 63+ nimeshuhudia mbinu ya patience na calculated move inavyomfanya adui akijiangamiza na mtego wake. Nashauri wachangiaji wenzangu tutoe changamoto pale inapojionyesha uzembeaji wa wazi na MMK singependa kutafsiri bandiko lako kama uchochezi kwa CDM kwa sababu siku zote wako makini.

YOTE KWA YOTE NAPONGEZA UONGOZI WA CDM KWA KUTOKUKURUPUKA KWA FURSA YA TAARIFA HIZI. NI MATUMAINI YANGU HATUA WATAKAZOCHUKUA ZITAKUWA NA IMPACT INAYOTARAJIWA
 
Narudia,

Tumetafakari na kujua kwamba Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ni ya Serikali na makamishna wake akiwamo Mwenyekiti huteuliwa na Rais? Na kwamba ofisi zake zipo pale Magogoni, jirani kabisa na Ikulu?

Hilo lisiwafumbe macho kujadili kwa haki kwamba hata vyombo vya umma vinaweza kutenda haki vikipewa nafasi na watendaji wakiwa wazalendo.

Je, wajumbe wa tume/kamati nyingine wana kaulu gani.? Ama Tume ya Jaji Manento imefanya kusudi kuwaumbua ama kuwakoroga? Je, wao hawajaingilia uhuru ww mahakama?

Nahoji tu jamani. Tujadili tukiwa tunafahamu, ili pia tusiingie mtegoni na tusishambulie watu bila kuwa na uelewa wa mambo.
 
Huyu raisi tozi inamana hayaoni haya au jf aingii nini watu tume achoka na angalie asije akashindwa kumaliza kipindi chake,mana watu ambao wana mtetea na kumpendapenda niwale ambao wanaubinafsi na uwakika wakula na kulala,sio kuangalia watanzania we nzao wanavyo teseka uwa naumia sana sana na ubinafsi ulio tujamaa wa bongo.
 
Mkuu Magesi, mimi sio mshabiki wala mfuasi wa Chadema, mimi wa maslahi ya taifa mbele!. Kwa 2015, mgombea mwenye maslahi ya kupatikana kwa ukombozi wa pili wa kweli kwa Mtanzania ni EL akifuatiwa na Membe!, ndio maana nampigania EL.

P.

Pasco heshima yako mkuu.
Nadhani unapotoka au umeamua kwa makusudi kujipunguzia kiwango chako cha umakini.

El ni miongoni mwa watu ambao wananchi wanao taka mabadiliko (ukombozi wa pili)wanamuona kuwa ni miongoni mwa watu ambao yeye pamoja na chama chake wamesababisha wananchi wayatafute mabadiliko na matumaini mapya ambayo hayapo na hayawezekani ndani ya ccm kuelekea ukombozi wa pili wa mtanzania, vipi uwaaminishe watu kwa ukame wa maono kuwa watu walewale wa chama kilekile walio sababisha matatizo wakiwa na akili zilezile kuwa wana uwezo wa kutatua matatizo yaliyo washinda kwa miaka 50?

Umeanza rasmi na wewe kufikiria kwa tumbo kuelekea 2015 maana nafasi ya Rweyemamu itakuwa haina mtu maana kila kitabu na zama zake?!

Nikuache na haya machache "Aidha uko upande wao uwe-adui yetu kimabadiliko au uwe upande wetu uwe-rafiki yetu kuelekea mabadiliko ya kweli kwenye mbusi mkubwa wenye plate namba T2015CDM
 
Mkuu Mzee Mwakijiji, nakuomba usiendelee kuwaambia!, wasaidie!. Tukubali tukatae, Chadema needs help on this!. Siubezi uwezo wa JJ. Mnyika kama Msemaji, Ofisa Habari etc, Chadema inahitaji a " Strategic Communicator" ili afanye strategic communication!. Sifa kuu ya kwanza kwa any any strategist, ni "nose for news" kuweza kuzinusa hizo "opportunities" ndipo waweze kuzi "seize"!.

Amini usiamini, inawezekana kabisa mpaka sasa, Chadema hawajaziona hizo opportunities kwa sababu hawana "nose for news"!. Hivyo pale makao makuu, wanakuhitaji sasa mtu kama wewe Mzee Mwanakijiji!.

Nakuomba Mzee Mwanakijiji, ihesabu Chadema kama Mwanamke wa Kiasili wa Kiafrika!, hata apende vipi, kamwe hathubutu ku mua approach mwanaume na kumwambia anampenda!, atajipitisha pitisha kuweka mazingira ya kujiavail ili wewe umuanze ndipo akumwagie penzi lake!.

Chadema inashida sana ya mtu wa communications za watu wa strategies wa type kama yako, Nguruvi3, Mchambuzi, etc on board. I hesabu inaona aibu kutoa siri za udhaifu wake kwa kujitongozesha, inahitaji kuwa approched na kusaidiwa!.

Kama kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru, "Nasari" aliutoa ule "waraka" na ukasaidia leo tumeona matokeo na mpaka leo wana Arumeru, wanafaidi matunda, why don't you help by proxy?!.

Please do!.

Mimi kwa vile sina chama, kazi yangu ni kuendelea kusema tuu!, soon nita put up another talk show on air, kazi yangu ni kuwapa opportunity ya kusema wasikike, nitawapa vyama vyote, wasipo utilize such opportunities, wenzao watazi utilize na come 2015, matokeo yakitoka, tusilaumiane maana tuliwaambia, tukawapa fursa wakashindwa wenyewe kuzitumia!.

Nakuomba na wewe jitolee, stretch your helping hand uwasaidie on "strategic communications" wakipokea mkono wako, they will never be the same again, wakikataa, unaendelea na maisha yako but with clear conscious kuwa "at least I tried to help!".

Watch out yasije kuwa kama zile "Burundi Peace Talks" za enzi zile, watu walipenda zaidi per diem ziendelee kuliko kufikia makubaliano!. Usikuta kuna vyama vinapenda kuwa wapinzani wa kudumu, viendelee tuu kuhamasisha maandamano na kuendesha mikutano ya hadhara!.
Pasco.

Pasco
Ofcourse this is the best u can offer kwa mjadala kama huu. Wanaokusoma vyema kila siku hapa na wanaokujua pia, nafikiri wana kuelewa kwa maandishi yako haya. Umechagua maneno mwili matatu yenye ukweli, ukitaka kuwaaminisha wasomaji kuwa hoja ulizoweka hapa ndiyo ukweli wenyewe.

Chama kinatumia nose for news hiyo hiyo (ambayo ni terms za siku ya kwanza kbs kwa mwanafunzi wa uandishi wa habari akiingia darasani) ku-communicate strategically, hitting at the right time at the right place. Mara kadhaa, tunafanya kazi na ku-act faster kuliko baadhi ya newsroom unazoziheshimu huko mjini. Kadri inavyohitajika. Kwa hiyo hata katika hili wala usiwe miongoni mwa wanaofikiri tumeshindwa kutumia opportunities. Lakini nakuhurumia kuwa miongoni mwa watu ambao wanafikiri kuwa CHADEMA imesafishwa kwa propaganda zilizokuwepo. Nani alikuwa anaziamini propaganda za akina Chagonja na wenzao katika suala hili?

The issue here is beyond CHADEMA kusafishwa. Ukiangalia kwa mtazamo huo utakuwa umeamua kuingilia dirishani wakati mlangomupo. Ukifikiria maneno hayo, ndiyo unaweza kuona kwa nini kila kimoja kinafanyika hatua kwa hatua, wakati gani na nani afanye au aseme nini na wapi. Lakini kikubwa ni kwamba kwa kila hatua iliyopigwa katika suala hili, CHADEMA imesikika ikisema na kuchukua hatua fulani. Lakini kwa namna ulivyaoandika hapa, it looks like ure not in touch kabisa tangu manzo. Narudia kuwasihi, someni vizuri ripoti zote tatu, hasa ripoti zenyewe kamili, si executive summaries.

Otherwise we consider some of the truly challenges here and work for them, as most of u here know, to us, at the DIP especially at the info depart, challenges are there to make us think bigger and work harder than ever before to offer the best services for the people.
 
Maslahi ya taifa mbele si nimeyataja?!. Au nirudie tena?. Masllahi ya taifa ni kuhakikisha katika uchaguzi wa 2015, Tanzania tunapata ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania!.

yakhe paka shume alinde kitoweo?
 
Mzee Mwanakijiji chunga intelijensia ya polisi, watasema wamepata taarifa za kiitelijensia kuwa unaleta uvunjifu wa amani.
 
Tumaini; kabla ya Nyerere kuzungumza mlitoa taarifa kuwa alikuwa anapanga kuzungumza hili kama mwitikio wa chama au mlijua tu kuwa anataka kuzungmza lakini hamkuandaa mazingira ya taarifa yake kuonekana ni msimamo wa chama kizima? Maana tuliomsoma inaonekana ni uamuzi wake kama Waziri Kivuli na suala hili angeliileta kwenye vikao vya juu? Halikutakiwa kuzungumziwa kama suala la kibunge bali kama suala la kiutawala wa taifa.

Vicent Nyerere amezungumza vizuri tu kwa nafasi yake lakini hakuzungumza katika mwanga wa uzito wa jambo lenyewe. Tulitarajia viongozi wa juu ndio watoe kauli. Lakini kuja kutoa kauli siku saba baada ya tukio ni kutoonesha umakini. Hivi unafikiri kwanini Jaji Manento aliamua kutoa taarifa yake siku moja baada ya ile ya Ihema? Mnafikiri alikuwa amepanga kutoa siku hiyo anyway?
 
MMK Naheshimu hisia zako ila siamini kuwa hisia zinatawala busara bali busara inatawala hisia

1. Uongozi makini huwa unajipanga ili kufanya kitu kunachokuwa na impact inayostahili wanapochukua hatua that is the CDM I know

2. Kwenye hili sakata, CDM wamekuwa kisingizio cha ubakaji wa demokrasia, haki za binadamu kinachotumika na dola; waathirika wakubwa ni sisi sote tumetafakari na kuchukua hatua gani? Kama ni kuwashinikiza CDM waongoze mkakati na harakati za kuibana dola wamelifanya kwa ujasiri tayari kulingana na ripoti hizi zote. Basi mwenye busara ye yote atatoa kamba ndefu ili mhusika ajinyonge. Watawala wanasubiliwa wafanye move yao ya mwisho ili wapewe kibano watakapo chakachua.

3. Hatua za awali zimechukuliwa na CDM kupitia Mh. V. Nyerere; na katika busara ya hali juu ametaka ripoti kamili zipelekwe bungeni kwa hoja ya upinzani rasmi bungeni. (Bila shaka watawala watajitahidi kuzima lakini hapo hapo utakuwa ushahidi tosha wa mapungufu ya dola)

4. CDM wamebambikiwa taswira ya vurugu, je wathibitishe hiyo kauli kwa kufanya matendo yatakayojenga taswira hiyo? Mahesabu ya muda yanasemaje? Is it the right time for right impact with available resource (ie reports and responses)

Katika umri wangu wa 63+ nimeshuhudia mbinu ya patience na calculated move inavyomfanya adui akijiangamiza na mtego wake. Nashauri wachangiaji wenzangu tutoe changamoto pale inapojionyesha uzembeaji wa wazi na MMK singependa kutafsiri bandiko lako kama uchochezi kwa CDM kwa sababu siku zote wako makini.

YOTE KWA YOTE NAPONGEZA UONGOZI WA CDM KWA KUTOKUKURUPUKA KWA FURSA YA TAARIFA HIZI. NI MATUMAINI YANGU HATUA WATAKAZOCHUKUA ZITAKUWA NA IMPACT INAYOTARAJIWA

Tunawaangalia; kuna vitu ambavyo vinatakiwa kufanywa kwa sababu ni lazima kufanywa. Kwa sababu siyo tu vya kibunge lakini pia vya kisiasa. Suala hili toka mwanzo lilikuwa na muhuri wa siasa. Kushindwa kuelewa siasa iliyomo katika jambo hili ni kushindwa kuonesha umakini unaohitajika katika kushinda kwenye propaganda. Matokeo yake Kamuhanda bado yupo, Kagonja yupo, Mwema Yupo, Nchimbi yupo na msipoangalia mtaenda kwenye majanga mengine na watu hawa hawa wataendelea kuwepo! Hili siyo suala la Bungeni! Ni suala la siasa. Ni suala linalohitaji shinikizo la kisiasa (political pressure).

Katika hili kubwa siyo kusema mnafanya nini bali kurespond. Binafsi siku ile ile ilipotolewa ripotiya Manento CDM walitakiwa kutoa their initial reaction wakiliambia taifa kuwa hatua x, y na z zinafuatia katika kufuatilia kilichosemwa n.k. Ukiangalia tamko la Nyerere lilihusiana zaidi na ripoti ya Nchimbi kuliko ya Manento. At least thats how I read it.
 
Chelian ya ulimboka na hili kesi tofauti: ww ulitaka ulimboka aongee ni nini tena?
Kila kitu alishaweka wazi pindi alipookotwa mabwe na kama hiyo haitoshi kubenea wa mwanahalisi alimwaga kila kitu hadi gazeti likafungiwa.. Tatizo watu hapa harakati zenu mnaendeshea nyuma ya keyboard..

There is no different man, coz what they mention is kujipanga kufanya jambo fulan baada ya tukio flan kufanyika,
mi nafatilia sana vyombo vya habari baada ya kakangu Ulimboka kupatiwa matibabu na kurudi bongo na kusema amepona aliahidi watz kuwa anjipanga kusema kila kilichomtokea na kuwataja wahusika matokeo yake siku zinakwenda na tukio lenyewe lishapoteza umaarufu,
Sa hv ni Mwangosi,...
wahusika wakuu ni Chama changu CHADEMA na (Polisi ambao mi nawaita ni serikali..) Mambo yako wazi kila kitu open
but wanasema wanajipanga!!!
kufanya nini na marehemu ndo ansahaulika hivyoo!!
 
Pasco
Ofcourse this is the best u can offer kwa mjadala kama huu. Wanaokusoma vyema kila siku hapa na wanaokujua pia, nafikiri wana kuelewa kwa maandishi yako haya. Umechagua maneno mwili matatu yenye ukweli, ukitaka kuwaaminisha wasomaji kuwa hoja ulizoweka hapa ndiyo ukweli wenyewe.

Chama kinatumia nose for news hiyo hiyo (ambayo ni terms za siku ya kwanza kbs kwa mwanafunzi wa uandishi wa habari akiingia darasani) ku-communicate strategically, hitting at the right time at the right place. Mara kadhaa, tunafanya kazi na ku-act faster kuliko baadhi ya newsroom unazoziheshimu huko mjini. Kadri inavyohitajika. Kwa hiyo hata katika hili wala usiwe miongoni mwa wanaofikiri tumeshindwa kutumia opportunities. Lakini nakuhurumia kuwa miongoni mwa watu ambao wanafikiri kuwa CHADEMA imesafishwa kwa propaganda zilizokuwepo. Nani alikuwa anaziamini propaganda za akina Chagonja na wenzao katika suala hili?

The issue here is beyond CHADEMA kusafishwa. Ukiangalia kwa mtazamo huo utakuwa umeamua kuingilia dirishani wakati mlangomupo. Ukifikiria maneno hayo, ndiyo unaweza kuona kwa nini kila kimoja kinafanyika hatua kwa hatua, wakati gani na nani afanye au aseme nini na wapi. Lakini kikubwa ni kwamba kwa kila hatua iliyopigwa katika suala hili, CHADEMA imesikika ikisema na kuchukua hatua fulani. Lakini kwa namna ulivyaoandika hapa, it looks like ure not in touch kabisa tangu manzo. Narudia kuwasihi, someni vizuri ripoti zote tatu, hasa ripoti zenyewe kamili, si executive summaries.

Otherwise we consider some of the truly challenges here and work for them, as most of u here know, to us, at the DIP especially at the info depart, challenges are there to make us think bigger and work harder than ever before to offer the best services for the people.
Mkuu Tumaini Makene,

Nilichosema point blank ni kuwa Chadema, mna matatizo upande wa "communications"!. Mkubali mkatae, mnahitaji msaada!. Inawezekana nyie mlio ndani hamuona kama kuna tatizo kwa ama kwa kutokujua, hivyo hamuombi msaada wowote ili kusaidiwa!. Kwa vile humu jf, kuna watu wenye mapenzi mema na mmoja wapo ni Mzee Mwanakijiji, amelisemea hapa!. Mimi nimemshauri, asiendelee kusema tuu, kama ana weza kusaidia lolote kwenye hili, nimemshauri asaidie!.

Mimi nimeshajitanabaisha wazi sina chama, sio mwanachama, mfuasi wala mshabiki wa chama chochote cha siasa, hivyo hata kama ninaweza kuwasaidia Chadema on communications, siwasaidii kwa sababu!,.

Please take time to read this kuhusu matatizo na udhaifu wenu Chadema katika mawasiliano!. Ila pia unaweza kunitembelea hapa nimetoa maoni yangu kuhusu Chadema. Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If.

Mkuu jmushi1, kama nilivyoahidi nipo. Ingawa mjadala unaonekana kufungwa hakika sitasita kutupa neno moja au mawili hasa kujibu hoja yako ya kuwa inaonekana nakubaliana na Pasco.

Ni kweli nakubaliana naye kwa asilimia kubwa sana hata kama si mia moja. Na sababu za kufanya hivyo ni:
1. Kama alivyosema CCM imechokwa, si tu imechokwa bali imechokwa na matendo yake. Chama kilichopo madarakani miaka 50 hakionekani kuwa tumaini kwa Wananchi, badala yake kimegeuka kuwa genge la waporaji na waporaji hao kulindwa kwa kura za wananchi licha ya kuwa uporaji ni wa kodi zao.

2.Wananchi wametafuta mbadala kwa miaka mingi na hakika 'ndele' ya kupendwa imeangukia Chadema.
Ndele hiyo inatokana na jitihada hasa zilizofanyika bungeni kuuonyesha umma wapi tatizo lilipo.
Yule mama aliyehojiwa Iringa yeye alisema 'Anaipenda chadema kwasasababu kama si wao, yeye asingejua uhuni na udhalimu unaoendelea nchi hii'.Hadi hapo Chadema wame win nyoyo za watu kwa kutambua kuwa wapo wanaosimama nao.

3.Mikutano inayoendelea ya M4C ni jambo sahihi, lakini haitoshi tu kuwa sahihi ni lazima ifanyike kwa usahihi.
Mfano, je kila baada ya mkutano kuna ufuatiliaji wa kuimarisha chama eneo husika? Au ni kugawa kadi tu na kukusanya watu na kama ni hivyo je huo ni usahihi hata kama jambo lenyewe ni sahihi?

4.Juzi tumeona picha za CDM mji mwema. Tena viongozi wakionekana kuwa makini. Aliyeleta picha ni mkereketwa wa Chadema na haikuwa na maelezo nini kimesemwa. Mkutano ni jambo sahihi, je, wamelifanya kwa usahihi? Jibu ni hapana kwasababu hawajawasiliana na umma kama ilivyokuwa mwazoni.
Wamekuwa 'out of touch' kwa public kama walivyo kwa JF.
Tayari wameshau ngazi iliyowapindisha na hiyo tu ni tatizo.

5.Pasco amesema lazima wawe tayari kukubali ushauri, na ushauri tuliwahi kutoa kwa kitengo cha mawasiliano ya umma 'public relationship' na ni wazi hawajaufanyia kazi. Hapo nakubaliana na Pasco kuhusu hoja hiyo.

Hapo ndipo niliposema Chadema lazima iwe na clear demarcation iliwatu waone mbadala walio na matumaini nao.
Ni lazima kuwe na demarcation katika kutoa misimamo ya mambo ya kitaifa. Chadema kama chama pinzani na tegemo kwa wakati mfupi ujao inapaswa kuwa mstari wa mbele katika kujibu, kupendekeza na kunyumbulisha hoja zinazohusu utaifa.
Mfano, nini msimamo wa Chadema kuhusu muungano?

8.Chadema wanapaswa kusimama kama taasisi na si kundi la watu fulani maarufu. Taasisi ina namna ya kupanga na kushughulikia mambo yanayohusiana nayo. Suala la Iringa ni mfano mzuri tu. Imewachukua wiki moja kukabiliana na uharibifu wa taswira ya chama uliohusishwa na tukio. In fact kauli ya Mbowe ilikuwa 'damage control' badala ya statement. Tatizo lisiloonekana kwa wengi ni hili la kutokuwa taasisi kikamilifu na ni ngumu kuliona kirahisi.

9.Kama Chadema hawatajipambanua kama Chama kinachosimamia na kueleza sera zake basi ipo siku wananchi watasema tofauti iko wapi? Hawa wanatenda wale wanakosoa nini kilitakiwa kifanyike!
Kwa maneno mengine ukosoaji pekee hautoshi ni lazima kuwepo na makusudi ya kueleza sera zao.

Chadema isimamie sera zake na kuzieneza na si kubaki katika makabrasha au kukaa kimya zikiporwa.
Hoja kama ya katiba, utawala wa majimbo wameziacha zimeporwa na sasa kuonekana kama za CCM.
Kwanini hili linatokea? Hoja ya katiba ilikuwa sahihi, je ilifanywa kwa usahihi?

Kwa ufupi, Chadema sasa kimekuwa na ni wakati kiongoze. Hoja za kukubaliana na CCM kama ya katiba haionyeshi mbadala. Kwangu mimi CDM walikuwa na hoja na waliwaacha wananchi porini. Nitty gritty!
Pamoja na ukosaoaji sasa ni wakati waeleze wao wana matarajio gani kwa njia gani, rasilimali gani na kipaumbele gani.

Vinginevyo wananchi watasema 'better the devil you know than the angel you don't know'.
The simple way CDM could counter act this arguement is to set a clear goal, and make a clear distinction between the past and the future.
 
Ni rahisi kulaumu cdm sana. Ni rahisi kusema kuwa cdm hawatumii fursa zilizopo kufanya kile watanzania wanataka. Ni lini cdm wamelala bila kufanya jambo la kujulisha umma kuwa wapo macho? Paradoxically, i wish watanzania na wapenda mabadiliko wana mwamko kama waislam. Ni sindano gani watanzania wachomwe ili wawe na munkari wa mabadiliko? Ni mara ngapi cdm wametaka na kutoa matamko kuwa nchimbi na wenzake watoswe na hayajatekelezwa? Ccm watakubali kuwatosa watu wake kwa shinikizo la chama kingine cha siasa? So long as wananchi wapo kimya na kuonekana kuridhika, ccm hawawezi na hawana mpango wa kusikiliza hoja ya chama chochote.

Tunisia kama si nguvu ya wananchi serikali ingesalimu? Misri je? Watanzania hawana mpango wa kupoteza nafsi zao katika kudai mabadiliko. Na huu woga wa wananchi ndio mtaji wa ccm. Ni hadi pale wananchi watakapoamua kuwa wamechoshwa na hao watumishi wahuni wa umma ndipo kwa shingo upande watasimamishwa kazi. Mbona waislam (ni mfano tu japo sipendi wanayofanya kwa sasa) wameweza kushinikiza matakwa yao kutekelezwa na yakatekelezeka? Sio cdm wanaostahili gunia la chawa bali ni wananchi ndio stahili yao. Cdm kuwepo frontline tangu uchaguzi uliopita hadi leo si kazi ndogo. Ni kazi kwetu wananchi.
 
Mkuu Mzee Mwakijiji, nakuomba usiendelee kuwaambia!, wasaidie!. Tukubali tukatae, Chadema needs help on this!. Siubezi uwezo wa JJ. Mnyika kama Msemaji, Ofisa Habari etc, Chadema inahitaji a " Strategic Communicator" ili afanye strategic communication!. Sifa kuu ya kwanza kwa any any strategist, ni "nose for news" kuweza kuzinusa hizo "opportunities" ndipo waweze kuzi "seize"!.

Amini usiamini, inawezekana kabisa mpaka sasa, Chadema hawajaziona hizo opportunities kwa sababu hawana "nose for news"!. Hivyo pale makao makuu, wanakuhitaji sasa mtu kama wewe Mzee Mwanakijiji!.

Nakuomba Mzee Mwanakijiji, ihesabu Chadema kama Mwanamke wa Kiasili wa Kiafrika!, hata apende vipi, kamwe hathubutu ku mua approach mwanaume na kumwambia anampenda!, atajipitisha pitisha kuweka mazingira ya kujiavail ili wewe umuanze ndipo akumwagie penzi lake!.

Chadema inashida sana ya mtu wa communications za watu wa strategies wa type kama yako, Nguruvi3, Mchambuzi, etc on board. I hesabu inaona aibu kutoa siri za udhaifu wake kwa kujitongozesha, inahitaji kuwa approched na kusaidiwa!.

Kama kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru, "Nasari" aliutoa ule "waraka" na ukasaidia leo tumeona matokeo na mpaka leo wana Arumeru, wanafaidi matunda, why don't you help by proxy?!.

Please do!.

Mimi kwa vile nina chama, na sio Chadema, kazi yangu ni kuendelea kusema tuu!, soon nita put up another talk show on air, kazi yangu ni kuwapa opportunity ya kusema wasikike, nitawapa vyama vyote, wasipo utilize such opportunities, wenzao watazi utilize na come 2015, matokeo yakitoka, tusilaumiane maana tuliwaambia, tukawapa fursa wakashindwa wenyewe kuzitumia!.

Nakuomba na wewe jitolee, stretch your helping hand uwasaidie on "strategic communications" wakipokea mkono wako, they will never be the same again, wakikataa, unaendelea na maisha yako but with clear conscious kuwa "at least I tried to help!".

Watch out yasije kuwa kama zile "Burundi Peace Talks" za enzi zile, watu walipenda zaidi per diem ziendelee kuliko kufikia makubaliano!. Usikuta kuna vyama vinapenda kuwa wapinzani wa kudumu, viendelee tuu kuhamasisha maandamano na kuendesha mikutano ya hadhara!.
Pasco.
Mkuu, ukipata nafasi kiambie chama kuwa JJ siyo mtu mwenye charisma au mvuto wa public speaking, anafaa zaidi kufanya kazi za ofisini na kufuatilia masuala ya utekelezaji wa maazimio ya chama. Mtu anayefaa kutoa somo la hadharani ni mtu mwenye mvuto kusikilizwa, kwa hiyo chama kitafute mtu wa aina hiyo. JJ hana huo mvuto.
Mkuu Umkonto, UmkhontoweSizwe, utakuwa humjui vizuri JJ. Mnyika!, he is one of the very few fine and the good ones Chadema has!. JJ. Mnyika is very good kwenye data collection ila sio kwenye kushindilia misumari, ili Mnyika afanye vizuri he needs a team mzuri to play with, kwa sasa team play hiyo haipo Chadema!. Zamani JJ. Mnyika akiwa Bungeni huku Zitto Kabwe, kule Tundu Lissu, Mnyika ataibua hoja full of dataz, Zitto ambaye ni mjenga hoja mzuri, ataiongezea momentum kisha Lissu ambaye ni mlipuaji mzuri, atabutua!, Spika chali!. Hata mfugaji mzuri wa ambao, hawezi kufunga kama hakuna mtu wa kumpelekea mipira ya kubutua na kufunga mabao!.

Enzi zile wakati PPR ilikuwa ni PPR kweli, wakati vikao vya Bunge vikiendelea Dodoma, nikapenyezewa dossier fulani vyeti, kesho yake nilikwea the first flight to Dodoma, kumfuata JJ. Mnyika kumkabidhi Gesi asili: Is it "day light robbery?" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe!

Hata ule moto ambao Tundu Lissu huwa anawasha Bungeni from time to time, the data collector ni JJ Mnyika!, ilifikia kipindi tulimuomba Lissu apunguze kumpelekea moto Madam Speaker, Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu! Unammaliza Kabisa Hadi Ameshindwa Kazi!.

Kwenye uchaguzi Mkuu wa 2010 JJ Mnyika ndie alikuwa mgombea wa kwanza kujihakikishia ushindi na aliyeutangaza ushindi wa JJ Mnyika sio mwana jf mwingine bali ni huyu huyu Elections 2010 - Mchakato Majimboni: JJ. Myika, Ubungo Yako, Njia Nyeupe

JJ Mnyika is damm good!, but hana team work nzuri to play with na kwa maoni yangu Chadema hii haina team work, angalia hapa Lissu anavyowaita viongozi wenzake Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?

Kiukweli kabisa uchaguzi wa 2025 upinzani wana kazi kweli kweli to regain back the control of what it used to have!.

P
 
JJ. Mnyika is very good kwenye data collection ila sio kwenye kushindilia misumari,
Mkuu Pascal, mbona naona unakubaliana na nilichosema japo umetumia maneno tofauti!
Hata mimi sijasema kwamba JJ ni mbaya, hata kidogo. Namkubali JJ kuliko viongozi wengi wa chadema! Tatizo langu liko hapo ulipopaita kwenye "kushindilia misumali". Mnapotaka kuushawishi umma uwaunge mkono kwenye issue ya msingi kama katiba kwa kutumia jukwaa la radio, ni vizuri mara mia kutumia mtu mwenye uwezo mkubwa wa kushindilia misumari.
Nakubaliana na wewe, chadema sasa hivi hawana mtu mwenye uwezo huo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom