CHADEMA mnataka mteremshiwe gunia la chawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA mnataka mteremshiwe gunia la chawa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 11, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Ningetaka kuandika kwa kirefu sana kuelezea jambo ambalo labda kwa kifupi lingetosha kuelezewa. Sijaelewa kwanini hadi leo hii masaa zaidi ya 24 tangu Jaji Manento atoe muhtasari wa ripoti yake ya Tume ya Kudumu ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iliyonyoshea kidole serikali (Polisi na Msajili wa Vyama vya Siasa) kuwa ndio walioingilia kati uhuru wa CDM kufanya mikutano yake na kusababisha uvunjwaji wa amani, kupigwa kwa wananchi na kuuawa kwa mwandishi wa habari Daud Mwangosi.

  Inashangaza kuwa CDM ambao siku mbili nyuma walilaumiwa na Kamati ya Nchimbi kuwa ndio chanzo hasa cha vurugu wamejikuta wakisafishwa na chombo cha juu zaidi na chenye nguvu zaidi za kisheria na badala ya wao kutumia nafasi hiyo wameamua kukaa kimya kana kwamba lililosemwa ni dogo. Ikumbukwe kuwa tangu tukio lile la Iringa litokee ni CDM ambao walikuwa wanafanywa mashetani wa tukio hilo huku viongozi mbalimbali wakikituhumu kuwa ndiyo kilichosababisha tukio hilo baya kwa kutotii amri 'halali' ya serikali.

  Tume imeweka wazi kuwa amri iliyotolewa haikutolewa kihalali na hivyo CDM hawakutakiwa kutii isipokuwa kwa busara tu lakini hakukuwa na legal basis ya wao kutii amri isiyo halali. Kumbe tukio zima linawaangukia Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwa na Kamishna Kamuhanda pamoja na viongozi wa juu wa jeshi la Polisi waliohalalisha uvunjivu wa haki za binadamu na matumizi mabaya ya madaraka.

  Yale maandamano ambayo wamekuwa wakiyanfay kwa M4C hadi hivi sasa hayajabadilisha mfumo wowote, hayajamuondoa mtu yeyote madarakani na kwa hakika yamekuwa ni maandamano ya kuhubiria waumini tayari! Sielewi kwanini Kamuhanda bado yupo, Kagonja bado yupo na Tendwa bado yupo?

  I mean najua sehemu ya jibu - wanasubiri kukaa kama kikao cha kamati kuu ili waamue kwa pamoja bla bla bla bla bala... well.. ukivumilia ujinga utatendewa kijinga! CDM needs to seize this opportunity to force the resignations of those who were implicated! Vinginevyo kama nilivyowahi kuwaambia huko nyuma.. wasubiri kuendelea kubeba majeneza na kutoa hutuba za uchungu hadi qiyama.

   
 2. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,870
  Likes Received: 1,559
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji, tunakuhitaji makao makuu Chadema usaidie kwenye mambo ya communication.
   
 4. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwanakijiji, nimekupata. Ni ukweli ulio wazi kuwa CHADEMA wamepewa penati dakika za lala salama...
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji, chunga usijekuangukiwa na kitu 'kizito' chenye ncha kali!
   
 6. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Niliwahi kusema maneno ambayo si matamu kwa baadhi ya watu kwamba Chadema wanaachezezea shilingi chooni na kuna mambo ambayo wanafanya kwa mazoea hadi kufikia mahali watu makini wanashindwa kuwatofautisha na vyama vingine ikiwamo CCM.

  Tuwe wakweli kwamba kuna mambo ambayo yanawasaidia sana CDM ambayo yanatokana na udhaifu wa CCM na baaadhi watendaji serikalini mambo ambayo wahusika wakiyafanyia kazi (japo nu ndoto) Cdm watakua na kazi ngumu zaidi ya kufikia malengo yao ya kisiasa ikiwa ni pamoja na kushika dola. kuhusu Ripoti yaJaji Amiri Manento, naungana na Mwanakijiji kwamba CDM walipaswa kufanya siasa mapema tena mara tu tume mbili zilipowasilisha taarifa zake kwani Tundu Lissu alishazikataa mapema na hapo ndipo palikua mahali pa kuanzia.
   
 7. n

  nemasisi JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 1,881
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wametoa tamko kupitia waziri kivuli wa mambo ya ndani vincent nyerere kwamba wanamtaka waziri nchimbi ajiuzulu na akikataa rais kikwete amuwajibishe
   
 8. Dangire

  Dangire JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  u've made a point!
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  mimi mwenyewe nna vibrate kila dk watanzania tumelala jamani kwa nini tusiingie mtaani tukamtimue yule mpangaji fedhuli pale magogoni? aaaaaaaaargh
   
 10. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mzee Mwanakijiji kwa mambo kama haya yanayofanywa ni nahakika waathirika wa watukio hayo sio CDM bali ni ukandamizaji na uonevu dhidi ya uma.
  Watanzania wanatakiwa waamke na uchukua hatua kukomesha ubaladhuli huu na sio kua na Taasisi, vyama na mashirika ya kutoa kauli tu bila kuonyesha vitendo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  matamko hadi lini?
   
 12. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli katika hili viongozi wangu wamechelewa, mimi nilitarajia hata baada ya ripoti za MCT na ile ya Nchimbi mara moja lingetolewa tamko zito sana, bahati nzuri tume ya haki za binadamu na utawala bora inekuja kumaliza kazi.

  Kama alivyosema mdau hapo juu VUTA-NKUVUTE, tumepata penalty dakika ya mwisho ya muda wa nyongeza. Natarajia hadi kesho tutakuwa tumesikia kauli rasmi ya chama juu ya hizi ripoti.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. n

  nemasisi JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 1,881
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hatahivyo nikubali chadema walipaswa kutoa tamko la nguvu zaidi ambalo lingepaswa kutolewa na ama slaa au mbowe ili lipate heading za kutosha kwenye vyombo vya habari ili kufukia mashimo yaliyochimbwa na wenzao
  kusema kweli ni Golden chance!
   
 14. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Naona kila mmoja anajitoa anamsukumizia mpira mwenzake kama kweli Chadema mpo na mnakubalika mnataka nini.
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Mbona mnakuwa waoga kiasi hicho wakati nyie mnataka kuwakomboa watanzania.
   
 16. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #16
  Oct 11, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Baada ya ripoti ya tume ya jaji Manento ambayo ndio tume halali yenye mamlaka ya kisheria yanatakiwa yafanyike maandamano ya yasiyo kuwa na kikomo mkoani Iringa kuhakikisha kuwa Kamanda Kamuhanda,Mwema, chagonja na Nchimbi wanang'oka kwenye nafasi zao. Kuna mambo viongozi wetu wa chama wanatakiwa kuongozwa na busara lakini sio hili ambalo mara baada ya tukio chama kikapakwa matope kupitia vipindi vya kupika kwenye runinga.

  1. Dr slaa.
  2. Mbowe
  3. Lissu
  4. Zitto
  Popote mlipo, amkeni mhamasishe umma wa wana Iringa ili kumtendea haki marehemu Daudi Mwangosi,ally zona na wengine wengi walio uwawa mikononi mwa Polisi, ile kauli ya hakuna kulala mpaka kieleweke ndio inatakiwa kutumika hapa kuwaondoa mabaradhuri walio sababisha vifo vya watanzania wenzetu! Chama kitatuangusha kama kitanyamaza baada ya kutolewa ripoti yenye nguvu za kisheria.

  Tusisubiri kesho, tuanze sasa maana ukimya wetu ni mauti kwa wengine, 'hakuna kulala mpaka haki ipatikane, na ikipatikana wahusika wawe wameshapoteza nafasi zao'
   
 17. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tujadili tukitambua kwamba Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ni chombo cha serikali na kwa kweli huu ni mfanomhai kwamba kuna mambo hayahitaji tume wqla kamati bali tunahitaji uwajibikaji wa vyombo vilivyopo. Kama ni suala la haki za binadamu kuna chomo, kama ni rushwa kuna chombo kama ni jinai kuna chombo, tatizo kubwa ni hajuna uwajibikaji kila eneo na hapo ndipo zinaibuka tume kufunika kombe na kuwapa watu ulaji na kudhulumu haki za wengine. Watu ama vyombo visivyowajibika viwajibishwe na watawala kwani na wao wwtawajibishwa na umma kupitia kura. Tutengeneze mfumo wa uwajibikaji na Chadema kama chama mbadala kifanye kazi ya kutoa mawazo mbadala ya kubadili mfumo na si kujiandaa kuongoza kwa mazoea.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hapo anamtahadharisha tu kwakuwa serikali yenu dhaifu inajua kuonea wananchi wanyonge, hao polisi wakipigiwa simu kwamba majambazi wamevamia sehemu hawfiki hadi wajiridhishe kwamba wameshaondoka.

  Chadema si waoga na ndio maana pamoja na vitisho, mateso na mauaji bado tu tunaendelea na movement zetu.
   
 19. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,515
  Likes Received: 1,684
  Trophy Points: 280
  Sijaona kosa la chadema. Kimya chao kimeleta funzo kubwa kwa jamii
   
 20. Chelian

  Chelian Senior Member

  #20
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 1, 2012
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtajipanga hadi lini jamani?
  Angalia Ulimboka baada ya mateso yote aliyoyapata lakini hadi leo hii anasema anajipanga kuwataja wahusika
  na nini na nini,au mshalogwa??
   
Loading...