Lema awashukia Chawa wa CCM

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Godbles Lema, ameonyesha kuchukizwa na maneno ya Wanachama wa CCM mitandaoni kuhusu Huruma ya Rais Samia kwa Chadema.

Kupitia mtandao wake wa X Lema ameandika, "Kuna haya maneno mnasema , Mh Rais SSH amewafutia kesi,mlikimbia Nchi lakini ameruhusu mrudi na vile vile tumewatoa watu wenu magereza na kuwaachia huru bado mnaona Mama ajafanya kitu ?mnataka maridhiano gani ?

Haya maneno ni kejeli na dharau kubwa kwa wale mliowaumiza na kuwatesa.Mnapaswa kuwa na aibu kama Chama kinachotesa watu. Kwamba badala ya nyie CCM kujisikia vibaya na kuomba radhi kwa matendo mabaya mliyo watendea binadamu wenzenu , mnataka waliotendewa wawaabudu ? Yaani unanichapa halafu nilikilia unajisikia vibaya ? Roho mbaya sana.

Hatukustahili rafiki zetu kuuwawa wala kupigwa risasi , hatukustahili wenzetu kuteswa. Uhuni na ukatili huu ulipaswa kuwajibishwa kwa kiwango cha juu kabisa,lakini badala yake manajivuna juu yake na kutaka mliowatesa wawe wanyonge mbele yenu eti kuwa kuna upendeleo mliwapa wao kuwa huru kwa kesi za uongo na mambo mengine mengi yenye sura kama hizi.

Mlivunja sheria kuzuia mikutano ya hadhara,mkafanya ukuuaji wa demokrasia na haki za binadamu kudumaa sana maiti ziliokotwa mchangani kama takataka na hata pale mlipovunja Sheria na Katiba hamkuona aibu na sasa mnapopaswa kutii sheria kidogo nayo mnataka tuone kuwa mnatoa upendeleo ?Kwamba Rais kusimamia Sheria na Katiba ni Upendeleo anaotupa sisi ? This is IMPUNITY.

Tukinyamaza kuongea mambo hayo Nchi itakuwa mbaya sana.Tutukaneni lakini jaribuni kutazama kesho vizuri. Hatutafuti ajira kwenye wajibu huu kwani hakuna kazi yenye mateso kama kazi ya harakati za kupigania haki za binadamu,ni risk kubwa sana kupishana na mifumo yote mikubwa ya Nchi mpaka Rais.Tumechagua kwa sababu tumejua kusudi la kuishi".

NINI MAONI YAKO?
 
Kwani hakuvaaa baibui?

Nani aliyewatukana wananchi waliombeba kwenye pikipiki zao;

" ...ni laaana hiyo...' G. Lema

Nani aliyewatukana Mama zetu pale Arusha?


Narudia, sababu kubwa ya CHADEMA kuingia Maridhiano, ni kutaka kujificha kwenye chaka la 'Reconciliation' huku wakitaka 'Forgiveness' ili kuficha madhambi yao ya uhasi waliyoyafanya dhidi ya Serikali na Nchi hii. Wamekiri wenyewe.

Wanataka wasamehewe kwa yapi waliyoyafanya?
 
Back
Top Bottom