CHADEMA: Lissu atoka ICU, anaweza kukaa...Kamera za CCTV karibu na aliposhambuliwa zimeondolewa

Tunamuimbea Lissu apone aje aendelee na majukumu yake kama kawaida. Hakuna kitu cha thamani zaidi kwa binadamu zaidi ya uhai, hata kama ni adui yako, muombee njaa, usimuombee kifo.

Natumai huyo jamaa atapona na atakuja kuendelea na majukumu yake na kuungana na familia yake.
Kumuombea mgonjwa ama mtu yeyote aliyepatwa na kadhia yoyote ni jambo la kiungwana na linalofanywa na binadamu wenye utu kinyume na wafanyavyo baadhi ya wanadamu wenye roho za fisi kama sio nguruwe.

Kurudi kwa mh. TL Kutazidi kupeperusha na kutapanya manyoa ya kuku yaliyokwishafunuliwa na upepo kwa hakika tutaona zaidi ya nyeti za kuku.
 
Ndugu, siyo jambo baya ukitumia muda wako kujiendeleza kielimu kidogo ili upate uwezo wa kupambanua mambo. Una tatizo kubwa sana la uelewa lakini bado una nafasi.
Kuna msemo unasema " Mtu akifa huwa haumii kwasababu hajui linaloendelea huku duniani ila sisi tulio hai ndo tunaumia kwa kumpoteza yeye, Hii ni sawa na mtu mpumbavu... Ukiwa mpumbavu wala hujijui sisi tunaokuangalia ndo tunaoumia kutokana na upumbavu wako."
 
""Vyombo vyetu vya ndani havina dhamira ya kumtafuta Mhalifu kwa sababu tunapenda kuamini kwamba wanamjua mhalifu." - Freeman Mbowe.

Red Brigade...wametanda kila kona ...............ahahhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh
 
Wakati mwingine uhaba wa maneno katika lugha ya kiswahili husababisha baadhi ya taarifa kueleweka ndivyo sivyo mbele ya jamii. Jana nimemsikia Mbowe akidai Lissu baada ya kupata nafuu atapelekwa sehemu isiyotangazwa kwa hatua ya mwisho ya matibabu yake, na kwamba wamefanya hivyo kwa kuhofia " watu wasiojulikana " wasije kumdhuru. Lakini Mbowe huyu huyu anasema, Lissu anapaswa kugharamiwa na serikali matibabu yake kwa mujibu wa sheria halafu anauliza " mtu aliyekukosakosa atakulipiaje matibabu? " Kiukweli hapo ndipo nilipochanganyikiwa na kufikiri labda tafsiri ya kiingereza itanisaidia. Wachungaji wanapopata utata wa tafsiri ktk Bible ya kawaida huenda kwenye version ya King James, then kilatini, kiyunani na ikiwa bado ngumu huiangalia kwa kiebrania. Wanasiasa msaada tafadhali, je wanaitwa unknown people au.......?!!!
 
Kwani huo uhalifu walifanyia Scotland ana Great Britain? watu wasiojulikana wanajulikana...hakuna mtu asiyejulikana!
 
Wakati mwingine uhaba wa maneno katika lugha ya kiswahili husababisha baadhi ya taarifa kueleweka ndivyo sivyo mbele ya jamii. Jana nimemsikia Mbowe akidai Lissu baada ya kupata nafuu atapelekwa sehemu isiyotangazwa kwa hatua ya mwisho ya matibabu yake, na kwamba wamefanya hivyo kwa kuhofia " watu wasiojulikana " wasije kumdhuru. Lakini Mbowe huyu huyu anasema, Lissu anapaswa kugharamiwa na serikali matibabu yake kwa mujibu wa sheria halafu anauliza " mtu aliyekukosakosa atakulipiaje matibabu? " Kiukweli hapo ndipo nilipochanganyikiwa na kufikiri labda tafsiri ya kiingereza itanisaidia. Wachungaji wanapopata utata wa tafsiri ktk Bible ya kawaida huenda kwenye version ya King James, then kilatini, kiyunani na ikiwa bado ngumu huiangalia kwa kiebrania. Wanasiasa msaada tafadhali, je wanaitwa unknown people au.......?!!!
Mbona rahisi tu!! muuaji alikuwa anatafuta upenyo wa kumalizia azma yake. Ni haki ya mbunge kutibiwa na Bunge kama kawaida, awe amepigwa na ndugai au kuanguka bungeni ni haki yake!
 
Uelezwe we nani? Onesha Tin amba yako kwanza kama unalipa kodi kweli. Isije kuwa unalipa kodi ya chumba. Na pia uelewe hata kama unalipa kodi, kodi yako hutumika kununua risasi pia.
Hivi kumbe Hosp. zetu za wagonjwa maalumu zimeboreshwa kiac hiki hadi intenet zipo! Kumbe hata mirembe mnaruhusiwa kuingia wodini na simu?
 
yeye gharama zake za kutumbua nairobi kaziminya kimya.Hajataja hizo gharama za hao wanaokaa nje ya hospitali kumuuguza akiwemo ,yeye ,mke wa lisu,akina msigwa nk wamelamba shilingi ngapi kwa siku walizokaa Nairobi.Ukiangalia hajaitisha michango mipya.Kuna porojo kibao kwenye uwakilishaji hiyo ripoti.Chama kimetoa specifically shilingi ngapi anaruka ruka ohhh kinaziba gap ni kama 40%.Wataalamu wa hesabu chukueni hizo pesa zote alizosema toeni hiyo 40% anayosema chama kimetoa mtamdaka uwongo sasa hivi.mtagundua kuwa kuna tofauti ya zilizochangwa nje ya chama hazi tally na hesabu zake.

Hiyo ripoti ya michango yote akabidhi wakaguzi kabla ya kuingia awamu ya tatu ya matibabu ya LISU.Si vibaya akakabidhi ripoti ya mapato na matumizi kwa CAG kwa ukaguzi
Lumumba shida yako nini kupona Lissu au fedha??
Kamata wauwaji tukuone ni mtaalamu@!
 
Na Thadei Ole Mushi.

[HASHTAG]#Inashangaza[/HASHTAG] kidogo

1. Nyumba ya Tundu lisu haikuwa na CCTV kamera wakati alikuwa anajua anafuatiliwa na kutishiwa kwa muda mrefu. Eti walikuwa wanategemea cctv za jirani....

2. Nyumba ya Lisu haikuwa na Mlinzi hata mmoja anayelinda nyumba yake hiyo. Eti alikuwa anategemea ulinzi wa jirani......

3. Kwa mujibu wa Mbowe anadai kuwa kamera za cctv zilizokuwa kwa jirani amesikia zimeondolewa huu ni kwa mujibu wa uchunguzi wao. Kwa maana hiyo Chadema wana kikosi chao cha uchunguzi sasa wanachosumbua waje wa kutoka nje ni nini?

4. Mbowe kalishutumu moja kwa kwa moja Jeshi la Polisi kuwa ndio wahusika kama anajua kwa nini asiende mahakamani?

5. Inaendelea kushangaza Dereva kuweza kukwepa risasi zote 30. Na actually hili ndio swali la Msingi analolikimbia Dereva.....

6. Inaendelea kushangaza aliyepatwa na risasi kupona kabla ya aliyesikia mlio wa Risasi only in Chadema........

7. Inashangaza kwa kuwa wagonjwa wapo wawili ila hatujajua huyu mwingine gharama zake za matibabu ni shilingi ngapi hadi sasa. Au anatibiwa bure?

[HASHTAG]#KWA[/HASHTAG] NINI MBOWE ANATULAZIMISHA TUAMINI WAHALIFU NI SERIKALI TU?

[HASHTAG]#Nawaambia[/HASHTAG] Watanzania wenye Akili wananza kuondoa huruma yao juu ya hili swala. Mbowe analibeba mno kisiasa niliwahi kuandika hapa kuwa maadui wa Tundu Lisu walikuwa ni wengi nje ya chama chake na ndani ya Chama chake.

[HASHTAG]#Mbowe[/HASHTAG] analazimisha watanzania wajenge assumption moja tu kuwa ni Serikali inahusika na shambulio la Lisu.....

[HASHTAG]#Kwenye[/HASHTAG] utafiti huwa hatubebi assumption (Hypothesis) moja ni lazma tuwe nazo zaidi ya Moja. Uchunguzi wa Polisi ni utafiti kwa 100% wana assumption nyingi kama na raia walivyo na assumption nyingi tunahitaji tuzithibitishe zote kwa hiyo atulie.

[HASHTAG]#Swala[/HASHTAG] la kuondolewa CCTV inawezekana ulikuwa ni mpango wa wenye shambulio kutaka kupoteza ushahidi. Huyo aliyekuwa anazifuatilia mpaka akajua zimeondolewa tutajuaje kama alitaka kuziiba?

[HASHTAG]#Mbowe[/HASHTAG] awasiliane na Jeshi la Polisi kujua uchunguzi umefikia wapi kabla ya kuja kuongelea kwenye vyombo vya habari huu utamaduni wa hivi sijui kwa nn Polisi wetu wapo tu kimya....

[HASHTAG]#KINACHOWEZA[/HASHTAG] KUFANYIKA.

1. Kwa kuwa Mbowe analituhumu jeshi la polisi kuwa ndilo linalohusika na Shambulizi aitwe ahojiwe na awe mshahidi wa kwanza kuthibitisha hilo.

2. Polisi wanaweza kuwanyima watu wasiliongelee swala hilo mpaka ripoti yao itakapotoka ili wasivuruge uchunguzi. Huu ni utamaduni wa kawaida wa kiupelelezi.

3. Kwa Order ya Interpol dereva wa Lisu arejeshwe nchini kwa mahojiano. Si lazma polisi wetu wamfuate huko kwa mahojiano ni kutumia Kodi za wananchi vibaya.

Ole Mushi
Huna lolote umebuma.
Kamata wauwaji acha kujibaraguza.
 
Eneo lote lile linalindwaa kuna walinzi na makamera kwa nini polisi wasiwahoji na ushahidi upo??
wahusika wanajulikana ndo maana mpaka Jeshi la Polisi wameshindwa kuwahoji walinzi walikiwepo siku mpaka CCTV wamezindua kuficha ushahidi
 
Kuna msemo unasema " Mtu akifa huwa haumii kwasababu hajui linaloendelea huku duniani ila sisi tulio hai ndo tunaumia kwa kumpoteza yeye, Hii ni sawa na mtu mpumbavu... Ukiwa mpumbavu wala hujijui sisi tunaokuangalia ndo tunaoumia kutokana na upumbavu wako."
Na ndio maana nikakwambia una tatizo kubwa sana la uelewa. Sasa ulicho quote ni msemo au ni maelezo ya hotuba?
 
WanaJF

Ni Asubuhi tulivu ya Jumanne tayari tupo hapa makao makuu ya chama kikuu cha upinzani Tanzania Chadema.

Watendaji kadhaa wameshaanza maandalizi ya mkutano wa wanahabari na Mwenyekiti Mbowe.

Hali ya Usalama inaimarishwa hapa huku vijana wa ulinzi wa chama Red Brigade wakiwa wametanda kila kona ya kuelekea makao makuu kudhihirisha ujio wa kiongozi mkuu wa Upinzani Tanzania.

Taarifa za uhakika tulizo nazo ni kwamba Mwenyekiti Mbowe leo ataeleza mazito kuhusu mwanasiasa maarufu zaidi Afrika Mashariki Tundu Lissu na yanayoendelea nchini.

Tunatarajia kuwaletea live coverage ya tukio lote kupitia ukurasa huu hapa JF

Karibuni sana.

Updates

Tayari viongozi kadhaa wameshaanza kuwasili huku kukiwa na Idadi kubwa ya waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi...

Mwenyekiti Freeman Mbowe ameanza kuzungumza: Mbowe anasema....

CHADEMA Tunaamini kabisa waliomdhuru Lissu wapo na wanajulikana. Tunaamini vyombo vya usalama wanawajua waliomshambulia Lissu.

Mh Lissu ni jirani wa Waziri,tuna taarifa kuwa ile cctv Camera iliyokuwepo eneo la tukio imeondolewa,imeondoolewa na nani?

Hatuna imani na Vyombo vya Dola vya ndani si kama havina uwezo, ni kwa sababu havina dhamira.

Nieleweke kwamba hatuvidharau Vyombo vyetu vya ndani, ila vinafanya kazi kwa mashinikizo, maelekezo ya viongozi wa Serikali."

Vyombo vyetu vya ndani havina dhamira ya kumtafuta Mhalifu kwa sababu tunapenda kuamini kwamba wanamjua mhalifu.

HALI YA TUNDU LISSU KWA SASA:

Tundu Lissu ametoka ICU wiki iliyopita na mashine zote zilizokuwa zikimsaidia zimetolewa. Hivi sasa anaweza kukaa.

Baada ya siku takribani 40 za matibabu, hatimaye TunduLissu ametolewa ICU na sasa anaweza kula na kukaa mwenyewe

Mh Lissu anaendelea vizuri hatumii tena mirija kula chakula,anakula chakula anachokitaka yeye"-

Lissu amepewa damu nyingi kuliko mgonjwa mwingine yeyote aliyewahi kuwa kwenye hospitali ya Nairobi kwa miaka 20 iliyopita.

Lissu anatarajiwa kumaliza awamu ya 2 ya matibabu ndani ya wiki 1 na atapelekwa nje ya Nairobi kwa ajili ya Rehabilitation

Tunajua kabisa uharamia huu kwa Lissu umetendwa na hao tunaowatuhumu na waliotenda wanajulikana na mfumo wa kutenda uliandaliwa

Limeanzia kwa Mh. Lissu na wengine tupo kwenye 'wanted list' huu utamaduni hatukuuzoea hivyo hatuwezi kulichukua kama jambo jepesi.

Nilikuwa nasita kutoa taarifa za mgonjwa kwa sababu ni haki ya mgonjwa na si jambo la chama.

Katika awamu ya tatu ya matibabu,tutaiachia familia nafasi kufanya maamuzi, tutasaidia pale tutakapohitajika kusaidia.

Kwa sasa anaendelea vyema na tutarajie kumsikia akizungumza kuanzia leo.

Pia tutaweka picha zake kwenye mitandao kwa mara ya kwanza tokea apigwe risasi. Kama kuna picha zozote zinazomuonesha Lissu akiwa hospitali hizo sio za kweli bali za kutengeneza.

Lissu ameshambuliwa imechukua masaa mawili polisi kufika kwenye eneo la tukio, Sisi tuamini akina nani waliotekeleza tukio hilo.

Ni kweli kuna mazungumzo yalifanyika kati ya Ofisi ya Bunge na Ofisi ya KUB kuhusu haki na stahiki za Tundu Lissu kama Mbunge

Ni ukweli usiopingika kuwa mgonjwa kutibiwa na Bunge ni haki yake ya kisheria. Haya mambo yana mihemko na hutulia baada ya muda.

Suala la Lissu lina hisia kali ndani yake. Msifikiri ni rahisi mtu akukosekose kukuua halafu aseme akulipie ukatibiwe.

Tunafahamu njama zinazopangwa, lakini hatutarudi nyuma. Tunaitwa viherehere kwa kumpigania Lissu lakini tunasema, hatutaukiri umauti

Kipaumbele chetu hakijawa fedha bali kumsaidia mgonjwa apone, mambo ya fedha tutayakuta tu.

Kama mtu ni haki yake asipoipata leo, iko kesho, iko keshokutwa. Hatuzungumzi kuhusu fedha, wakati utafika muafaka.

Michango ya Wabunge wote kwa kukatwa nusu ya posho zao za siku; kundi hili limechanga Tsh Milioni 43.

Wabunge wa CHADEMA wamechanga Tsh Mil 48, viongozi na wananchi Tsh Mil 24, wanachama mbalimbali Tsh Mil 90.

Misimamo ya Chama chetu haitayumbishwa na fedha pamoja na umasikini wetu. Tunajali utu, ulinzi na kila mtanzania apate haki ya kuishi.

GHARAMA ZA MATIBABU MPAKA SASA
Hadi tarehe 12 mwezi huu wa 10 gharama ya kila kitu kilichotumika kumtibu Lissu ni 18,352, 156 kwa Pesa za Kenya sawa na Mil 412,472,250 za Tanzania.

Tunawashuru wote kwa kutufuatilia LIVE hapa JF na kupata kile kilichosemwa na Kiongozi mkuu wa Upinzani Tanzania Freeman Mbowe kuhusu Yatokanayo na Afya ya Mwanasiasa mashuhuru zaidi Afrika Mashariki Tundu Antipas Lissu.

Mungu Awabariki Nyote.

Asanteni sana..

Km Wamendoa CCTV Dereva Wa nini
 
Back
Top Bottom