CHADEMA: Lissu atoka ICU, anaweza kukaa...Kamera za CCTV karibu na aliposhambuliwa zimeondolewa

WanaJF

Ni Asubuhi tulivu ya Jumanne tayari tupo hapa makao makuu ya chama kikuu cha upinzani Tanzania Chadema.

Watendaji kadhaa wameshaanza maandalizi ya mkutano wa wanahabari na Mwenyekiti Mbowe.

Hali ya Usalama inaimarishwa hapa huku vijana wa ulinzi wa chama Red Brigade wakiwa wametanda kila kona ya kuelekea makao makuu kudhihirisha ujio wa kiongozi mkuu wa Upinzani Tanzania.

Taarifa za uhakika tulizo nazo ni kwamba Mwenyekiti Mbowe leo ataeleza mazito kuhusu mwanasiasa maarufu zaidi Afrika Mashariki Tundu Lissu na yanayoendelea nchini.

Tunatarajia kuwaletea live coverage ya tukio lote kupitia ukurasa huu hapa JF

Karibuni sana.

Updates

Tayari viongozi kadhaa wameshaanza kuwasili huku kukiwa na Idadi kubwa ya waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi...

Mwenyekiti Freeman Mbowe ameanza kuzungumza: Mbowe anasema....

CHADEMA Tunaamini kabisa waliomdhuru Lissu wapo na wanajulikana. Tunaamini vyombo vya usalama wanawajua waliomshambulia Lissu.

Mh Lissu ni jirani wa Waziri,tuna taarifa kuwa ile cctv Camera iliyokuwepo eneo la tukio imeondolewa,imeondoolewa na nani?

Hatuna imani na Vyombo vya Dola vya ndani si kama havina uwezo, ni kwa sababu havina dhamira.

Nieleweke kwamba hatuvidharau Vyombo vyetu vya ndani, ila vinafanya kazi kwa mashinikizo, maelekezo ya viongozi wa Serikali."

Vyombo vyetu vya ndani havina dhamira ya kumtafuta Mhalifu kwa sababu tunapenda kuamini kwamba wanamjua mhalifu.

HALI YA TUNDU LISSU KWA SASA:

Tundu Lissu ametoka ICU wiki iliyopita na mashine zote zilizokuwa zikimsaidia zimetolewa. Hivi sasa anaweza kukaa.

Baada ya siku takribani 40 za matibabu, hatimaye TunduLissu ametolewa ICU na sasa anaweza kula na kukaa mwenyewe

Mh Lissu anaendelea vizuri hatumii tena mirija kula chakula,anakula chakula anachokitaka yeye"-

Lissu amepewa damu nyingi kuliko mgonjwa mwingine yeyote aliyewahi kuwa kwenye hospitali ya Nairobi kwa miaka 20 iliyopita.

Lissu anatarajiwa kumaliza awamu ya 2 ya matibabu ndani ya wiki 1 na atapelekwa nje ya Nairobi kwa ajili ya Rehabilitation

Tunajua kabisa uharamia huu kwa Lissu umetendwa na hao tunaowatuhumu na waliotenda wanajulikana na mfumo wa kutenda uliandaliwa

Limeanzia kwa Mh. Lissu na wengine tupo kwenye 'wanted list' huu utamaduni hatukuuzoea hivyo hatuwezi kulichukua kama jambo jepesi.

Nilikuwa nasita kutoa taarifa za mgonjwa kwa sababu ni haki ya mgonjwa na si jambo la chama.

Katika awamu ya tatu ya matibabu,tutaiachia familia nafasi kufanya maamuzi, tutasaidia pale tutakapohitajika kusaidia.

Kwa sasa anaendelea vyema na tutarajie kumsikia akizungumza kuanzia leo.

Pia tutaweka picha zake kwenye mitandao kwa mara ya kwanza tokea apigwe risasi. Kama kuna picha zozote zinazomuonesha Lissu akiwa hospitali hizo sio za kweli bali za kutengeneza.

Lissu ameshambuliwa imechukua masaa mawili polisi kufika kwenye eneo la tukio, Sisi tuamini akina nani waliotekeleza tukio hilo.

Ni kweli kuna mazungumzo yalifanyika kati ya Ofisi ya Bunge na Ofisi ya KUB kuhusu haki na stahiki za Tundu Lissu kama Mbunge

Ni ukweli usiopingika kuwa mgonjwa kutibiwa na Bunge ni haki yake ya kisheria. Haya mambo yana mihemko na hutulia baada ya muda.

Suala la Lissu lina hisia kali ndani yake. Msifikiri ni rahisi mtu akukosekose kukuua halafu aseme akulipie ukatibiwe.

Tunafahamu njama zinazopangwa, lakini hatutarudi nyuma. Tunaitwa viherehere kwa kumpigania Lissu lakini tunasema, hatutaukiri umauti

Kipaumbele chetu hakijawa fedha bali kumsaidia mgonjwa apone, mambo ya fedha tutayakuta tu.

Kama mtu ni haki yake asipoipata leo, iko kesho, iko keshokutwa. Hatuzungumzi kuhusu fedha, wakati utafika muafaka.

Michango ya Wabunge wote kwa kukatwa nusu ya posho zao za siku; kundi hili limechanga Tsh Milioni 43.

Wabunge wa CHADEMA wamechanga Tsh Mil 48, viongozi na wananchi Tsh Mil 24, wanachama mbalimbali Tsh Mil 90.
k
Misimamo ya Chama chetu haitayumbishwa na fedha pamoja na umasikini wetu. Tunajali utu, ulinzi na kila mtanzania apate haki ya kuishi.

GHARAMA ZA MATIBABU MPAKA SASA

Hadi tarehe 12 mwezi huu wa 10 gharama ya kila kitu kilichotumika kumtibu Lissu ni 18,352, 156 kwa Pesa za Kenya sawa na Mil 412,472,250 za Tanzania.

Tunawashuru wote kwa kutufuatilia LIVE hapa JF na kupata kile kilichosemwa na Kiongozi mkuu wa Upinzani Tanzania Freeman Mbowe kuhusu Yatokanayo na Afya ya Mwanasiasa mashuhuru zaidi Afrika Mashariki Tundu Antipas Lissu.

Mungu Awabariki Nyote.

Asanteni sana.

Molemo.

katika tamko la Mh.Mbowe kuwa hana imani na dola,niile tabia ya vyombo vya nchi zetu kupuuza matendo yanayofanywa kwa chama cha upinzani na wanachama wake.Tuna kubenea (yeye alimwagiwa tindikali),tuna Ulimboka aliyeumizvibaya ,na huyu Lissu huoni vyombovya dola vikiuna vichwa kwa nini wanfanyiwa hivi?Ninachofikiri,hivi una baba aliyena watoto na mkewe,watoto wanapotea mke anamweleza mmewe kupotea kwa mtoto lakini Baba wala hahangaiki kufuatilia kupotea kwa mwanawe ,Mama atasema nani anatowesha watoto kama sio Mzazi wao?

hii ndiyo sifa ya waafrika,na niabu kwa mataifa ya nje,yanatuona hamnazo na ndio maana taasisi za nje na raia wa nje wanatuona Manyani
 
Freeman Mbowe "Mh Lissu ni jirani wa Waziri,tuna taarifa kuwa ile cctv Camera iliyokuwepo eneo la tukio imeondolewa,imeondoolewa na nani?"-
ni mwezi sasa vyombo vya dola vinasubiri dereva niajabu,na yule wa Nape ambaye walisema sio askari wa nini wasifanye juhudi kumkamata aeleze ameitoa wapi?,Jamani nilichojifunza nikuwa ukiishi kwa uongo uwezo wako wa kutafakari mawazo ya kimantiki unapungua,unaweza kusema aliyemnyooshea bastola Nape nivibaka wa Tandale
 
Duh, ila tunatofautia wanadau!! Kweli kwako wewe umeona ahadi ile mpaka unakuja kuizungumzia humu jamvini? Yote aliongea jana, uliloliona wewe la maana ni picha tu au? Kweli za kuambiwa changanya na zako.

Ndio, kupewa ahadi za uongo is worth bringing up. The bar is set higher kwa upinzani, viwango na vipimo vya upinzani lazima viwe juu zaidi.

Hayo mengine aliyoyaongea Mbowe wapo watu wanayajadili mahala pengine, si lazima na mimi niyaongelee.

Lakini naona mada hii haijapendwa, hata jukwaa limefichwa ndani ya thread nyingine inayoipa CHADEMA taswira chanya. Naelewa JF wanafanyiwa udhalimu na watawala kwa hiyo lazima wawe biased against serikali, lakini cha ajabu mada ya Mbowe katoa ahadi mbovu inazimwa halafu inayoachwa mpaka inakuwa sticky ni hoja za Wema kalala Madale.
 
Tunaomba usimpangie mbowe cha kufanya. Akiwa tayari atazitoa. Ukionyeshwa au usipoonyeshwa unapungukiwa na nini?

Kwa hiyo kama Magufuli hapangiwi cha kufanya Mbowe nae anafuatisha modus operandi ya Magufuli? CHADEMA lazima wajitofautisha na C.C.M.

Kiongozi anaeheshimu watu hawezi kusema "msinipangie cha kufanya."

Na kapangiwa na nani? Yeye mwenyewe ndio katoa ki-ahadi kimemshinda.

kwahiyo ulichanga ili uone picha za mgonjwa?

Hapana, nimeulizwa tu kama nilichanga. Sikujiongelea from the blue sky.

Mbowe ndio hakuulizwa, ametoa tu ahadi out of thin air.
 
Hakika Mbowe hukua mwenyekiti kwa bahati mbaya. Umekua kiongozi bora kwa kundi la viongozi wenzako, hakika inatia moyo sana.
 
Picha za nini, we ni mkewe.?

Okay, kwa hiyo picha wanapewa wake zake Lissu, Mwenyekiti Mbowe alipoahidi picha alitufanya sisi wake zake Lissu?

Matusi kama haya ni dhihirisho mojawapo la saratani inayokula upinzani wa Tanzania, hakuna mfumo wa kusahihishana.

Weka za baba yako mpuuzi mkubwa

Again, kushambuliana na maneno ya ngebe, a salient feature ya upinzani wa Tanzania, hakuna mfumo wa kujisahihisha na kukosoana. Mnakosoaje serikali nyinyi msiguswe?

Tundu Lissu mwenyewe, an iconic opposition figurehead though he may be, is patently guilty of this, wanaendekeza infighting, wamekosana na Zitto, wamekosana na Slaa, wamekosana na Gwajima, wamekosana na Lipumba. Hawana mfumo wa kukosoana bila kuzua tafrani.

Kwa hiyo hii tyranny ya watawala ipo mpaka kwa wapinzani na raia.

Wanasema societies get the leaders they deserve. Watawala huwa wanafanana na watu wao.
 
Picha kwani humjui?

It is a point of principle.

Ukiahidi hata madogo deliver madogo! Heshimu hadhara inayokusikiliza.

Usipande jukwaani kujiongelea ongelea mambo tu tena kwa msisitizo KUANZIA LEO MTAONA PICHA. Ziko wapi?

Samahani mkuu nataka kufahamu elimu yako

Well, sina elimu kubwa kwa kweli, that I can tell you, lakini masuala ya siasa nimeyafahamu kiasi kwa kuyafuatilia kwa karibu nilipokuwa nchi za wenzetu waliopevuka kisiasa, lakini hata kabla ya hapo tangu nikiwa mdogo mno nilikuwa napenda kupekua-pekua makabrasha ya baba kutafuta magazeti aliyokuja nayo, kazini walikuwa wanapewa majarida kama Newsweek, Economist, etc...

Kamwe huwezi kusikia kiongozi wa nchi za watu wenye upeo wa civic affairs anaahidi leo nitafanya a-be-che halafu anaingia mitini siku inapita, not in a million years! Hapa Mbowe amekosa penalti, ametoa ahadi ya uongo.
 
WanaJF

Ni Asubuhi tulivu ya Jumanne tayari tupo hapa makao makuu ya chama kikuu cha upinzani Tanzania Chadema.

Watendaji kadhaa wameshaanza maandalizi ya mkutano wa wanahabari na Mwenyekiti Mbowe.

Hali ya Usalama inaimarishwa hapa huku vijana wa ulinzi wa chama Red Brigade wakiwa wametanda kila kona ya kuelekea makao makuu kudhihirisha ujio wa kiongozi mkuu wa Upinzani Tanzania.

Taarifa za uhakika tulizo nazo ni kwamba Mwenyekiti Mbowe leo ataeleza mazito kuhusu mwanasiasa maarufu zaidi Afrika Mashariki Tundu Lissu na yanayoendelea nchini.

Tunatarajia kuwaletea live coverage ya tukio lote kupitia ukurasa huu hapa JF

Karibuni sana.

Updates

Tayari viongozi kadhaa wameshaanza kuwasili huku kukiwa na Idadi kubwa ya waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi...

Mwenyekiti Freeman Mbowe ameanza kuzungumza: Mbowe anasema....

CHADEMA Tunaamini kabisa waliomdhuru Lissu wapo na wanajulikana. Tunaamini vyombo vya usalama wanawajua waliomshambulia Lissu.

Mh Lissu ni jirani wa Waziri,tuna taarifa kuwa ile cctv Camera iliyokuwepo eneo la tukio imeondolewa,imeondoolewa na nani?

Hatuna imani na Vyombo vya Dola vya ndani si kama havina uwezo, ni kwa sababu havina dhamira.

Nieleweke kwamba hatuvidharau Vyombo vyetu vya ndani, ila vinafanya kazi kwa mashinikizo, maelekezo ya viongozi wa Serikali."

Vyombo vyetu vya ndani havina dhamira ya kumtafuta Mhalifu kwa sababu tunapenda kuamini kwamba wanamjua mhalifu.

HALI YA TUNDU LISSU KWA SASA:

Tundu Lissu ametoka ICU wiki iliyopita na mashine zote zilizokuwa zikimsaidia zimetolewa. Hivi sasa anaweza kukaa.

Baada ya siku takribani 40 za matibabu, hatimaye TunduLissu ametolewa ICU na sasa anaweza kula na kukaa mwenyewe

Mh Lissu anaendelea vizuri hatumii tena mirija kula chakula,anakula chakula anachokitaka yeye"-

Lissu amepewa damu nyingi kuliko mgonjwa mwingine yeyote aliyewahi kuwa kwenye hospitali ya Nairobi kwa miaka 20 iliyopita.

Lissu anatarajiwa kumaliza awamu ya 2 ya matibabu ndani ya wiki 1 na atapelekwa nje ya Nairobi kwa ajili ya Rehabilitation

Tunajua kabisa uharamia huu kwa Lissu umetendwa na hao tunaowatuhumu na waliotenda wanajulikana na mfumo wa kutenda uliandaliwa

Limeanzia kwa Mh. Lissu na wengine tupo kwenye 'wanted list' huu utamaduni hatukuuzoea hivyo hatuwezi kulichukua kama jambo jepesi.

Nilikuwa nasita kutoa taarifa za mgonjwa kwa sababu ni haki ya mgonjwa na si jambo la chama.

Katika awamu ya tatu ya matibabu,tutaiachia familia nafasi kufanya maamuzi, tutasaidia pale tutakapohitajika kusaidia.

Kwa sasa anaendelea vyema na tutarajie kumsikia akizungumza kuanzia leo.

Pia tutaweka picha zake kwenye mitandao kwa mara ya kwanza tokea apigwe risasi. Kama kuna picha zozote zinazomuonesha Lissu akiwa hospitali hizo sio za kweli bali za kutengeneza.

Lissu ameshambuliwa imechukua masaa mawili polisi kufika kwenye eneo la tukio, Sisi tuamini akina nani waliotekeleza tukio hilo.

Ni kweli kuna mazungumzo yalifanyika kati ya Ofisi ya Bunge na Ofisi ya KUB kuhusu haki na stahiki za Tundu Lissu kama Mbunge

Ni ukweli usiopingika kuwa mgonjwa kutibiwa na Bunge ni haki yake ya kisheria. Haya mambo yana mihemko na hutulia baada ya muda.

Suala la Lissu lina hisia kali ndani yake. Msifikiri ni rahisi mtu akukosekose kukuua halafu aseme akulipie ukatibiwe.

Tunafahamu njama zinazopangwa, lakini hatutarudi nyuma. Tunaitwa viherehere kwa kumpigania Lissu lakini tunasema, hatutaukiri umauti

Kipaumbele chetu hakijawa fedha bali kumsaidia mgonjwa apone, mambo ya fedha tutayakuta tu.

Kama mtu ni haki yake asipoipata leo, iko kesho, iko keshokutwa. Hatuzungumzi kuhusu fedha, wakati utafika muafaka.

Michango ya Wabunge wote kwa kukatwa nusu ya posho zao za siku; kundi hili limechanga Tsh Milioni 43.

Wabunge wa CHADEMA wamechanga Tsh Mil 48, viongozi na wananchi Tsh Mil 24, wanachama mbalimbali Tsh Mil 90.

Misimamo ya Chama chetu haitayumbishwa na fedha pamoja na umasikini wetu. Tunajali utu, ulinzi na kila mtanzania apate haki ya kuishi.

GHARAMA ZA MATIBABU MPAKA SASA

Hadi tarehe 12 mwezi huu wa 10 gharama ya kila kitu kilichotumika kumtibu Lissu ni 18,352, 156 kwa Pesa za Kenya sawa na Mil 412,472,250 za Tanzania.

Tunawashuru wote kwa kutufuatilia LIVE hapa JF na kupata kile kilichosemwa na Kiongozi mkuu wa Upinzani Tanzania Freeman Mbowe kuhusu Yatokanayo na Afya ya Mwanasiasa mashuhuru zaidi Afrika Mashariki Tundu Antipas Lissu.

Mungu Awabariki Nyote.

Asanteni sana.

Molemo.

Mbwembwe tu. Hivi CHADEMA ndo chama kikuu cha upinzani tanzania au chama kikuu cha kufanya udalali wa wabunge na madiwani?
 
Mtu anayejenga kauli za kujihami kila siku mara nyingi huwa ni ndie muhusika. Na kwa hili Mbowe ni mmoja kati ya watuhumiwa wa tukio hili. Ndio maana anatumia nguvu kubwa kutaka watu waamini kile anachokisema yeye. Ni suala la muda tu kila kitu kitajulikana.
Ni mawazo yako na wewe, ingawa kwa mtazamo wangu ni MJINGA tu ndio anaweza fikiria hivyo. Mwenye kujihani amehoji kuhusu kuondolewa kwa camera za cctv. Hivi mtu mwenye akili anaweza kumuhusisha huyu msemaji na shambulio lile kweli!? Yaani Mbowe au mtu wake anayo mamlaka ya kwenda kuondoa camera kwenye nyumba za/ya mkubwa serikali!? Hata kama Tanzania tuna ambiwa kwamba tunayo IQ ndogo ya kufikiri but not at that extend. (Sorry, unaitwa Maboso? mimi ni mtu wa Iringa, maboso ni yale makapi ya pombe inayoitwa Ulanzi mara baada ya kugema, don't know kama ndio una maana hiyo pia, mhehe/mbena yoyote abishe hili)
 
Kwa hiyo kama Magufuli hapangiwi cha kufanya Mbowe nae anafuatisha modus operandi ya Magufuli? CHADEMA lazima wajitofautisha na C.C.M.

Kiongozi anaeheshimu watu hawezi kusema "msinipangie cha kufanya."

Na kapangiwa na nani? Yeye mwenyewe ndio katoa ki-ahadi kimemshinda.

Hapana, nimeulizwa tu kama nilichanga. Sikujiongelea from the blue sky.

Mbowe ndio hakuulizwa, ametoa tu ahadi out of thin air.
Kwani magufuli anavyotoa ahadi uwa anapangiwa na Nani?
Katimiza?
Kwanza wewe unataka picha za lisu za nini?
 
Mbowe anapoongea kwa authority yeye ni nani hadi alipangie jeshi la polisi jinsi ya kufanya uchunguzi? All ni all hakuna kitu kinachoitwa wachunguzi huru kutoka nje period. Vyombo vyetu vya ndani haviitaji usaidizi wa kibaraka yoyote kutoka nje.

Mkuu Mh Mbowe, 1. Ni Mbunge 2. Ni kiongozi wa kambi ya upinzani kwenye bunge, 3. Ni mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani ambacho, mwanachama wake ambae ni mbunge na raisi wa TLS amepigwa risasi mchana kweupe na watu ambao vyombo vya ulinzi vina waita wasiojulikana. Mkuu nadhani unaelewa sasa authority aliyonayo Mh Mbowe kuongelea swala la kuleta wachunguzi toka nnje. Sasa mkuu we unamamlaka yepi? Wewe ni mkulu, baba J au bashite?
 
Kwa akili zako za kuambiwa ndo unaamini Dereva siyo shahidi namba moja wakati alikuepo nayye katika eneo la tukio same as Lissu. Kwsbb wanajua Lissu hawezi kuhojiwa kutokana na hali yake ndo wanajitia Lissu ndo shahidi namba moja
Ndugu, siyo jambo baya ukitumia muda wako kujiendeleza kielimu kidogo ili upate uwezo wa kupambanua mambo. Una tatizo kubwa sana la uelewa lakini bado una nafasi.
 
Kwani magufuli anavyotoa ahadi uwa anapangiwa na Nani?
Katimiza?

Taja ahadi moja ya Magufuli ambayo aliiwekea time frame, ikashindikana katika tarehe hizo.

Mbowe katoa ahadi na time frame, siku nyingine ajifunze kwamba binding statements zenye tarehe ya kutimiza ahadi hazifai.

LEO TUNATOA PICHA!

Leo imekuwa jana. Ziko wapi?

Halafu ni aibu kwa wapinzani kujipima kwa mizani ya Magufuli. You must set the bar a little higher than Magufuli. Magufuli akiiba pesa na nyinyi itakuwa sawa kuiba?
 
By the way, speaking of pesa, Mbowe kashindwa kutoa hesabu ya chama kimetoa shilingi ngapi. Alionekana hakutegemea swali lile in a million years! Manake kaja pale hakujiandaa anaomba calculator apige mahesabu pale kwa pale. Jamani, kweli hela ya mamilioni ya umma unayapigia ma calculation as you go along? Jukwaani? Hahahahaaaaa.....

Akasema chama kimejazia jazia pale pesa ilipopungua. Kimejazia jazia?

Hell no! Tupe hesabu zilizokokotolewa kwa kila shilingi ya chama iliyotumika kwa lipi lini kama ulivyoleta hesabu za michango kwa kila shilingi iliyotolewa na nani lini kufanyia nini.
 
NDUGU MWENYEKITI MBONA CCTV CAMERA YA UHAKIKA UNAYO MWENYEWE?!

Acha nikandamize kidogo maana nishachoshwa na hizi KIKI! Huyu mwenyekiti wenu sasa naona hajui anachoongea! Anazungumzia CCTV camera ambayo imeondolewa na kuhoji nani kaiondoa! mbona anahangaika wakati CCTV kamera ya uhakika (MOVABLE CCTV CAMERA) anayo ameizuia Nairobi!

Huyo dereva ni CCTV Camera tosha tena ya uhakika kuliko hiyo DEVICE ambayo mnaulizia nani kaiondoa! Dereva aliwaona hao jamaa kabla hajafika eneo ilipo hiyo CCTV Camera! Dereva alikuwa eneo la tukio na kama binadamu kuna angles ambazo ameona matukio sehemu ambayo lens ya CCTV haiwezi kuona. MSITUCHANGANYE...mleteni Dereva kwani tunaamini yeye ni zaidi ya CCTV CAMERA.

- J. Tindikai
 
Taja ahadi moja ya Magufuli ambayo aliiwekea time frame, ikashindikana katika tarehe hizo.

Mbowe katoa ahadi na time frame, siku nyingine ajifunze kwamba binding statements zenye tarehe ya kutimiza ahadi hazifai.

LEO TUNATOA PICHA!

Leo imekuwa jana. Ziko wapi?

Halafu ni aibu kwa wapinzani kujipima kwa mizani ya Magufuli. You must set the bar a little higher than Magufuli. Magufuli akiiba pesa na nyinyi itakuwa sawa kuiba?
Kwanini picha za lisu zimekushughulisha sana? Unataka kujua jaribio lenu limefanikiwa kiasi gani?
 
97 Reactions
Reply
Back
Top Bottom