CHADEMA kuweni makini na mapokezi ya Lissu wakati huu wa msiba, mnafanya kosa la kiufundi, mtawapa watu mtaji wa kiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu


Ni kipi kimepangwa na cdm kikawa kizuri kwako au nyie? Wakati walipotaka kukusanyika ili kumuombea kulikuwa na msiba pia? Huu msiba mnataka kuutumia kama kificho, ila hata kama kusingekuwa na msiba, bado cdm wasingeruhusiwa kumpokea kwa shangwe. Nionyeshe post yako ambayo cdm wamefanyiwa ndivyo sivyo, kisha ww ukaanzisha uzi kuwa hawahafanyiwi sawa, ili nijue kuwa huwa unasimamia haki?

Narudia tena, Mkapa alikuwa ni kada wa ccm aliyewahi kuwa rais wa Tanzania. Ni wapi nimekosea hapo? Na alipostaafu kwenye urais, bado alikuwa akizunguka kwenye majukwaa vya ccm, kueneza siasa za chuki dhidi ya wapinzani. Hili wala hakulifanya kwa kificho. Nadhani una kifua kidogo cha kusikia ukweli usioupenda, ndio maana unapata tabu unapokutana na ukweli unaokera. Siku huyo Mbowe au yoyote akiwa rais, unaweza kusema ni kamanda wa Cdm aliyekuwa rais wa Tanzania, na utakuwa sahihi kabisa.

Usitake kunilazimisha kumuita mtu alikuwa rais wetu tu, huku nikiacha sifa yake nyingine ambayo hakuona aibu kujihusisha nayo, tena mara nyingi sifa hiyo ya ukada, aliitumia kwa namna hasi dhidi vya upinzani.
 
Uko sahihi mkuu Tindo , huwezi kuwa Rais wa nchi hii bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa..mkapa alikuwa mwanaccm anayebusha hilo ni pimbi tu ...
 
Yako mengi tu ambayo sikukubaluana nayo katika nyanja tofauti tofauti na sina muda wa kukuaminisha. Tatizo lako ni kwamba kila siku unawashambulia wana ccm ukidai kuwa wanasifu na kuabudu kila kitu huku na wewe ukiwa na tatizo lile lile la kusifu na kuabudu kila kitu kinachotoka Chadema, yaani huna tofauti yoyote nao, tofauti pekee ilipo kuwa wewe ni Chadema na hawa wenzako nao ni ccm.

Sasa mbona hueleweki mkuu, wewe ulikuwa hutaki yeye kujihusisha na ccm wakati ndio Chama chake, ulikuwa hutaki aonekane kwenye majukwaa ya ccm kwani huo urais aliupata akiwa chama gani? Au alikuwa mgombea binafsi? narudia tena mfano siku Mbowe akiwa rais vipi ajitenge sasa na Chadema tusiwe tunamuona kwenye majukwaa ya Chadema?

Nakwambia hivi hata Rais atokee chama gani lakini bado hajondoi maana kuwa ni rais wa wote na sio wa chama fulani, najua unaelewa vizuri tu ila hizo itikadi zako ndio zinakupeleka vibaya kutaka kubadili ukweli kuwa uongo jambo ambalo haliwezekani kamwe.
 
Uko sahihi mkuu Tindo , huwezi kuwa Rais wa nchi hii bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa..mkapa alikuwa mwanaccm anayebusha hilo ni pimbi tu ...
We nae naona ni wale wale tu sasa aliye bisha kwamba Mkapa hajihusishi na ccm ni nani? Soma vizuri hiyo comment hapo uone msimamo wa hoja yake ni upi mkuu usikurupuke.
 

Hawa watu umewasahau? Kelele nyingi na matusi mtandaoni tu. Kumbuka issue ya UKUTA, hakuna aliyetoka nje, issue kulinda kula ndani ya mita 100, hakuna aliyebaki kituoni, Maandamano ya Mange, nani aliingia mtaani? Amini usiamina, j3 hakuna atakaye toa pua nje eti anaenda Airport kumpokea mtu. Ukipenda pia kumbuka azimio la Zanzibar hivi liliishia wapi?
 

Mkapa kafa kwa CORONA, manina itawamaliza maana mlikuwa wote Dodoma. Mkufe tu na ccm yenu hadi raha
 

Aliyekufa alikuwa mtu mbaya sana mwache akapate anachositahili
 
Mkapa kafa kwa CORONA, manina itawamaliza maana mlikuwa wote Dodoma. Mkufe tu na ccm yenu hadi raha
Sasa wewe mbona unataka kuchekesha watu mkuu. Kama hiyo Corona ipo na inamaliza watu namna hiyo sasa kwanini mnapanga kwenda kukusanyika huko airport kwenye hayo mapokezi hamjui kuwa ndio mnaenda kujikaanga hapo? Si mngejifungia ndani kujikinga na hiyo Corona? Wakati mwingine fikiri kanza kabla ya ku comment.
 
Lissu anawasumbua Sana.Kwa nini hujasema CCM wasisitishe kura za maoni za udiwani?Kwa Nini hijazungumzia mechi za soka zinazoendelea hapo kesho Kama kawaida?Chili yako ninkuona Lissu hapokelewi kwa uZuri.Unafiki na wivu mwisho wake Ni wanga au uchawi,we jamaa utakuwa mchawi kwa mawazo Kama haya.Utakuja kula wanao bure.
 
Haahaa yaani makamanda wataunga juhudi kisa makamu mwenyekiti Wa chama kaenda kupolewa airport? Ni miongoni mwa ushauri Wa hovyo kabisa
 
Bravo!!!
 
Mtego kivipi, unataka kusema CCM mmemuua mkapa ili uwe mtego juu ya ujio wa Lisu? Au nyie mnatumia msiba wa mkapa ka mtaji wa kisiasa wa CCM.?

Kama ni mtego kwa nini mtumie kifo cha mkapa kua mtego kwa chadema?
 
Waache wawape watu chakusema, yani we bendera zinapepea nusu mlingoti hadi nchi jirani, watu wanaacha shughuli zao za kitaifa kwenye nchi zao huko wanakuja hapa nchini alafu eti wewe mtanzania unaenda kufanya maandamano ya mapokezi.
Mkuu hivi mchakato wa Uchaguzi ndani ya CCM umesimamishwa?
 
Ushauri Kuntu...
Ushauri Maridhawa Kuliko....
Ushauri Adhimu........

Wanasema MKANYE AKIRUDI,AKENDA MWACHE...mtoa POST amefanya kinyume kwa kuwatakia WEMA...
Yeye anasema MKANYE AKENDA,AKIRUDI MWACHE....


AKILI KUMKICHWA...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…