Elections 2010 CHADEMA iwaachilie walioshinda kura za maoni wagombee

Status
Not open for further replies.
kama huna nia mbaya basi unasomeka vibaya ,just choose your words so careful zaidi ya hivyo unavyosema "nachagua maneno yangu vizuri" kama unaona unachagua maneno yako vizuri basi ongeza iwe na vizuri zaidi na zaidi.

Ningekuwa nazungumza na watu ambao wanashida ya kuelewa nilichoandika ningetafuta maneno mengine "mazuri zaidi". Kwa sasa ninayotumia yanajitosheleza.

Watu wame quote hapa maneno yako kuhusu CCM (NEC) kurudisha watu fulani kwa sababu unazoona ww za msingi ,Lakini hapa hutaki kitu kama hicho .Je leo ndio unaelewa maana ya demokrasia?

Kama hujasoma jibu langu, halafu nirudie jibu lile lile na wewe uulize swali lile lile hatutafika.

My take: kuhusu chama chochote kinacofanya kuhusu kuhusu wagombea wao ni kwa maslahi ya chama na wanakuwa na sababu na lazima kutakuwa na maongezi kwa wahusika na makubaliano.

Ni mfumo mbovu wakati wowote ambapo wapiga kura waliopiga kura kutoa pendekezo lao wanapopigiwa veto na watu ambao hawakupiga kura kwenye maeeneo hayo. Vinginevyo wasingewapa nafasi ya kupiga kura.

Pia kama mtu yeyote anaweza kujibu je ,je kura za maoni kwa kiasi gani zina reflect kura za wananchi wa jimbo hilo(ushindi)?Je analysis ikifanyika kuakikisha ushindi si vyema makubaliano yakawepo.?

Haijalishi; kura za maoni ni kwa ajili ya kupata mgombea wa chama fulani. Sasa kama wanachama wa huko watachagua mtu ambaye hachaguliki na wapiga kura wote hilo ni swala jingine.

Kwa kuwa hiini tetesi ,na mmoja wawahusika ni member hapa ,basi mimi naimani tutie subira tutakula vitamu.

hiyo inaitwa hekima.
 
Hakuna namna yoyote ile habari kama hii, kama itatokea kuwa si ya kweli, inaweza ikatetewa kuwa ilitolewa kwa nia nzuri. Kama aliyeileta atajitetea kuwa ilikuwa ni tetesi then it is one in very bad taste - angalia hukumu dhidi ya Chadema ilivyopamba moto humu. Imefikia mahali hata watu ambao kwa kawaida misimamo yao ni kama mwanga na giza wamepata mahali wanapokubaliana, kuilaani Chadema. Sisiti kutamka kuwa hata mimi nitaungana nao katika kufanya hivyo but only if any of this is true.

Wasiwasi wangu mwingine ni timing ya hii habari - ni kama vile lengo la aliyeileta ni kuplay down hayo yanayotokea CCM kama alivyofanya Msekwa akielezea vitendo vya rushwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM, kwamba tatizo la rushwa si la CCM peke yake !

Mag3.. kwa kweli fikiria hivi:

Chadema na CCM wote wamefanya kura za maoni katika majimbo mbalimbali.

Hadi hivi sasa sijakumbuka kama kuna mtu yeyote wa Chadema ambaye aidha amekamatwa na TAKUKURU au kutuhumiwa kuwa alitumia rushwa au kuvunja taratibu na kushinda kwa jimbo.

Hivyo, kwenye majimbo ambayo Chadema tayari wamesimamisha wagombea matokeo ni safi na yanatakiwa yasimame yalivyo.

CCM hata hivyo imeamua kuwaengua wagombea wake mbalimbali (na tutajua zaidi kesho) kwenye majimbo kadhaa kutokana na kati ya mengi vitendo vya rushwa n.k

Wagombea watakaoengeliwa na CCM watajikuta wanakimbilia kwenye Chadema (ambako wapo walioshinda kihalali!).

SAsa ubovu ni kuwa Chadema imekopy na kupaste mfumo ule ule wa CCM wa kutumainia Kamati Kuu kufanya maamuzi ya mwisho nani agombee na nani asigombee (regardless kama ameshinda kihalali au la). Sasa Chadema ikiamua kumwomba, kumtaka, kumshawishi au kutumia proxies kupeleka ujumbe kuwa fulani ajitoe ili kumpisha mtu mwingine (awe wa CCM au mwingine tu wa Chadema) basi inaingia kwenye mtego ule ule wa CCM.

Binafsi naamini on principle kwamba CHadema kama kuna majimbo ambayo wanajua kuna wana CCM wanataka wakitemwa basi majimbo hayo wasingepiga kura za maoni. Lakini mahali pale ambapo wagombea wameshinda Chadema inatakiwa kuheshimu matokeo hayo no matter what. Suala la "CHama kimeona hekima, chama kimemuomba naye amekubali kwa moyo mkunjufu, au Chama kimeonelea x anakubalika zaidi" ni suala la kinyume cha demokrasia na ni mfumo wa utawala wa ukuu wa chama na siyo kanuni ya demokrasia.

Chadema ni lazima siyo tu ioneshe kuwa ni bora kuliko CCM, lakini itende kuonesha ubora wa utofauti huo? Kama tunakataa nguvu kubwa kuwa ndani ya CCM kama Chama kwanini tuje kujikuta tunakubali kuwa nguvu kubwa ziwekwe ndani ya Chama? Kama Kamati Kuu ya CCM inatupelekesha hivi kila wakifanya kikao si itakuwa vurugu kama kamati kuu ya chadema nayo itafanya yale yale? Mimi nataka Chadema iwe juu ya kufanana na CCM. Najua hili limechelewa lakini limechelewa si kwa sababu halijasemwa bali kwa sababu baadhi hawaamini kuwa ni muhimu sana.

Na miye nasubiria kusikia wagombea wote waliopendekezwa na wananchi wanasimamishwa kugombea bila y akujali gharama vinginevyo, wangewachuja kabla ya kura za maoni kujipunguzia kazi baadaye.
 
Kinachonisukuma kuwasikiliza pande zote mbili na bila shaka kama uongozi utaridhia hilo, i will support them under the following conditions;
  • Mfumo wa CHADEMA kwenye kura za maoni ni tofauti na CCM. just imagine kwenye mkutano mkuu kulikuwa na watu not more than 800. Hata mimi nikienda wilaya fulani nikaenda kugombea CHADEMA bila shaka watanipitisha lakini kama akitokea mtu potenial, ruksa kunitupilia mbali (SITAUZIKA). Mfumo wetu kama kweli tunataka kubase on primary vote basi wa CCM ndo mzuri zaidi kwani uwanja ni mpana, kwani wasifu wako unajulikana zaidi na kabla ya kuvote waliweza kupata maoni ya ambao sio wa CCM. Hii ndo ilimwangusha Bashe kwa kiasi kikubwa pale Nzega. Hakika walikuwa wanansubiri Bashe arudishwe ili upinzani (CUF) wachukue.
  • Resources: Networking. uzoefu katika eneo husika, kwa mfano wakazi wa segerea nahisi mnajua wengi wametoka wapi. MONEY. tunahisi watz wote wanahulka kama ya kwetu ila kwenye mchakato wa upigaji kura mpaka matokeo hapa ndo tumbwili za CCM zinapofanya kazi, hasa kama majamaa hayajapata lunch na uhakika wa maji ya pansiasi au ilala. Hakika ubunge katika kipindi hiki ni suala la mtu binafsi kwa kiasi kikubwa kwani chama sidhai kama kinaweza kukidhi mahitaji ya kila mtu/mgombea.
  • Mtandao wa chama: bado upo at the middle and high level. naamanisha mkoani na taifa. Kuna baadhi ya wilaya CHADEMA haina ofisi na kama kuna ofisi ni few people who can make decision ikaonekana kama ni ushindi lakini tukubali bado.
  • Uwezo binafsi wa watu: nausoma uwezo wa GS hapa, naupenda sana ila ni mapenzi yangu binafsi. Huenda opponent wake ni vema akapambana na fulani halafu fulani GS apewe upendeleo. Haya yote yanawezekana kwa nilimsikia Mbowe akisema kuwa wanataka wale wa viti maalumu ambao wapo tayari kupigania jamii sio matumbo yako. Kwa kuangalia mchango wao huenda ni vizuri wakabaki makao makuu this time kushughulikia majeshi yalio mstari wambele ili kufanyikisha lengo then watapendelewa.
based on that, nasubiri muongozo wa chama kama ya MKJJ yana ukweli bila shaka watatuambia maana Mbowe amekataa kubadili kule Tarime kwa msemo kuwa maoni ya wenyeji yaheshimiwe. Je itakuwa Kilombero au Segerea? je kwanini walipoteza muda wa watu while wanajua potential candidates? tusubiri, tuone ila tusihukumu haraka haraka.
 
Some quick explanations:

i) Utaratibu wa CHADEMA wa kuteua wabunge ni kama ifuatavyo:
  • Kamati Tendaji ya Jimbo inafanya uteuzi wa awali, kwa kuwa-rank wagombea kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho. Kamati Tendaji ya Wilaya inaweza kushirikisha wanachama wengine katika jimbo kwa njia ya kura ya maoni ili kujiridhisha na uungwaji mkono wa wagombea husika. Kwa mwaka huu, kulikuwa na waraka maalumu wa Katibu Mkuu unaowataka Makatibu wa Wilaya, pale inapowezekana, kufanya kura ya maoni kabla ya kufanya uteuzi wa awali.
  • Kamati Kuu inafanya utafiti kuhusu wagombea wa kila jimbo. Kwa kutumia matokeo ya utafiti na maoni ya Kamati Tendaji za Jimbo inafanya uteuzi wa mwisho. Uteuzi wa Kamati Kuu unaweza kuzingatia maoni ya Kamati Tendaji, Taarifa za utafiti au yote.
  • Katika uteuzi wake, Kamati Kuu inazingatia mambo makubwa mawili: Kuchagulika kwa mgombea kwa wananchi wa jimbo na jinsi mchakato wa kumpata mgombea ulivyofanyika-lengo ni kuhakikisha kuwa wagombea wote wanapatikana kwa utaratibu unaozingatia misingi mama ya CHADEMA, namely: maadili na uadilifu, pamoja na taratibu za uchaguzi ndani ya CHADEMA.
ii) Kuhusu majimbo ya Kilombero na Segerea: Kulikuwa na rufaa kutoka kwa wagombea waliopata kura chache zikilalamikia kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi na misingi ya chama.
iii) Kamati Kuu ilikubaliana na rufaa ya Kilombero na inaendelea kushughulikia.
iii) Kamati Kuu haikukubaliana na rufaa ya Jimbo la Segerea na hivyo iliitupalia mbali.
iv) Katika taarifa ya utafiti iliyowasilishwa, pamoja na umahiri wa kisiasa wa Mhe Masishanga, Kamati Kuu ilijiridhisha kabisa kuwa Mhe Mpendazoe ana nafasi zaidi kwenye nafasi ya ubunge kwa sasa. Mazungumzo yanaendelea kuhakikisha kuwa wananchama hawa wawili wanafanya kazi pamoja kuhakikisha kuwa CHADEMA inashinda ubunge na nafasi za madiwani katika jimbo la Segerea.

Kwa hiyo utaona hapa kuwa utaratibu wa kuwapata wagombea ubunge ndani ya CHADEMA unatofautiana mno na ule wa CCM. Kwa hiyo ulinfganifu uliofanywa sio wa kimantiki.
 
Nyongeza: Hii ndio kusema kuwa uamuzi wa nani atagombea Jimbo la Kilombero haujafanyika, na utatolewa by end of kesho
 
SAsa ubovu ni kuwa Chadema imekopy na kupaste mfumo ule ule wa CCM wa kutumainia Kamati Kuu kufanya maamuzi ya mwisho nani agombee na nani asigombee (regardless kama ameshinda kihalali au la). Sasa Chadema ikiamua kumwomba, kumtaka, kumshawishi au kutumia proxies kupeleka ujumbe kuwa fulani ajitoe ili kumpisha mtu mwingine (awe wa CCM au mwingine tu wa Chadema) basi inaingia kwenye mtego ule ule wa CCM.

Mkuu,with all due respect, hiyo nukuu fupi tu inaashiria kana kwamba Chadema wameshapitisha wagombea na kuchuja baadhi ya walioshinda kura za maoni.Kwanini tusiihukumu Chadema kwa facts na sio tetesi?

Nahofia tetesi za aina hii kwa vile hata huko nyuma CCJ "walipozembea" kushughulikia usajili wao tuliambiwa habari zenye kila dalili ya uhakika (kama hii) kuwa tutarajie makubwa...mara sijui kwa mabalozi,na hadithi kama hizo...leo hii CCJ ni marehemu!

Sidhani kama ni sahihi kuihukumu Chadema kwa misingi ya tetesi.Haraka ya nini ilhali jua liwake lisiwake lazima chama hicho kitatangaza waliopitishwa?Kwahiyo laiti majina yanayodaiwa kuenguliwa yakiwepo kwenye orodha ya wagombea itamaanisha "tahadhari yako" imesaidia "kuepusha ubabaishaji wa Chadema"?

Again,with all due respect,kama ambavyo sitegemei Makamba au Mrema "kuitakia mema Chadema" sidhani kama die-hards wa CCJ wanaweza kuitakia mema Chadema...hasa ikizingatiwa kuwa siku chache tu zilizopita baadhi ya wenzetu mlionyesha bayana kutoamini kuwa chama hicho kinastahili kupewa dhamana ya uongozi wa nchi yetu.

Pamoja na reputation ya mwandishi husika,ukikutana na tetesi kuhusu Chadema katika jarida la Rai,Mtanzania,Habari Leo,Uhuru au Mzalendo,na hata kama mwandishi anadai habari hiyo ni ya "kuisaidia Chadema",ni vema msomaji akaisoma with suspicion...
 
Politically tuseme watu wa Tanzania bado tuko weak, kutokana na hiyo vitendo vya corruption haviepukiki. Katika hali ambapo corruption haiwezi kuepukika anything can happen; Chama tawala kinaweza kutumia kupenyeza watu wake ndani ya upinzani. Kinaweza vile vile kutumia vyombo vya dola ambavyo tunajua wote kuwa bado viko very weak na open to manipulations by politicians. Polisi na hata UWT mara nyingi vimeonekana kufanya uwakala kwa chama tawala na katika hali kama hii inakuwa ni vigumu sana kwa vyama vingine kushindana kwani playing field haiko level.

Hata hivyo, katika hali kama hii transparency ndo best weapon. Transparency sometimes inakuwa na costs zake, lakini ndo njia pekee ya kuhakikisha mambo yanaenda. Sasa hivi hali ilivyo ni kuwa Tanzania kwa kweli vyama vya siasa hakuna idiological differences kwa hiyo mara nyingi hawajiungi vyama kwa sababu ya idiology. Watu wanajiunga vyama kwa sababu ya kuona political opportunity ya kukua haraka iwezekanavyo na kufikia kwenye position of power. Katika hali kama hii ni vigumu sana kwa vyama vya siasa kuendesha shughuli zake, lakini hata pamoja na hiyo umakini na transparency ni vitu vinavyotakiwa.

Ikiwa vyama vinalengo la ku-filter out wagombea na kuhakikisha kuwa vinapitisha wagombea ambao wanachagulika na wanashindana transparently iko sababu ya kuwafanyia wagombea interviews. Tatizo la watanzania sehemu zote ni competence. Ukisema zifanyike interview mwanzoni kuna uwezekano mkubwa interview hizi ikawa ndo chanzo cha malalamiko. Kwa hiyo utaratibu wa sasa wa kila mwenye nia kuingia kugombea unaonekana kufaa. Lakini si kila mwenye nia anakuwa na uwezo wa kutosha. Kwa hiyo vyama vinaona kuwa iko sababu ya kuwa na last say katika kuamua nani awe mgombea. Hili ni jambo linaloeleweka. Lakini hatari yake ni hii ya kufanya maamuzi kama vyama vya Kikomunist bila kuwa na transparency. Ikiwa kuna lazima kwa vyama kubadilisha maamuzi ya kura za maoni, ni lazima mchakato wake uwahusishe wapiga kura. Kama mgombea ana tuhuma, transparently ni lazima vyama viwahusishe wapiga kura. Hili la kukaa kwenye vikao vya siri, kushughulika na taarifa za siri na kutoa maamuzi ambayo hatimaye huwa bayana ndo tatizo hasa.

Ikiwa wapiga kura wa maeneo husika wangehusishwa kushauliwa haya malalamiko yasingekuwepo. Mara nyingine maamuzi huwa ni supprise hata kwa wagombea wenyewe. Sasa hili ni tatizo.

Sasa kama CHADEMA ilikuwa na sababu za msingi kabisa za kuwabadilishia mgombea wanachama wao, zoezi hili lingefanyika transparently na wanachama wakajua sababu za kufanya hivyo isingekuwa tatizo. CCM wamekuwa wakifanya hivyo muda mrefu na tumeona maeneo mengi hili limekuwa likileta matatizo sana. Sasa kwa chama kinachotoa matumaini ya mbadala kuangukia kwenye mtego ule ule si jambo jema. Ilitakiwa umakini mkubwa utumike kufikisha habari kwa wapiga kura wa Chadema wa Majimbo husika wajue sababu za maamuzi hayo. Kama hilo litakuwa limefanyika hakuna tatizo. Lakini kama ni yale yale ya kamati kuu na halmashauri kuu za CCM; chama ambacho bado kinanuka mbinu na mikakati ya kikomunisti; basi Chadema itakuwa na kazi ngumu ya kuushawishi umma wa watu makini.

Nimekuwa nikielezea sana umuhimu wa Chadema kusimamisha wagombea bora wa Ubunge majimbo yote ya uchaguzi. Lakini katika kutekeleza hili ni lazima Chama kihakikishe kinatumia uwazi na umakini wa hali ya juu ili kuepuka matope kama haya kukifuata chama.
 
Kama ni kweli....Chadema hawapaswi kufanya hivyo..ni vema Demokrasia ikafuata mkondo wake..but sina uhakkika na hili MM..!Kwani baada ya Mpendazoe kuanguka Segerea ilikuwa ajaribu bahati yake tena pale Kinondoni sasa..hili ni jipya kwangu..!
 
KUtokana na maelezo mazuri ya Kitila mkumbo inaonyesha wazi mwanakijiji unadandia gari LA jeshi kwa mbele ,you try to be smart !!! Unalisha watu sumu hapa
 
Some quick explanations:

i) Utaratibu wa CHADEMA wa kuteua wabunge ni kama ifuatavyo:
  • Kamati Tendaji ya Jimbo inafanya uteuzi wa awali, kwa kuwa-rank wagombea kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho. Kamati Tendaji ya Wilaya inaweza kushirikisha wanachama wengine katika jimbo kwa njia ya kura ya maoni ili kujiridhisha na uungwaji mkono wa wagombea husika. Kwa mwaka huu, kulikuwa na waraka maalumu wa Katibu Mkuu unaowataka Makatibu wa Wilaya, pale inapowezekana, kufanya kura ya maoni kabla ya kufanya uteuzi wa awali.
  • Kamati Kuu inafanya utafiti kuhusu wagombea wa kila jimbo. Kwa kutumia matokeo ya utafiti na maoni ya Kamati Tendaji za Jimbo inafanya uteuzi wa mwisho. Uteuzi wa Kamati Kuu unaweza kuzingatia maoni ya Kamati Tendaji, Taarifa za utafiti au yote.
  • Katika uteuzi wake, Kamati Kuu inazingatia mambo makubwa mawili: Kuchagulika kwa mgombea kwa wananchi wa jimbo na jinsi mchakato wa kumpata mgombea ulivyofanyika-lengo ni kuhakikisha kuwa wagombea wote wanapatikana kwa utaratibu unaozingatia misingi mama ya CHADEMA, namely: maadili na uadilifu, pamoja na taratibu za uchaguzi ndani ya CHADEMA.
ii) Kuhusu majimbo ya Kilombero na Segerea: Kulikuwa na rufaa kutoka kwa wagombea waliopata kura chache zikilalamikia kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi na misingi ya chama.
iii) Kamati Kuu ilikubaliana na rufaa ya Kilombero na inaendelea kushughulikia.
iii) Kamati Kuu haikukubaliana na rufaa ya Jimbo la Segerea na hivyo iliitupalia mbali.
iv) Katika taarifa ya utafiti iliyowasilishwa, pamoja na umahiri wa kisiasa wa Mhe Masishanga, Kamati Kuu ilijiridhisha kabisa kuwa Mhe Mpendazoe ana nafasi zaidi kwenye nafasi ya ubunge kwa sasa. Mazungumzo yanaendelea kuhakikisha kuwa wananchama hawa wawili wanafanya kazi pamoja kuhakikisha kuwa CHADEMA inashinda ubunge na nafasi za madiwani katika jimbo la Segerea.

Kwa hiyo utaona hapa kuwa utaratibu wa kuwapata wagombea ubunge ndani ya CHADEMA unatofautiana mno na ule wa CCM. Kwa hiyo ulinfganifu uliofanywa sio wa kimantiki.

Mh. Kitila Ikiwa Mashishanga kakataa kumpisha Mpendazoe, Chama kitalazimisha kumsimamisha Mpendazoe?

Siasa ni kamari ngumu sana.
 
ai .....mwanakijiji alikuja na mfumo dume! kazi kweli kweli, wakati kuna rufaa imekatwa. Mwanakijiji ulikuwa unalijua hilo kwa nini ulipuuzia fact hiyo muhimu?
 
We Kitila, acha kuwa kama Makamba na kufanya spinning za kitoto. Kama rufaa ya Mpendazoe ilishindwa na Rachel ndie mshindi halali iweje tena Kamati kuu ione Mpendazoe ana "nafasi zaidi?" na hayo mazungumzo yanayoendelea ili kuhakikisha wawili hao wanafanya kazi pamoja ni porojo za kisiasa kwani ina fahamika wazi Mpendazoe kishachukua form kwa baraka zote za chama na Rachel ndio kishapigwa chini.

Kitila you can do better than this, kwenye hili taratibu zote kama ulivyo zianisha hapo juu zimefuatwa na Rachel kashinda na Mpendazoe akakata rufaa ambayo imetupwa sasa huko kukubalika kwa Mpendazoe kumetoka wapi?

Huyo Regina nae ndioe mshamtosa mnamlia timming tu, yale yale mizengwe mizengwe, ujanja ujanja basi
 
Kwa heshima ya viongozi wangu chama CHADEMA, ni matumaini yangu hawata fanya kosa CCM walilolifanya kwa DR. W.P. SLAA mwaka 1995.
Mtu mwenye akili timamu akachukua form akafanya kampeni akashinda primary, akamshinda na mpendwa wa viongozi wa kitaifa akaombwa ampishe mwenye alama ndogo kwa sababu alipitiwa tu ila ndiye wananchi wanamtaka. Namkumbuka Liberman, aliwambia wenzake naipenda USA kwani ina wagombea binafsi.

Hapa siasa za africa ni maigizo, unaweza kuwekeza kichakani. Demokrasia bado ni kitendawili Tanzania hata ukiwa Professor. Sasa kweli kule kijijini kwetu kibondo mtawalaumu? Ninyi wasomi hamueleweki?!!!!

Next time nitagombea uenyekiti wa CHADEMA taifa natumaini nitashinda, jina langu hakuna mtu atakayekubaliwa kuliondoa hata mfanye vikao vya kuua mtu. Nikishinda nitaifumua hiyo katiba kwa gharama yeyote. Primary zitakuwa kwa wananchi wote. mwenye nyingi bila ya rushwa atakuwa mgombea hakuna kikao wala majungu. Viongozi wa wananchi kutoka kwa wananchi, kuongoza wananchi kwa ajili ya nchi yao hakuna wa kuogopwa. Wakimtaka wenyewe ni wao.

Jitahada za mwanachama zitaheshimiwa, kazi za wanachama zitaenziwe, washindi watapata tunzo ya kuwa viongozi kwa mujibu wa katiba. Hakutakuwa na tabaka wala wateule, hakutakuwa na woga kwamba kuna kundi linangojewa, wanachama watakuwa hai siku zote, mamia watapenda chama kwani watapata ladha tofauti. Kutakuwa hakuna kupeana madaraka kwa kisingizio usubirie cha bure. Viti maalumu havitakuwa sadaka, tutataka tuone uwiano na kukubalika kwenye kundi husika. Demokrasia na misingi imara inagharama tutalinda na tutakuwa tayari kugharamia.
 
Mh. Kitila Ikiwa Mashishanga kakataa kumpisha Mpendazoe, Chama kitalazimisha kumsimamisha Mpendazoe?

Siasa ni kamari ngumu sana.

Sawa kabisa!
Na kwanini huyo Mpendazoe asipelekwe kwingine au kwanini Ms Masishanga ndio "atoe sadaka" nafasi yake ilhali tunataka kuwapa fursa wanawake wenye uwezo nao wapambane badala ya kupewa viti vya upendeleo?
 
Nadhani kati ya wengi mimi naitakie Chadema mema zaidi; lakini not at the expense of other values. Na hapana sijawahi kusema kuwa lengo lisiwe kuing'oa CCM madarakani mwaka huu. Napima maneno yangu vizuri.
MKJJ

Wakati najiunga JF nilikuwa naheshimu sana topic zako MKJJ lakini kadri muda unavyokwenda nagundua kuwa you are not the one I was thinking, you like controversial issues ziwe habari za CCM, Chadema au vyama vingine bila kukiacha chama Chako cha CCJ.

Unapenda kusema lakini ukiwa pin pointed unakana uliyoyasema na huwa unatumia neno la msiniwekee maneno, angalia maneno kama haya kama kweli wewe unaitakia mema Chadema, kwa mtu mwelevu na mpenzi wa chama atataja haya katika kipindi hiki Chadema ilivyo vitani?
Kwamba wagombea kama Regia Mtema (kilombero) na Rachel Mashishanga (Segerea) wameombwa kuachia nafasi zao kuwapisha watu wengine (wote wanaume) ....(umeweka brackets kuonyesha msisitizo kwa ulichotaka watu wakichukue) .........

Lakini haya ya kuonekana kubebwa na chama kwa sababu yoyote hayaoneshe "demokrasia" bali ukiritimba wa mfumo dume ambao utawasumbua Chadema baadaye. Ni kweli kuwa katika nafasi karibu zote za juu za Chadema zinashikiliwa na wanaume lakini sitaki kuamini kuwa hilo pekee linaweza kuwafanya wasione umuhimu wa kuwalinda wagombea wake waliojitokeza.

Lengo lako hapa si kuwatetea Regia na Rachel ni kutaka ku create controversy katika jamii na ndani ya Chadema kwa kigezo cha jinsia, Period, kwa kutumia kigezo cha Regia na Rachel tu kwako Chadema ndiyo imekuwa chama cha wanaume?, hapo utasema unaisaidia Chadema kweli? Pamoja na hayo maneno yako tukija kukuuliza baada ya mwezi mmoja utayakana kama ulivyofanya wakati wa CCJ.

Navyoona wewe MKJJ si mtu wa kuaminika, hata kama unaisaidia CCM lakini nayo isikuamini kwa 100%. Ushauri wangu kwako you can opt to take it or not, hadi sasa watu wameshakuelewa na malengo yako ni yepi unatumia umaarufu wako JF kutimiza malengo yako, to mention a few hata Chadema kama chama nafikiri wanakujua you are not on their side even if you are pretending to be. Therefore choose one side and sticky to them I can assure you will be a geat person.
 
Nyongeza: Hii ndio kusema kuwa uamuzi wa nani atagombea Jimbo la Kilombero haujafanyika, na utatolewa by end of kesho

jimbo la kishapu mshapata mtu wa kumsimamisha au bado? kama bado huoni kama mpendazoe anaweza kushinda kule kwa ajili alikuwa kule na ana network kubwa.....
je jimbo la segerea mapatano yamefikia wapi???

lini orodha ya wabunge wenu itakuwa tiyari
 
MKJJ naomba nikuulize swali dogo tu, kama CCJ kingesajiliwa na wewe ukagombea say ubunge au uenyekiti. Kwenye mchujo wa kwanza wajumbe walikuwa 20 ukachaguliwa kwa kura 12, kabla ya uchaguzi akaja mtu potential say Butiku au SAS watu wakakuomba umpishe ili akijenge chama busara yako ikoje hapo utakataa.
 
Demokrasi bila busara nayo ni hatari, tunajua Chadema bado ni chama kichanga hakijafika kila sehemu, chukulia mfano jimbo fulani chama kipo kama hakipo ofisi iko nyumbani kwa mwenyekiti, siku ya primaries watu 12 tu wanajitokeza kuchagua mgombea mmoja kati ya watatu waliojitokeza, mgombea X anapata kura 6 mgombea Y kura 4 wa tatu Z kura 2, definitely mgombea X kapita.

Hapo demokrasia imetumika mgombea X ameteuliwa kugombea kwa kupata kura 6 na kuwazidi wapinzani wake wote. Tuseme jimbo zima lina wapigakura 25,000 na huyo mgombea X wa Chadema aliyepata kura 6 anatarajiwa kupambana na mgombea wa CCM aliyemaliza muda wake ambaye ameteuliwa kulitetea jimbo lake.

Sasa jamani MKJJ na wengine tujiulize na tujaribu kutumia busara akitokea mtu potential figure ameombwa na chama kugombea dakika za mwisho tutamkataa kwa kuhofia kuvunja demokrasia au zile kura 6 alizozipata X tutazipoteza? Hebu tuwe wakweli.

Mimi bado naendelea kusema na nitasema kwa sauti kubwa lengo la MKJJ si kutetea demokrasia au jinsia ndani ya Chadema lengo lake ni ku create co motions ndani ya chama na jamii, lakini bora naona watu wengi wamemshtukia mapema na nashukuru Kitila amejitokeza mapema na kuliweka sawa jambo hili.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom