Elections 2010 CHADEMA iwaachilie walioshinda kura za maoni wagombee

Status
Not open for further replies.
hii ya Mwanakijiji ya kufikia hatua ya ku-imply kuwa ndani ya chadema kuna mfumo dume naona ni hatua mbaya sana hata kama unapigania wagombea unaowapenda wewe kurudi bungeni. You have done more harm than good kwa wagombea hao na chama.

Lakini labda iwe ndio dhamira iliyokuwepo tokea awali.
 
Yaani huyu binti Regia ameondolewa kwenye kinyang'anyiro kile pamoja na uimara wake wote katika kujenga na kutetea hoja alionyesha hapa? Mbona naona kizunguzungu kabisa.
 
endapo chama kitasema kuwa vyanzo vyangu havikuwa sahihi na wote niliowataja wakaruhusiwa kugombea basi lengo litakuwa limefanikiwa. Lakini kwamba wamekusudiwa kuenguliwa halina shaka.

Kama hii habari ni kweli inakatisha tamaa. Demokrasia ya kweli inagharama zake, kubwa ya gharama ni kuheshimu kura na matokeo yake. Kama hawa walishinda lazima waachwe labda wao wenyewe bila ya kushinikizwa waamue kuachia ngazi. Natumaini wanalizingatia hilo.
Kwa sababu wahanga ni wana jamvi watakuja kutoa maelezo. nami nalifuatilia makao makuu kupata udhibitisho.

Ila mzee wa jamvi swala la kuendeleza udume nalo liko nyuma ya kuenguliwa wadada hawa?
 
Yaani huyu binti Regia ameondolewa kwenye kinyang'anyiro kile pamoja na uimara wake wote katika kujenga na kutetea hoja alionyesha hapa? Mbona naona kizunguzungu kabisa.

Mwl. Kichuguu, Kwa jinsi nilivyomsoma Mkjj, nadhani amefanya hivyo kwa lengo la ku-pre-empt tetesi/habari aliyokuwa ameambiwa ili fursa hiyo isitokee. Na ndiyo maana hapo juu amesema kwamba, kama hilo halitafanyika basi ujumbe utakuwa umewafikia. Na umeona reaction ya wanaJF hapa kama hilo lingefanyika ndani ya Chadema...
 
Karaga bao mpendazoe amesha chukua form za ubunge jana!
 
Umeanza kubadili kauli. Unasingizia "chanzo changu" sasa.

Eti "wamekusudiwa kuenguliwa." Ulisema hivi:

"Kwamba wagombea kama Regia Mtema (kilombero) na Rachel Mashishanga (Segerea) wameombwa kuachia nafasi zao kuwapisha watu wengine (wote wanaume) ni jambo la kufanya watu kutikisa vichwa vyao. Chadema haiwezi kuendelea kusubiria viti vya vijana au wanawake ili kuwapa nafasi za kugombea."

Wameombwa na nani? Wadau wanakuuliza.

Unapoandika kwenye Tanzania Daima, na Michuzi, na hapa JF, kumbuka kutofautisha walengwa ni kina nani haswa, kukaa kote Michigan mvua kibao hujajifunza umakini wa uandishi wa kiukweli?

Sasa, chama ambacho kinataka kuleta mabadiliko cha CHADEMA kinasikitisha kuwa nacho kimerithi na kukumbatia mfumo huo huo mbovu. Habari kwamba baadhi ya wagombea wake walioshinda katika kura za maoni baada ya kufanyia jasho kuenguliwa na vikao vya juu vya "chama" ni habari za kusikitisha na zinaonesha kuwa mfumo ule ule mbovu wa demokrasia ya 'chama' umerithishwa ndani ya Chadema na utaleta matatizo yale yale (kama bado haujaleta).
 
Asante sana Tindikali nilikuwa natafuta makala hii niibandike.

MMKJ anasema wanaCCM wamefanya makosa kuwaondoa wapiganaji warudishwe hata kama hawakushinda, kwa CCM ni sawa, likifanywa na Chadema the same MMKJ anasema 'Chadema iwaachilie walioshinda kura za maoni wagombee' kama si kutafuta angalau kadosari kokote ndani ya Chadema ili aiseme ni nini.

Infact i dont understand this guy nowdays, toka ajichanganye na CCJ ame lose control ya kufikiri he is not the same again. Anajitahidi sana asionekane kijani kwa kujifanya yeye nuetral kama yupo kama hayupo red(Chadema).

Nilisha mwambia asipoangalia atapoteza credibility yake lakini yeye he doesn't care anasema hatafuti umaarufu ni sawa basi uwe consistent na mambo yako uta lose kote kote. This is another grave mistake to you like that of CCJ.

Luteni, kama unaamini hayo yote kwamba kaandika Mkjj; vipi, utaamini na yafatayo katika mantiki ile ile??! :

Mtu akisoma hiyo topic bila background kidogo inatoa impression kuwa nataka watu wabebwe na NEC. Hapo nitakuwa najipinga misimamo yangu and I don't like kujipinga. Makala hii niliituma ili itoke siku ya Jumapili (August 1, 2010) siku ya kura za maoni. Lakini Mhariri kaamua kuitoa kwenye makala yangu ya kawaida ya Jumatano; kwa hivyo inasomwa ikiwa siku nne baada ya tukio iliyotakiwa kuzungumzia. So, isome ukifikiria unaisoma Jumapili siku ya kura za maoni. M. M.

Kutoka thread hii: Wabunge waliogongana Richmond warudishwe- Mzee Mwanakijiji
 
Kwa sababu ni wanawake watapewa viti maalum. Je kama wamepewa option hiyo na wahusika wenyewe wakaamua kuchagua the easiest way? Utasemaje?

Na vizuri umetumia neno wameombwa. Hiyo kuomba ni demokrasia tayari . Wahusika wangekubali au kukataa. Na zaidi ya kuombwa kuachia ngazi za kugombea nini zaidi waliongea na wahusika ??? Nadhani kama ni kweli kuna scope zaidi ya haya uliyoyawakilisha.
 
Karaga bao mpendazoe amesha chukua form za ubunge jana!

Una uhakika amechukua form? Vipi kwa Regia "G.S."?

Ninavyojua ni kwamba viti vya upendeleo huendana na idadi ya wabunge wa kuchaguliwa kama sikosei. Sasa kama CHADEMA ita-field candidates goigoi kwa kutegemea kuwapa candidate hawa wa kike ambao walikuwa wameshinda kwenye kura za awali, wanaweza kujikuta wamepoteza nafasi nyingi sana za ubunge wa kuchaguliwa na hivyo kubakia na viti vichache sana vya upendeleo ambavyo havitatosha kuwagawia hao walioenguliwa.
 
Yaani huyu binti Regia ameondolewa kwenye kinyang'anyiro kile pamoja na uimara wake wote katika kujenga na kutetea hoja alionyesha hapa? Mbona naona kizunguzungu kabisa.

Na bado utapatwa na kihindi hindi wakati walio "teuliwa" kushika nafasi za viti maalum watakapo tangazwa uone msururu wa Lyimo, Lucy Ndesamburo, Mdee et al
 
Mnashambulia CHADEMA kwa kosa la kufikirika? Kuna ushahidi gani kwamba CHADEMA wamewaengua waliopata ushindi kwenye kura za maoni? Kama kuna "negotiations" zinazofanyika basi imeshakuwa kulazimisha?

Mimi nadhani MMKJ haitakii mema CHADEMA. Kuna wakati alisema lengo lisiwe kuing'oa CCM madarakani mwaka huu.

It is not possible to be a little bit pregnant. Aidha unataka mabadiliko (in which case you should not try to smash CHADEMA) au unataka tuendelee kama tulivyo. Kuishauri CHADEMA sawa, lakini kuuma na kupuliza kama hivi si sawa.
 
Nadhani kati ya wengi mimi naitakie Chadema mema zaidi; lakini not at the expense of other values. Na hapana sijawahi kusema kuwa lengo lisiwe kuing'oa CCM madarakani mwaka huu. Napima maneno yangu vizuri.

It is not possible to be a little bit pregnant
. Aidha unataka mabadiliko (in which case you should not try to smash CHADEMA) au unataka tuendelee kama tulivyo. Kuishauri CHADEMA sawa, lakini kuuma na kupuliza kama hivi si sawa.

this is the fallacy of false dilemma. There are more possibilities than the two presented.
 
Nadhani kati ya wengi mimi naitakie Chadema mema zaidi; lakini not at the expense of other values. Na hapana sijawahi kusema kuwa lengo lisiwe kuing'oa CCM madarakani mwaka huu. Napima maneno yangu vizuri.

this is the fallacy of false dilemma. There are more possibilities than the two presented.

kama huna nia mbaya basi unasomeka vibaya ,just choose your words so careful zaidi ya hivyo unavyosema "nachagua maneno yangu vizuri" kama unaona unachagua maneno yako vizuri basi ongeza iwe na vizuri zaidi na zaidi.

Watu wame quote hapa maneno yako kuhusu CCM (NEC) kurudisha watu fulani kwa sababu unazoona ww za msingi ,Lakini hapa hutaki kitu kama hicho .Je leo ndio unaelewa maana ya demokrasia?

My take: kuhusu chama chochote kinacofanya kuhusu kuhusu wagombea wao ni kwa maslahi ya chama na wanakuwa na sababu na lazima kutakuwa na maongezi kwa wahusika na makubaliano.
Pia kama mtu yeyote anaweza kujibu je ,je kura za maoni kwa kiasi gani zina reflect kura za wananchi wa jimbo hilo(ushindi)?Je analysis ikifanyika kuakikisha ushindi si vyema makubaliano yakawepo.?
Kwa kuwa hiini tetesi ,na mmoja wawahusika ni member hapa ,basi mimi naimani tutie subira tutakula vitamu.
 
Sasa, chama ambacho kinataka kuleta mabadiliko cha CHADEMA kinasikitisha kuwa nacho kimerithi na kukumbatia mfumo huo huo mbovu. Habari kwamba baadhi ya wagombea wake walioshinda katika kura za maoni baada ya kufanyia jasho kuenguliwa na vikao vya juu vya "chama" ni habari za kusikitisha na zinaonesha kuwa mfumo ule ule mbovu wa demokrasia ya 'chama' umerithishwa ndani ya Chadema na utaleta matatizo yale yale (kama bado haujaleta).

Hakuna namna yoyote ile habari kama hii, kama itatokea kuwa si ya kweli, inaweza ikatetewa kuwa ilitolewa kwa nia nzuri. Kama aliyeileta atajitetea kuwa ilikuwa ni tetesi then it is one in very bad taste - angalia hukumu dhidi ya Chadema ilivyopamba moto humu. Imefikia mahali hata watu ambao kwa kawaida misimamo yao ni kama mwanga na giza wamepata mahali wanapokubaliana, kuilaani Chadema. Sisiti kutamka kuwa hata mimi nitaungana nao katika kufanya hivyo but only if any of this is true.

Wasiwasi wangu mwingine ni timing ya hii habari - ni kama vile lengo la aliyeileta ni kuplay down hayo yanayotokea CCM kama alivyofanya Msekwa akielezea vitendo vya rushwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM, kwamba tatizo la rushwa si la CCM peke yake !
 
Mnashambulia CHADEMA kwa kosa la kufikirika? Kuna ushahidi gani kwamba CHADEMA wamewaengua waliopata ushindi kwenye kura za maoni? Kama kuna "negotiations" zinazofanyika basi imeshakuwa kulazimisha?

Mimi nadhani MMKJ haitakii mema CHADEMA. Kuna wakati alisema lengo lisiwe kuing'oa CCM madarakani mwaka huu.

It is not possible to be a little bit pregnant. Aidha unataka mabadiliko (in which case you should not try to smash CHADEMA) au unataka tuendelee kama tulivyo. Kuishauri CHADEMA sawa, lakini kuuma na kupuliza kama hivi si sawa.

Hata kama angesema, Mwanakijiji angekua right on this one... kama lengo la chadema ni kuingia madarakani mwaka huu, basi imekwisha moja kwa moja... MMM anaangalia sustainable opposition and proper foundation and building blocks for the country's politics. Kwa ushauri tu, chadema ipambane at least ifikie 30-40% ya representation ndani ya bunge. huwezi kuchukua kirahisi hivyo saha kama imekulia kwenye woga, sintofahamu, njaa, umaskini na rigin socialist background

Amka uelewe kwamba change has its course and anything has its elastic limit; kwa pesa zipi nchi hii chadema itapambana na CCM nchi nzima? wakati kwenye primaries za CCM tu matimuzi yanaweza kuzidi hata ndoto za bajeti ya chadema? hapo bado CUF, NCCR nk?

Je kuna uwezekano kweli wa kuweka hata wabunge 120 kwa mwaka huu tu?

Augustine, hakuna kitu kizuri kama a realistic SWOT analysis, it the only tool to give you strategies
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom