Elections 2010 CHADEMA iwaachilie walioshinda kura za maoni wagombee

Status
Not open for further replies.
Sio tu kuwa Regia Mtema (kilombero) na Rachel Mashishanga (Segerea)warudishwe haraka kwenye nafasi za kuwa wagombea halali wa majimbo waliyoshinda kwenye kura za maoni kupitia CHADEMA bali pia Kamati kuu ya CHADEMA iwaombe radhi wagombea hawa wawili haraka sana kwa mtafaruku huu usio na ulazima wowote ule!

Kumtoa mgombea aliyeshinda kwenye kura za maoni kwa sababu yeyote tofauti na yeye mwenyewe kujiuzuru au kuachia jimbo kwa hiari yake ni ubakaji mkubwa wa kidemokrasia;na hali inakuwa mbaya zaidi kama anayeomba aachie jimbo aliloshinda ni Mwanamke na anayepigiwa chapuo nje ya kidemokrasia kulichukua ni Mwanamme;watu wanaweza wakahusisha jambo hili la CHADEMA na "Gender biased"na sidhani kama CHADEMA watakuwa na jibu lolote valid kutujibu wakihusishwa na "unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya mwanamke"!

Acheni demokrasia ichukue mkondo wake;Regina na Rachel waachiwe nafasi zao maana walishinda kihalali kabisa;kama uliwaomba na wao walikataa hamna cha kufanya isipokuwa ni kuheshimu matakwa yao,kujaribu kutumia aina yeyote ile ya ushawishi tofauti na matakwa yao basi tusubiri aibu kubwa toka kwa watu wapenda demokrasia na tutahoji sasa CHADEMA inatofauti gani na kamati kuu ya CCM?

Gender sensitivity ni kitu cha kukiangalia sana mnapofanya uamuzi wenu wa nani agombee nyie CHADEMA;kumtoa Mwanamke aliyeshinda na kumpa nafasi hiyo Mwanamme ambaye ama alishindwa au hakuwepo kwenye kinyang'anyiro cha mwanzo kutaifanya CHADEMA nayo ihesabiwe kama chama hovyohovyo tu!
 
.. maneno hayo mekundu ya kwanza si ya kwangu; ni ya mhariri.
Mzushi!

Wewe uliidhinisha maneno hayo. Kikanuni za kutuma makala. Bado uko kwenye orodha ya walipwa halafu unataka kumpakazia mhariri, hata hutumii umakini. Mhariri wa Tanzania Daima hawezi kubadilisha maneno yako akaweka jina lako wewe bila wewe kuidhinisha.

Wewe Mwanakijiji umeandika kwamba CCM-NEC iwarudishe kina Selelii. Usimsingizie Mhariri wa Tanzania Daima. Leo unajikasirisha tetesi za CHADEMA kumuengua Mtema?
 
Niliapa kutokupiga kura mwaka 1995 baada ya mbunge mmoja kushinda ambaye alikuwa waziri wa afya kwenye serikali iliyopita ya 1990-1995 . mbunge huyu nilimuuliza swali baada ya kumsomea taarifa iliyoandikwa kwenye Daily news kipindi hicho kuwa alizembea na hela za kununulia madawa zikapotea(zikatafunwa) wizarani kwake. mgombea huyo alijitafuna sana kujibu swali hilo hadi wananchi wakaamua kuondoka mkutanoni na kumuacha pekeyake na wajumbe wenzake walikuja kumpigia kampeni lkn cha kushangaza alipata kura nyingi mno. kutokana na ushindi wake Nikaapa kuwa sitopiga kura tena. mwaka huu nikawa na imani kuwa angalau naweza piga kura lakni kwa utumbo huu inabidi nianza kufikiria kuendelea na msimamo wangu wa kutokupiga kura na mama kasimba123 naye itabidi asipige kwani lzm anifuate mimi kama mumewe

Sijui mtanilazimishaje nisiendelee na msimamo wangu wa kutokupiga kura?

Kwa Hili kwakweli Chadema mmechemsha na sioni demokrasia toka kwenu heri nisipige kura kama zamani kwani unakosema kuna afadhali ni madudu matupu

Dada Regia nasubiri ufafanuzi wako
 
Unazungungumza kwa uhakika, kama unajua; una uhakika nimeidhinisha?

Kamani kweli walikulisha maneno yao kwa maandishi, Mwnakijiji ninaye mjua, mzee wa Jamvi, mwenye internet radio, gazeti na vipeperushi kwenye Net, hujawahi kuikataa habari wala kusema imepikwa. ni vigumu kujijitetea baada ya kabanwa. naamini yote niyasomayo kwenye magazeti chini ya jina la mtu ni maandishi yake mpaka atakapokanusha mara baada ya toleo kutoka sio kusubiri miezi au miaka baada ya kuhojiwa uandishi wake.
 
Mzee Mwanakijiji said:
Kwamba wagombea kama Regia Mtema (kilombero) na Rachel Mashishanga (Segerea) wameombwa kuachia nafasi zao kuwapisha watu wengine (wote wanaume) ni jambo la kufanya watu kutikisa vichwa vyao. Chadema haiwezi kuendelea kusubiria viti vya vijana au wanawake ili kuwapa nafasi za kugombea.

Umesema wameombwa, wameombwa na nani! Kwa hiyo hapa unaona sio utaratibu wa CHADEMA kukata majina ya walioshinda. Pili unaleta swala la jinsia, unataka kuaminisha umma kwamba chadema ni chama kinachobagua maslahi ya wanawake. Tuletee ushahidi wa habari yako, na utuhakikishie ni vipi katiba imevunjwa. Na kama hao uliowataja wakichukua form za kugombea na mwisho kugombea na Chama kukanusha uliyoandika itakuwaje?
 
sasa kwa nini chadema waliwaruhusu hao akina dada kugombea kwenye kura
za maoni wakati walijua fika kwamba chaguo lao ni hao akina
mpendazoe? au chadema waliamini r na r wangeshindwa kura
za maoni hivyo kungekuwa hakuna lawama?

chadema inabidi mmje na sababu tosha za kueleza tukio hili
vinginevyo mtakuja jilaumu wenyewe ooohh
 
Matatizo ya kutokuwa na mgombea binafsi ndiyo haya. Chadema kama chama pamoja na kuwa wameniuzi kwa hili lakini wana haki ya kuhakikisha kuwa wanapanga safu ya watu wanaogombea vizuri. Tatizo langu ni kuwa njisi walivyofanya mambo yao ni aibu tupu. Ilionekana wazi kabisa tangia mwanzo kuwa makao makuu wanamtaka mpendazoe. Tarehe ya kupiga kura za maoni ilibadilishwa mara mbili bila sababu yoyote na kusingizia kuwa Mpendazoe alikuwa kwenye msafara wa kusaka wadhamini, baadaye tukaja kujua kuwa hakwenda ila makao makuu walikuwa wanataka ku buy time ili mpendazoe afanye kampeni. hatimaye walipopanga tarehe mpendazoe akashindwa na sababu ya kushindwa ni kwa sababu ya vitu viwili.

Moja, hili sio siri ni kwamba rachel ndiye aliyejenga matawi ya jimbo la segerea, amaefanya kazi ya kutafuta vijana na kuwaunganisha na kutengeneza network, hata leo ukifanyika uchaguzi tena mpendazoe anakwenda na maji tena kwa sababu tu si siri rachel ndiye aliyehangaika na kuweka uhai wa chadema kwenye jimbo la segerea.

Pili siku ya kura za maoni Mpendazoe aliulizwa maswali matatu na majibu yake kweli yalikuwa ki ccm zaid kuliko ki chadema kama kusema kuwa nilitekeleza ilani kwa asilimia 94. Maswali yalikuwa kama

i)Kwa nini hujangombea kishapu
ii)Tutajie mafanikio yako uliyoyapata kishapu
iii)Kwa nini ulipotoka CCM ulienda CCJ na si Chadema straight.

Yote hayo yalikuwa mawe tu ukilinganisha na maswali aliyoulizwa rachel ambaye amekuwa muhangaikaji humujimboni kwa muda mrefu.

Athari za huu ujinga ni kwamba hawa wanazoofisha base yao wakati ccm base yao iko energizes ile mbaya. Makongoro amemwaga kifusi kwenye barabara inayotoka Majumba sita mpaka segerea kituo cha mafuta na nyani wa segerea wameanza kufurahia hilo. Viongozi wa Chadema kwa lipi sijui wameshindwa kabisa hata kumwita Rachel mpaka sasa ingalau kumwambia na kumpa maelezo kwa nini wamefikia uamuzi huo na kujaribu kuwapatanisha na mpendazoe.

Mimi mpendazoe kwa mambo yake CCJ pamoja na mkuu Mwanakijiji walishanitoa stimu kabisa!
 
Umesema wameombwa, wameombwa na nani! Kwa hiyo hapa unaona sio utaratibu wa CHADEMA kukata majina ya walioshinda. Pili unaleta swala la jinsia, unataka kuaminisha umma kwamba chadema ni chama kinachobagua maslahi ya wanawake. Tuletee ushahidi wa habari yako, na utuhakikishie ni vipi katiba imevunjwa. Na kama hao uliowataja wakichukua form za kugombea na mwisho kugombea na Chama kukanusha uliyoandika itakuwaje?

Safi sana mkuu, kuna wakati mwingine mzee mwanakijiji anafikiri anapoandika, labda wasomaji hawana nafasi ya kufikiri kilichoandikwa, mie nakuambia atakuja hapa kukanusha kwamba hakusema hivyo, anatuona sie tunaosoma hizo thread zake kama hatuna uelewa wa mambo vile.
Isitoshe hiyo habari chanzo chake ni kipi maana tunaweza kujikuta tunajadili vitu ambavyo havipo, mtu katunga ili aweze kupima joto lake.
Nakubali kuwa makala nyingi Mzee Mwanakijiji huwa anjitahidi lakini kuna zingine zinaenda nje ya maada, anajaribu kuweka vitu vyake vya kusadikika. Be careful! utajikuta unakuwa kama MS.
 
sasa kwa nini chadema waliwaruhusu hao akina dada kugombea kwenye kura
za maoni wakati walijua fika kwamba chaguo lao ni hao akina
mpendazoe? au chadema waliamini r na r wangeshindwa kura
za maoni hivyo kungekuwa hakuna lawama?

chadema inabidi mmje na sababu tosha za kueleza tukio hili
vinginevyo mtakuja jilaumu wenyewe ooohh

Nadhani kuna mambo mawili ya kufafanuliwa hapa,

1) Kuna move huwa zinafanyika ndani ya chama na mara nyingi wanapenda kuziita, "kuimarisha chama au mara Nyingine wanasema kwa Maslahi ya chama" na hii mara nyingi utakuta wagombea wanatolewa chenye kinyanganyiro ama kwenye uongozi ili kumpisha mwingine "kwa maslahi ya chama" nadhani hii ni politic ya Africa na Tanzania ikiwemo, kwa Tanzania CCM ndio mafundi wa hizi move kwa sababu tumeshuhudia mengi kama haya, lakini kwa Vyama vingine pia zipo, Mabere Marando alimpisha Mrema kuchukua uenyekiti pale NCCR kwa kigezo hichohicho cha kuimarisha chama, Lakini kwa Chadema pia kitendo kama hicho kimetokea pale walipomshinikiza/kumwomba Bw Zitto Kabwe asigombee/ atoe jina lake kwenye uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chadema na kauli inayotumika ni ile ile kwa maslahi ya chama, Mara nyingi hizi move huwa zinakubalika na waliowengi kwenye chama na kwa mara ya mwanzo huwa zinaleta uwezo na kweli chama uimarika

2) la pili, ni hili la kuwashindanisha watu kwenye mchakato wa kampeni, na mwisho wa siku mshindi mmoja kati ya wengi anapatikana kwa demokrasia, lakini kinachokuja kusikitisha ni pale mshindi anapoenguliwa bila sababu za msingi kabisa,

nikiiongelea hii issue ya Chadema na wagombea wao wawili Regia na rachel, kwa kweli ni habari ya kusikitisha na ni ukiukwaji mkubwa wa demokrasia na pia upindaji mkubwa wa haki za wapiga kura, hapa point ni hii, kweli Mpendazoe ni muhimu na uwezo wake biungeni ni mkubwa, lakini hana sifa ya kupita kugombea ubunge kama wananchi walishamkataa, japokuwa na umuhimu wake lakini kumkosa bungeni si tatizo ni wananchi ndio walioamua hivyo, kumkosa Mpendazoe Bungeni hakuna tofauti kama tutakavyo mkosa Slaa pia, ina maana Slaa akishindwa uraisi basi tutakuwa tumemkosa bungeni na pia tumemkosa Ikulu, lakini lano sio tatizo ikiwa Demokrasia itachukua mkondo wake


Hii Move ya kuwatoa hawa wagombea waliochaguliwa Kidemokrasia ikifanikiwa, hapo nadhani unaweza ukawa ndio mwanzo wa mwisho wa Chadema
 
Umesema wameombwa, wameombwa na nani! Kwa hiyo hapa unaona sio utaratibu wa CHADEMA kukata majina ya walioshinda. Pili unaleta swala la jinsia, unataka kuaminisha umma kwamba chadema ni chama kinachobagua maslahi ya wanawake. Tuletee ushahidi wa habari yako, na utuhakikishie ni vipi katiba imevunjwa. Na kama hao uliowataja wakichukua form za kugombea na mwisho kugombea na Chama kukanusha uliyoandika itakuwaje?

endapo chama kitasema kuwa vyanzo vyangu havikuwa sahihi na wote niliowataja wakaruhusiwa kugombea basi lengo litakuwa limefanikiwa. Lakini kwamba wamekusudiwa kuenguliwa halina shaka.
 
mimi nachukia hii dhana ya kufanya 'ni kwa sababu wanawake' ndio maana wameondolewa ambayo naona ndio imejitokeza.

Si amini kuwa kuna mfumo dume wa kiasi hicho ndani ya chadema kama mnavyotaka tudhani.Naamini wameondolewa kwa sababu nyengine (japo siungi mkono kuwaondoa), kuzishikia bango kuwa ni kwa sababu wanawake ni kuwavunjia heshima walioombwa wajitoe na kuwawekea mazingira magumu ya kuendelea na kazi zao (ikiwa wataingiza akili mwao kuwa wameondolewa kwa kuwa wanawake)
 
endapo chama kitasema kuwa vyanzo vyangu havikuwa sahihi na wote niliowataja wakaruhusiwa kugombea basi lengo litakuwa limefanikiwa. Lakini kwamba wamekusudiwa kuenguliwa halina shaka.

Mpendazoe kachukua form jana na alisindikizwa na katibu wa jimbo ambaye alipigiwa simu kutoka makao makuu. Huwezi amini kuwa mwenyekiti wa jimbo ni Rachel mwenyewe wala hakupewa habari. Haya mambo watu mnaanza kuisema chadema lakini ni ya watu wachache tu. Sasa kuna mambo sio vizuri kuyasema kwa sababu alternative ni CCM (uuuiii) lakin i kungekuwa na alternative huyu mpendazoe asingepita!
 
endapo chama kitasema kuwa vyanzo vyangu havikuwa sahihi na wote niliowataja wakaruhusiwa kugombea basi lengo litakuwa limefanikiwa. Lakini kwamba wamekusudiwa kuenguliwa halina shaka.

....muda mwingine nashindwa kukuelewa MM huwa una malengo gani! Inaonekana ni kama mtu unayependelea controversy, naweza kuwa si sahihi, lakini ndivyo ninavyoelekea kukuelewa. Siafiki uvunjaji wa sheria au taratibu katika kukabiliana na changamoto za kisiasa na kijamii, lakini muda mwingine approach unayoitumia huwa inakuwa hasi, si kwa lengo la kujenga ila ni kwa ajili ya kubomoa. Licha ya ukweli kuwa una vyanzo vyako vya kuaminika, ambavyo vinaweza kuwa ni wahusika wenyewe, lakini la kusema kwa kuwa ni wanawake sijajua kama ni kigezo kilichotumika kama unavyojaribu kuwafanya watu waamini.
Tutasubiri taarifa zao, kwa kuwa Regia ni mwanachama hapa, tutajua ukweli...
 
This is really heart breaking... hasa kwa vijana waliodhani kuna mwanga ndani ya chadema... it is even worse kuona jinsi walivyocuruga uchaguzi wa viti maalum kiais cha kitila kusema hawakua na mwongozo!! Hivi kweli wako tayari kuwana na miongo alfu lela u lela?

Regia is a good and potential candidate... i have personally seen her and she is composed, anakipenda chama na yuko tayari kuwa mpiganaji, ameshinda kura za maoni, na kwa wanaokumbuka signature yake, it said alot about her readiness... labda wameona kitu tusichoona maana wanajiana wenyewe

Kuhusu Rachel, simjui ila masikitiko yangu ni jinsi wanavyolazimisha kuchomeka hili garasha la CCM lisilo na subira wala staha... lilikurupuka wakati treni iko 120 likaruka na kutua kwenye robota la pamba.. sasa linachefua hewa kwa kupuma ndani ya chadema

Freeman, yes chadema may have started as your NGO, but the wind of change is here and you have to let go, chadema is not an NGO no more... change has come and you shoul let it prevail

HAYA MADUDU NDIO YANAMFANYA SLAA KUWA KAMA SHREK TU
 
....muda mwingine nashindwa kukuelewa mm huwa una malengo gani! Inaonekana ni kama mtu unayependelea controversy, naweza kuwa si sahihi, lakini ndivyo ninavyoelekea kukuelewa. Siafiki uvunjaji wa sheria au taratibu katika kukabiliana na changamoto za kisiasa na kijamii, lakini muda mwingine approach unayoitumia huwa inakuwa hasi, si kwa lengo la kujenga ila ni kwa ajili ya kubomoa. Licha ya ukweli kuwa una vyanzo vyako vya kuaminika, ambavyo vinaweza kuwa ni wahusika wenyewe, lakini la kusema kwa kuwa ni wanawake sijajua kama ni kigezo kilichotumika kama unavyojaribu kuwafanya watu waamini.
Tutasubiri taarifa zao, kwa kuwa regia ni mwanachama hapa, tutajua ukweli...

drama queen to say the least
 
endapo chama kitasema kuwa vyanzo vyangu havikuwa sahihi na wote niliowataja wakaruhusiwa kugombea basi lengo litakuwa limefanikiwa. Lakini kwamba wamekusudiwa kuenguliwa halina shaka.

Umeanza kubadili kauli. Unasingizia "chanzo changu" sasa.

Eti "wamekusudiwa kuenguliwa." Ulisema hivi:

"Kwamba wagombea kama Regia Mtema (kilombero) na Rachel Mashishanga (Segerea) wameombwa kuachia nafasi zao kuwapisha watu wengine (wote wanaume) ni jambo la kufanya watu kutikisa vichwa vyao. Chadema haiwezi kuendelea kusubiria viti vya vijana au wanawake ili kuwapa nafasi za kugombea."

Wameombwa na nani? Wadau wanakuuliza.

Unapoandika kwenye Tanzania Daima, na Michuzi, na hapa JF, kumbuka kutofautisha walengwa ni kina nani haswa, kukaa kote Michigan mvua kibao hujajifunza umakini wa uandishi wa kiukweli?

 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom