CHADEMA imewasaliti Watanzania

Umeona masharti ya mazungumzo?
Mkuu Mshana

Wazo zima la kufanya mazungumzo na CCM/Serikali linaonekana kuwa na kasoro tangu mwanzo. Je, CHADEMA wanaanzaje kufanya mazungumzo na wale waliokataa kufanya mazungumzo nao kabla ya tarehe 29 Oktoba?
 
Punguza mihemko; kila mtu ana nafasi yake binafsi ya kutoa mchango katika kupigania haki katika nchi hii.

Suala la Lissu kutoka gerezani linapaswa kushughulikiwa kwa kuzingatia kanuni za kimahakama, si kwa ajili ya kupata faida za kisiasa.
 
Watanzania gani waliosalitiwa na kwa kipi hasa? Yani mtu akae ndani kwa mateso hiyo Mitanzania ina kazi ya kumsifia Diamond huku nchi ikatafunwa.
 
Wakati yeye anafia jela ww uko happy na familia yako nyumbani kwako umetulia au sio?

Since amekaa jela umefanya jambo gani kwa ajili yake?

Umewahi kukaa gerezani?

Mwache atoke, aje uraiani
Ni nani mwenye mamlaka ya kuamua mtu atoke gerezani katika nchi hii?
 
Spinning za kitoto kabisa!
It was seen coming..hamna jipya..mwachien jamaa aje afundishe siasa wajinga wajinga!
Ni nani mwenye mamlaka ya kuamua mtu atoke gerezani katika nchi hii?
 
Watanzania gani waliosalitiwa na kwa kipi hasa? Yani mtu akae ndani kwa mateso hiyo Mitanzania ina kazi ya kumsifia Diamond huku nchi ikatafunwa.
Ni nani mwenye mamlaka ya kuamua mtu atoke gerezani katika nchi hii?
 
Watanzania wote wako kifungoni, tofauti ni kwamba Lissu yuko katika gereza la kuta.
 
Sasa kukubali kuingia kwenye mazungumzo kuna shida gani
You are becoming soft.

Je, unafahamu kwamba kabla ya uchaguzi, CCM/Serikali walikataa kufanya mazungumzo au maridhiano?
 
Hapo napo huoni tofauti?

Umemsikia Lissu mwenyewe anasemaje?

Lissu kasema

" Kesi zote zinazomkabili yeye na Chama zifutwe na kwamaba yupo tayari kwa mazungumzo..."

 
Hadi sasa hatujasikia kauli ya TAL na kesi iko active mahakamani na jamhuri wameweka mpira kwapani kuelekea mahakama ya rufani.

Swali ni jepesi tu kama TAL angekuwa na kesi ya kujibu hadi sasa jamhuri wasingekuwa wanakimbia kuleta mashahidi ukiachilia mbali vielelezo viwili kama ushahidi vilvyotupiliwa mbali na mahakama.

Mimi kwa maoni yangu mpaka nisikie TAL mwenyewe atasema nini siku akionekana kutoka huko gerezani tofauti na hapa nachokiona ni sarakasi tu za watu na mkakati wa machawa na vyombo vya habari kuhamisha magoli ukitaka kuamini angalia vichwa vya habari baada ya hii kauli ya juzi.

Wanasema "TAL yuko tayari kwa maridhiano" kwanini wasiandike "TAL atoa masharti 7 baada ya kutembelewa na Chakwera gerezani"

Simuoni TAL akiingia mkenge kuridhiana na watu waliomtesa na pia TAL huwa hafichi kitu kama kimepotoshwa najua akionekana tena public ataeleza uhalisia wa mambo.
 
Hayo kasema Lissu mwenyewe?
Iwapo ameyasema mwenyewe au la, hilo ni jambo linalotia wasiwasi.

Kinachoshangaza wengi ni kwamba taarifa hizo zilitolewa kupitia wakili Kisabo, na CHADEMA ikaandaa taarifa rasmi kwa umma.

Baadaye waliithibitisha taarifa hiyo, na hivyo kauli hiyo ni ya Tundu Lissu.


 
Lakini CHADEMA wametoa taarifa rasmi na kidhibitisha kwamba hiyo ni kauli ya Tundu Lissu.

 
Linatia wasiwasi kwa nini?

Unafahamu strategy za chama nanza Lissu ni zipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…