Mzee Mwanakijiji,
[Je Chadema ilivyo sasa iko tayari kuongoza taifa la watu milioni 40 kwa ubora na kwa maono bora zaidi na mfano mzuri wa kiuongozi katika ngazi zote kuliko CCM? Ni nini msingi wa imani ya wale wanaoona kuwa iko tayari?
Mkuu sasa naiona sababu ya watu kukuita wewe CCM.. wakati wewe unajiuliza uwezo wa chadema ukilinganisha na CCM ni vichekesho vitupu kwani ni sawa na mwanamke anayekataa kuomba talaka kwa kuazama wanaokuja kuposa, akidhani hakuna mwanamme mwingine anayeweza kuwa mume zaidi ya mumewe.
Kama swali lako lingekuwa kwa nini Chadema na sio CUF au TLP au NCCR ungeweka urahisi wa watu kukujibu lakini unapotumia chama kinacho ku abuse kuwa ndio kipimo cha Uongozi ni lazima hutawaelewa wengine.
Mimi nitakujibu vizuri tu, CUF siwaamini kwa sababu wamejikita Zanzibar kiasi kwamba wamefikia Muafaka na CCM ktk utawala wa Zanzibar..they are more interested in Mustakabali wa Muungano ambalo sii jambo baya.. Wanayo right hiyo kama chama kwani hata hapa Canada kuna PQ wanaosimama kwa maslahi ya Quebec. Above all, I don't trust Seif Sharrif Hamad..
TLP ni chimbuko la mgawanyiko wa NCCR ambao nina uhakika kuna Mapandikizi ya CCM ambao ndio chanzo cha kugawanyika baada ya Uchaguzi wa mwaka 1995. Halafu tatizo kubwa la vyama hivi ni wahusika wake wakuu ambao ndio waamuzi wa kila kitu...
Chadema nao wana matatizo yao kuhusiana na viongozi wake pamoja na kwamba chama hiki kimetokana na fikra halisi ya Upinzani wa Itikadi toka enzi ya mzee Mtei... Ni chama ambacho kwa miaka ya hivi karibuni tumeona vichwa tofauti vikisimama kwa Upinzani ila kumetokea mahusiano mabaya baina ya viongozi kutokana na kosa moja kubwa la kiutawala - Kila mtu ni mwakilishi na msemaji wa chama,jambo ambalo lilisababisha mgongano baina ya wananchama.
Pili, chama kinashindwa kuvumilia upinzani wa ndani katika maswala yasiyohusiana kabisa na itikadi,sera au ilani ya chama isipokuwa challenges ktk nafasi za madaraka...Hata hivyo ni ktk kushindana huko tumeona mabadiliko makubvwa ya viongozi ngazi tofauti za utendaji kiasi kwamba leo kina Zitto, Dr.Slaa, Mnyika, Kitila na wengineo wameshika nyadhifa kutokana na uwezo wao na bado wanakuwa challenged kufanya zaidi..
Mkuu kama nilivyosema huko nyuma, mimi ni conservative sikubaliani na itikadi ya mrengo wa kati isipokuwa kila kitu kina wakati wake kulingana na watu na Mazingira. Katika hali tulokuwa nayo, mrengo wa kati nadhnai ndio itikadi inayotakiwa kutuunganisha ili kupata mabadiliko..kuwaunga mkono haiondoi imani yangu ktk mrengo wa kulia hata kidogo, kwani kinachotakiwa kufanyika sasa hivi ni kufunga mikanda yetu na kwenda vitani. Wanajeshi wanapokuwa vitani huweka kando imani zao za itikadi hadi ushindi upatikane..same with the war against Terorism,vita hii has nothing to do with Itikadi ya kiongozi, wananchi au wanajeshi kwenda Afghanistan..Tunachoweza kujiuliza ni Je, vita against Terrorism (CCM) ni halali au sio halali?