CHADEMA iko tayari kuongoza?

Jamani kazi sio kuingia Ikulu, kazi ipo kwenye grass roots...bila kufanya kazi huku chini kuingia Ikulu itakua ni ndoto tu!
 
Tunasukumiziwa katika makoo yetu chama kimoja tu kuwa ndicho pekee chafaa kuungwa mkono katika kuiangusha CCM. Tunaambiwa vyama vingine viungane nacho kwa sababu kimeonesha uongozi na kuwa ndiyo "upinzani" wa kweli. Wapo watu wanaoamini kabisa jambo hili. Wanaamini kuwa CHADEMA ndicho chama hasa mbadala kinachoweza kuchukua uongozi wa taifa letu toka mikononi mwa CCM.

Kama nilivyouliza huko nyuma ni mambo gani Chadema wamefanya kustahili kuongoza leo naomba nidokeza swali hili ambalo ni muhimu.

Je Chadema ilivyo sasa iko tayari kuongoza taifa la watu milioni 40 kwa ubora na kwa maono bora zaidi na mfano mzuri wa kiuongozi katika ngazi zote kuliko CCM? Ni nini msingi wa imani ya wale wanaoona kuwa iko tayari?

Mwenyewe ni na maoni yangu.. naomba nisikie ya kwenu.

Ukiwa makini utaona swali linahusu Chadema na utayari wao kuongoza.. nje ya hapo ni red herring.

Wewe ni mmoja wa watu ninao waheshimu sana humu ndani ya JF hasa ktk suala zima la kuchangia mijadala yenye tija kwa taifa hili ila TABIA yako mbaya ya kuuliza maswali huku mujibu ya wazi ukiwa nayo ndiyo inayonikera pengine yawezekana unasukumwa na mapenzi binafsi ila nilazima uonyeshe ukomavu wa kisiasa kwa kukiri kwamba CHADEMA kwa sasa ndo chama mbadala kwa sisiem yao!
 
Bado kuna mambo ambayo yanaifanya Chadema kutokuwa mbadala kuongoza. Kwa mfano, walipofanya uchaguzi wao, waliikanyaga chini demokrasia kiasi kwamba wakaanzisha tension zisizo za lazima ndani ya chama. Halafu kutegemea sana watu wawili watatu kam ndio financier wa chama nayo ni hatari kubwa maana chochote wanachoweka wangependa kupata returns, maana nafikiri wengi wao ni wafanya biashara. Na cha mwisho inaonekana kuna watu hawataki kuambiwa chochote tofauti na wanachofikiri ndio maana Marehemu Wangwe na hata Zitto pia waliandamwa na kashkash za hapa na pale.
Tumefundishwa kuwa mtu asiyeaminika katika kitu kidogo, hawezi kupewa dhamana na kuheshimika katika jambo kubwa. Kama mambo haya madogo madogo yanawasumbua, kuwapa nchi yenye vurugu za kila aina hapa hawa watu naona kama bado hawako tayari. Hawana systems zinazojitegemea na kujiendesha ndio maaana wana migogoro isiyo ya lazima.
 
Mkuu Mwanakijiji,
Naona baada ya SisiJe-CCJ kuvurunda sasa unaishabikia SisiEM- Swali lako ni kama kuuliza mume kijana akifariki mke kijana anaweza kuolewa tena ? Tanzania bado haijazeeka! (Don't take it seriously)

Turudi kwenye mada, nimeelewa unauliza je CHADEMA inaweza kuingoa CCM na kuongoza nchi?Ndio, CHADEMA inaweza kuingoa CCM maana dhumuni la Chama Cha Siasa ni kuchukua dola kwa njia za kidemokrasia.

Tukiitazama Afrika iliyo Kusini mwa jangwa la Sahara ni Tanzania na Botswana tu ndio bado zinaongozwa na vyama vilivyoleta 'uhuru'. Tanzania ni TANU kwa Tanganyika na kwa Zanzibar(Mapinduzi kupitia ASP) na TANU na ASP kuungana kuwa CCM. Huko Botswana chama tawala ni kilekile cha Botswana Democratic Party bado kipo madarakani toka 1966 mpaka leo hii 2010.

Kwa nchi zingine kama Zambia, Malawi, Uganda, Kenya n.k vyama vyote vilivyoleta uhuru vimeng'olewa madarakani , hivyo sioni kwa nini CCM isiweze kung'olewa madarakani na nchi ya Tanzania ikatawaliwa vizuri tu na chama kingine cha siasa kama CHADEMA. Kwa sasa CCM inacheza na wakati mfupi wa kuwepo Ikulu kwani nchi imewashinda.
 
Kwanza hivi vyama nini source ya finance ? Tukijua hili tunaeza tukaanza hapa kutoa tathmini sahihi.
 
Ngosha you are joking, right?

Ndo maana kuna 'Labda'.............inawezekana hii ndo sababu ya kuifanya iingie madarakani...Ukiuliza nini mafanikio ya CHADEMA utatajiwa operesheni Sangara na vita dhidi ya ufisadi.........zaidi ya hapo mhhhhhhhhhhhhhhh
 
Yote haya yanajadiliwa ni harakati za kukipigia kampeni chama kisicho na usajili. Tukiunge mkono chama chenye usajili kwanza, then hivyo vingine tutaviangalia baadaye vitakaposajiliwa. Tukirudi kwenye topic, naungana na aliyezungumzia suala la idadi ya wabunge, kwani hao ndo wanaweza wakatoa mwelekeo wa uwezo wa chama kuongoza ambao kwa sasa hakuna chama cha upinzani kinaweza kuongoza.

Umeona eeh.Mwanakijiji mjanja ile mbaya.Sasa hata kama kwa mtazamo wake akiona CHADEMA haifai anafikiri ndio CCJ iko tayari?je na wao wamefanya nini kustahili kupewa nchi?
 
Ustadh bana unakuwa kama hujazaliwa bongo hii hii?

Kuna maswali ya msingi ambayo watu wana-ignore lakini ni very paramount hapa..Tunasikiaga tu CCM wanachangiwa na 'wafanyabiashara' wakubwa ambao badaye it turns out wanakuja kula kivulini kilaini kwa kuchukua tenda na mambo mengine ambayo wanayajua wenyewe huko chemba. Sasa hapan'shaka ni vyema kujua wenzetu wa huku 'nje' wao nao wanafanyejefanyeje? Maana siasa is a million dollar deal business.
 
SOurces ambazo ni...?

Kuna soucres nyingi Mkuu.
1. Goverment subvention kulingana na formula ambazo zimetolewa na ofisi ya Msajili kama vile,1. Idadi ya wabunge wa kila chama watakaopata 2.At least 5% ya total votes 3.Idadi ya madiwani kila chama itakaopata..Mpaka uquelify ndio unapata ruzuku toka serikalini.

2.Michango ya wanachama-hii ni michango ya hiyari
3. Ada za uanachama-
4. Uuzaji wa vifaa vya uenezi-bendera,beji,fulana n.k
5.Vyanzo toka vyama rafiki-hawa mara nyingi hufadhili huduma kama vile kutoa mafunzo,vifaa n.k
6.Investment kama chama inayo..

Nadhani nimejibu swali lako..haya tuendelee na mjadala.
 
Kuna soucres nyingi Mkuu.
1. Goverment subvention kulingana na formula ambazo zimetolewa na ofisi ya Msajili kama vile,1. Idadi ya wabunge wa kila chama watakaopata 2.At least 5% ya total votes 3.Idadi ya madiwani kila chama itakaopata..Mpaka uquelify ndio unapata ruzuku toka serikalini.

2.Michango ya wanachama-hii ni michango ya hiyari
3. Ada za uanachama-
4. Uuzaji wa vifaa vya uenezi-bendera,beji,fulana n.k
5.Vyanzo toka vyama rafiki-hawa mara nyingi hufadhili huduma kama vile kutoa mafunzo,vifaa n.k
6.Investment kama chama inayo..

Nadhani nimejibu swali lako..haya tuendelee na mjadala.

NAona hujamwelewa huyu ukisoma vizuri haina hata haja ya kumjibu
 
Kuna soucres nyingi Mkuu.
1. Goverment subvention kulingana na formula ambazo zimetolewa na ofisi ya Msajili kama vile,1. Idadi ya wabunge wa kila chama watakaopata 2.At least 5% ya total votes 3.Idadi ya madiwani kila chama itakaopata..Mpaka uquelify ndio unapata ruzuku toka serikalini.

2.Michango ya wanachama-hii ni michango ya hiyari
3. Ada za uanachama-
4. Uuzaji wa vifaa vya uenezi-bendera,beji,fulana n.k
5.Vyanzo toka vyama rafiki-hawa mara nyingi hufadhili huduma kama vile kutoa mafunzo,vifaa n.k
6.Investment kama chama inayo..

Nadhani nimejibu swali lako..haya tuendelee na mjadala.

Ok fine.

Unaeza kutuekea mchanganuo in terms of % kwene hivo vyanzo ulivoweka? I mean say for past 1, 2 or so years. I'm about to UNDERSTAND you answer.
 
Balantada mimi nikijibu humu itaonekana navutia kwangu nitakuwa bias kama Mwanakijiji anavyokuwa bias,yeye tayari ni mCCJ kwahivyo hoja zake zitakuwa ni kuiponda CHADEMA tu ili kuipa nguvu na uhalali CCJ ionekane ndio chama mbadala.Hajui kuwa mpaka chama kionekane kinaweza kuongoza nchi sio kazi rahisi kama anavyodhani.Anafikiri kuwepo kwa CCJ leo ndio kukubalika kwake,haya yanawezekana nchi nyingine lakini sio kwetu Tz kwa wapiga kura wasiojua wajibu wala maana ya kura yake.Mwanakijiji nadhani CCJ watachukua nchi kirahisi wakati hata kupata hao wabunge kwao kwa mwaka huu ni kizungumkuti.Anafikiri ni sawa na mijadala ya humu JF rahisi rahisi. Field ni kugumu kuliko anavyodhani. Mie ni bora niwe msomaji tu nisije kujipendela ila ikibidi sana kuchangia itabidi nifanye hivyo..naangalia maoni ya watu wenye dhamira ya dhati(wanaosema ukweli na sio ushabiki wa kivyama)
Nafikiri ndo sababu watu wengi wanaquestion mwanakijiji ni nani. . . .Lakini kama kweli nia ni kupigia chapuo CCJ si dhani kama dhana ya kuidhoofisha chadema ni sahihi. anaweza akaelezea uzuri wa CCJ na kama anaona chadema si chama mbadala na ndivyo pia CCJ basi atakwa anasema CCM iendelee daima
 
Ok fine.

Unaeza kutuekea mchanganuo in terms of % kwene hivo vyanzo ulivoweka? I mean say for past 1, 2 or so years. I'm about to UNDERSTAND you answer.

Dia kama hujanielewa hapo sidhani kama utanielewa hata nikichanganua..Naanza kumuelewa Shalom kwanini alisema nisingekujibu kama nilivyojibu..

Asante,byeee!see you then!
 
Back
Top Bottom