CHADEMA iko tayari kuongoza?

Tunasukumiziwa katika makoo yetu chama kimoja tu kuwa ndicho pekee chafaa kuungwa mkono katika kuiangusha CCM. Tunaambiwa vyama vingine viungane nacho kwa sababu kimeonesha uongozi na kuwa ndiyo "upinzani" wa kweli. Wapo watu wanaoamini kabisa jambo hili. Wanaamini kuwa CHADEMA ndicho chama hasa mbadala kinachoweza kuchukua uongozi wa taifa letu toka mikononi mwa CCM.

Kama nilivyouliza huko nyuma ni mambo gani Chadema wamefanya kustahili kuongoza leo naomba nidokeza swali hili ambalo ni muhimu.

Je Chadema ilivyo sasa iko tayari kuongoza taifa la watu milioni 40 kwa ubora na kwa maono bora zaidi na mfano mzuri wa kiuongozi katika ngazi zote kuliko CCM? Ni nini msingi wa imani ya wale wanaoona kuwa iko tayari?

Mwenyewe ni na maoni yangu.. naomba nisikie ya kwenu.

Ukiwa makini utaona swali linahusu Chadema na utayari wao kuongoza.. nje ya hapo ni red herring.

Hakuna chama cha upinzani ambacho kipo tayari kuongoza iwe Chadema, CUF au hata CCJ. Upinzania haipo tayari kuongoza si kwa sababu hawana viongozi wazalendo wenyewe uwezo na nia ya dhati bali kutokana na mfumo uliopo. Kabla upinzani haijaweza kuongoza nchi ni lazima wawe wame jijengea nguvu Bungeni kiasi cha kupata wabunge wa kutosha. Hamna chama Tanzania kinacho weza kuongoza kikamilifu bila majority bungeni.

Kufafanua zaidi hoja yangu ngoja ngoja nitoa statistics na mifano. Katika Bunge la sasa CCM ina viti 206 wakati CUF ina 19, Chadema 5, kimoja kwa TLP na UDP(IPU PARLINE database: UNITED REPUBLIC OF TANZANIA (Bunge ), Full text). Ina maana hakuna chama cha upinzani chochote chenye hata "strong minority" na leo hii hata vyama vya upinzani vyenye wabunge viungane watakua na wabunge 26 tu dhidi ya 206 ya CCM. Hii ndiyo composition ya Bunge letu kwa sasa na sidhani kama 2010 composition hii ita badilika sana......

Sasa nitoe mfano wangu. Tuassume Chadema ina baki na wabunge wake watano na tuassume mgombea wao wa uraisi anashinda. Je raisi huyo wa Chadema ata ongozaje na wabunge watano tu Bungeni? Kwa vile raisi anaweza kuteua wabunge wachache tuseme idadi hiyo ina panda mpaka 10. Ata pitishaje sheria na mabadiliko anayo taka? Hata awe na coalition ya wabunge wapinzani bado hana asilimia ya kufanya chochote Bungeni. Pia kwa sheria za Tanzania mawaziri tu wa serikali lazima watoke bungeni. Je raisi huyo ataweza hata kuunda baraza la mawaziri na kuteua wasaidizi kutoka chama chake? Waziri mkuu ni lazima atoke kwenye chama chenye majority bungeni kwa hiyo waziri mkuu ambae ndiyo msaidizi mkuu wa raisi na kiongozi wa serikali bungeni hata kua wa chama chake. Barabara zote katika mfano huu zinaelekea kwa Chadema kuomba msaada kutoka chama kitakacho kua na nguvu bungeni na chama hicho kwa hali ya sasa inaelekea kuwa ni CCM. Kwa hiyo utawala utabaki wa CCM, serikali itabaki ya CCM, Bunge litabaki chini ya CCM.

Nime tolea mfano Chadema kwa vile mada ni kuhusu Chadema lakini ukweli una baki pale pale kwa hata iwe CUF, CCJ, TLP, UDP nk wata kumbana na hali hiyo hiyo. Kabla chama hakija wazia kutoa raisi ni lazima wajiimarishe bungeni. Rasilimali na nguvu nyingi za upinzani zinge wekezwa katika kuimarisha idadi ya wabunge wa upinzani. Kama chama haki wezi kufikisha hata asilimia 25 bungeni ita kuaje na umaarufu wa kutosha wwa kutoa raisi? Vyama vyote vya upinzani pamoja na "die hard" fans wao na uongozi wenyewe wana kosea katika priorities zao. Chama cha upinzani kwa sasa kina hitaji kiongozi ambae atajua njia na jinsi ya kweli ya kuimarisha chama kwa siku za mbeleni na si viongozi wa sasa ambao wao wana wazia kugombea uraisi tu, uraisi ambao hawawezi kupata, uraisi ambao hawata weza kutumia kikamilifu hata washinde.
 
Ili kujenga nguvu bungeni ndipo napokubaliana na Zitto kuwa ni muhimu, kwa jinsi siasa zetu za sasa zilivyo bongo, vyama vya upinzani viwe na ushirikiano wa kuachiana na kushirikiana katika majimbo. Sababu ni kweli CCM ina wabunge wengi lakini si wote ambao walipata zaidi ya nusu ya kura zote. Hivyo inamaana wapinzani wakisimamisha mtu mmoja wataongeza nafasi yao kuchaguliwa bungeni, badala ya kuwa na wapinzani watano kwa kila jimbo.

Nakubaliana msingi uanzie bungeni tuongezi jumla ya viti ambavyo CCM hawana na hii itaongeza nguvu..

Vilevile Katiba haikatazi Rais kuchaguwa mawaziri toka vyama tofauti ingawa hii ni unlikely chini ya CCM, CUF siko zote walisema wakishinda uchaguzi wataingiza baadhi ya wabunge wa CCM kwenye baraza la mawaziri. Ni kweli itakuwa ngumu kupitisha sera zozote bila majority bungeni...hivo basi kuongeza idadi ya wabunge muhimu
 
I think we will be making a very subjective and non scientific judgement. Chadema ni chama. Na once ikishakuwa madarakani haina maana kwamba wanachama wenyewe ndiyo watakao tekeleza sera mbalimbali za maendeleo. Ila watakuwa wanaiongoza nchi kwa mikakati na mifano mizuri itakayokuwa na tija kwa serikali na wananchi kwa ujumla. Watumishi wa umma watakua wakiendelea na utimisha but under new supervision.

Kama tunataka kufanya fair judgement tuipe nchi kwa miaka mitano kwanza. Wakishindwa we can have something to say. After all, hiyo CCm iliyoko madarakani yenyewe ina utayari gani? Mbona ni wizi mtupu!!! Serikali inakopa pesa kutoka kwa mabenki ambayo serikali ndiyo inayopaswa kuyalinda badala ya kufikiria mikakati bora ya kukusanya kodi. Hiyo pesa italipwa vipi? Acha bana. CHADEMA WANAWEZA SANA!!!
 
Kwa hakika CHADEMA inaweza na ipo tayari kuongoza. Kwa vyovyote vile haitakuwa CHADEMA peke yake na wala hakuna chama cha upinzani peke yake kinaweza kuleta mabadiliko katika Taifa letu na kuongoza DOLA bila mashaka. CHADEMA lazima ishirikiane na vyama vingine vya siasa, vikundi vya kijamii vinavyodai mabadiliko katika Taifa letu na watu wengine mmoja mmoja ambao wana maono ya nini Taifa linataka.

Kwa vyovyote vile CHADEMA inaihitaji sana CUF katika kuhakikisha tunashika dola vizuri. najua kuna watu watasema mbona tuliweza wenyewe Biharamulo na Busanda au hata Tarime. Mazingira ya by election ni tofauti sana na mazingira ya Uchaguzi Mkuu na ndio maana CUF waliweza pia peke yao TUNDURU. Sote tukafanya kinyume na matarajio Kiteto na Mbeya Vijijini.

Ugonjwa uliowapata NCCR-M mwaka 1995 kuwa wanaweza peke yao ndio huo huo uliowapata CUF mwaka 2000 mpaka mwaka 2005 na CHADEMA is vulnerable to that mwaka 2010. Hata hivyo, coalition ya Watanzania kwenye CHADEMA, CUF, NCCR-M nk na sasa hawa waliopo CCJ na hata watu safi waliopo CCM tunaweza kuivusha nchi katika mpito.

Kwa vyovyote vile ushindi wowote ule tutakaoupata kama opposition lazima uwe ni wa kulipitisha Taifa katika mpito ili kufanya mabadiliko makubwa ya mfumo wetu wa utawala na uongozi wa nchi. Mabadiliko ambayo hayatateteresha dola letu na hata Muungano wetu.

Kama CCJ walikuwa wanadhani watafanya peke yao inawezekana ndio changamoto wapatazo sasa. Nimeshtuka kweli kusoma mwananchi kuhusu uhakiki wa CCJ ambapo hata 'viongozi wao' wanatishia mashaka umakini wao kwa kukosea vitu vya kawaida kabisa. Kama kawaida wanakimbilia kusema CCM imewahujumu. Tatizo lile la kila siku la vyama vyetu kutoangalia changamoto za ndani na kukimbilia kulaumu (actually ni tatizo la watanzania wengi sana kutafuta 'mbuzi wa kafara'.

Nina imani kubwa kabisa kuwa CHADEMA kwa kushirikiana na vyama vingine wanaweza kushika, kuongoza na kuendeleza Dola yetu.

Tatizo si vyama vya upinzani kushirikiana au la. Chama kimoja kina weza kujijenga kuishinda CCM peke yake. Ukweli ni kwamba muungano wa upinzani au ushirikiano rasmi wowote wa upinzani una manufaa zaidi kwa CCM kuliko kuimarisha upinzani. Kila chama cha upinzani kina nia ya kuikomboa Tanzania na kuiletea maendeleo nchi, sawa nakubali. Lakni vyama vyote vya upinzani vina itikadi tofauti na njia tofauti za kufikia malengo kwa nchi.

Tatzio kubwa la upinzani Tanzania including chama chako mheshimiwa ni kwamba zina lack vision. Vyama vya upinzani lazima vijijenge kuanzia chiini kwenda juu. Advantage kubwa ya CCM ni kwamba wana ground roots support. Umesema mwenyewe kwenye thread nyingine kwamba katika moja ya chaguzi organizers katika grassroots level walikua kumbe wana CUF ambao wali chukua kadi za chama chenu, kuingia kwenye organization yenu na kuhujumu chama chenu. Kama hali ndiyo hiyo mta weza kushirikiana kwa kuaminiana? Kama siyo viongozi wanacham wenu wataweza? Je tatizo kama hilo linaweza kuikuta CCM ambao ina grassroots support?

Vyama vya upinzani vimekua kama watoto ambao wana kimbilia utu uzima bila kujua utu uzima si umri bali hekika na upeo na majukumu. Vyama vingi vya upinzani sasa ni vikubwa kutokana na umri tu lakini tokea mwaka 1992 hazija piga hatua yoyote ya maana. Kama mpaka leo upinzani unaweza kuwa na wabunge 29 tu kwa pamoja bungeni basi inaonyesha vyama vya upinzani bado havija kua na pia inaonyesha ushirikiano wowote kati ya upinzani wala hauta wasaidia chochote.

Kwa hiyo mkuu kwa napingana na wewe. Si Chadema wala chama chochote ambacho kipo tayari kuongoza. Bado mna safari ndefu na ina sikitisha hamna chama chochote cha upinzani chenye short term na long term goals zinazo tambulika na ambazo zimeonyesha kuzaa matunda yoyote. Tatizo la upinzani ndiyo tatizo la serikali na taifa letu kiujumla......mipango tunaweza kuongelea lakini utekelezaji ni sifuri.

Kama chama chochote cha upinzani kina nia ya kuja kushika hatma ya uongozi wa nchi hii kwanza lazima chama kiwe na viongozi bora na si bora viongozi. Viongozi ambao hawa angalii leo tu bali kesho na kesho kutwa. Viongozi ambao wapo tayari kukipa chama muda na nafasi wa kukua badala ya kukimbilia tu uongozi wa juu wa nchi.

Kama upinzani utakuja kuongoza nchi kwa sasa lazima mambo mawili yatokee
1. Kujipanga kutoka chini mpaka juu. Kujenga mahusiano na wananchi wa kawaida mpaka wananchi wenye ushawishi mkubwa katika jamii. Kuanzia wananchi wa kijijini "Sitimbi" mpaka wananchi wa mkoa kama Dar. Msingi wa vyama vya upinzani hauja jengwa vizuri kwa maana hiyo hata nyumba iki kamilika haita simama.
2. Chama kilengee kuvutia Watanzania mbali mbali wenye vipaji vya uongozi na uwezo wa kupanga mikakati ya chama. Katika vyama vyote kuna wale wanasiasa wanao onekana lakini pia kuna watu behind the scenes ambao kazi yao ni kupangia mikakati na kutekeleza mipango ya chama, ngoja niiite "bureaucracy" ya chama. Kwa hiyo wote kuanzia viongozi na watu ambao hawaonekani lazima wawe watu wenye uwezo wa juu. Chama kiwe tayari kuvutia na kusaka vipaji na kuwa shawishi wajiunge nao.

CHAMA NDIYO KIFUATE WATU NA SI WATU WAKIFUATE CHAMA!

Ila naomba nisi chukuliwe vibaya. Upinzani umefanya mambo mengi hata ndani ya bunge. Wabunge wa upinzani wameibua mambo mengi sasa bungeni. Ila strategy ya kuibua mambo bungeni na kuongea kwa niaba ya wananchi ni tofauti na strategy ya kushika uongozi. Mpaka leo hii upinzani haija onyesha uwezo wa kukaribia hata nusu ya wabunge hata wauongane kwa maana hiyo bado upinzani haija onyesh wata wezaje kuongoza nchi.
 
Ili kujenga nguvu bungeni ndipo napokubaliana na Zitto kuwa ni muhimu, kwa jinsi siasa zetu za sasa zilivyo bongo, vyama vya upinzani viwe na ushirikiano wa kuachiana na kushirikiana katika majimbo. Sababu ni kweli CCM ina wabunge wengi lakini si wote ambao walipata zaidi ya nusu ya kura zote. Hivyo inamaana wapinzani wakisimamisha mtu mmoja wataongeza nafasi yao kuchaguliwa bungeni, badala ya kuwa na wapinzani watano kwa kila jimbo.

Mkuu vyama vya upinzani kuachiana majimbo itakua ngumu kwa sababu sidhani kama wapo tayari kufanya hivyo na kwa jinsi uongozi unavyo nga'nga'niwa sidhani kama wata achiana. Ikitokea basi ni vyema lakini kwa kuangalia hulka ya kibinadamu hili swala litakua ngumu sana.

Nakubaliana msingi uanzie bungeni tuongezi jumla ya viti ambavyo CCM hawana na hii itaongeza nguvu..

Hapa tupo wote mkuu.

Vilevile Katiba haikatazi Rais kuchaguwa mawaziri toka vyama tofauti ingawa hii ni unlikely chini ya CCM, CUF siko zote walisema wakishinda uchaguzi wataingiza baadhi ya wabunge wa CCM kwenye baraza la mawaziri. Ni kweli itakuwa ngumu kupitisha sera zozote bila majority bungeni...hivo basi kuongeza idadi ya wabunge muhimu

Mkuu ni kweli katiba haikatazi lakini ukweli ni kwamba ili raisi aongozi vizuri zaidi kwa amani zaidi ni lazima awe na watu wa chama chake katika baraza. Sijaona bado uzalendo wa kiasi kwamba waziri wa chama X akiteuliwa basi atakua tayari kumtumikia raisi wa chama Y bila hujuma yoyote. Itakua ngumu sana kwa raisi kuongoza na mawaziri wasio wa chama chake. Kuwaweka baadi ya watu wa chama tofauti ni swala lingine lakini kuwa na baraza ambalo majority ni mawaziri wasio wa chama chako hiyo ita muwiwa ngumu raisi yoyote.
 
Tunasukumiziwa katika makoo yetu chama kimoja tu kuwa ndicho pekee chafaa kuungwa mkono katika kuiangusha CCM. Tunaambiwa vyama vingine viungane nacho kwa sababu kimeonesha uongozi na kuwa ndiyo "upinzani" wa kweli. Wapo watu wanaoamini kabisa jambo hili. Wanaamini kuwa CHADEMA ndicho chama hasa mbadala kinachoweza kuchukua uongozi wa taifa letu toka mikononi mwa CCM.

Kama nilivyouliza huko nyuma ni mambo gani Chadema wamefanya kustahili kuongoza leo naomba nidokeza swali hili ambalo ni muhimu.

Je Chadema ilivyo sasa iko tayari kuongoza taifa la watu milioni 40 kwa ubora na kwa maono bora zaidi na mfano mzuri wa kiuongozi katika ngazi zote kuliko CCM? Ni nini msingi wa imani ya wale wanaoona kuwa iko tayari?

Mwenyewe ni na maoni yangu.. naomba nisikie ya kwenu.

Ukiwa makini utaona swali linahusu Chadema na utayari wao kuongoza.. nje ya hapo ni red herring.

Kwa mtazamo wangu, hawajafanza chochote cha maana kusema kustahili kuongoza taifa. Nasema hivi si kwao tu bali kwa vyama vya upinzani vyote tulivonavyo. Sababu zangu very simple, njia wanayoichukua ni ileile ambayo CCM wameichukua. Magenge ya kibinafsi, yenye fikra tengetenge, za kibiashara, sifa binafsi, maslahi binafsi, maono ya muda mfupi, zero vision etc etc..Hii ni bila kusahau ukweli kwamba siasa is not a way forward for development, sustainability and survivability of mankind.

Nimemaliza.
 
Balantada mimi nikijibu humu itaonekana navutia kwangu nitakuwa bias kama Mwanakijiji anavyokuwa bias,yeye tayari ni mCCJ kwahivyo hoja zake zitakuwa ni kuiponda CHADEMA tu ili kuipa nguvu na uhalali CCJ ionekane ndio chama mbadala.Hajui kuwa mpaka chama kionekane kinaweza kuongoza nchi sio kazi rahisi kama anavyodhani.Anafikiri kuwepo kwa CCJ leo ndio kukubalika kwake,haya yanawezekana nchi nyingine lakini sio kwetu Tz kwa wapiga kura wasiojua wajibu wala maana ya kura yake.Mwanakijiji nadhani CCJ watachukua nchi kirahisi wakati hata kupata hao wabunge kwao kwa mwaka huu ni kizungumkuti.Anafikiri ni sawa na mijadala ya humu JF rahisi rahisi. Field ni kugumu kuliko anavyodhani. Mie ni bora niwe msomaji tu nisije kujipendela ila ikibidi sana kuchangia itabidi nifanye hivyo..naangalia maoni ya watu wenye dhamira ya dhati(wanaosema ukweli na sio ushabiki wa kivyama)

haijajibu swali na kama nilivyoonesha hapo juu maada inahusu uwezo wa Chadema kuongoza siyo CCJ kwani CCJ siyo chama chenye usajili wa kudumu, ni hoax n.k chama kikweli cha upinzani nchini ni Chadema.. turejee kwenye swali.
 
Ni chama chenye individuals wazalendo! Wame risk sana kufichua maovu yanayofanywa na serikali ya CCM. Vyama vingine vya upinzani viko wapi? CHADEMA wanamchango mkubwa sana katika kubadili mwelekeo wa siasa ya Tanzania wamekuwa waaanzilishi wa hoja muhimu sana, wafichuzi wa mafisadi na wanaangazia watanzania kuhusu mbwa mwitu ccm aliyejivika ngozi ya kondoo!

mbona wapo wengine weengi tu walio nje ya chadema ambao wamerisk mengi vile vile kufichua ufisadi on individual level labda kuliko wengine wengi tu walio ndani ya vyama? Au hawa siyo wazalendo?
 
Kumbe kazi uliyokuwa unaifanya kwa miaka minne sasa ndiyo inaanza kuonekana at least now unaanza kuonyesha a true colour of you, kuzunguka kote huko kumbe mwisho wako ndio huu, Nina sababu 51 kwanini nisimchague Kikwete LOL! lakini umewahi sana kujionesha ungevuta muda kidogo uwakamate wengi, tchao.

hahahaha.. Luteni.. jifunze vizuri kwa makamanda vitani.... kuna bao litafungwa ambalo wachache watajua limefungwa vipi... vita ni pamoja na kujua kumzidi maarifa adui siyo wingi wa makombora.. read the "art of war'..
 
haijajibu swali na kama nilivyoonesha hapo juu maada inahusu uwezo wa Chadema kuongoza siyo CCJ kwani CCJ siyo chama chenye usajili wa kudumu, ni hoax n.k chama kikweli cha upinzani nchini ni Chadema.. turejee kwenye swali.

Nilimjibu Balantanda alitaka nijibu nami nikaeleza kuwa nikijibu nitakuwa najipendelea..Jibu langu obvious litakuwa kule kule kwenye postive hivyo wacha niwaache wengine wajibu.
 
Let's face it. CCM wenyewe hawawezi kuongoza. Kwa kifupi ni hakuna anayeweza kuiongoza Tanzania kwa sasa. Kama yupo mtajeni tumchambue hapa. Hili linchi linajiendesha lenyewe tu.
 
Kama ni hivi, nani au chama gani kinaweza kuwa chama mbadala?

ni lazima tujibu kwanza swali la msingi; mengine yatajijibu kwa kadiri. Yawezekana ni Chadema au TLP au CUF.. lakini kwa wakati huu tumeuliza swali moja lenye kuhitaji majibu yenye kushawishi.
 
CHADEMA ni NGO na siyo chama cha kisiasa. Kwa hio haifai kuchukua serikali
Vyama vyote tu NGO. Ni NGO kwa maana kwamba wapo kuteteana na ku-keep image hata kama sio kwa maslahi ya wengi. Vyama vingine vinakwenda as low as kuwa na njia kharamu za kupata fedha, vingine vina mpaka death squads...na etc etc. Na hii yote inasababishwa na misingi yenyewe ya hivi vyama. UBINAFSI.
 
CHADEMA wamefanya mengi kuliko CCM kwa nafasi yao..
(1) Mapamba dhidi ya UFISADI mzizi wake ni CHADEMA---reffer the list of shame by Dr. Slaa at Mwembe yanga...na hata hao wanaopelekwa mahakamani kwa kuzuga wapo kwenye ile list, thats is to say CHADEMAis against Corruption as compared to CCM.

Kinafaa kwa sababu ya list of shame! - got that..

(2)Reffer to Hoja za wabunge kama Dr. Slaa, Zitto (ingwa siku hizi simuelewi elewi) ambazo kimsingi ndo zimeibua mijadala mingi bungeni amabayo wabunge wa CCM hwana ujasiri hata wa kuizungumzia na familia yao.

Kinafaa kwa sababu kina hoja za wabunge zenye kuibua mijadala mingi.. got that!

(3) Chadema ni wavumilivu (political tolerant party)...reffer rafu walizochezewa Busanda na Kwa Marehemu Wangwe.

kwa sababu ni wavumilivu wa kuchezewa rafu - got that too

(4)CCM wamepoteza sifa za kuongoza nchi..so chama mbadala kwa Tanganyika ni CHADEMA

kwa sababu CCM wamepoteza sifa ya kuongoza nchi.. got that

well! hizi ni sababu tosha za kuwa chama mbadala kuongoza taifa?
 
Chadema kama vyama vingine vya upinzania, kwa kuongoza watu milioni 40 bado. Huu ni wakati mzuri kwa CHADEMA kujipanga vizuri kuongeza majimbo (wabunge), wanachama na viongozi wataoweza kuleta mabadiliko makubwa kuiangusha CCM. Ni wakati wa kurekebisha kasoro zilizopo. Katika moja ya badiko langu, nilitoa mfano kama leo CHADEMA wanaongoza nchi, ningependa kujua japo listi ya mawaziri na naibu mawaziri tukiacha wakuu wa mikoa, wilaya, tarafa nk.
 
Yote haya yanajadiliwa ni harakati za kukipigia kampeni chama kisicho na usajili. Tukiunge mkono chama chenye usajili kwanza, then hivyo vingine tutaviangalia baadaye vitakaposajiliwa. Tukirudi kwenye topic, naungana na aliyezungumzia suala la idadi ya wabunge, kwani hao ndo wanaweza wakatoa mwelekeo wa uwezo wa chama kuongoza ambao kwa sasa hakuna chama cha upinzani kinaweza kuongoza.
 
Back
Top Bottom