Vipimo tunavyoweza kutumia kuwapima CHADEMA ni kupitia viongozi wao tuliowachagua kuwa Wabunge wetu au madiwani wetu, pamoja na utekelezaji wa sera zake. Kwenye ishu ya ukabila sipo kabisa.
Sina data sana ila nadhani Dr. Slaa amefanya vizuri sana kwenye jimbo lake na amekuwa kiongozi mzuri sana kwenye kamati ya Bunge aliyomo. Ukimwangalia Zitto Kabwe nae kuna mambo mengi sana mazuri amewafanyia wananchi wa jimboni kwake, na amesaidia sana kwenye kamati ya madini (though at some point nilitofautiana nae kimtazamo). Halima Mdee nae amehangaika sana na kuwasaidia kina mama, watoto na vijana.
Ila nadhani bado wahitaji watu zaidi kuweza kuiongoza serikali, maana ukiangalia watendaji wazuri tunaowajua toka CHADEMA sidhani kama wanazidi kumi. Na hapo ndio umuhimu wa kuungana na vyama vingine vya upinzani unapokuja. Ila suala la kuungana linahitaji kukaa chini na kuanza kuangalia mwisho utakuaje tukishaunga - kimadaraka, kimtazamo(ilani), uteuzi wa wagombea, jinsi ya kuiongoza serikali etc.
All in all nna imani kiutendaji CHADEMA wanaweza kufanya mambo mazuri, ila angalizo langu nikuwa, sio lazima mtendaji mzuri kuwa kiongozi mzuri.