Chadema Baada ya Uchaguzi 2015--Great Thinkers Only! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema Baada ya Uchaguzi 2015--Great Thinkers Only!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rosemarie, Sep 27, 2012.

 1. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Iwapo Chadema itashindwa uchaguzi Mkuu 2015 maisha yataendela kama kawaida,hakuna kiongozi au Mwanachama yeyote wa Chama atakaye chukua hatua za kujiondoa uhai, Chadema tumeshakubalika na kuaminika kwamba tunaweza kusogeza nchi yetu hapa ilipo na kuipeleka mbele,nilifanya research yangu binafsi hapa Arusha,niliongea na watu 47 kwa week moja na kutaka kujua uwezo wao wa kuelewa nini maana ya Serikali na uongozi wake,niligundua watanzania wengi sasa hivi wanaelewa maana ya Serikali na wajibu wa serikali kwa wananchi wake,swali la mwisho nililowauliza utachagua chama gani iwapo uchaguzi mkuu utaitishwa leo,watu 45 kati ya 47 walisema watachagua chadema,2 walisema hawajui,hakuna hata mmoja aliyesema atachagua ccm.

  Hii inaonyesha wazi ni jinsi gani Chadema ilivyofanya kazi kubwa ya kuwaelimisha watanzania kujua haki zao na uwajibikaji wa serikali yao kwa ujumla Kama mwanachama wa kawaida wa Chadema nimeona nitoe maoni yangu hapa JF kwa kuwa viongozi wa Chama na wapenda mabadiliko wenzangu mpo hapa
  Nisingependa kusubiri 2015 kuona matokeo yakitangazwa na tume ya uchaguzi ambayo ipo chini ya ccm na kuitangazia ushindi ccm,nini kifanyike ili kwa vyovyote vile uchaguzi 2015 tuwe na uhakika 100% tutaondoka na ushindi wa kishindo?

  Chadema ilikuja na kelele za ufisadi na wizi wa raslmali za taifa letu,kelele hizo zilifanya kazi kubwa ya kuwaamsha watanzania waliokuwa wamelala usingizi mzito na kuwafanya kuwa na hasira kali dhidi ya serikali ya ccm, tunakoelekea hizi kelele zitakosa ile nguvu yake ya asili na kubakia kama kelele za kawaida kwa sababu watanzania ni watu wa kusahau haraka na pia kwa jinsi maisha ya mtanzania yalivyo itakuwa ngumu sana kukumbuka yote haya,nini cha kufanya ili hizi kelele zibaki na nguvu yake mpaka november 2015?

  Kuna haja ya Chadema kusogea another level???

  yes ipo haja sasa kwa sababu tayari Chadema imeshakubalika nchi nzima,na kelele zote za ufisadi na wizi zimesikika kwa wenye nchi yao, je kuna haja ya kuendelea kupiga kelele za ufisadi tena??jibu ni noo!
  nasema hivyo kwa sababu ngoma ikilia sana mwisho hupasuka,Chama kwenda another level ni kuchukua hatua na kusonga mbele kuangalia jinsi ya kushawishi wapiga kura wakichague. Chadema inatakiwa kupunguza kelele za ufisadi kwa sababu moja tu!CCM inajipanga upya,nani anajua labda watakuja na safu mpya isiyoshutumiwa??

  kama ikiwa hivyo kelele za chadema zitaenda wapi??we need to go another level now! Chadema ikianza sasa hivi kupigia kelele kazi na mabadiliko watakayofanya kwa watanzania,na kuwafundisha watanzania kuhudhuria mikutano yao na kalamu na daftari ili waandike watakachofanya watakapoingia madarakani itakuwa ni another level!

  watanzania wakianza kusikiliza na kuandika nini kitafanywa na serikali na sio kunyanyua vidole viwili juu itakuwa ni hatua kubwa kuelekea ukombozi, wingi wa watu kwenye mikutano sio wingi wa kura,kunyanyua vidole viwili juu kama tulivyozoea sio wingi wa kura, Chadema hakuna njia mmbadala zaidi ya kuanza kueleza sera zako na kuzipigia kelele za nguvu hadi watanzania wasikie na kuelimika kwani hiyo ndiyo nguvu pekee ya kushinda hii vita ingekuwa ni rahisi kuondoa CCM madarakani ingeondoka 2010,lakini bado ipo na wanajua walitakiwa watoke wakalazimisha,ni nani anajua kama hawatalazimisha 2015??

  Kila la kheri Chadema   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Good research!
  Ungeendeleza utafiti wako hadi pale Tanga, Singida, Lindi Mtwara na Dar Es Salaam ili tujue tutashinda kwa kiasi gani!
   
 3. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  ni ngumu sana kufanya research mikoa uliyotaja kwa kuwa mimi ni mkaazi wa Arusha
   
 4. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,302
  Likes Received: 10,341
  Trophy Points: 280
  Kumbe mnajua CCM inajipanga na mnajua 2015 hamuwezi kupata uraisi. Vizuri sana vijana.
   
 5. I

  IBRAAH Senior Member

  #5
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 3, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sera za cdm zinaeleweka na wananchi wanajua nini watafanyiwa na CDM na wamekiamin kama ndio mkombozi wa hi nchi.pia ufisad ndiio uliopelekea watu kuwa masikini sasa sion haja ya kuto endelea kuliongea wakati bado rasilimali zetu na fedha zinaibiwa hadi leo mafisadi wapo na halionei uchungu taifa hili wakinyamaza si ndio wataiba zaida?.maisha mazur hayawezi kuwepo kama ufisadi utakuwepo.NI LAZIMA CDM KUENDELEA KULIKEMEA JAMBO LA UFISADI.
   
 6. I

  IBRAAH Senior Member

  #6
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 3, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapiga kura wa sasa sio wale wa zamani ambao walikuwa wanapiga kura wanarudi nyumbani na mlikuwa mnatumia mwanya huo kuiba wa sasa wanapiga kura wanalinda pia sahauni kuiba mmesahau vituo vyote vilivyo lindwa CDM ilishinda.

  MMEJIPANGA KUIBA KURA TUMEJIPANGA KUPIGA KURA KUKICHAGUA CDM NA KUZILINDA KURA ZOTE HALALI ZA CDM. M4C~daima.
   
 7. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  ccm ikishinda 2015 nitakuwa disappointed sana na wananchi,.cdm ikishinda itabidi iende extra mile kuibadilisha hii nchi maana imeharibiwa vya kutosha
   
 8. Wile GAMBA

  Wile GAMBA JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 1,809
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  ni muhimi sana kuendelea kupiga kelele za ufisadi, kwa sababu mafisadi bado wako mtaani. kama unapiga kelele kwa ushahidi tu hiyo sawa, maana ya kukisimamia kitu ni kukiongelea na kuhakikisha kimefanyiwa kazi, bado ufisadi upo sasa kwanini watu wakae kimya. na kitu muhimu sana kuhusu ushindi wa CCM ni namna ya kuangalia kudhibiti wizi wa kura. hilo ndiyo la muhimi, wakati nyie mnaelimisha wananchi na kuuza sera zenu, wao wana panga namana ya kutoa rushwa na kuiba kura hili ni tatizo kubwa sana. na nina wasiwasi mkubwa sana kama mwaka 2015 tume ya uchaguzi ya CCM itatumika kuwapa ushindi mabwana zao kama kawaida yao. basi hapo ndiyo tutagundua Tanzania siyo inchi ta amanani, bali uvumilivu umefika mwisho.
   
 9. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  ndio maana nikasema great thinkers only,watanzania walishajua kuhusu ufisadi,we need to go another level
   
 10. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Ukae ukijua kwamba ni aibu kubwa sana kusema "CCM INAJIPANGA". CCM Imekuwa madarakani kwa kipindi cha miaka hamsini, inategemewa kuwa tayari kwa uchaguzi hata kesho. Huo ukweli tu kwamba CCM inalazima kujipanga kama mnavyosema wenyewe ni ushahidi kwamba CCM iko kwenye wakati mbaya sana katika historia ya uwapo wake.

  Mkae mkijua kwamba, hizo kelele zenu za kujipanga sio ishara za kuitishia CHADEMA, bali mnajivua nguo, mnachokifanya ni sawa sawa na mzee wa miaka 60 kumuambia kijana wa miaka 30 kwamba amejiandaa kumkabili kwenye mjadala wa kutatua tatizo la kifamilia.
   
 11. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  show us the way. What is that level?
   
 12. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Safi sana.
   
 13. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,302
  Likes Received: 10,341
  Trophy Points: 280
  Umejipanga pekee yako na kuanzia 2013 watu wataanza kurudi CCM ukiwamo wewe la sivyo utaachana na siasa.
   
 14. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,302
  Likes Received: 10,341
  Trophy Points: 280
  CDM haiwezi kushinda
   
 15. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Unasema wananchi wanajua juu ya ufisadi, we need to go another step foward! Jiulize hawa chama cha mabwepande wameacha KUIBA? Hawa jamaa ufisadi na wizi ni kama SALA YA BABA YETU ULIYE MBINGUNI...! NA SALAMU MARIA kwa mkristo wa RC. Chadema ikiacha tu kupiga kelele za ufisadi, hakika utaja sikia siku moja njia unayoendea kwako imeuzwa na unadaiwa kodi kwa kupita humo. Yaongezwe mengine lakini ufisadi pale pale.
   
 16. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #16
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,302
  Likes Received: 10,341
  Trophy Points: 280
  Mtaimba weee badae mtarudi
   
 17. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,302
  Likes Received: 10,341
  Trophy Points: 280
  Pigeni kelele tu lakini CCM iko juu siku zote hakuna chama kinachoweza kuitoa kwa sasa labda baada ya miaka 30 ijayo.
  Mtaimba nyimbo zote eti m4c eti mchaka mchaka mpaka ikulu, eti sikui sangara eti sijui nini.
  Hizo ni nyimbo tu viongozi wenu wanajua hawataki kuwadisapoint kwa sasa.
   
 18. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #18
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Simple Mathematics 80-60 =20 so 60-20=40. So Mnalazimika kushinda kwa 40% Good Lack.
   
 19. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #19
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,302
  Likes Received: 10,341
  Trophy Points: 280
  We piga kelele zako hebu waulize viongozi wako vizuri.
   
 20. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #20
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  How old are you ? .... I think we need baby diapers in jf now
   
Loading...