CHADEMA, anzisheni TV/Radio Station!

mwanza kwetu aliweka hii post yake
Agree

CDM
1. wawe na radio
2. wawe na TV ya mlengo wao
3. mkakati wao wa kwenda kijijini mhimu sana na uendelezwe bila kuchoka
4.bunge liendeleze vita kali sana ya utalaam ili activity yao iweze ku-outpay ccm na wingi wao; ref Lisu yesterday
5. kuongeza kada za aina na jamii zote kuanzia wasomi hadi wakulima na wajisikie wako huru na salamanhuko na waone huyo ndio mkombozi
6. waongeze na washinde propaganda ya Amani ambayo inatumia miaka yote na CCM; wapewe wananchi ujasiri kwa amani ili waone huko kuna amani maneno ya ccm yasiwe na guvu na kuepuka uhuni wa ccm ktk hilo
7. etc
na dk Slaa akamjibu hivi jana ilikua tr 18/04/2011

Mwanza Kwetu,
Thanks a lot. Ushauri umepokelewa na ninakuhakikishia yote yanafanyiwa kazi. Usichoke, na wana JF msichoke kutushauri. Ukombozi ni wetu sote na jamii yetu. Nguvu ya umma ni pamoja na mchango wa kila mmoja wetu. Thhanks a lot. Kesho tuko Jimbo laa Bukene na Nzega na Kesho kutwa tunaingia Igunga. Tusindikizane wote.
 
CHADEMA tupeleke 'nguvu za hoja' zetu huko huko ktk 'viwanja' wanavyotumia sasa CCM. Viwanja hivyo ni hapa JamiiForums ambapo tayari tumewazidi kete, kwenye magazeti yenye 'blogs' kama Mwananchi na Majira tayari CHADEMA tumewashinda CCM kwa hoja. Pia ndani ya Bunge huko Dodoma CCM wanahali mbaya hata wananchi wanaona hoja zetu madhubuti zenye mantiki toka CHADEMA. Ijumaa wakati wa kufunga kikao cha Bunge cha April, 15/04/2011 tumeona hata Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda alikubali hoja ya Mh. Tundu Lissu kwa kutamka 'NDIYO' anaunga mkono hoja ya CHADEMA kuwa Wakuu wa Mikoa kutojihusisha na Mahakama. Pia tuendelea na oparesheni kali zaidi za dizaini ya OPARESHENI SANGARA ambazo wananchi wanapata nafasi ya kuwaona uso kwa uso makamanda wetu wa hoja toka CHADEMA, hii inafanya wanachi kuwa karibu zaidi na chama chao CHADEMA.

Kwa sasa hivi ni muhimu popote tulipo kushikilia hoja ya kwamba ndani ya siku 90 mafisadi waumbuliwe na CCM yenyewe na kuhakikisha CCM inawapeleka mahakamani. Huko ni kuwapa CCM kitanzi wajinyonge wenyewe maana kila mtu Tanzania anaelewa sera ya CCM ni UFISADI na kuulinda UFISADI. Hivyo kama safu mpya ya uongozi wa CCM chini ya mwenyekiti wao Rais Kikwete ikitekeleza kujivua GAMBA a.k.a kuwaondoa chamani (CCM)mafisadi na kuwafikisha mahakamani mafisadi wote ndiyo itakuwa kifo cha CCM. Maana UFISADI umo ndani ya DNA ya CCM iwe walivue GAMBA au wabakie na GAMBA yote ni kitanzi cha kukimaliza chama chao cha CCM.

Kama wana-JF wengine walivyosema ruzuku za chama kwa CHADEMA na michango ya wapenzi wa CHADEMA ielekezwe kwenye mikakati ambayo inaonyesha kuipiga 'TKO' Technical-Knock-Out chama cha CCM katika raundi ya mwanzo kabisa ya mpambano huu wa kisiasa yaani ndani ya miezi 12 kuanzia leo 18/04/2011 maana mpaka sasa CCM imeshaanza kuonyesha uchovu wa hoja,fikra na mikakati ya kuinasua Tanzania toka kwa mafisadi.
 
REPOTI YA Dr. W. SLAA 17th April 2011 source: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...fanya-chadema-ni-kulipiza-kisasi-kwa-ccm.html

NANUKUU:
''Ni dakika chache tu nimeingia kutoka Kaliua na Urambo. Tumekuwa na mikutano mitatu ya hadhara, tumefungua ofisi na matawi ya Chama. Hivyo si kweli kuwa Chadema inalipiza kisasi kwa CCM.

1)Kwanza inaelekea wengi hawafahamu malengo ya mikutano ya vijijini, na hasa kwa kuwa wanapata magazeti, wanatazama TV wanaamini Watanzania wote wanafanana. Lengo la Chadema katika hatua hii siyo kuwaambia CCM mbinu ya kuleta maendeleo wala kuwapa mikakati ya maendeleo. Ikumbukwe kuwa Chadema haikusanyi kodi yeyote ya wananchi na hivyo katika kipindi katika ya Uchaguzi kazi ya Chama cha siasa ni kujijenga kwa uchaguzi ujao,kukosoa Serikali iliyoko madarakani katika sera,Ilani na utekelezaji wa sera na ilani hiyo,kwa lengo la kuwaelimisha wananchi kuelewa udhaifu wa Chama hicho Tawala ili katika uchaguzi ujao tuiondoe. Hii ndiyo kazi yetu ya kikatiba. Chama cha siasa chenye kujua wajibu wake hakiwezi kuwa wasindikizaji tu. Sisi si washauri wa Serikali kwa kuipatia mbinu za kuongoza au mikakati ya kuongza na kuleta maendeleo. Kama yuko anayefikiri hivyo ni vema arejea vizuri majukumu ya vyama vya siasa.

2)Sisi tunaofika vizuri ndio tuko kwenye mazingira ya kutafsiri nini kizungumzwe katika kijiji fulani tofauti na kingine. Hii inatokana na uelewa unaotofautiana. Katika kijiji kingine hata ajenda iliyokwisha kuzoeleka kwa watu wa vijijini kama Listi of Shame iliyotolewa 2007 inabidi itolewe upya kwa kuwa wananchi hawajawahi kujua ni kwanini nchi yeny utajiri mkubwa kama TZ inaweza kuwa maskini, au inakuwaje wako wanaoogelea katika utajiri mkubwa wakati wao hawana zahanati, maji, wanakula mlo mmoja bila kujua kuwa inatokana na rasilimali nyingi kutafunwa na mafisadi. Najua wako ambao wanaumia kwa sababu zao kila tunapowataja mafisadi, lakini katika mazingira kama hayo Mwanasiasa makini ni yule anayejua mahitaji ya wananchi wake. Hivyo, Msishangae wana JF kuona tunayarudia yale yale. Mtakuwa wabinafsi iwapo hamtapenda watanzania wenzenu wayajue mnayoyajua nyie.

3) WanaJF wako katika jamvihili wanaoishi dunia yao wenyewe, au kwa kutaka au kwa bahati mbaya. Mathalan, nimestuka sana, kama niliyoelezwa Kaliua ni ya kweli Tanzania kuna ndugu zetu wanaishi bado Tanganyika ni si mwaka 47. Kaliua mtu mmoja aliyetajwa kama Baraka,mtoto wa Kapuya amekuwa tishio kwa wana Kaliua wote.Wanakaliua wanapigwa,wanachomewa nyumba, wanauawa na wakilalamika polisi nao inafyata kutokana baba Baraka kuwa tishio. Katika mazingira kama hayo usifikirie utazungumzia maendeleo zaidi ya kuwajengea ujasiri,mbinu za ukombozi na hata kuwafafanulia ufisadi mkubwa katika Jimbo kama hilo. Haiingii akilini mwa yeyote, kwa umaskini mkubwa tulioona Kaliua, na bado 72 Millioni zimetafunwa kwa jina la au kupitia kasma ya Mishahara (mishahara hewa, mishahara kulipwa kwa watumishi waliofariki, waliofukuzewa watoro n.k.) Kwa bahati mbaya hata tunapokuwa na Waandishi wa habari katika ziara mazingira na hotuba kama hizo hazipati nafasi kwa sababu yeyote ile, au hata kwa vile tu mwandishi anachagua anayotaka yeye.

Hali inatisha, ndiyo maana Chadema tumedhamiria kutoa elimu katika vijiji mbalimbali kati ya sasa na 2015. Wanaoumia na hiyo waumie tu. Wananchi wengi vijijini ndicho wanachohitaji kwa CCM siku mmoja haitawapa elimu hiyo. Wilaya/Jimbo Maskini kama Kaliua haingii akilini inapotokea Halmashauri inashindwa kutumia Tshs 659,697 Millioni katika mwaka wa Fedha, na hatimaye isionekane katika B/F kwa kuwa mfumo wa uhasibu wa almashauri hauna utaratibu huo. Matokeo yake hakuna anayejua fedha hizo zimeenda wapi. Kama Madfiwani wa Kamati ya Fedha hawajapangia matumizi ni nani anapangia matumizi. Kama Chadema hatutakemea ufisadi wa namna hiyo nani akemee. Ikumbukwe hii ni wilaya iliyokuwa hadi mwaka wa ukaguzi yaani Juni 30, 2010, mawaziri wawili na Spika wa Bunge.

Ndugu zangu wengine kwenye jamvi hili wanazungumza tu nadharia bila kujua hali halisi ya nchi yetu, au kwa makusudi tu wanataka kutuondoa kwenye ajenda zetu. Hatoki mtu hapa "ngo"(kwa lugha ya kina Kombani. Atakuwa mwanasiasa wa ajabu ambaye anahutubia mbele ya Ofisi ya "Spika" iliyojengwa Urambo, wakati Urambo haina Bunge na hivyo haina Spika. Hii ni ofisi iliyojengwa kwa milioni zaidi ya 300 na kuwekewa fenicha ya zaidi ya 170 Millioni, katika jimbo ambalo hakuna zahanati, vituo vya afya n.k. Mwanasiasa atakayeacha kutaja Ufisadi huu kwa kuwa wanaJamvi wachache wadhani wamechoka kusikia habari ya ufisadi atakuwa siyo mwanasiasa Makini. Kafiribigiri,naamini nimeeleweka.

Tushuke chini, tusidhani maisha ndani ya jamvi hili ndivyo yalivyo vijijini. Hata kama sisi tuna maisha mazuri, tuwafikirie wazazi wetu,shangazi zetu,wajomba zetu ambao bado wanaishi nyumba za tembe na majani, ambao mlo wa siku ni shida, ambao wameacha kula nyama kwa kuwa bei haishikiki nakadhalika. Hizi ni ajenda za kudumu na ndiyo namna ya kuondoa umaskini wa wananchi wetu kwa kuikaba serikali ngazio zote iache ufisadi na ielekeze rasilimali zote kuwahudumia wananchi badala ya kujijengea mahekalu, kutembelea mashangingi ya millioni 500. Hii ndiyo ajenda,inaewzerkana wewe huipendi lakini vijijini ndiyo mambo yenye "mshiko"- MWISHO WA KUNUKUU.

MAONI YANGU:
ZIARA ZA MASHINANI ZINAELIMISHA WANANCHI NA VIONGOZI WA CHADEMA KUHUSU MATATIZO HUSIKA YA SEHEMU MBALIMBALI NA KILA ENEO KUNA KERO TOFAUTI TOFAUTI KAMA RIPOTI YA Dr. W. SLAA kwa JAMIIRORUMS hapo juu na kutoa mwanga wa namna gani ya kuwapa matumaini pale pasipo tumaini kuwa CHADEMA ndiyo mkombozi wao na CHADEMA inafaa kuchukua dola.
 
Yote haya ni mazuri mno. yangenoga kama yangeonekana kwenye TV na kusikika kwenye radio. Babu nae anataka kuona na kusikia, yuko ng'ende.:whoo:
 
Wakati umefika wa mabadiliko
Je, wewe umechangia nini kuleta mabadiliko?
Angalau sisi tunaouwezo wa kupata mawasiliano ya mtandao,
Kulingana na tafiti zilizofanyika mwaka jana kipindi cha uchaguzi, njia kuu ya habari/taarifa kuwafikia wananchi ni kwa njia ya radio (By Dr. Kitila Mkumbo). CDM kama wanataka kuwafikia wananchi waliowengi ni bora waanze na kituo cha radio na mengine yatafuata.:yawn:
 
Nawaona njia wanayotumia kwa sasa ndio sahihi then baada ya watu kuelimika wabadilike na kuanzisha media,..................... Kwa sasa njia hii ni sahihi.
 
Wakati umefika wa mabadiliko
Je, wewe umechangia nini kuleta mabadiliko?
Angalau sisi tunaouwezo wa kupata mawasiliano ya mtandao,
Kulingana na tafiti zilizofanyika mwaka jana kipindi cha uchaguzi, njia kuu ya habari/taarifa kuwafikia wananchi ni kwa njia ya radio (By Dr. Kitila Mkumbo). CDM kama wanataka kuwafikia wananchi waliowengi ni bora waanze na kituo cha radio na mengine yatafuata.:yawn:

Good Comment
Hapa naona kuna mamluki ambao wanataka ku downplay umuhimu wa radio na TV katika harakati za kuwakomboa wana nchi, Wamesahau kwamba hapa kulikuwa na external service ya RTD miaka hiyo ya harakati ya ukombozi wa Afrika.
Mjasusi kwa hili mmekula chaka.:whoo:
 
Jamani hawa viongozi wetu wa CDM Regia, Mnyika Na Zito mbona hamsemi kitu chochote ? Ninawataka hawa kwa sababu huwa wanapita humu ndani.
 
Unajua sisi wana JF tunafaidi sana, tunapata habari hot, lakini unajua tupo 40,000 tu. hayo mamilioni ya watanzania wanahitaji hiyo radio na TV. CDM Toeni tamko tekelevu.:whoo:
 
Ujumbe huu,tumeshaupenyeza sana kwa Dr Slaa,mara nyingi pia kwa Regia Mtema,zaidi kwa viongozi wa juu cdm. Nadhani wanalifanyia kazi na namtaka Dr Slaa au Regia(MB) achukue muda wake,awashe komputa na kuitafuta jf ili aweze kutuliza wote wenye hamu na shauku ya kuwa na vyombo huru vya umma wa watanzania,ikumbukwe kuwa kwa sasa hatuna vyombo vya umma kwa kuwa TBC Corporation imebinafshwa,je hapo 2015 chama tawala chadema itawezeje kutufikia wananchi? Katibu mkuu chadema hitimisha thread hii! Thanks Jf.

Gsana kumbe mlishapenyeza ujumbe huu kwa Dk. Dk Please we need these radio and TV:sleepy:
 
Angalizo: NGO yenu hiyo itawashughulisha sana mwishowe itawadodea....

Kabla ya TV kuweni kwanza na sytem nzuri ya ku manage funds mnazopata kutoka kwa wanachama na serikali....

Hakikisheni mmeshamlipa mwenyekiti mkopo wa aliowapa wa helkopta...
 
Hoja ya Chadema kuwa na mtandao wake wa TV ni ya msingi. Kumbuka historia inaonyesha mafanikio makubwa ya kisiasa na kijamii yameweza kupatikana kwa matumizi ya mawasiliano ya radio na televisheni katika nchi mbali mbali na hasa zenye mafaniko ya ''utawala ulio bora'', hata kama si kwa asilimia zote. Lakini zaidi ya hapo Chadema ifikirie kuwa na kituo chake cha Redio pia!!!
 
Cha msingi ni kupima kama inawezekana kuanzisha CDM TV na kwa gharama zipi. Tujifunze kwa wenzetu. 2. Tusidharau mawazo na maoni ya mtu hata kama anatoka ndani ya familia ya ''wana-magamba''. Mbona Makongoro Nyerere aliwahi kuwa mbunge nje ya chama cha baba yake wakati huo! Kwa sasa chama cha wana-magamba ni cha mafisadi tangu J.Nyerere ang'atuke. Aliwahisema CCM (wana-magamba) sio mama yake angeweza kuachana nacho wakati wowote.
 
Kwa nini isiwezekani ??? Kwani CCM wao ni nani ?? Nchi hii ni ya waTanzania sio ya CCM.:spy:
 
Back
Top Bottom