Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,363
- 58,386
mbona bado wapo kimya? au hii thhread haiaisomagi wahusika? au kuna vikwazo vyovyote huko?
mbona bado wapo kimya? au hii thhread haiaisomagi wahusika? au kuna vikwazo vyovyote huko?
Mkuu nakubaliana na wewe kwamba chadema ina nafasi kubwa katika kuelimisha wananchi kupitia vyombo huru vya habari.Usitake kuingiza CHADEMA kwenye mkenge. Chadema staili yake ya kuendesha 'elimu kwa umma' kwa kutumia mikutano ya wazi na wananchi inatosha kuwaelewesha wananchi haki zao za msingi.
Historia inaonyesha kuwa ukianzisha vyombo rasmi vya kuwasiliana na wananchi kwa njia ya radio, TV au gazeti unakaribisha 'mamluki' kujipenyeza na kuchafua hali ya hewa.
CHADEMA iendelee kutumia mikutano na wanachi ili kuishitaki serikali ya CCM kwa kutowajibika kwa wananchi masuala ya RADIO UHURU, STAR TV, magazeti ya UHURU/MZALENDO/DAILY NEWS waachiwe CCM. CHADEMA tayari ina safu za viongozi na makada na wapenzi wake ambao wanatosha kusambaza 'elimu kwa umma juu ya siasa' na hakuna mantiki ya kuingia gharama ya vyombo rasmi vya habari.
Midahalo ambayo CCM huikimbia CHADEMA wanaitumia kikamilifu, vyombo huru kama JamiiForums CHADEMA inashiriki kikamilifu kutetea hoja zake. Mitego hii ya kutaka kuingiza mkenge CHADEMA gharama zisizo na tija inafaa kuepukwa kama suala hili la kuwa na TV/RADIO/Magazeti rasmi.
Tutafuata kila sheria inayotakiwa kufuatwa sasa wakileta mizengwe kutuzuia tunaingia mitaani!! umesahau kuhusu katiba mwanzoni walibana je tunakoelekea unaonaje?mnachekesha, usajili huo atatupa nani? Labda tuanzishe strategy ambayo inaweza kuwalazimisha hawa mafisadi kutoa hiyo leseni ya mawa7iliao6
Naunga mkono na mimi pia niko tayari kuchangia kama wengine wengi walivyo tayari!!Wazo zuri sana la kuwa na Vyombo vya habari, itasaidia hata kupata habari zikiwa na ukweli, Vyomb vingine vikichakachua CDM TV inaweka ukweli hazarani, tupo tayari kuchangia.
tupo wengi sana wapenda Chadema, na tukihamasishana yanaweza kusanywa mamilioni.
Unamatatizo ya akili huwezi kuchanganua kati ya kashifa na ukweli kinachofanya na chadema ni kuwapa wananchi ukweli kuhusu wahujumu wa rasilimali za nchi yao!!!! kwa akili yako mtu akisema Rostam Azizi ni mwizi amekashifu, kweli unahitaji kikombo cha Babu ili ukombolewe kifikira.Hiyo Tv itakuwa ya kukashifu watu nini?!
Licha ya kuelimisha na kuhabarisha umma Pia TV na redio ya chadema itakuwa ni chanzo cha mapato kwa chama na hivyo kuimarisha chama!!CHADEMA Television
Chama cha Democrasia na Maendeleo (CDM) kina kila sababu sasa kuhakikisha kinaa zisha kituo cha TV ili kuondoa hujuma tunzozishuhudia katika TV yetu ya umma TBC dhidi ya kile kinachoonekana dhahili kuziminya habari za chama hiki na wakati mwingine kutokukipa muda wa kutosha ukilinganisha na CCM.
Wote tunaelewa kuwa chama hiki kimeonesha kukubalika na wengi hasa vijana wengi wao wakiwa mijini, nadhani hapa jitihada za maksudi zinahitajika zifanyike ili elimu ya mabadiliko ifike mpaka vijijini ambako ccm bado imepafanya kama mtaji wa chama.
So nafikiri,kama cdm tv itaanzishwa na ikawa na uwezo wa kuchana mawimbi nchi nzima basi moja kwa moja CCM ijiandae kuzikwa rasmi 2015.
Wito wangu kwa viongozi wa cdm kuandaa mkakati kabambe wa kitaifa waje nao kwa wapenzi na wanachama wote wa cdm bila kuwasahau hata wasiokuwa na chama ili kuendesha mchango wa fedha nchi nzima wa kuanzishwa kwa tv chadema je tuko tayari?
Lakini nikileta hoja hii kwenu naomba pia nijulishwe je mamlaka ya anga hapa tz ina kizuizi kisheria juu ya jambo hili kufanyika?naomba kuwasilisha.
NB: Haya maneno si ya kwangu bali tu ni kwamba hata na mie hapa nilitamani kuyaona uzuri zaidi, kuyasoma na kuyaelewa.
Hii TV tunalihitaji kama tangu juzi vile!!!
Wakati mwingine huwa najiuliza kama kuna tofauti kati ya ccm na Chadema katika kusikiliza maoni ya wananchi na kuyafanyia kazi. Pengine tungejua kwanza wasifu wa timu ya mawasiliano ya Chadema. Wamelalamikiwa mno, mara nyingi sana na mara zote hawajawahi kujibu lolote wala kutekeleza chochote. Prove me wrong
mi siongei tena mpaka siku wanaJF kama Mbowe,zitto,dr mkumbo,dr slaa,mnyika,regia mtema, et all walio jf watoe majibu . Si lazima mmeseme kuwa mmeanza kutekeleza au hamtatekeleza bali mwaweza kutueleza kama mnaona inafaa au hapana,gharama hamuiwezi au vp,etc etc. Viongozi wetu,sema neno tu,nafsi zetu ziwaelewe! Tunawasubiri.
Hoja zinazotolewa ati si busara kwa CHADEMA kuanzisha vituo vyake vya mawasiliano bado ni dhaifu na zinahitaji tafakuri ya kina. Kwa vyovyote vile vyombo vya mawasiliano vinabaki muhimu kabisa katika kuendeleza propaganda kama wanavyofanya CCM na Radio yao ya UHURU na TBC, Channel Ten na mara nyingine ITV ambavyo mara kadhaa vimeegemea chama Tawala.
.....haingii akilini hata kidogo kwamba vyombo vinavyoisaidia CCM kueneza propaganda zake kwa mafanikio vilete matokeo tofauti katika CHADEMA. Kama hivyo ndivyo kina RA et al wasingehaha kuinunua Habari Corporation iliyokuwa very critical kwa CCM na uongozi wake mbovu.
.
mi siongei tena mpaka siku wanaJF kama Mbowe,zitto,dr mkumbo,dr slaa,mnyika,regia mtema, et all walio jf watoe majibu . Si lazima mmeseme kuwa mmeanza kutekeleza au hamtatekeleza bali mwaweza kutueleza kama mnaona inafaa au hapana,gharama hamuiwezi au vp,etc etc. Viongozi wetu,sema neno tu,nafsi zetu ziwaelewe! Tunawasubiri.