Pili, vyombo vya habari vitapunguza gharama ya mikutano. Mikutano husika itatangazwa ktik gazeti la Chama na Tv yake, badala ya kukodi gari na vyombo vya muziki na kuzunguka mitaani kwa siku mbili kwa gharama kubwa kabla mikutano husika.
[*]Pia CHADEMA kupata source/vyanzo vya hela nje ya ruzuku(matangazo ya biashara/wadhamini) kwa sasa ni mtihani mkubwa
Mimi mjumbe wa baraza kuu siwezi kulismea kamati kuu na secretarieti kuhusu hili, wewe unawezaje?
[*]Gharama za kuendesha Vyombo vya TV/Radio zitadhoofisha harakati zingine za kuwafikia wananchi kule walipo.
wewe umefanyia wapi utafiti? Je, kama mikutano lengo ni kufikia wananchi si Tv nayo inafikia wanachi? Kama mikutano ikipungua sababu ya TV na TV ikawafikia watu wengi zaidi kuliko mikutano, je hiyo si faida? Kwa taarifa, TV inaweza kuwafikia watazamaji mil moja kwa dk 5. Je CHADEMA inahitaji Tsh Ngapi kufanya mikutano mingapi kwa muda gani kuwafikia idadi hiyo?
[*]Ikiwa gharama za TV/Radio ni Tshs. Billioni 1(Clouds FM/Radio Uhuru bajeti zao ni mfano) kwa mwaka kwa uchache ni project isiyowezekana na ukienda ndani zaidi kufikia umma kona zote kupitia vyomb hivyo TV/Radio ni changamoto.
Sina hakika na data zako hapo juu, hii nayo inahitaji utafiti. Suala la uwezo ni la ndani sana ya Chama si hoja kwa sasa. Tunahitaji ukweli kuhusu IMPACT ya Tv kufikia wanachi kila kona. Kwani TBC inawafikiaje wanachi kila kona. Hapo inapoishia propaganda za TBC dhidi ya CHADEMA ndipo nasi tunapotaka kuishia.
[*]Mamluki kuingiza studio 'nyaraka za siri za serikali' na kisha kukilaumu CHADEMA ni rahisi
Hoja iwe tutazuiaje nyaraka feki na si tusianzishe TV. Kama Dr Slaa anaweza kupembua nyaraka feki na halisi na akaweza kuitikisa serikali, atashindwaje TV iliyoko chini yake kama katibu mkuu isitangaze nyaraka feki?
au hata kuchoma moto vifaa ghali vya kutendea kazi studio baada ya gharama kubwa kuvinunua ni rahisi kwa mafisadi na kupelekea kukidhoofisha chama cha CHADEMA.
Hii ni hoja dhaifu sana pia.
Mosi kila kitu kina risk yake. Hata kuendesha gari au kupanda dala dala ina riski. Je, tuache kupanda dala dala au tusinunue magari binafsi na tutembee kwa miguu? Kuchoma tv station ni changamoto tu, siyo sababu ya kutoanzisha tv au magazeti.
Pili, wewe bagamoyo hufahamu kuwa kuna kampuni za Insurance? Si tutaweka comperesive insurance tu? Wakichoma the next week tunafunga vipya na kupata attention kubwa zaidi itakayoongeza watazamaii.
[/LIST]Niishie hapo kuna sababu nyingi tu za 'kiintelejensia' ila kwa mikakati iliyopo ya sasa ya CHADEMA kuwafikia wananchi ni tosha kabisa kuleta mageuzi nchini.