johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,956
- 141,942
Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema mh Cecil Mwambe amesema haitaji watu wa kumchukulia fomu kwani zoezi hilo atalifanya yeye mwenyewe kwa kuwa anajiamini.
Mwambe amesema anachoomba ni ushirikiano kutoka kwa wale wote wenye mapenzi mema na Chadema ili kwa pamoja waweze kushinda.
Source Global tv
My take; Nakubaliana na Mwambe mambo ya kuchukuliana fomu ni mbinu za kizamani zilixotumiwa na akina rip Bamchawi pale Simba SC!
Mwambe amesema anachoomba ni ushirikiano kutoka kwa wale wote wenye mapenzi mema na Chadema ili kwa pamoja waweze kushinda.
Source Global tv
My take; Nakubaliana na Mwambe mambo ya kuchukuliana fomu ni mbinu za kizamani zilixotumiwa na akina rip Bamchawi pale Simba SC!
Cecil Mwambe: Mbowe msalaba umemuelemea na mimi ndiye Simoni Mkirene nipo tayari kubeba msalaba huo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, mgombea wa uenyekiti CHADEMA taifa Cecil Mwambe amedai kwamba kwa hali ilivyo sasa Mh. Mbowe ameelemewa sana na msalaba wa kuongoza CHADEMA hivyo anahitaji mtu wa kumtua na kumsaidia msalaba huo.
Cecil Mwambe amefafanua kwamba yeye ndiye mtu pekee anayeweza kumpokea Mbowe msalaba huo wa uenyekiti taifa kwani kwa sasa Mbowe ameprove failure katika kuongoza CHADEMA kama mwenyekiti taifa.
Cecil Mwambe amefikia hatua ya kujifananisha na Simoni Mkirene yule mpita njia aliyekuwa akitoka mashamba ambaye baadaye alibeba msalaba wa Yesu ambaye Yesu kwa kipindi hicho alikuwa ameelemewa na msalaba huo.
Cecil Mwambe amesisitiza kwamba lazima CHADEMA wajue kwamba mabadiliko ya kuongozi ndani ya chama yanahitajika sana kipindi hiki kwani Mbowe ameshaelemewa hivyo hakuna namna lazima aje mtu wa kumsaidia ambaye ndiye yeye Cecil Mwambe.
Pia Cecil Mwambe amewaonya wale waliopanga kumnyima fomu ya kugombea uenyekiti na pia amewaonya waliopanga kugoma kupokea fomu yake kipindi anairejesha ikiwa imeshajazwa. Kwani kuchukua fomu na kuirejesha ni haki yake ya kikatiba ndani ya chama.
Cecil Mwambe ameahidi kuboresha chama na kuleta mabadiliko makubwa sana endepo atashinda na kuwa mwenyekiti CHADEMA taifa.
Source: online TV.