Cecil Mwambe: Sihitaji mtu anichukulie fomu, nitaenda kuchukua mwenyewe ila tuwe pamoja kwenye kampeni kama mnanikubali

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,562
Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema mh Cecil Mwambe amesema haitaji watu wa kumchukulia fomu kwani zoezi hilo atalifanya yeye mwenyewe kwa kuwa anajiamini.

Mwambe amesema anachoomba ni ushirikiano kutoka kwa wale wote wenye mapenzi mema na Chadema ili kwa pamoja waweze kushinda.

Source Global tv

My take; Nakubaliana na Mwambe mambo ya kuchukuliana fomu ni mbinu za kizamani zilixotumiwa na akina rip Bamchawi pale Simba SC!

Cecil Mwambe: Mbowe msalaba umemuelemea na mimi ndiye Simoni Mkirene nipo tayari kubeba msalaba huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, mgombea wa uenyekiti CHADEMA taifa Cecil Mwambe amedai kwamba kwa hali ilivyo sasa Mh. Mbowe ameelemewa sana na msalaba wa kuongoza CHADEMA hivyo anahitaji mtu wa kumtua na kumsaidia msalaba huo.

Cecil Mwambe amefafanua kwamba yeye ndiye mtu pekee anayeweza kumpokea Mbowe msalaba huo wa uenyekiti taifa kwani kwa sasa Mbowe ameprove failure katika kuongoza CHADEMA kama mwenyekiti taifa.

Cecil Mwambe amefikia hatua ya kujifananisha na Simoni Mkirene yule mpita njia aliyekuwa akitoka mashamba ambaye baadaye alibeba msalaba wa Yesu ambaye Yesu kwa kipindi hicho alikuwa ameelemewa na msalaba huo.
Cecil Mwambe amesisitiza kwamba lazima CHADEMA wajue kwamba mabadiliko ya kuongozi ndani ya chama yanahitajika sana kipindi hiki kwani Mbowe ameshaelemewa hivyo hakuna namna lazima aje mtu wa kumsaidia ambaye ndiye yeye Cecil Mwambe.

Pia Cecil Mwambe amewaonya wale waliopanga kumnyima fomu ya kugombea uenyekiti na pia amewaonya waliopanga kugoma kupokea fomu yake kipindi anairejesha ikiwa imeshajazwa. Kwani kuchukua fomu na kuirejesha ni haki yake ya kikatiba ndani ya chama.

Cecil Mwambe ameahidi kuboresha chama na kuleta mabadiliko makubwa sana endepo atashinda na kuwa mwenyekiti CHADEMA taifa.

Source: online TV.
 
Wee Jo ni kigeugeu kinyonga kasingiziwa

Hapo anauzungumzia Uenyekiti wa Kanda ya Kusini. Sidhani kama inawezekana kwake kugombea Uenyekiti wa Kanda na wa Taifa.

Punguza kulazimisha mada za kitoto kama hizi. Uwe unafuatilia mambo na kuyajua kabla ya kukurupuka na kuanzisha mada humu.

Uione: johnthebaptist
Hahahaaa....... hahahaaa....... Wasomi wa jalalani bhana!
 
Mama, utaweza kulala sero? kwanza ushalala hata mara moja? sisemi kwamba kigezo ni kulala sero hapana ila kwenye kazi hii ya uwenyekiti sero na central na mahakamani ni kama vile sebureni kwako....yaani ni uji kwa mgonjwa...

Kheri maneno hayo angeyasema Mdee walau ningeshawishika......mama yangu nikwambie kitu kwa mtu mwaminifu kabisa kabisa kazi ya uwenyekiti wa CDM Taifa si ya kukimbilia hata kidogo....ni kujitoa maisha...je umeshainyesha hata mfano wa kujitoa? Yaani kukipigania chama kwa jasho na damu?
 
Si afadhali sisi wa jalalani kuliko wewe tapeli wa mtaroni? Kutwa nzima ni kutuhamishia humu vihabari vyako vya kizushi. Acha hayo mambo yako binti. Jifunze kujenga hoja!
Mimi sijasoma bhana kama nyie wanasheria nguli mnaosota jalalani.

Mimi na mdogo wangu Mbowe " tulizungusha" form six na safari yetu ya jalalani iliishia pale.......ndio maana Freeman anakulaani hadi kesho kwa kumdanganya aruke dhamana akasota keko miezi mitatu ilhali wewe ni msomi uliyetukuka from jalalani!

Wakili mzima nimekuwekea hadi source ya taarifa bado unaleta ubishi wa kimbegembege eti anagombea jimbo la kusini...........pua kawabanie kina Kubenea Ufipa huko!
 
Mimi sijasoma bhana kama nyie wanasheria nguli mnaosota jalalani.

Mimi na mdogo wangu Mbowe " tulizungusha" form six na safari yetu ya jalalani iliishia pale.......ndio maana Freeman anakulaani hadi kesho kwa kumdanganya aruke dhamana akasota keko miezi mitatu ilhali wewe ni msomi uliyetukuka from jalalani!
Haya. Kumbuka kula na kunywa na upumzike.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom