Mimi huyu kocha amenishangaza sana,amelalamikia goli walilofungwa akidai kuwa wachezaji walikuwa wakigombana nje alafu refa akaruhusu mpira urushwe na hatimae Yanga kujipatia goli la kuongoza dakika ya 100. Pili,huyu kocha amelalamikia kitendo cha mchezaji kutibiwa kwa dakika 6 uwanjani,nadhani alitafsiri kuwa ulikuwa ni upotezaji wa muda. Sasa hapa cha ajabu ni kwamba,kwa nini alilalamika kwa msisitizo kuwa "THIS IS AFRICA...",je,alimaanisha Africa hakuna waamuzi wenye akili au wachezaji pia hawana uwezo wa kutosha na ndio sababu ya wao kujidai wameumia mara kwa mara ili kupoteza muda?
Pia nikajiuliza,kama huyu kocha amefikia kuidharau Afrika,sasa anafanya nini huku,si aende Ulaya au mabara mengine akafundishe soka?
Ndo hayo tu niliya-note leo baada ya mecì kati ya APR FC VS YANGA FC.