CECAFA Kagame Cup 2012 - Live updates

CECAFA Kagame Cup 2012 - Live updates

Kitendo cha APR kuingia nusu fainali si habari nzuri hata kidogo kwa wana Yanga. Mechi itakuwa ngumu sana kwa vile timu hizi zilishacheza katika hatua ya makundi. APR siyo timu mbovu hata kidogo na itataka kulipa kisasi kwa Yanga, bahati mbaya hatua hii ni mtoano, ikiwa hivyo basi wana Yanga tutakuwa tumepata msiba wa mwaka. Nakumbuka mwaka 1993 kule Nakivubo stadium, Yanga ililala kwa 3-1 kwa SC Villa ya Uganda katika hatua ya makundi, timu hizi zilikutana fainali, mechi ilikuwa ngumu ajabu lakini mwisho Yanga waliibuka na kikombe katika nchi ya ugeni.

Nashauri benchi la ufundi la Yanga liweke mikakati maalum kuiong'oa APR, vinginevyo msiba unanukia.

Mnaanza mipango ya mbele wakati mafunzo wanawatoa jasho.
 
Mkuu Katavi uko sawa, siyo vyema kutukana mamba kabla ya kuvuka mto,hata hivyo hako kagoli kamoja katarudishwa na wataongezewa na kitolewa.

rejea post polisi utapata jibu lakini tym bado.. yasijekuwa ya simba na as vita..
 
Yanga wanataka kutukwepa tusikutane nao..Refa wape hata penati hao yanga..
 
Back
Top Bottom