Balantanda,
nakuona uko online tena kwenye hii thread lkn kimyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, subiri kesho uone faida ya kombe la urafiki.
Chukua tano mkuu...! Ulisema haya mwanzoni wakakuandama....ona sasa pwaaa kama CCM itakavyopigwa chini...!! Haya Yondan, hongera combination yako na Canavaro hakuna mfano afrika...lol
Watani msikate tamaa, kundi lenu linatoa timu tatu kwenda robo fainali kwa hiyo mkingangamala dhidi ya APR mtaqualify na kuna hatari yakukutana na mnyama kama mtashika nafasi ya tatu au URA.
Mtaalamu wangu ''Balatanda'' ni vyema ukahama timu mapema hii Yanga mlionayo kwasasa itakuzidishia presha, mnasema mmesajiri vizuri kuliko Simba lakini kila mara mtakua mnatoka uwanjani vichwa chini na huo usajiri wenu mzuri kisa Yondani na Nizar.
hongera sana yanga nina uhakika mngemchezesha kelvin yondan mgeshinda tena nyingi tu...ushauri wa bure mnaonaje tukiwapa sunzu awasaidie michuano hii maana mna weza kuvuna aibu..
kwa uzoefu walionao wachezaji wa Yanga pamoja na mafunzo waliokuwa wakipata kutoka kwa makocha waliokwishapita kwa mechi hii ata-kama wasingekuwa na kocha walitakiwa washinde, sasa kama wanaitaji kufundishwa mara kwa mara eti ndo wapate ushindi uwanjani basi hawastahili kuitwa ma-profesheno.
Head Coach: Tom Saintfiet Assistant Coach: Fred Felix Minziro,
Goalkeeper Coach: Mfaume Athumani
Team Physician: Dr Sufian Juma
Massagist: Jacob Onyango
Kit Manager: Mahmoud Omary (Mpogolo)
hongera sana yanga nina uhakika mngemchezesha kelvin yondan mgeshinda tena nyingi tu...ushauri wa bure mnaonaje tukiwapa sunzu awasaidie michuano hii maana mna weza kuvuna aibu..
Kiukweli Atletico ni wazuri sana...Kipindi cha pili wamecheza vizuri zaidi na waliwazidi Yanga katika kila Idara.....Kocha wa Yanga inabidi ajiangalie fomesheni yake ya kumuondoa Haruna Niyonzima kwenye kiungo na kumpeleka mbele kama mshambuliaji.....Chuji na Gumbo hawakuelewana kipindi cha pili...
Yaw Berko amefanya kazi kubwa sana leo,bila yeye Yanga wangefungwa magoli mengi sana......
Kelvin Yondani amecheza vizuri sana,tatizo lilikuwa kwa beki ya kulia na wakati fulani kwa Nadir Haroub....
Safu ya ushambuliaji ni butu......Ni bora Buhanuzi angeanza......
Mechi hii imepita,tusubiri zijazo sasa na APR na W. Salaam.......
Kesho Simba wanacheza na Azam pia wanacheza....Binafsi nitazishangilia timu zote hizo mbili so ndetichia, Crashwise na mtani wangu wa ukweli Masuke tegemeeni support yangu....Tupo pamoja kesho wakuu....