CCM yaunda 'ukawa' yake dhidi ya CHADEMA

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Mwaka 2015 CHADEMA na vyama vingine vya CUF, NCCR - Mageuzi na NLD, viliunda umoja uliojulikana kama UKAWA dhidi ya Chama cha Mapinduzi CCM kwa lengo la kuiondoa madarakani.

Mwaka huu 2020 CCM imeunda muungano wake na vyama vingine vya CUF, NCCR na TLP dhidi ya CHADEMA.

Ina maana CCM pamoja ya kuwa ina dola imeshindwa kupambana na CHADEMA peke yake hadi inaazima majeshi ya kukodi? Halafu bado kuna watu wanasema CHADEMA imekufa.

IMG_20200531_103555.jpg

Picture speeks a thousand words.

ACT-Wazalendo wanabaki kama watazamaji au swing voters?
 
CCM ya Jakaya 2015 ili kupambana nayo, Chadema ilibidi itafute majeshi ya ziada NCCR, CUF na NLD ili kuongeza nguvu maana uwezo wa CCM ulikuwa mkubwa.

Lakini miaka mitano baadae yaani 2020 CCM ya John imeshuka daraja na viwango na ili ipambane na Chadema sasa CCM inabidi itafute majeshi ya kuongeza nguvu nayo ni NCCR, CUF na TLP.

Ukiangalia kwa jicho lisilo ushabiki mpambano huu utakuwa mgumu sana maana CCM pamoja na usaidizi huo wa vyama vingine bado wana usaidizi wa Polisi na Tume.

Lakini pia upande wa Chadema nao nafasi ya nguvu ya watu kusimama upande wao (peoples power) ni tishio pia kwa wapinzani wao.

Nini sababu ya CCM kushuka daraja kiasi hiki hadi kutegemea msaada wa vyama vingine, vyombo vya dola hadi Tume ya uchaguzi wakati walikuwa na nafasi ya kujenga maisha bora na kuaminika?

IMG_20200531_103700.jpg
 
Quinine,

CCM imeshatambua kwamba inapambana na wananchi, siyo Chama.

Nguvu na ujumbe wa vitisho ambavyo wamekuwa wakipewa CHADEMA ni ujumbe kwenda kwa wananchi kwamba hata mtumie mbinu gani hampati kitu. Ujumbe huo pia unawalenga walio ndani ya CCM kwamba mkijifanya ku side na wananchi mjue hampo salsma, sasa hivi hata Jaji Warioba, Kabudi na akina Polepole wameshaikana ile rasimu ya katiba ya wananchi ambayo kwao walishaiona kama ni misahafu.

CHADEMA inapinzwa tu na wananchi wengi waliochoka, sababu CHADEMA kama chama hawana jipya wala tofauti na NCCR, CCM na CUF, kamavwangekuwa na kitu cha tofauti kamwe wasingefanya mabadiliko ya dakika za nyongeza kwenye nafasi ya mgombea wa nafasi ya urais.

Siku zote nitaendelea kumheshimu sana Dr. Slaa kwa mikakati na nguvu aliyoitumia kuijenga CHADEMA na kupelekea wananchi kuamua kukiunga mkono, pili msimamo wake wa kusimamia anachokiamini. Tatu utiifu wake kwa mamlaka zake za uteuzi, tuliona alivyokua mtiifu na mnyenyekevu kwa Mbowe na sasa alivyo kwa Magufuli.

CHADEMA haina cha tofauti, watu ndiyo wameamua kuichagua na nguvu inayotumika ni dhidi ya wananchi ndiyo inaiumiza CHADEMA. Kama kuna point itaonekana CHADEMA ni threat kiasi hicho basi ingefutwa kitambo tu.
Lakini wananchi hauwezi ukawafuta, ndiyo chanzo cha hasira na vitisho.
 
CCM imeshatambua kwamba inapambana na wananchi, siyo Chama.
Nguvu na ujumbe wa vitisho ambavyo wamekuwa wakipewa CHADEMA ni ujumbe kwenda kwa wananchi kwamba hata mtumie mbinu gani hampati kitu. Ujumbe huo pia unawalenga walio ndani ya CCM kwamba mkijifanya ku side na wananchi mjue hampo salsma, sasa hivi hata Jaji Warioba, Kabudi na akina Polepole wameshaikana ile rasimu ya katiba ya wananchi ambayo kwao walishaiona kama ni misahafu.

CHADEMA inapinzwa tu na wananchi wengi waliochoka, sababu CHADEMA kama chama hawana jipya wala tofauti na NCCR, CCM na CUF, kamavwangekuwa na kitu cha tofauti kamwe wasingefanya mabadiliko ya dakika za nyongeza kwenye nafasi ya mgombea wa nafasi ya urais.

Siku zote nitaendelea kumheshimu sana Dr. Slaa kwa mikakati na nguvu aliyoitumia kuijenga CHADEMA na kupelekea wananchi kuamua kukiunga mkono, pili msimamo wake wa kusimamia anachokiamini. Tatu utiifu wake kwa mamlaka zake za uteuzi, tuliona alivyokua mtiifu na mnyenyekivu kwa Mbowe na sasa alivyo kwa Magufuli.
CHADEMA haina cha tofauti, watu ndiyo wameamua kuichagua na nguvu inayotumika ni dhidi ya watu diyo CHADEMA. Kama kuna point itainekana CHADEMA ni threat kiasi hicho basi ingefutwa kitambo tu.
Slaa alikuwa sahihi lkn alichokosea ni kuungana na watesi wake.
 
Quinine,

Hii picha imenitafakarisha sana.

CCM ilipiga marufuku mikutano ya kisiasakwa vyama pinzani nchi nzima, ikabaki yenyewe ikizunguka na kufanya mikutano nchi nzima wakitumia rasilimali za watanzania.
Kinachoshangaza mpaka sasa bado hawajiamini na wametumia hila mbalimbali kufifisha vyama pinzani hasa chadema.

Lakini mwisho wake ndiyo hiyo picha inavyoonekana.
 
Mwaka 2015 CHADEMA na vyama vingine vya CUF, NCCR - Mageuzi na NLD, viliunda umoja uliojulikana kama UKAWA dhidi ya Chama cha Mapinduzi CCM kwa lengo la kuiondoa madarakani.

Mwaka huu 2020 CCM imeunda muungano wake na vyama vingine vya CUF, NCCR na TLP dhidi ya CHADEMA.

Ina maana CCM pamoja ya kuwa ina dola imeshindwa kupambana na CHADEMA peke yake hadi inaazima majeshi ya kukodi? Halafu bado kuna watu wanasema CHADEMA imekufa.

View attachment 1464247

Picture speeks a thousand words.

ACT-Wazalendo wanabaki kama watazamaji au swing voters?
Selasini Katibu mkuu Nccr mageuzi, Lwakatare Katibu mkuu Cuf and soon Lema Katibu mkuu TLP......... Chadema lazima waombe pooo!
 
Back
Top Bottom