CCM ya Jakaya 2015 ili kupambana nayo, Chadema ilibidi itafute majeshi ya ziada NCCR, CUF na NLD ili kuongeza nguvu maana uwezo wa CCM ulikuwa mkubwa.
Lakini miaka mitano baadae yaani 2020 CCM ya John imeshuka daraja na viwango na ili ipambane na Chadema sasa CCM inabidi itafute majeshi ya kuongeza nguvu nayo ni NCCR, CUF na TLP.
Ukiangalia kwa jicho lisilo ushabiki mpambano huu utakuwa mgumu sana maana CCM pamoja na usaidizi huo wa vyama vingine bado wana usaidizi wa Polisi na Tume.
Lakini pia upande wa Chadema nao nafasi ya nguvu ya watu kusimama upande wao (peoples power) ni tishio pia kwa wapinzani wao.
Nini sababu ya CCM kushuka daraja kiasi hiki hadi kutegemea msaada wa vyama vingine, vyombo vya dola hadi Tume ya uchaguzi wakati walikuwa na nafasi ya kujenga maisha bora na kuaminika?