Quinine,
CCM imeshatambua kwamba inapambana na wananchi, siyo Chama.
Nguvu na ujumbe wa vitisho ambavyo wamekuwa wakipewa CHADEMA ni ujumbe kwenda kwa wananchi kwamba hata mtumie mbinu gani hampati kitu. Ujumbe huo pia unawalenga walio ndani ya CCM kwamba mkijifanya ku side na wananchi mjue hampo salsma, sasa hivi hata Jaji Warioba, Kabudi na akina Polepole wameshaikana ile rasimu ya katiba ya wananchi ambayo kwao walishaiona kama ni misahafu.
CHADEMA inapinzwa tu na wananchi wengi waliochoka, sababu CHADEMA kama chama hawana jipya wala tofauti na NCCR, CCM na CUF, kamavwangekuwa na kitu cha tofauti kamwe wasingefanya mabadiliko ya dakika za nyongeza kwenye nafasi ya mgombea wa nafasi ya urais.
Siku zote nitaendelea kumheshimu sana Dr. Slaa kwa mikakati na nguvu aliyoitumia kuijenga CHADEMA na kupelekea wananchi kuamua kukiunga mkono, pili msimamo wake wa kusimamia anachokiamini. Tatu utiifu wake kwa mamlaka zake za uteuzi, tuliona alivyokua mtiifu na mnyenyekivu kwa Mbowe na sasa alivyo kwa Magufuli.
CHADEMA haina cha tofauti, watu ndiyo wameamua kuichagua na nguvu inayotumika ni dhidi ya watu diyo CHADEMA. Kama kuna point itainekana CHADEMA ni threat kiasi hicho basi ingefutwa kitambo tu.