CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!



Wakati mwingine uchambuzi wa namna hii unanishangaza sana ... na ndiyo maana itachukua muda kuondokana na hizi dhana za alinacha ... ilipotokea Mbeya Vijijini, ikadaiwa kwamba ni kwa sababu ya mgombea wa Chadema alienguliwa na hivyo wananchi walisusia ... sasa huko Busanda ni sababu nyingine kabisa ... halafu eti ni wachambuzi wa masuala ya uchaguzi ... lol!!!

Subirini 2010 ndiyo mtajua idadi halisi ya wapiga kura ...
 


Haya mambo ndiyo yanapotosha ukweli ... hakuna chama kilichokuwa na wagombea wawili ofauti (mmoja wa mjini na mwingine wa vijijini). Wagombea walikuwa ni mmoja kwa kila chama ... na ni kwa jimbo la Busanda ...Ushindi ni kwa jimbo; hayo mambo ya mjini na vijijini kwani uliambiwa huu ulikuwa ni uchguzi za serikali za mitaa? Kinachoongelewa hapa ni hizi biased analysis ... yaani wewe unakaa hapo Katoro tu na kuleta analysis ya upande mmoja as if Busanda ni Katoro na Katoro ni Busanda. Ulitakiwa kuleta taarifa za pande zote mbili; ama haukujua kwamba kuna vijiji huko Busanda ...

Haya maoni yakusaidie ili utakapoenda Biharamulo au mahali pengine, ulete taarifa sahihi na zisizoelemea upande mmoja ... mwana-demokrasia wa kweli kama unavyojitambulisha ni yule anayewatendea haki hata wale anaowaletea habari kwa kuhakikisha zinakuwa sahihi na zilizofanyiwa kazi sawa sawa na siyo almradi tu liende.

Acheni kabisa kuwadharau watu wa vijijini ... hao ndiyo wanaowalisheni ninyi wa mjini ... na ndiyo hao hao wametufanya wengine tukawa hivi tulivyo kiasi cha kuweza kutumia hata hii teknolojia ya kisasa. Siyo wote "tulijaaliwa" kuzaliwa na kuishi mijini kama ninyi wenzetu.
 
Naunga mkono bwana Ng'azagala aliyeshauri pesa za helikopta wangepewa wapambe wanakijiji ili wakawanyweshe pombe wenzao. Sasa hivi CHADEMA wangekuwa wanacheka.

Pia CHADEMA wangeazima trick ya Obama na kuanza kuandika vitabu vya kutambulisha key figures kama vile Mbowe mwenyewe kwa jamii. Watu wengi wanajua Mbowe alikuwa DJ wa Billicanas profile ambayo sio nzuri sana kwa mtu anayetaka uraisi.
 


Mkuu Domisianus, sina uhakika kuhusu
kupendwa zaidi kwa CCM iwe mijini au vijijini. Sina uhakika hata kama CCM kweli inapendwa.

Nikianza na mijini ambapo inaelekea unataka tuamini CCM haipendwi zaidi, takwimu zinaonyesha tofauti. Katika miji yote mikubwa ya nchi hii, CCM imekuwa ikishinda karibu majimbo yote (kwa Ubunge) na karibu kata zote (kwa udiwani).
Nionavyo mimi ni kwamba, hata tukichukizwa na CCM kiasi gani, inaelekea baada ya siku, tunarudi na kuiunga mkono tena katika uchaguzi mkuu. Nadhani sababu kubwa katika hili ni options zilizopo kutoka kwa wapinzani. Watu wengi pamoja na chuki zao kwa CCM, hukosa option zinazofaa kutoka upinzani na hatimaye kuishia kuipigia
tena kura CCM siku ya Uchaguzi. Nadhani kuanzia hapo, ndipo fumbo kubwa linapoanzia.

Kwa upande wa vijijini, nadhani ni kinyume kwa kiasi fulani. Maana kura nyingi za upinzani hutokea huko. Japokuwa bado hazitoshi kuleta mabadiliko makubwa. Ninavyodhani mimi ni kwamba, kwakuwa watu wa vijijini husikiliza zaidi watu wa mijini, baadhi ya watu hudhani ni rahisi zaidi kumshawishi mtu wa kijijini kufanya uamuzi anaoutaka. Mara nyingi hiyo sio fikira sahihi. Watu wa vijijini wengi wao pamoja na hali duni kuliko wa mijini, huwa na misimamo thabiti kuliko wale wa mijini. Hujua kila mgombea kwa kina zaidi (kwa kuwa ni mtoto wao, na pengine amekulia pale pale kijijini). Wagombea wengi ni wazaliwa wa huko huko vijijini, tofauti na ilivyo kwa wagombea wa mijini.


Nadhani wengine wanaweza kusaidia zaidi. Ila ni kweli kuwa sababu zinahitajika kufumbua fumbo hilo la kisiasa.
 
Huu ni ushauri ama ulaghai? Jamani uchambuzi wa siasa ni proffesion sio biashara ya kuuza njugu.........Ishhhhhhh

omarilyas

Mkuu Omarilyas, mimi nimetoa mtazamo wangu. Wewe pia unaweza kuwa na mtazamo wako ambao mimi nitauheshimu (uwe sahihi au wenye na mapungufu).

Ili niweze kuwa mtaalamu wa siasa kama wewe, unaonaje ukanisaidia kuelewa zaidi kwa kubainisha ulaghai uliopo kwenye post niliyoitoa na upo kwa jinsi gani. Maana hapa ukweli huwekwa wazi na uongo hukemewa.

Niko tayari kupata somo mkuu. Ama linalipiwa?
 

hehe..... nafikiri ile bendera bado ina jembe na nyundo.
 
acheni unafiki,na msijidai hamuuoni UKWELI...CCM inashinda vijijini coz uelewa wa watu wa huko bado ni mdogo sana kwenye mambo ya siasa, THAT'S ALL!! ni mjinga tu ndio anaweza akaamini vinginevyo...BUSANDA wameongea, ila mnafahamu SAUTI yao ilikua ni YAO kwa kiasi GANI??
 

Mjini Dar Salaam kuna wabunge wangapi wa upinzani oooops sorry! huko mbali sana... kuna madiwani wangapi wa upinzani?
 
About 135,000 people were expected to vote but only 55,460 participated in the election with eligible votes being 53,309 after 2,029 were declared invalid according to the returning officer, who is also the Geita District Executive Director (DED).
source ippmedia

135000 - 55460 = 79540

acheni kuwalaumu chadema hapa lazima kuna wizi wa kura, inawezekanaje watu 79540 hajapiga kura, this is a day light robbery
 

Mhe. Lolesia Bukwimba


Picha kwa hisani kubwa ya Mzee wa Sumo.
 

Attachments

  • CCM_Lolesia_Bukwimba_1.JPG
    10.3 KB · Views: 109
  • 5.JPG
    27.9 KB · Views: 115

hapo mdau kama unafikiri vijijini wana uelewa mdogo kwenye siasa? sasa unapropose nini? Je upinzani wasishiriki maeneo ya vijijini? say something upinzani wanahitajika kushinda na si porojo zako? hivi unajua TZ % ya population ya vijiji ni kiasi gani 80%? that means upinzani hawawezi kushinda?
mbona majimbo mengi ya mijini yanashikiliwa na CCM? naona hapo unajichanganya
 
Masatu,
Unajua mkuu wangu mimi hutazama mbali sana ktk maswala kama haya na nimejaribu sana hapa kijiweni kuwaamsha wana Chadema na Wapinzani wote lakini tamaa zao za ruzuku na Ubwana.. kuitwa Mheshimiwa kumewalegeza zaidi..
Ukweli ni kwamba uchaguzi wa mwaka 2005 nili ufanyia uchunguzi wangu binafsi na kugundua kwamba CCM imeshinda sana sehemu zote kutokana na utengano wa Wapinzani.
CCM sehemu nyingi ilishinda kwa asilimia 50 hadi 60 ktk kura za Wabunge na Madiwani karibu nusu ya mikoa yote.. Na nikasema ikiwa wapinzani wanataka kuleta ushindani wa haki ni bora kabisa wamsimamishe mgombea mmoja ktk kila jimbo..
CCM mara nyingi inashindwa kwa sababu ya migogoro kati ya Wapinzani..CCM wakitumia mbinu ya udini na Ukabila ktk kujenga hoja zao kuvishutumu vyama vya CUF na Chadema mbavyo kwa nyakati tofauti vilipata umaarufu..
Lakini kama siku itatokea CUF na Chadema wakiungana wataondoa hizo dosari ambazo kila siku huwaumiza na CCM wanafahamu wapi pa kubonyeza..Nina hakika kabisa wakiungana hawa wengine watafuata na wananchi watavitazama vyama hivi kama vyama pinzani badala ya kupachikwa majina ya chama cha Walalahoi, Wapemba, Waislaam, Wakristu na Wachagga!..
Hakuna mtu wala kiongozi anayeweza kuondoa dosari hizi kwa sababu zimeisha pandikizwa siku nyingi sana na vyombo vya habari..
Ni kweli kabisa CCM ina madiwani wengi mijini na vijijini lakini yote haya yanatokana na vyama pinzani kugawana kura..Dar hawana kwa sababu hiyo hiyo wapinzani waligawana kura CCM akaondoka mshindi tena sehemu nyingine kwa asilimia 40 tu..
Kuna Washikaji wangu kibao ambao walipigia kura chama cha CUF mwaka 2000 wakiwa wakristu, lakini hofu za udini na Upemba zilipoingia tu baadhi walihamia Chadema na wengine kurudi CCM na hawa mwaka 2005 nina hakika walipiga kura against CUF chama ambacho wanaamini mrengo na sera zake kuwa ni bora..Na bila kuficha hata mimi nimeshaulizwa kuwepo kwangu Chadema kama naelewa kinachoenelea ndani ya chama hiki..
Majibu yangu siku zote yamekuwa mimi ni Conservative, siwezi kuondoka chama kwa sababu ya mambo yao binafsi nikaacha imani yangu ktk mrengo unaoweza kuiendeleza nchi yangu..Kesho ukinambia CCM ni Conservative nitahamia huko na kuondoka Chadema kama wao watageuka kuwa Progressive bila kujali akina nani ndio viongozi.. Huu ndio mtazamo wangu wa siasa na ndio maana sintaweza kuingia siasa za Bongo..
Na bahati mbaya hakuna demokrasia Tanzania na haitapatikana tusidanganyane!.. haiwezi kuwepo demokrasia kwa sababu tupo wachache sana wanaotazama Siasa za Tanzania kwa jicho la mrengo..Hivyo mategemeo yangu hayawezi hata siku moja kuzaa matunda kwani watu wote Tanzania wanakichagua chama kutokana na sura za watu, ahadi pamoja na kuendekeza imani za kidini kwamba ukizaliwa Muislaam au Mkristu huwezi kubadilisha dini..Sisi sote tumezaliwa Wana CCM na tunapojiunga na vyama vingine ni sawa na kubadilisha dini.. hivyo tunaonekana kuwa waasi na mara zote waasi hawana sifa nzuri ktk jamii ya Kidanganyika...
 
Nimejaribu sana kuweka hesabu sawa naona sipati majibu na ninaomba yeyote ambaye ana-data au ujuzi wa kuvumbua hili fumbo anieleze.

Kwanza ningeomba tabia ya watu wa busanda kujiandikisha na kupiga kura miaka ya nyuma. je niwangapi huwa wanajiandikisha na wangapi huwa hawatokei kwenye booth kupiga KURA.

Halafu ningependa kujua nini hasa kilitokea kwa zaidi ya 77,000 kutokupiga kura au kutokea kwenye vituo vya kura.

Je wanangu Chadema nini kiliwasibu kutokulijua hilo au CCM ilinunua shahada zote na wapiga kura wakaingia mitini.

Naomba kujua kura zilivyopigwa kila kituo ili kujua athari za Chadema zililetwa na kura za vijijini au vyote au rafu. Uwiano wa vijijini na mjini ulikuwajE wakati wa kupiga kura bahati mbaya hapa nyumbani huwa hatuweki ankara za umri wa wapiga kura, kazi, elimu nk.

Nawapa Hongera Chadema kwani wameonyesha mapinduzi ni matumaini yangu 2010 hawawezi kwenda nchi nzima kila mtu atakuwa kwake. Ni kuongeza nguvu kwenye majimbo yao kwani kama hawataiba fedha nyingi wengi watakwenda na maji.

KUKATA TAMAA NI DHAMBI YA MAUTI. MOTO KWA KWENDA MBELE
 
Nakushukuru Mkuu kulisemea hili, kwa mtazamo wangu, nimewagawanya wanasiasa katika makundi makuu matatu.
Kundi la Kwanza:Ni wanasiasa wanaipenda siasa kwa dhati, na wenye uwezo wa uongozi, hawa sio wapiga domo wazuri, ni makini kwenye mambo yao na wengi wao ama lazima washawishiwe na watu, ama wateuliwe. Wengi wa kundi hili wanashughuli zao hivyo hawawi mstari wa mbele kugombea nafasi za uongozi kutokana na uchafu katika mchezo wa siasa.
Kundi la Pili:Ni la wanasiasa oportunists ambao wanaingia kwenye siasa kutafuta madaraka kutokana na njaa zao. Kwao siasa ni ajira, wengine wana uwezo wa uongozi na wengine hawana ila lengo lao ni moja, kuchumia tuu na kutaka kuula. Wengi wao hata baada ya kuukwaa ubunge, huwa wanasikitika kuukosa ulaji wa uwaziri. Hawa huwa tayari kufanya lolote ili kupata wanachokitaka. Hili ndilo kundi kubwa la wanasiasa wetu wakiwemo wengi walio kwenye upinzani.
Kundi la Tatu:Ni la wanasisa walioshiba wanaoingia kwenye siasa kutafuta power. Hawa wanafedha zao ambazo huweza kuzitumia kupata uongozi wanaoutaka na mara nyingi, hawana uwezo wa uongozi na wala siasa hawazijui, wao kila kitu itaongea pesa tuu.
NB, Hii tathmini yangu haihusiani na Natural Born Leaders, Self Made Leaders na Opportunists.
Lengo la kutanguliza tathmini hiyo ni ili kukuongoza kujua kwa nini wapinzani hawataki kuungana na kamwe hawataungana kutokana na wengi wa viongozi wake kuangukia kwenye kundi la pili ambao ni wanasiasa njaa wenye uchoyo na ubinafsi wa umimi hali inayopelekea kila chama kung'ang'ania kusimamisha wagombea wake na kushindwa kusimamisha mgombea mmoja.
Mimi naamini wale waliosusia uchaguzi Busanda, ni wafuasi wa CUF na UDP ambao walishakatishwa tamaa na uwezekano wa kushinda wagombea wao, wakaona kuliko kupoteza muda kwenda kupiga kura, bora wajipumzie na kujilia raha zao na muda wao.
Kama wapinzani wangesimamisha mgombea mmoja, Busanda wangeiteka kwa ulaini kama kumsukuma mlevi.
Ubinafsi na umimi ndio unawaponza wapinzani, mathalan, baada ya Chadema kuenguliwa Mbeya vijijini, walikuwa hawana sababu ya kususa, bali kuunganisha nguvu kumuunga mkono mgombea anayekubalika zaidi, kwa kususa kwao, CCM wamepeta, na Busanda hali ni hiyo hiyo.
Swali ni lini wapinzani watafungua macho na kuukubali ukweli halisi kuhusu siasa za Tanzania.
 
kwa kuwa uchaguzi mkuu ni karibu 2010, kwenda mahakami inaweza kuwa ni kupoteza muda, hivyo labda aanze kampeni mapema , mfano kwa kuwashawishi hao amba hawakupiga kura , basi 2010 wampigie pamoja na hizo alizo pata sasa.
 
uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi wapinzani walishinda, ccm waka hujumu na tume ya uchaguzi kwa madai vifaa vilichelewa etc etc, hivyo yalivyo rudiwa huku ccm ilisha pata ushindi sehemu kubwa ya nchi ili wakatisha tamaa wapiga kura kwenda kwenye uchaguzi wa marudio, uchaguzi wa 2005, Watu wengi wa DSM walikuwa na Imani na Kikwete, na pia kuibuka kwa wagombea wengi wapya, badala ya wale wa zamani ukiachilia Chenja? ubungo na Rita Mlaki Kawekama sikosei , hivyo watu wakawa na matumaini mapya ya wabunge wapya "vijana" kwamba mambo yao yatakuwa ya kimaendeleo kama Abbas Mtemvu temeke, Idi Azzan ? kinondoni na Yule wa Ilala , na kigamboni na wa Ukonga ni "Kijana" sio wale wazee tulio kuwa tumewazoea, sasa hii mix na kuongezea na Kikwete for Presidence, iliwashawishi watu kukipigia kura CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…