Vitabu nilivyosoma 2023

EJM_

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,836
2,093
Mwaka jana 2023 niliamua pia kusoma vitabu vya riwaya za kiswahili ambapo niliegemea zaidi kwenye zile za ujajusi. Katika hizi niliamua kusoma riwaya za waandishi watatu
1. Calvin Mponda
2. Richard Mwambe
3. Patrick CK

Kwa waandishi Hawa niliweza kusoma vitabu 9
1. Julai 7 - Richard Mwambe
2. Kitanzi Cha mwisho - Richard Mwambe
3. Msako wa mwanaharamu - Richard Mwambe
4. Ufukwe wa Madagascar - Kelvin Mponda
5. Siri - Patrick CK
6. Maisha na Kifo Cha Melanie Chuma - Patrick CK
7. Jasusi/Gaidi - Patrick CK
8. Scandal (Kashfa) - Patrick CK
9. Kiapo Cha Jasusi - Patrick CK

Utaona nimesoma vitabu vingi vya Patrick CK ni kwasababu Kuna ambavyo vilikuwa kama series hivi (Siri - Scandal) kwahiyo nilijikuta nasoma vyote Ili kupata mwendelezo japo Kila Moja ina theme tofauti Ili zilizounganishwa na baadhi ya matukio na wahusika.

Sasa waandishi Hawa Kila mmoja ana style yake ya uandishi na namna anavyotoa masimulizi ya kile anachokifikisha kwa hadhira yake.

Kelvin Mponda anaweza kukufanya ukahisi na wewe ni sehemu ya hicho unachosimuliwa yaani kama na wewe ni mmoja wa character wa hadithi zake. Mfano anapokuelezea matukio yanayotokea mji wa Bujumbura atakufanya mpaka na wewe uhisi umewahi kufika mji huko maana utapigishwa mtaa mmoja mmoja kwa majina yake na namna mtaa huo ulivyo na kuhisi kama unaangalia movie vile. Wakati nasoma kitabu Cha kwanza Cha Kelvin Mponda (Tai kwenye Mzoga) Kuna sehemu nilifika nikapumua utafikiri na Mimi nilikuwa napitia matukio ya mule ndani.

Patrick CK ana aina ya usimuliaji ambayo inakufanya ujikute unachagua upande au unachukizwa na baadhi ya characters na kuhisi namna ambayo kwenye maisha ya kawaida hao watu watakuwa wanafananaje. Ila kikubwa anachokifanya Patrick ni namna anavyoweza kutengeneza mtiririko wa matukio hata matano halafu yakaja kuconnect mwisho na ukaishia kusema eewhhh kumbe! Ila pia ni mtaalamu sana wa suspense stories, political espionage and international espionage. Huyu Jamaa kwenye eneo hili ni balaa sana kwa kweli kwa mwaka 2023 nimeenjoy kumsoma Mathew Mulumbi, Gosugosu, Rubi na kiasi Peniela.

Richard Mwambe ana muunganiko wa hao wote wawili lakini anachokifanya ni kupunguza maelezo ya masimulizi yake na ndio maana vitabu vyake sio vikubwa kulinganisha na hao wengine wawili. Changamoto niliyoiona tu ni kuwa Kuna sehemu anamfanya Kamanda Amata kuwa super human na kuhisi kama unaangalia Marvel movies hivi. Ila Bado nimeenjoy kumsoma Kamanda Amata na timu yake inayoongozwa na Madam S.

Mwaka huu naendelea nannataka nisome kama vitabu 10 hivi au 15 kama mnaweza kunipendekezea itakuwa poa. Please tafuteni hivi nilivyosoma nanhamtajutia.
 
Tafuta mtutu wa bunduki- Kelvin mponda
 
Vya patrick vk nimevipitia karibu vyote.jamani kuna watu wanajua kuteka akili za watu kwangu ilikua ni kawaida kufika saa kumi usiku niko macho kwa story za huyu jamaa

Ufukwe wa madasca hii nayo ilikua ni moto wakuote mbali. Sema sijaimaliza mwandishi akakimbia madasca nae
 
Soma kitabu Cha Ujasusi wa kidola na kiuchumi ameandika Yerico Nyerere utajua mengi pia
 
Back
Top Bottom